MAELEZO YA IMANI

STATEMENT OF FAITH

Isaya 61

1 Roho ya YAHUVEH I juu yangu; kwa sababu YAHUVEH amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao;
2 Kutangaza mwaka wa YAHUVEH uliokubaliwa, na siku ya kisasi cha Mungu wetu; kuwafariji wote waliao;
3 Kuwaagizia hao waliao katika Sayuni, wapewe taji ya maua badala ya majivu, mafuta ya furaha badala ya maombolezo, vazi la sifa badala ya roho nzito; wapate kitwa miti ya haki, iliyopandwa na YAHUVEH, ili atukuzwe.
4 Nao watajenga mahali pa kale palipoharibiwa, watapainua mahali palipokuwa ukiwa zamani, watatengeneza miji iliyoharibiwa, mahali palipoachwa kizazi baada ya kizazi.
5 Na wageni watasimama na kulisha makundi yenu, na watu wa kabila nyingine watakuwa wakulima wenu, na watunzaji wa mizabibu yenu.
6 Bali ninyi mtaitwa makuhani wa YAHUVEH; watu watawaiteni wahuduma wa Mungu wetu; mtakula utajiri wa mataifa, na kujisifia utukufu wao.
7 Badala ya aibu yenu mtapata maradufu, na badala ya fedheha wataifurahia sehemu yao; basi katika nchi yao watamiliki maradufu; furaha yao itakuwa ya milele.
8 Maana MIMI, YAHUVEH naipenda hukumu ya haki, nauchukia wivi na uovu; nami nitawalipa malipo katika kweli, nitaagana nao agano la milele.
9 Na kizazi chao kitajulikana katika mataifa, na uzao wao katika kabila za watu; wote wawaonao watakiri ya kuwa wao ni kizazi kilichobarikiwa na YAHUVEH.
10 Nitafurahi sana katika YAHUVEH, nafsi yangu itashangilia katika Mungu wangu; maana amenifunika vazi la haki, kama bwana arusi ajipambavyo kwa kilemba cha maua, na kama bibi arusi ajipambavyo kwa vyombo vya dhahabu.
11 Maana kama nchi itoavyo machipuko yake, na kama bustani ioteshavyo vitu vilivyopandwa ndani yake; ndivyo YAHUVEH MUNGU atakavyootesha haki na sifa mbele ya mataifa yote.

YAHUSHUA ni Mwana wa Mungu YAHUVEH aliyedhihirishwa kwa mwili! YAHUSHUA ni Masihi wetu! YAHUSHUA ni Mfalme wa Wayahudi, Mfalme wa Wafalme, Bwana wa Mabwana! YAHUSHUA ni Bwana Arusi wetu anayekuja! YAHUSHUA alizaliwa kutoka kwa bikira na Baba yake wa pekee ni YAHUVEH! ! YAHUSHUA alizulubiwa awe tabihu wa pekee Takatifu kwa pahala petu, na akafufuka siku ya tatu. Tunangojea kwa hamu kurudi kwake tena, kwa kuwa atakujia Bibi Arusi wake, wanaolinganishwa na wanawali watano wenye busara. NJOO YAHUSHUA NJOO UPESI NI OMBI LETU!

Tunaamini…
YAHUSHUA pia anajulikana kwa jina YESU KRISTO, lakini Huduma huu unaamini tunapaswa kumwita Masihi wetu kwa Jina lake la Kihebrania linalomaanisha “YAH anaokoa.” Jina hili ni ukumbusho ya kuwa Muumba wetu, ambaye ni MUNGU Baba YAHUVEH wa Mbingu na Dunia na yote yalio katikati anaokoa roho zetu kupitia kwa Mwanawe mzaliwa wa pekee YAHUSHUA. Jifunzeni kuhusu Majina yao Takatifu

Tunaamini…
Njia moja tu ya kurudi Mbinguni ni kupitia kwa kumkubali YAHUSHUA, aliyezaliwa kupitia kwa bikira, aliyesulubishwa kwa pahala petu na akafufuka siku ya tatu, baada ya siku arobaini na mbele ya mashahidi alipaa juu Mbinguni.

Tunaamini…
YAHUSHUA alikuja duniani kutoka mbinguni, yeye ni Mwana mzaliwa wa pekee wa YAHUVEH, ambaye yeye pekee ndiye dhabihu wa damu ya kikamilifu aliyekuja hapa duniani afe kwa ajili ya dhambi zetu. YAHUSHUA hakubaki akiwa amekufa bali kwa siku ya tatu alifufuka na sasa amepewa nguvu zote kutoka kwa YAHUVEH. Tunaamini YAHUSHUA atarudi tena kwa ajili ya waaminifu wake anaowaita Bibi Arusi wake, wanaolingalishwa na wanawali watano wenye busara, inayoitwa unyakuzi.

