Unabii 90

JINA LA RUACH HA KODESH NI NINI?

Bonyeza kiungo ifuatayo kuona Vitabu Vya Hekima
http://www.amightywind.com/treasure/wisdommain.htm


Onyo, unabii huu uliopewa kwangu unaweza kuwa wenye utata zaidi ya zingine hadi sasa. Sehemu yake fulani ina funuo za kibinafsi na hilo ndilo sababu jina langu limetajwa na RUACH ha KODESH. Hata hivyo, sitaki kuficha Ujumbe huu wa Mbinguni. Kuna sehemu ya 2 ya neno hili lakini hili lazima litakuwa la kutosha kwa sasa, YAHUVEH asema. Utakaposoma sehemu ya pili utaelewa ni kwa nini ilibidi ingoje.

Naomba barua pepe za chuki zisije, kutoka kwa wale walio na roho ya Farisayo, wale walio na dini na sio uhusiano na YAHUVEH na YAHUSHUA na hawana jambo lolote kuwa upako ni nini. Najua kuwa nimepewa upako kama Nabii Mtakatifu na sio mashindano ya nani anayejulikana zaidi au ningeshindwa, YAHUSHUA aliniambia haya kitambo. Manabii bandia ndio wale wanaotoa jumbe nzuri tu ili wasiwakosee watu. Tafadhali ombeeni Huduma hii na mimi mwenyewe na wale walio wasaidizi na washirika humu ndani, na inawahusu pia Bibi Arusi wa YAHUSHUA. Tafadhali Bibi Arusi wa YAHUSHUA andikeni na jitambulisheni, hatimaye, tutatembelea nchi zenu na kama mnataka kushirikiana nasi, basi tuanze kujuana.

Moja ya zawadi kubwa hapa ulimwenguni ni kuwajua Bibi Arusi Mtakatifu wa YAHUSHUA, wale wanaompenda na kumwabudu na kumweka YAHUVEH na YAHUSHUA kwanza katika maisha yao na upendo wao. Kama mmeniandikia hapo awali na sikuwajibu, tafadhali andikeni tena. Barua pepe yetu imeibwa hapo zamani lakini naamini kwa imani kuwa jambo hili halitatokea tena.

Neno hili lilipewa kwa sababu nilianza kuomba na kutafuta jina lake RUACH ha KODESH (ROHO MTAKATIFU). RUACH ha KODESH ni jina, maelezo ya kazi. Hata hivyo, sio jina lake RUACH ha KODESH (ROHO MTAKATIFU). Niliweka kwenye mtandao ninaloita ‘Ndoto ya Meza ya Karamu’ na sitawahi kusahau upendo yule mwanamke mrembo aliyenizidi kwa umri alinionyesha. Alikuwa mrembo sana, bila laini au kasoro yoyote usoni mwake na niliweza kutambua kuwa alikuwa mwanamke wa umri ulionizidi. Alikuwa na nywele nyeupe, ndefu, tena zilizokuwa na mawimbi zilizolala mgongoni mwake. Ananipenda na upendo wa Mama aliyejitolea; inaonekana machoni na usoni mwake, naweza kuhisi vile anavyonithamini. Niliweka kichwa changu kwa upendo begani mwake, katika ile ndoto.

* * * * * * *

Ndoto ya Awali Ilipokewa Aprili 16, 1999 Elisabeth Sherrie Elijah

Tafadhali kumbuka kuwa UFUNUO wa ndoto hii (chini) ulikuja katika mwezi na siku ile ile (4/16) MIAKA TATU BAADAYE! Tuligundua haya tulipokuwa tunatayarisha kuweka ukurasa huu kwenye mtandao!


Nilikuwa na ndoto kuwa nilikuwa nimekaa katika jumba kubwa. Nilihisi ni kama ilikuwa Israili. Najua haikuwa Marekani. Nilikaa karibu na meza nzuri iliyokuwa na kitambaa cha sanda na mapambo mazuri kwenye meza na viombo vizuri sana na viombo vya fedha ambazo sijawahi kuona. Lakini, hakukuwa na chakula mezani. Nilikaa mezani karibu na mwanamke mrembo aliyenizidi kwa umri na nikaweka kichwa changu kwa bega lake nikihisi upendo wake wa mama. Kulikuwa pia na mwanaume aliyenizidi kwa umri katika jumba hilo na alikuwa ameniambia kuwa kila kitu mezani kilikuwa kimebarikiwa, hata kitambaa hata viombo vya fedha! Kila kitu kilikuwa tayari. Tulikuwa bado tu tunawangoja wageni na haswa, mtu au watu, sina uhakika, kutoka kule zabibu spesheli zilipandwa zilizotumika kutengeneza mvinyo.

