UNABII WA 9

YAHUBIRI, YAFUNZE, FANYA WENGINE KUYAAMINI!

Ilipewa kwake Mtume Sherrie Elijah Tarehe Oktoba 16, 1997


* * * * * * *

Mpendwa WANGU, Ninaujua moyo wako na wale wanaokuhukumu kwa uongo hawajui ni nini wanachozungumzia. MIMI Ndiye hakimu na baraza la waamuzi lako, na sio wale wanaoandamana kotini bila ruhusa YANGU. Songa kando na usiulize kwa nini, kwa kuwa wasipokutetea sasa kwa vitu vidogo, hawatakutetea baadaye kwa mambo makubwa.

Wewe ni Mpendwa WANGU, na wale wanaoandamana kotini dhidi yako bila ushahidi wowote wataona kuwa MIMI sijafurahia. Nilikuleta kwa mtandao huu kukupa moyo na kuubembeleza moyo wako uliouvurugwa. Kwa kuwa MIMI na wewe tunajua uchungu unaohisi. Ingawa, kukataliwa huu sio wako, lakini wanakataa sehemu YANGU MIMI.

Una ucheshi wako kwa kuwa MIMI Nimekupa ucheshi huo, Nilikuita na kukukadiri jinsi ulivyo. Umepewa karama ya kicheko, kusaidia kupunguza mizigo yako na ya wengine pia. Kicheko hufanya mazuri kama dawa nzuri. Lakini hata kicheko na ucheshi zina usawa. MIMI simo katika harakati za makanisa ambamo pepo za kishenzi hujionyesha na huwafanya wajinga Watu WANGU.

Jihadhari popote ambapo chochote kinaendelea, maonyesho yoyote ambayo hamwezi kuona YAHUSHUA akijihusisha nayo. Je, MUNGU wenu anabweka kama mbwa, kulia kama paka na kunguruma kama simba? Nakejeli Neno LANGU? Je, RUACH ha KODESH anaweza kumwaibisha yeyote na kuwafanya watu wajisahau hadi wakawa wasumbufu? Maonyesho haya ya kishetani na mabaya zaidi yanaruhusiwa kuendelea na hawawezi hata kutenganisha harakati halisi za RUACH ha KODESH (Roho Mtakatifu) WANGU, na harakati bandia za mpinga-kristo. Wale wanaosimama nyuma ya mimbari na hujifikiria wenye busara wanatenda ujinga. Wanajifungua wao wenyewe na kusanyiko kwa maonyesho ya kishetani, umilikaji na ukandamizaji.

Ukombozi lazima ufanywe na usafishaji wa Hekalu ZANGU kutoka kwa wale walioitwa viongozi wa kiroho wa leo walioheshimiwa zaidi. Kwa sababu ya ujinga huu sasa Ninakusanya vikosi kote duniani. MIMI huwa kamwe sifungi mlango bila kuufungua mwingine. Usifikirie kuwa huu ndio mwisho kwa kuwa ni mwanzo tu wa kazi kubwa Nitakayokutumia. Usimbadilikie mtu yeyote ila tu Mwenyezi MUNGU YAHUVEH unayemtumikia. Hauwezi kufurahisha kila mtu, kila wakati, kwa hivyo acha kujaribu. Katika moyo wako unajua nini ni sawa, endelea kuyafanya.

Sikiza sauti YANGU, zungumza Maneno YANGU. MIMI sikuhukumu wala kukulaani, lakini wale waliokushtaki kwa uongo watahukumiwa. Wasamehee, kwa kuwa walitumiwa na adui wa nafsi yako na hawakujua. Mvinyo mpya na mvinyo wa kale hauwezi na kamwe hazitachanganyika. Mvinyo mpya Niliokujaza nao hadi kufurika utatoboa kontena ukijaribu kuchanganya wa kale na mpya. Mvinyo wa kale hautaki sehemu yoyote ya mvinyo mpya, usihuzunike kwa yale yote unayofikiria kwamba umepoteza, kwa kuwa haujapoteza chochote ambacho sitaweza kurudisha tena zaidi, kilichofinywa chini na kutingishwa pamoja na kufurika. Utabarikiwa.

Lazima uachilie upako wa kale ili kufungua njia kwa upako mpya. Uweke masikio na macho yako wazi na zungumza yote Ninayokuambia useme, ingawa utahukumiwa vikali unajua sauti YANGU, na unayo ujasiri wa Yohana Mbatizaji kuzungumza Maneno YANGU. Unapofikiria kuwa unashuka chini KWANGU MIMI, kwa kweli umepanda juu na mbele. Usihuzunike kwa ajili yako, lakini huzunika kwa wale Nitakaowaadhibu kwa kumfanya mdogo WANGU awe na huzuni. Huzunika kwa wale waliokushtaki kwa uongo.

Ninakupenda Mpendwa WANGU na ni MIMI tu Nijuaye moyo wako. Unanionea shauku MIMI kama vile kongoni aioneavyo shauku maji. Unapohisi mateso kwa JINA LANGU kwa kweli umebarikiwa. Mtumishi hayupo juu ya bwana wake, Nilihisi mateso sanasana kutoka kwa wale wanaojiita wanadini, nawe pia wafahamu haya. Ninajua nyoyo zao kama Ninavyojua wanaokuhukumu kwa uongo, weka mikono yako mbali na ghadhabu, na Niache MIMI Nilipishe kisasi. Kwa kuwa wasipotubu mbele YANGU, basi wataona kisasi ni YANGU Ndivyo Asemavyo YAHUVEH na kwa kweli Nitalipisha. Usinihukumu MIMI katika njia ambayo wengine wanaodai kuniwakilisha MIMI hukuhukumu.