Tunaamini…
kwa kumpokea YAHUSHUA kama MASIHI na kutubu kwa YAHUVEH na YAHUSHUA kwa ajili ya dhambi zako, ukigeuka mbali na dhambi hizo na kufanya unavyoweza kuwatii, kuwapenda, kuwaabudu, kuwatumikia na kuwaweka wa kwanza katika kila njia, wapendwa wetu BABA YAHUVEH na YAHUSHUA ha MASHIACH( inayomaanisha Masihi), ataokoa roho zetu na kutupeleka Mbinguni tutakapokufa ama kunyakuliwa.

Tunaamini…
tukifanya hivyo, RUACH HA KODESH, ambaye pia anaitwa ROHO MTAKATIFU ataingia miilini mwetu ambao sasa itaitwa hekalu ya RUACH HA KODESH. Tunaamini tunapaswa kumchukia ibilisi na kazi zake kama vile tunavyowapenda YAHUVEH na YAHUSHUA na RUACH HA KODESH. Tunapaswa kutetea yale yote yaliyotakatifu na kukemea na kuachana na yote yasiyotakatifu. Tunapaswa kuishi maisha ya utakatifu kwa MASIHI wetu na kufuata mfano wake wa utakatifu.

Tunaamini…
sisi si wakamilifu, kwa kuwa YAHUSHUA ndiye pekee aliyemkamilifu, lakini tukitenda dhambi kwa maneno ama matendo yetu tunaitana katika jina la YAHUSHUA na kumwomba Baba wetu YAHUVEH atusamehe, tukiomba damu iliyomwagika ya YAHUSHUA juu ya dhambi zetu na kuomba zisamehewe, na baadaye kufanya tuwezavyo kubaki tukiwapendeza YAHUVEH na YAHUSHUA.

Tunaamini…
YAHUSHUA pekee ndiye mtetesi wetu wala si Mama yake Maria, hata hivyo tunamheshimu na kumpenda kwa kuwa yeye ni mamake YAHUSHUA. Walakini hatumwabudu kwa vyovyote vile ama kumwomba, kwa kuwa YAHUSHUA, hata ingawa yeye ni mwanawe wa kidunia, ni Masihi wake pia, kwa kuwa pia alimwita BWANA. Kama Maria angekuwa hana dhambi, basi angestahili kuwa dhabihu la damu mle Kalvari. Kosa la kanisa la Kikatoliki ni kumfanya Maria kuwa sawa na YAHUSHUA. Kuna utatu moja tu na ni BABA YAHUVEH, Mwanawe YAHUSHUA na RUACH ha KODESH. Hakuna hata mmoja wetu angeokoka kama RUACH ha KODESH hangetuelekeza tumpende na kumkubali YAHUSHUA kama MASIHI.

Tunaamini…
kwamba tunahitajika kujifunza na kusoma kuhusu Uyahudi wa MASIHI wetu ambaye pia anaitwa Mfalme wa Wayahudi. Huduma huu pia unaamini tunapaswa kuheshimu Sherehe Takatifu kama vile YAHUSHUA alivyozingatia na YAHUVEH aliamuru na hii ni pamoja na kuheshimu Siku ya Sabato na kuiweka Takatifu ambayo ni siku ya saba Ijumaa Jioni hadi Jumamosi Jioni. Huduma hii ina majukumu yaliyoko ISAYA 61. Huduma huu unaamini kuna Mbinguni ya kuipata na Jehanamu ya kujiepusha nayo na kila mtu aliye hai hujitayarishia nafasi katika Mbinguni ama Jehanamu kulingana na vile wanavyomtendea YAHUSHUA. Je! Wamemfanya YEYE kuwa MUNGU na MASIHI wao, ambaye pia anaitwa Mwokozi?

Tunaamini…
Bibilia pekee ndiyo neno la YAHUVEH lililo na pumzi Ya YAHUVEH na ni kamilifu katika maandiko ya awali. Tunaamini Neno la YAHUVEH, Bibilia na Torati hawezi kusema uongo. Kwamba YAHUVEH ndiye pekee Baba wa Mbinguni, Muumba wa wote.

Tunaamini…
Huwezi kuishi kama shetani na tena upate kwenda Mbinguni. Lazima kuwepo kujitenga mbali na dhambi, na kuamini kupitia kwa YAHUSHUA, YAHUVEH atakufanya kiumbe kipya katika YAHUSHUA kama vile Bibilia inasema, “Mambo yote ya kale yamepita na yamekuwa mapya." YAHUSHUA hana dhambi kamwe na damu yake ni safi na ni takatifu na hiyo ndiyo sababu YEYE pekee ndiye sadaka ya damu iliyo kamilifu kwa ajili ya dhambi zetu.