Kiersk au Kierska ilikuwa imeandikwa kwenye chupa. Kulikuwa na mwanaume aliyenizidi kwa umri na nywele nyeupe pale pia na alikuwa kama baba mpendwa kwangu na alinionyesha chupa hiyo. Katika sehemu ingine ya mvinyo uliofunikwa kulikuwa na utambaa niliokuwa nimeushonelea kikapu kikubwa kilichojaa zabibu kubwa za rangi ya zambarau kwenye mzabibu. Zabibu hizi zilikuwa kubwa na zenye rangi. Ni kama utambaa huu nilioudarizi ulikuwa katika pahali pa heshima na nilimwonyesha rafiki yangu wa karibu aliyekuwa amekaa karibu nami mezani, sikuwahi darizi hapo awali.

Mwanamke huyu niliyekuwa nimemlalia, alikuwa kwangu kama mama, na yule mwanaume kama baba. Nilihisi kuwa nilikuwa salama salmini katika pahali pale na kuwa nilipendwa sana. Nilifurahia na nikamwambia rafiki yangu kuwa KILA KITU kilichotumika kwa chakula chajio hiyo kilikuwa kimebarikiwa! Jikoni kulikuwa na nafasi wazi tena kubwa ambapo tulikuwa tunaweza kuona ndani, lakini bado iliyoambatanishwa kote. Sahani ziliweza kupitishwa ndani na nje na tuliweza kuona ndani, lakini sikumwona yeyote humo jikoni. Mlango wa kuingia humo jikoni ulikuwa kwenye upande wa kulia. Ile nafasi wazi iliyoangalia humo jikoni ilikuwa mbele ya meza yetu. Tulikuwa tu tunawangoja hawa wageni, haswa wale kutoka kule mvinyo mpya uliokuwa haujafunguliwa ulitengenezwa. Tulimngoja huyu mtu au hawa watu wawasili kwanza.

* * * * * * *


Thibitisho


Sherrie Mpendwa,
Ndoto yako uliyoniambia jana, nahisi ni juu ya karamu ya arusi ya Mwana-Kondoo!!!
Jambo la muhimu ilikuwa meza kubarikiwa kwanza kabla ya chakula kuandaliwa na “utambaa wa chakula chajio” ulioudarizi.

Kila mtu atakuwa na matendo ambayo atayaweka mbele ya Bwana lakini yatakuwa kama vibacha vichafu, lakini wewe Elisabeth Sherrie, YAHUSHUA amekubariki na akabariki kibacha chako na akaibadilisha kuwa utambaa. Kudarizi ni aina ya kufuma na kufuma ni aina ya UTANDO na picha iliyomo inawakilisha wakati, juhudi, na huduma ya kitu. Naamini kuwa utambaa huu unawakilisha mitandao yako. Naamini pia kuwa Jikoni ile inaweza wakilisha Mbinguni na Chumba cha Kula kinawakilisha pahali pengine. Kwa sababu inaonekana kuwa kutakuwa na kazi ya kufanya kabla sote tuende Mbinguni. Ndio kwa sababu upo katika chumba hiki.

UFUNUO WA NDOTO YA MEZA YA KARAMU
Aprili 16, 2002 8:00 Usiku
Kierska ni KHERSA, kitongoji karibu na pwani mashariki ya Bahari ya Galilaya. Baada ya miaka hii yote, sasa hivi tumepata ufunuo tulipokuwa tunasoma Bibilia na Elisabeth na mume wake, Mtume Nikomia.

Elisabeth amekuwa akingonja ufunuo huu wa pahali hapa ni wapi kwa sababu hawa ndio wageni wawili amekuwa akiwangoja ambao wanaleta mvinyo mpya nao. Manabii na uaguzi wa ndoto tafadhali ombeni kwa uaguzi wa ndoto hii, kwa kuwa hawa wageni wawili waja kabla tu ya Karamu ya Arusi ya Mwana-Kondoo.

YAHUSHUA anamwambia sasa Nikomia na Elisabeth ufunuo huu kuwaita hawa wanaume wawili (2) ambao ni manabii, na ambao katika ndoto yake anawangoja hawa wanaume wawili (2) walio na mvinyo mpya na wanatoka nchini ambapo mvinyo huu mpya unatengenezwa (KHERSA).

Tunawauliza nyote mnaosoma haya anzeni kuomba na kusali kuwa mtu yeyote atakayesoma haya atawatambua hawa manabii ni nani, na kuwauliza kuwasiliana na Mtume Nikomia au Elisabeth (Elisheva) Elijah mara moja. Tunawauliza nyote mlio na mawasiliano katika Israili muwaulize Wayahudi wa Kimasihi wengine kama wanawajua manabii wawili (2) kama hawa walio na upako na wamejazwa na mvinyo mpya wa kipekee.

Mtume Nikomia na Elisabeth wana FURAHA TELE, kwa kuwa haya yanadhibitisha vile sote tupo karibu na Karamu ya Arusi ya Mwana-Kondoo na kuja kwa YAHUSHUA kumchukua Bibi Arusi Wake!