Wewe ni Mpendwa WANGU na Shujaa WANGU na Nimekuita na kukukadiri na hakuna mtu yeyote anayeweza kuchukua haya kutoka kwako. Njia ya Nabii imejawa na majaribio na dhiki na kutoelewana wa huzuni. Ni wachache tu wanaotaka kusikia ni nini Mwenyezi MUNGU YAHUVEH anachosema. Wanataka kuamini kuwa MIMI ni upendo na huruma pekee, na kusahau MIMI NIKO ni MIMI NIKO na MIMI pia NI MUNGU wa usawa katika vitu vyote. Hiyo humaanisha kuwa pamoja na upendo na huruma, MIMI ni sawa na ghadhabu, na hukumu na ndio chuki, wengi sana husahau kuwa Nina ghadhabu na chuki kwa maadui WANGU.

Je, si Neno LANGU husema, “Yakobo Nimempenda, Esau Nimemchukia?” Je, si Neno LANGU husema, “Baraka kwa wale wanaotii. Laana kwa wale wasiotii?” Lazima uhubiri MIMI ni nani kwa ukamilifu. Sio tu sehemu ya YAHUVEH isiyowakera wengine, lakini pia sehemu ya YAHUVEH inayowakera wengi. DHAMBI NI DHAMBI na sijatikisika au kubadilika, wala sitawahi. Angalia Kitabu cha Mafunuo ya Yohana Sura ya 19 na 20. Ni wachache sana wanaofahamu kuwa MIMI Nilikuwa yule Mwana-kondoo aliyechinjwa, lakini mara moja tu. Nilikuwa mwathirika mara moja tu. Kwa ajili yenu, Nikawa mwathirika.

Lakini sasa MIMI sio huyo Mwana-kondoo mnyenyekevu, mpole, tena. Nitakapokuja tena kuwaangamiza wale wanaonipinga MIMI na Utakatifu utaona kuwa MIMI NI Mwenyezi hata katika vita. Watoto WANGU hawafai kuogopa, lakini Maadui WANGU watatetemeka, na wao hutetemeka kwa kuwa wanajua kuwa MIMI ni MUNGU atakayewalipisha kisasi maadui WANGU. Mimi Ndiye Alpha na Omega, mwanzo na mwisho. Nimeishikilia hasira ZANGU, Nikiijenga kwa siku iyo hiyo. Hamna yeyote atakayesimama njiani MWANGU.

Yahubiri, yafunze, ili wengine watayaamini. MIMI ni MUNGU ambaye haleti uokovu tu, lakini laana kwa wale wanaochagua kuipinga na kukataa Damu YANGU ya Kuokoa na JINA la kuokoa. Hakuna wokovu wowote ila tu kupitia Damu iliyomwagwa pale Kalvari na kupitia JINA la YAHUSHUA ha MASHIACH. Ninawajua Watoto WANGU, nao wananijua MIMI, na Ninajua wote ambao ni maadui WANGU. Wanapokushika, wananishika MIMI. Kama bila kujua wamewakera enyi Watoto WANGU, basi Nitawasamehe kwa kuwa adui yuatafuta kudanganya na kuchanganya. Lakini kama makusudi wanapanga kuwaangamiza, waambie wajihadhari.

Kwa kuwa ni ghadhabu YANGU watahisi ikipumua shingoni mwao. Ni katika kutubu tu ndio watapata fadhili ZANGU tena. MIMI huwaadhibu wale Niwapendao. MIMI huwaangamiza wale Ninaowachukia. Yote ambayo si Takatifu sio ya KWANGU. Haijalishi ni nani anayesimama nyuma ya mimbari na kusema, “Mungu ni upendo ataelewa.” DHAMBI ni DHAMBI! MIMI ni MUNGU asiyebadilika, binadamu hubadilika, MIMI, ‘MIMI NIKO’ mkuu sibadiliki. Yahubiri; yafunze, ili wengine watayaamini. Wale wanaojua sauti YANGU watatambua kuwa Nimezungumza, wengine watabaki viziwi. Kwa maadui WANGU ni jambo la kuogopa sana kujipata katika mikono ya MUNGU aliye hai, YAHUVEH na YAHUSHUA. Wakati mwingine ndio, lazima Niwapige viboko, lakini mikono YANGU pia huwafunika, huwaongoza na kuwalinda. Mikono YANGU kwa Watoto WANGU, wanaojaribu na kunitii MIMI, hawana chochote cha kuogopa, wale waliooshwa katika Damu YANGU ya kuokoa.

Lakini wale wanaonichukia MIMI, na kuchukia Ninachosimamia, wanayo kila sababu ya kutetemeka na itakuwa vivyo hivyo. Tubuni, Ufalme wa Mbinguni waja. Nimewapa tuzo la Wokovu, sasa ni chaguo lako kama utachagua wokovu au laana. Chagueni siku ii hii ni MUNGU yupi mtakayemtumikia. Yahubiri; Yafunze, ili wengine watayaamini.

* * * * * * *


Ilipewa kwake Mtoto huyu, Shujaa, Bibi Arusi wa YAHUSHUA ha MASHIACH Tarehe 10/16/1997
Nabii Sherrie Elijah