Tunaamini…
Tukishamkubali YAHUSHUA awe Mungu wetu, Bwana na mwokozi wetu, tutakuwa na nia ya kumtii kwa sababu tunampenda. Tunajua ya kuwa tukitenda dhambi, tunayo Damu Yake Takatifu inayosafisha dhambi zetu. Lakini hatuendelei kutenda dhambi, tunajaribu na kutii na kuwa watakatifu kama vile YAHUSHUA ni Mtakatifu.

Tunaamini…
kuna Mungu mmoja, anayekuwepo milele katika utatu: Mungu Baba, YAHUVEH. Mungu Mwana, YAHUSHUA, na Mungu Mama, RUACH ha KODESH [ROHO MTAKATIFU].

Tunaamini…
Katika Uungu wa YAHUSHUA, katika kuzaliwa kwake na bikira, katika maisha yake yasiyo na dhambi, katika miujiza wake, katika kifo chake kilichokuwa chungu na cha upatanisho, katika ufufuo wake kimwili, katika kupaa kwake kwa mkono wa kulia wa Baba, katika kurudi kwake binafsi Dunia hii siku zijazo kwa nguvu na utukufu na kupokea kwake, kanisa alilolinunua kwa damu yake, atakayetawala naye milele, BIBI ARUSI WA YAHUSHUA

Tunaamini…
katika kunyakuliwa, rapcha ya Bibi arusi wa YAHUSHUA ambao hawakuwekewa kupokea hasira za Baba YAHUVEH. Tunachukua msimamo kutojiita jina lolote, iwe Kabla ya Dhiki Kuu, Katikati ya Dhiki Kuu au Baada ya Dhiki Kuu, kwa sababu inawezekana ni mchanganyiko ya hayo yote. Lengo kubwa ni kuwa tayari bila kujali wakati YAHUSHUA anarudi kwa ajili ya Bibi arusi wake Mpendwa. Kaa katika imani na kushughulika mpaka atakapokuja, ukiishi kila siku kana kwamba ni wa mwisho kwetu.

Tunaamini…
Biblia ni YAHUSHUA, Neno aliyefanyika Mwili.Tunaamini YAHUSHUA amepaka mafuta huduma huu kufikia Wayahudi na watu wa Mataifa, kufikia jamii yote, jamaa, na lugha. Kufikia Mataifa yote. Sisi HATUNA ubaguzi unayohusiana na utajiri au umaskini. Wote watahudumiwa bure na wahudumu wote wanaohusiana na Huduma huu.

Tunaamini…
katika kuleta roho kwa YAHUSHUA kwa ajili ya Sifa zake, Heshima na Utukufu wake pekee.

Tunaamini…
Namna pekee ya kutakaswa kutokana na dhambi ni toba, kujitenga na dhambi, na kuungama hiyo dhambi mbele ya YAHUSHUA wa Kalvari na Nazareti, na kumwomba msamaha kwa ajili ya hiyo dhambi, na kuosha katika damu takatifu ya YAHUSHUA wa Kalvari, na kuwa na imani katika damu ya thamani ya YAHUSHUA, ubatizo kwa maji ni ishara ya nje kwa wengine kwamba sisi tunamkiri YAHUSHUA hadharani kama Bwana na Mwokozi na kukubali zawadi ya YAHUVEH katika Kalvari.

Tunaamini…
Yohane alibatiza kwa maji na YAHUSHUA anatumia RUACH HA KODESH (ROHO MTAKATIFU) kutubatiza na Moto wa Roho Mtakatifu kama vile ilivyokuwa katika siku ya Pentekoste. Tunaamini katika kunena kwa lugha takatifu na katika gharama zote za RUACH HA KODESH na ubatizo katika RUACH HA KODESH, kulingana na Matendo 2:4, alitolewa kwa waumini wanaoomba kwa ajili yake na wanaamini wanampokea kwa imani.

Tunaamini…
ishara hizi zitafuatana na hao waaminio: watatoa pepo kwa jina la YAHUSHUA, watanena kwa lugha mpya, wataweka mikono yao juu ya wagonjwa nao watapona. Tunaamini ishara, maajabu na miujiza yatafuatana na hao waaminio katika YAHUSHUA kama Mwokozi, Mkombozi, Mponyaji, ni yeye ambaye baraka zote zamimina kutoka kwake.