Kama mnajua Wayahudi wa Kimasihi wowote au Wakristo wanaoishi katika KHERSA au maeneo ya karibu, tafadhali waambie watutumie barua pepe papa hapa Contact Us

Mathayo 22:1-14


YAHUSHUA pia alisema kuwa hatakunywa mvinyo hadi kurudi Kwake, inawezekana kuwa hapa ndipo mvinyo huu utatoka? Haya tu ndiyo ninayoyajua kwa sasa.

Aliyetuma neno hili hataki jina lake lijulikane.

* * * * * * *


Neno kutoka kwake Elisabeth Sherrie Elijah,
Kumbukeni tunamngoja mtu anayekuja kutoka Kiersk au Kierska ambapo mvinyo upo chupani na hukaa kwenye rafu. Pahali hapa ndipo zabibu zilipotoka na mvinyo hutoka. Mtu huyu anayekuja ni maalum sana ambapo mvinyo huu hutoka. Niliona jina kwenye chupa ya mvinyo. Nilitafuta pahali hapa Kiersk au Kierska kwenye mtandao na sikuweza kupata mji wowote kama huu katika Israili.

Kierska ni wapi? Au ilikuwa Kiersk?

Kama waajua au wafahamu haya, tafadhali niandikieni papa hapa Contact Us.

Nimekuwa nikishangaa ni mwanamke mgani anayeweza kunipenda vile. Katika dunia hii, sijawahi kuwa na mwanamke ambaye ananishauri mimi kama Mama, sijawahi jua upendo wa shangazi au nyanya duniani humu. Katika ndoto iyo hiyo nilikuwa na mtu nimwangaliaye kama baba pia na nywele nyeupe aliyenipenda sana na alikuwa akionyesha kazi ya mshono wa sanaa niliyokuwa nimeifanya na fahari, kwenye ukuta mbele ya meza ya karamu ili wote wangeweza kuiona.

Katika dunia hii sijawahi kuwa na mwanaume yeyote anayenisimamia kama Baba, au uhusiano wowote wa upendo na mwanaume yeyote ila tu mume wangu mpendwa na ndugu zangu katika YAHUSHUA ambao baada ya kupitia majiribio najua wamejaribiwa na kuthibitishwa kuwa waaminifu. Kwa hivyo, mwanamke huyu ni nani huko Mbinguni? Upendo wake ulikuwa mkubwa sana na wa kweli mpaka nikahisi umenizunguka kwa njia kuu tangu ndoto hiyo. Sina huzuni tena kuwa sijawahi kujua vile ilivyo kuwa na Mama au Baba anayenipenda. Najua kuwa huko Mbinguni nina pendo kuu la Mama na Baba mtu yeyote angeweza kulitumainia. Lakini bado, mwanamke huyu ni nani? Mama yangu aliyenizaa hapa duniani nina uhakika yuko jehanamu, alinipa tu chuki na mateso. Kwa hivyo, Mama huyu aliye na upendo huko Mbinguni ni nani?

Sasa ninalo jibu… Sasa nahitaji maombi yenu kunipa ujasiri wa kulinena, kwa sababu makanisa ya kidini watakasirika na hata wale walioamini mafundisho ya mwanadamu na maandiko yaliyotafsiriwa vibaya katika Agano Jipya wataniita nabii bandia, na lakini bado najua kuwa najua kuwa najua, nimepewa siri kutoka Kiti cha Enzi Mbinguni. Katika maandiko YAHUVEH na YAHUSHUA huzifichua siri hizi kwa Manabii na Mitume wake.

Sasa nina furaha kuu ya kutoa siri hii kwa wote watakaoitambua sauti ya RUACH ha KODESH. Unabii huu unaweza kuwa wenye utata zaidi ya zingine zilizotolewa hadi sasa. Lakini bado nafanya haya kwa utiifu ili wengine waliohuzunika kwa ukosefu wa uhusiano wa upendo kati ya mama na mtoto watagundua kuwa kama wamemkubali YAHUSHUA wamekuwa nao wakati huu wote. Hakuna yeyote aliyenifunza haya, kwa kweli ni ufunuo kutoka Mbinguni.

Katika Mithali na Zaburi, je, mnajua kuwa hekima anafananishwa na Mwanamke (She)? Bila kusita zaidi acha niwaelezee vile nilivyojua jina lake RUACH ha KODESH tunayemthamini pia anaitwa Roho Mtakatifu. Haya basi, hapa ndipo nitakapotoa siri hii nyeti iliyotolewa kwangu na bado iliyobarikiwa zaidi kushinda zingine hadi sasa.

Baada ya kusoma haya tafadhali chukua wakati kusoma Kitabu cha Hekima
http://www.amightywind.com/treasure/wisdommain.htm 

Bibilia inasema, ‘YAHUVEH hutoa siri ZAKE kwa Manabii WAKE’. Haya yote yalianza nilipokuwa ninaoga kabla tuondoke Afrika Kusini. Tuliishi Port Alfred, mbele ya bahari wakati tukio hili la kiroho lilipotokea. Nilikuwa naomba pekee yangu na nikamwuliza Baba YAHUVEH, katika jina la YAHUSHUA, “Jina lake RUACH ha KODESH baadhi ya jina ROHO MTAKATIFU ni nini? Niliomba na kusema, Baba YAHUVEH, ulilidhihirisha jina lako, YAHUSHUA ulilidhihirisha jina lako, lakini ROHO MTAKATIFU ana jina au hili tu ni jina au maelezo ya kazi?