Tunaamini…
YAHUVEH, YAHUSHUA, na RUACH HA KODESH si Mwenyezi tu katika UPENDO lakini pia ni Mwenyezi katika vita dhidi ya maadui wake.

Tunaamini…
kwamba kuzaliwa upya na RUACH HA KODESH ni muhimu kabisa kwa ajili ya wokovu binafsi. Tunaamini kuwa ni RUACH HA KODESH anayeongoza roho hadi kwa neema ya wokovu wa YAHUSHUA na hakuna mtu awezaye kuokolewa bila kuongozwa na RUACH HA KODESH hadi kwa YAHUSHUA wa Kalvari na Nazareti.

Tunaamini…
Ruach HA KODESH huharibu nira na utumwa wote. Tunaamini RUACH HA KODESH bado anapaka mafuta na kuongea kupitia kwa Mitume, Manabii, Wainjilisti, Walimu, na Wachungaji.. Tunaamini kuwa sisi tunapaswa kuteuliwa na YAHUVEH na sio kuteuliwa na binadamu tu.

Tunaamini…
Tunapaswa kuishi katika dunia hii lakini si kuwa kama dunia hii. Tunaamini dunia siyo nyumbani kwetu, lakini Mbinguni ni nyumbani kwetu. Wakati kazi zetu duniani itakapomalizika sisi tutarudi kwa Baba wetu wa Mbinguni YAHUVEH.. Tunaamini haya miili tulionao sasa ni ya muda tu na ni udongo tu utakaorudi mavumbini baada ya kifo. Hata hivyo, tunaamini Roho uendelea kuwa hai Milele katika Mbinguni au Jahannamu. Hatuamini katika Reincarnation (inamaanisha kurudi tena katika mwili mwingine wa kibinadamu au mnyama baada ya kifo) tunaamini Bibilia: "Imekusudiwa kwa mtu kufa mara moja na kisha hukumu."

Tunaamini…
katika KUTOWEKA hazina zetu duniani, lakini katika Mbinguni ambapo nondo na kutu hayawezi kuharibu na wezi hawawezi kuiba.

Tunaamini…
kwamba kazi ya ukombozi wa YAHUSHUA juu ya msalaba hutoa uponyaji wa waumini katika YAHUSHUA, akili zao, miili, nafsi, na roho, kama jibu la maombi yetu ya imani katika YAHUSHUA akiwa Mungu na akiwa na mamlaka yote aliyopewa na Baba Yake YAHUVEH.

Tunaamini…
YAHUVEH na YAHUSHUA ni sawa Jana, leo na milele. HAWAWEZI kubadilika kulingana na nyakati zetu.

Tunaamini…
sisi tunapaswa Kuwa Watakatifu kama vile YAHUVEH na YAHUSHUA ni Watakatifu, angalau kuendelea kujaribu, ingawa hakuna mtu anayeweza kamwe kulinganishwa na Utakatifu wa YAHUVEH na YAHUSHUA, ambao sisi tunawatumikia.

Tunaamini…
kwa nguvu ya utakazo ya RUACH HA KODESH anayeishi ndani yetu ili kuwezesha Waumini kuishi maisha ya Utakatifu.

Tunaamini…
katika ufufuo wa wote waliookolewa na waliopotea, na moja kwa maisha ya milele na wa pili kwa hukumu ya milele. Tunaamini ni uchaguzi wa mtu kama atatumia milele yao Mbinguni au katika Jehanamu, ni uchaguzi wao peke yao.
Tunaamini…
YAHUVEH na Mwokozi wetu, YAHUSHUA tayari wanajua wale majina yao yameandikwa katika kitabu cha Uzima wa Mwana Kondoo kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu. Tunaamini katika Baba wa Mbinguni anayewabariki wale wanaomtii, na kulaani wale wanaouasi kama ilivyoelezwa katika Kumbukumbu la Torati 28.

Tunaamini…
katika kuadhimisha siku ya Sabato kwa Utakatifu, ambayo ni Ijumaa jioni mpaka Jumamosi jioni.. Si siku iliyotengwa na binadamu na kufanywa na Kanisa Katoliki ya Jumapili.

Tunaamini…
kwamba kutunza Sabato ni ishara kwamba tunataka kumtii Baba wetu wa Mbinguni na ingawa kutotii hii haitakusuhia kwenda Mbinguni, itakufanya usipate baraka na ulinzi zilizotengewa wale wanaotii, Heshimu Siku ya Sabato na uitakase. Hii inapaswa kuwa wakati wa mapumziko na kutafuta YAHUVEH na YAHUSHUA. Tunaamini YAHUSHUA atakuja tena na itakuwa katika siku ya Sabato. Hatujui ni Sabato gani.