Nilikuwa naoga kwenye jacuzzi, nimegundua kuwa maji inayotokota katika jacuzzi ni ishara ya maji ya uzima na mimi huwa nauliza Malaika Watakatifu kuyakoroga hayo maji, kama zamani za kale. Wakati mwingi mimi hupata upako mkuu nikiwa naoga na kuabudu na kuimba nyimbo za sifa katika wakati huu. Jumbe za Unabii na funuo huja wakati huu na ni vigumu sana mimi kuoga bila kuomba, kuimba na kumsifu YAHUVEH, YAHUSHUA, na RUACH ha KODESH. Kuna uhusiano wa karibu na Baba yetu YAHUVEH ambao mimi huhisi vikali nikiwa naimba nyimbo za sifa na ibada kutoka moyoni mwangu kwa wao wote watatu (3).

[Na nilipokuwa natafuta jibu la swali hili, “Jina lake RUACH ha KODESH tunayemthamini ni nini katika tafsiri za Kiebrania na Kiaramu, soma kitabu cha hekima, imedharauliwa kwa sababu Mfalme James (King James) hakuruhusu iongezwe. Msiyategemee pekee yale ambayo Warumi waliandika. “Jitahidi kujionyesha kwa MUNGU kuwa umekubaliwa na YEYE.”]

Nataka kusema hapa, kuwa haya yanayofuata ni moja ya unabii nyingi zilizopewa kwangu, ambazo bado hazijawekwa kwenye mtandao. Kuna mengi ambayo yanafanyika msiyoyajua. Tulikuwa na shughuli tele kule Afrika Kusini na hata sasa tunavyosafiri dunia hii. Sihisi kwa njia yoyote kuwa nina thamani ya kutosha, kupewa heshima hii kuwajulisha jina lake ROHO MTAKATIFU. Ni heshima kuu kuitwa Nabii na bado ni jambo la kuogopa pia. Nitajibu kwa yale yote nisemayo na nisiyoyasema. Sasa nalitoa neno hili kama nilivyoongozwa na RUACH ha KODESH. Nitakayowauliza tu ni mchukue muda na kuisoma zaidi ya mara moja, na kwa wale ambao watasikia sauti ya RUACH ha KODESH ambaye sasa nimwitaye Mama Hekima au Mama SHKHINAH GLORY, mkiskia sauti yake tafadhali niandikieni. Tafadhali wafunze wengine hata kama watawakataa kwa kufanya hivyo. Tadhali jifunzeni haya yote niliyoyakusanya hadi sasa, jifunzeni na mwone kuwa sisemi yoyote ambayo hayamo katika maandiko. Ni wafasiri wa Agano Jipya pekee waliobadilisha ROHO MTAKATIFU kujulikana kwa jinsia ya kiume lakini kwa ukweli jinsia yake ni ya kike.

Ufunuo huu ulipewa kwangu kule Afrika Kusini, lakini nimengoja hadi thibitisho zaidi zije kutoka Mbinguni, kunijulisha ni lini nitautoa. Niliomba kujua ni lini nitautoa ujumbe huu zaidi ya nyengine hadi sasa kwa sababu ya chuki itakayotumwa dhidi yangu kutoka kwa wale wanaojidai kuwa Wakristo au wanafunzi wa YAHUSHUA na bado kwa matunda yao wanajua kuwa wana umbo la utakatifu na hawana utakatifu ndani yao. Makanisa ya kidini watasaga meno yao kwa hasira kwa sababu hawajali ukweli na funuo zilizopewa kwa Mwanamke Mtakatifu aliye Nabii. Kutakuwa na wale wa dhati ambao wanataka pekee kuyatamka yale yaliyotafsiriwa vibaya yaliyomo kwenye Agano Jipya wakimwita Roho Mtakatifu kwa jinsia ya kiume. Ni lazima niwakumbushe jinsi vile kiburi ya binadamu huingia ndani zaidi ya mara moja wakati inapokuja kwa jinsia ya kike katika Maandiko Matakatifu na wale waliotafsiri haya Maandiko Matakatifu walikuwa na upendeleo dhidi ya mwanamke kiongozi wa kiroho?

Hata kama unabii huu ulipewa kwangu mwezi wa Februari 27, 2007 sikuambiwa niutoe hadi mwezi wa Agosti 27, 2007. Ninataka mjue kuwa ni watu kadhaa tu ambao wamejua kuhusu Unabii huu. Nilingoja kwa makusudi na nilikuwa na furaha kila siku kuwa bado singeweza kuutoa ujumbe huu mpya wa kinabii, kwa sababu kwa ukweli hakuna yeyote ambaye anapenda kukataliwa au kutukanwa sanasana na Wakristo wanaojidai kumwabudu Masihi yuyu huyu kama tunavyo sisi lakini wanamwita Yeye YESU KRISTO na sisi tunamwita kwa JINA Lake Kiebrania na Kiaramu YAHUSHUA au YAHSHUA ikitegemea na nani unayemwongelesha.