Tunaamini…
kutotunza Sabato ya kweli, pamoja na kutotii Amri zingine kati ya yale Kumi ni uasi wa makusudi na ni lazima kuziungama na kutubu usije ukaangukia hukumuni.

Luka 6:46 “Mbona mwaniita 'Bwana, Bwana,' na huku hamtimizi yale ninayosema?

Wafilipi 2:12 Basi, wapendwa wangu, kama vile mlivyotii siku zote, si wakati mimi nilikuwapo tu, bali sasa zaidi sana mimi nisipokuwapo, utimizeni wokovu wenu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka.

Waebrania 10:29 Je, mtu yule anayempuuza Mwana wa Mungu na kuidharau damu ya agano la Mungu iliyomtakasa, mtu anayemtukana Roho wa Mungu, anastahili kupata adhabu kali ya namna gani?

Tunaamini…
YAHUVEH na YAHUSHUA husema kupitia kwa Mitume na Manabii leo. Tunaamini RUACH HA KODESH hajali mtu ni wa jinsia gani, kama ni wa kiume au wa kike. RUACH HA KODESH huchagua yeyote anayempaka mafuta ili anene maneno Yake. Tunaamini katika kuonya pahali ambapo Mbwa mwitu, Wachungaji waovu na Manabii wa uongo au Walimu wa uongo. Maana tunaamini sisi pia ni Walinzi juu ya mnara, Ezekieli 3:17-21, tukipewa onyo sisi hupitisha au damu ya watu tunaotakikana kuwaonya itakuwa juu ya mikono yetu. Kama sisi tukiwaonya na hawatusikilizi watakufa katika dhambi zao, lakini sisi HATUTAKUWA na damu yao juu ya mikono yetu.

Tunaamini…
YAHUVEH na YAHUSHUA watawalinda watu Wake wakati wa Dhiki Kuu inayokuja, kama sisi tutapaswa kupitia yeyote ni YAHUVEH tu anajua. Tunaamini YAHUVEH atawaruzuku watoto wake wanaoweka imani yao kwake na kukidhi kwa kimiujiza mahitaji yetu yote kwa wingi sana kupita juu ya tunayothubutu kuota au kuuliza kwetu. Kama vile ilivyokuwa katika siku za Mose, Mungu YAHUVEH na YAHUSHUA tunaowatumikia Hawataacha wala kutupilia mbali Watoto wake, Bibiarusi, Waliochaguliwa, na Wateule, lakini atatugharamia kila haja zetu kwa kadiri ya utajiri wake katika utukufu.

Tunaamini…
Ruach HA KODESH hutumia huduma huu kufikia Dunia na Injili ya YAHUSHUA, na kuleta ujumbe wa kinabii kwa watu katika nyakati hizi za mwisho kwa ajili ya kutia moyo, kuonya, na kufundisha.

Tunaamini…
YAHUSHUA anaongoza, anatawala na atakuja tena kuangamiza maadui wake!

Tunaamini…
YAHUSHUA alikuja kama Myahudi na ni Mwokozi wa wote Myahudi na Myunani.

Tunaamini…
Damu ya YAHUSHUA husafisha dhambi zetu, na kutuweka huru na kutulinda sisi kutoka katika nguvu za shetani na laana za ushirikina au aina ya uchawi au aina yoyote ya uovu.Tunaimani kwamba hakuna chochote kilicho na nguvu zaidi kuliko jina la YAHUSHUA, damu ya YAHUSHUA, Neno la YAHUVEH na YAHUSHUA. Tunaamini kwamba mateso ya mwenye haki ni mengi, lakini Mungu wetu atatuokoa kutoka hayo yote.

Tunaamini…
Zaidi kuliko hayo yaliyotajwa hapa, Bibilia ina kila kitu tunachoamini. Kama unataka kujua ni nini tunachoamini, soma Bibilia, Torati na utaona maelezo kamili ya imani yetu. Sisi tunaofanya kazi katika huduma huu tunaomba kwamba tutakuwa wa baraka kwako kwa njia fulani, na kwamba kazi yetu haitakuwa wa bure, lakini siku moja tutaonana nawe uso kwa uso katika Mbinguni.

Yale YAHUVEH na YAHUSHUA walifundisha, tunaamini.

Tunaamini…
Tutakutana nanyi wote Mbinguni mnaokubaliana na kuishi kulingana na kauli hii ya imani. Tunatarajia kuonana huko!

MAELEZO YA IMANI
Mtume Elisabeth (Elisheva) Elijah
Mtume Nikomia