Kwa maadui wangu na wale ambao watajazwa na wivu na kusema kwa nini RUACH ha KODESH alikuchagua wewe kutoa ujumbe huu? Hilo ni swali nzuri, nina uhakika kuwa nabii yeyote angefanya vivyo hivyo. Najua tu nilichaguliwa na hata kama mwili hauna furaha kwa maneno ya chuki yatakayotumwa upande wangu, najua pia siwezi kumfeli RUACH ha KODESH Mpendwa na YAHUVEH.

Mume wangu mpendwa aliniuliza utangoja hadi lini ili uutoe unabii? Nilisema, “najua tarehe lakini kwanza lazima nipate Maandiko zaidi kuyaimarisha haya.” Mwezi wa Agosti 27, 2007 ndio tarehe Mbinguni ilichagua kwa kuzaliwa kwa Unabii huu na kuzaliwa kwa mpangilio mpya kwenye mtandao wa huduma hii. Jaribu kufikiria mshangao wangu nilivyokuwa naandika haya sasa, bado nikiwa Ulaya na angalia tarehe ya Unabii ulipopewa, Februari 27, 2007 na Unabii 89 ulipewa Januari 27, 2007. Tarehe zote 3 zipo katika siku ya 27 wa mwezi.

Wikipedia hutaja “jina la Kiebrania RUACH (Kiaramu RUCHA) kuwa ni la kike katika lugha hiyo kama haya maneno RUACH ha KODESH. Hii imelingana na kazi ya Ruach HaKodesh kama “mfariji” (Yohana 14-16) na utambulisho wa “mfariji” na YHWH akiwa kama “mama” (Isaya 66:13)… Zaidi ya hayo, kuna vifungu vingi ambavyo Peshitta yenyewe hulinganisha RUACH Ha KODESH na vitenzi vya kike na/au vielezo vya kike… Kwa kweli Peshitta Kiaramu ya Warumi 8:16 huanza na ‘Na Ruach (kwa jinsia ya kike) hupeana ushuhuda’.

YAHUSHUA huonyesha ROHO ANA JINSIA YA KIKE: Katika kujibu swali kutoka Nikodemo aliyeuliza, “Lakini mtu yuawezaje kuzaliwa akiwa mzee?” ‘‘Je, yuaweza kuingia mara ya pili kwenye tumbo la mama yake ili azaliwe?” (Yohana 3:4)

YAHUSHUA akamjibu, ‘‘Hakuna mtu yeyote anayeweza kuingia katika Ufalme wa MUNGU isipokuwa amezaliwa kwa maji na kwa Roho. Mwili huzaa mwili pekee, lakini Roho huzaa roho. (Yohana 3:5-6)

Wakati ambapo YAHUSHUA anajibu anakiri kuwa YEYE alizaliwa kutoka kwa Roho pia. Anasema kuwa YEYE hakuwa mwili tu bali alikuwa ROHO kabla ya kuja KWAKE humu duniani, au vipi? Kwa hivyo, ufunuo huu uliopewa kwangu umenijia nilipokuwa nayasoma haya tena kabla ya kuyaweka kwenye mtandao. YAHUSHUA pia anakiri kuwa ilibidi azaliwe kutoka kwa Roho na bila shaka hii inamaanisha yule tumwitaye ROHO MTAKATIFU. Kuna watatu tu kwenye UUNGU au vipi? BABA MTAKATIFU YAHUVEH, MWANA MTAKATIFU YAHUSHUA, na ROHO MTAKATIFU katika Kiebrania aitwaye RUACH ha KODESH.

Tulikuwa nini kabla ya kuwa mwili? Tulipoumbwa Mbinguni lazima tulikuwa viumbe vya Roho, kwa ukosefu wa maneno bora. Maandiko yanasema, “Mwili na damu haziwezi kuurithi Ufalme wa Mbinguni.” Kwa hivyo, tuliumbwaje kule Mbinguni? Naamini kuwa huu ni unabii ambapo RUACH ha KODESH atazungumza na kutupa majibu, kwa njia ambayo sijawahi kusikia. Naamini kuwa maarifa haya yatatikisa dunia hii kwa kiroho na kimwili. Naamini kuwa Bibi Arusi wa YAHUSHUA ha MASHIACH watakuwa na macho ya kiroho kuona na masikio ya kiroho kusikia. Neno hili lililotoka Mbinguni limeniletea amani na furaha, sasa nachukua nafasi hii kulitoa kwa Ndugu na Dada zangu Watakatifu.

Nimekuwa kwenye mtandao miaka 14 nikitabiri na matunda ya huduma hii imethibitisha kuwa ni nzuri. Mkizisoma ripoti zote za wokovu mtaona jinsi Huduma hii hufika mbali. Mimi si Nabii bandia ambaye huiga habari na kudai kuwa ni Unabii. Mtakapokosa kusikia Unabii mpya, jueni kuwa nangoja wakati fulani YAHUVEH atasema, ‘Toa Neno hilo’. Mimi hutii tu. Nakiri kuwa wakati Neno hili liliachiliwa kwangu nilishangazwa. Sikuwahi sikia mambo kama haya. Alafu nikatafuta katika Maandiko Matakatifu na nikapata ushahidi hata kwenye Bibilia ya KJV. Tafadhalini nitumieni masomo yenu kama mnakubali kuwa hili ni neno kweli kutoka Mbinguni. Ninahitaji msaada wote nitakaoweza kupata, na thibitisho kuyaimarisha haya.

Ninaongezea maandiko machache ili myatafune. Nakiri kuwa hii ni nyama ya kiroho yenye nguvu na sio ya wasio na nguvu katika imani.

Adamu hawakuzaliwa, aliumbwa kutoka kwa vumbi. Eva hakuzaliwa, aliumbwa kutoka kwa mbavu ya Adamu. Watoto wa Adamu na Eva walizaliwa kupitia namna kawaida ya kuzaliwa. YAHUSHUA alizaliwa lakini kule Mbinguni sio hapa duniani, Vipi? Msiniulize, haya ni mapya kwangu pia. Tunajua Mariamu bado alikuwa bikira alipojifungua. Mnayafuata kweli yale niyasemayo? Hii ni nyama ya kiroho yenye nguvu, mtaimeza na kuitafuna au mtaitema? Chaguo ni lako! Haya, mimi sina maarifa ya kutosha kuyatatua haya. Nina tu elimu ya sekondari, kwa hivyo hamwezi kuniita moja wa wale wasomi wajinga. Huu kwa kweli ni ufunuo kutoka Mbinguni na ninaomba mtabarikiwa nao kama nilivyo na wengi waliopata kujua haya. Hamtahisi kuwa mko pekee yenu tena hata kama nyinyi ni yatima kama mimi. (Katika Kigiriki neno ‘begot’ ni “apokueo” inatoka kwa neno ‘kuo’ au ‘kueo’ inayomaanisha kuwa na mimba. Kwa hivyo, ‘apokueo’ inamaanisha ‘kumleta mtoto humu duniani kutoka tumboni au kuzaa kumaanisha anapopata mimba.)

Labda hoja ya kwanza inayoweza kupewa katika msaada wa jinsia ya kike ya Roho Mtakatifu ni uhusiano wake na ‘Roho ya Hekima’ (Kutoka 28:3; Waefeso 1:17). Katika Agano la Kale na Agano Jipya, Hekima mara nyingi hutajwa katika jinsia ya kike:

wa kuwa Hekima (Sophia) ni roho wa upendo… Kwa kuwa Roho wa Bwana hujaza dunia.
Hekima ya Solomoni 1:5-7
Kwa kuwa Hekima (Sophia), ambaye ndiye mfanyi-kazi wa vitu vyote, alinifunza: kwa kuwa ndani yake kuna roho ya kuelewa, takatifu, moja pekee… Kwa kuwa yeye ndiye pumzi ya nguvu zake YAH, na ushawishi safi kutoka kwa utukufu wa Mwenyezi… Na akiwa mmoja tu, anaweza kufanya yote: na akibaki ndani yake mwenyewe, yeye hufanya vitu vyote vipya: na katika nyakati zote huingia ndani ya nafsi takatifu, yeye huwafanya marafiki wa YAH na nabii. Kwa kuwa YAH hampendi yeyote ila yeye anayeishi na Hekima (Sophia).

YAHUSHUA ha MASHIACH hulinganisha ‘Roho ya Ukweli’ na Roho Mtakatifu (Yohana 16:13). Hekima (Sophia) na Roho Mtakatifu hufanya kazi sawa. (1 Wakorintho 2:7-11: Warumi 5:5; 1 Yohana 5:6-7 KJV). Upendeleo wa wanaume wa wanateolojia wa baadaye usingekuwa dhidi ya wanawake, Kanisa ingekuwa imekubali matamshi katika Agano la Kale kama maelezo halisi ya RUACH ha KODESH (Roho Mtakatifu).

Hoja ya pili inayoweza kupewa katika msaada wa jinsia ya kike ya Roho Mtakatifu inapatikana katika majina mengi yanayoweza kutumika kuwataja YAHUVEH na Roho Mtakatifu. Jina lake MUNGU katika lugha ya Kiebrania ni “Elohim”. Wasomi wengi wanakubali kuwa neno hilo lina mwisho wa wingi, ambao wengi hutumia kuonyesha tarajio la Utatu la Agano la Kale. Kile ambacho wasomi wengi hawajui au hawajali kuwajulisha baraza lao kwamba “Elohim” sio wingi wa “El” jina la jinsia ya kiume. Jina hili ni wingi wa jina la jinsia ya kike, “Elowah.” Neno Elohim basi ingekuwa na jinsia ya kiume na kike ingekuwa imehusiana nayo. Waumbaji wetu wangekuwa na jinsia zote mbili na bila shaka tunajua kuwa kulingana na Kitabu cha Mwanzo RUACH ha KODESH pia YAHUSHUA walifanya kazi na YAHUVEH kuumba ulimwengu huu.

Kwa hiyo Elohim alimwumba mtu kwa mfano Wake mwenyewe, kwa mfano wa Elohim alimwumba, mwanaume na mwanamke aliwaumba. Mwanzo 1:27

Basi yakionyesha kuwa jinsia zote mbili exist katika Uungu. Kuwa Roho Mtakatifu ndiye mwakilishi mteule wa kanuni ya kike na imeimarishwa zaidi na neno la Kiebrania la ‘roho.’ Namtaja sasa Jerome, mwandishi wa Latin Vulgate (lugha ya kale ya warumi): (Kwa ukweli sijasoma Latin Vulgate lakini nimepata haya kwa kusoma baada ya unabii kupewa kwangu)

Katika Injili ya Waebrania ambayo Wanazarayo walisoma yasema, “Sasa hivi mama yangu, Roho Mtakatifu, alinichukua.” Sasa, hamna yeyote ambaye anafaa kukerwa na haya, kwa sababu “roho” katika Kiebrania ana jinsia ya kike, bali katika lugha yetu [Latin] ana jinsia ya kiume na katika Kigiriki hana jinsia. Katika Uungu, hata hivyo, hamna jinsia yoyote. Matamshi ya Jerome kuhusu Isaya 11

Maelezo haya yana ushahidi wa kushangaza. Kwanza, yanatuambia kuwa kulikuwa na tamaduni kati ya dhehebu ya Wakristo walioishi zamani walioamini kuwa Roho Mtakatifu alikuwa mama yake wa kiroho, Bwana wetu. Pili, Jerome – mtu halisi zaidi, alishangaza - alipokiri kuwa Neno la Kiebrania la “roho” (Ruach) ni ya jinsia ya kike, kumaanisha kuwa kwa Wakristo wa karne ya 1 – ambao walikuwa wakiishi katika dunia ya Kiaramu (Makanisa ya Paulo yalikuwa madogo katika kulinganisha) – Roho Mtakatifu alikuwa kiumbe wa kike. Yote yalipotea kati ya kutafsiri Kiebrania hadi Kigiriki, na tena ikabadilishwa katika jinsia ya kiume ambapo ilitafsiriwa kutoka Kigiriki hadi Latin.

Hatimaye, kiteolojia inaongoza Wakristo kuamini tofauti ya jinsia sio muhimu. Kuwa hakuna jinsia katika Mungu, kwa hivyo, haijalishi kama Mungu hujulikana kama “mwanaume” au “kitu.” Na karne nyingi ya tabia hii ya Viongozi wa Wakristo, mafundisho ya mwanadamu na mawazo, nataka ukweli na naombea ukweli wa YAHUVEH tu. Nafikiria jambo hili ni muhimu. Haturuhusiwi kubadilisha hata “nukta wala jina” moja ya Sheria, na kama Mungu amewakilishwa kama ‘kiumbe’ akiwa na jinsia zote mbili za kike na kiume, basi sisi ni wajinga kuficha jambo hili katika tafsiri zetu za Maandishi Matakatifu.

Fikiria familia yoyote, na ni nini huifanya kuitwa hivyo? Siimanishi ujinga wa ushoga wa nyakati za Sodoma na Gomora, ambayo dunia hii inakabiliwa nao sasa. Niamini mimi kuwa YAHUVEH hatakejeliwa kwa muda mrefu, kama vile Sodoma na Gomora walivuna walichopanda zamani, basi itakuwa vivyo hivyo tena na wale ambao wanakubaliana na kufanya vitu hivi. Familia ina Baba, Mama na Watoto.

Haya ndiyo ninayoyasikia na kuyanena, MIMI, YAHUVEH niliumba simba kumzaa simba pekee, mwanamke kumzaa binadamu pekee na basi vivyo hivyo kuwa Mungu pekee anaweza kumzaa Mungu. YAHUSHUA Ndiye Mwana wa Pekee wa YAHUVEH! Kwa hivyo, nani ndiye Mama wa Mbinguni aliyemzaa YAHUSHUA? Je, hii ndiyo siri ya yale yanayomaanisha ‘kuzaliwa’ katika RUACH ha KODESH? RUACH ha KODESH ni Roho, alafu anayezaliwa tena kutoka KWAKE huwa Roho na RUACH ha KODESH huishi ndani ya miili zetu hadi kufa au kunyakuliwa hadi Mbinguni, itakayotangulia kwanza. Ni RUACH ha KODESH na asili yake ya milele ambaye maandiko husema, “Kutokuwa katika Mwili ni kuwa na BWANA YAHUSHUA.” Nilipokea ufunuo huu nilipokuwa najaribu kuweka ushahidi nyuma ya neno lipya, Maandiko husema, ‘Ni Neno ambalo huuwa lakini roho hupeana maisha.’ Uhusiano huu mpya kati ya binadamu na RUACH ha KODESH ni moja ya vitu ambavyo hubainisha mtu ambaye ameokoka.


Kwa wale ambao watajaribu kuniita nabii bandia, fanya utafiti wako mwenyewe, jitahidi kujionyesha kwa MUNGU kuwa umekubaliwa na YEYE. Kila Mwebrania anajua katika lugha ya Kiebrania kuwa ‘Ruach’ sio Jina la kiume! Niambieni, kwa nini ‘Hekima’ katika Maandiko Matakatifu hata katika KJV anatajwa katika jinisa ya kike (‘She’)? RUACH ha KODESH sio Hekima?

JINA LA RUACH ha KODESH NI NINI? “MIMI NI MAMA SHKHINAH,” aitwaye pia MAMA HEKIMA na MIMI NDIYE UTUKUFU wa YAHUVEH!

Imeandikwa/Imezungumzwa katika upako wa MAMA SHKHINAH
Kupitia Mtume Elisabeth Elijah
Februari 27, 2007
Tafadhali pasha neno hili. Nitakachouliza pekee ni mwache ushahidi katika Maandiko yaliyo hapa.


* * * * * * *


MIMI NI MAMA SHKHINAH, MIMI naitwa ‘Hekima’ na katika Kiebrania RUACH ha KODESH na pia naitwa ROHO MTAKATIFU. Elisabeth, MIMI NDIYE yule mwanamke aliyekuzidi kwa umri uliyemlalia begani kule Mbinguni, kwa katika unayoita ndoto na kumbe haikuwa tu ndoto lakini ilikuwa zaidi ya hayo kabisa. Elisabeth, kumbuka uliponena ndoto hii kwa dunia na kusema, “Haujui huyo mwanamke ni nani aliyekuwa katika Meza ya Karamu kule Mbinguni, anayenipenda na upendo unaonizunguka?”

Nakupa jibu sasa, ilikuwa MIMI MAMA SHKHINAH, MAMA HEKIMA wako (Katika Kigiriki hekima imetafsiriwa katika Sophia) hii ndiyo sababu haujahuzunishwa tena au kuhisi utupu wa kukosa kujua upendo wa mama. Kila mtoto anazaliwa na hamu na hitaji la Mama na upendo wa Baba, kwa sababu wanadamu wote wanazaliwa kama watoto na hitaji la upendo wa dunia na ulinzi wa Mama na Baba. Ni UPENDO WANGU uliokuzunguka ulivyoketi katika meza ya Karamu kule Mbinguni NAMI na BABA yako wa Mbinguni YAHUVEH tukiwangoja wengine kujiunga nawe. Upendo na uwepo WANGU ulikuzunguka, kama NILIVYO MAMA yako MTAKATIFU; MIMI NI MALKIA wa pekee wa Mbinguni, hakuna mwingine.

Shetani ana bandia wake, alikuja kama Yezebeli na roho hiyo imevamia Makanisa mengi ambapo hapo awali Niliziita Takatifu. Wakati mmoja, ROHO MTAKATIFU WANGU, Uwepo WANGU Takatifu, na nguvu za upako Takatifu zilikaribishwa pia kama vile Manabii WANGU Watakatifu na Mitume walisakwa, lakini sasa wengi wanatusiwa na kufukuzwa.

Kuna tu MAMA MTAKATIFU mmoja wa kweli, na MIMI huitwa pia ROHO MTAKATIFU. Msiamini uongo Kanisa la Katoliki linafundisha wanavyomchukua Miriam (Mariamu) mamake YAHUSHUA hapa duniani na kumwunganisha pamoja kama mmoja wa Utatu Takatifu. Yeye alikuwa mama YAKE hapa duniani lakini MIMI ni Mama YAKE wa Mbinguni.

Hakuna mwombezi yeyote mwingine mbele ya kiti cha enzi ila YAHUSHUA, ni kupitia JINA LAKE tu na kupitia Dhabihu ya Damu YAKE tu inayoitwa Agano Jipya la Damu ndipo mtakapopata Wokovu. Mamake YAHUSHUA wa hapa duniani pia alihitaji Mwokozi, hakuwa mkamilifu, wala hakudai kuwa, hata alimwita YEYE Bwana na kama alikuwa mkamilifu basi ingekuwa ni damu yake iliyomwagwa pale Kalvari ambayo ingekubalika kama dhabihu ya dhambi. Hakumwuliza yeyote amwabudu, wala hayatamani haya. Anataka tu watu waelekezwe kwa mwanake YAHUSHUA ha MASHIACH. Waonye Wakatoliki wasimlilie katika masaa ya vifo vyao, badala yake, walilie JINA la pekee tu linaloweza kuokoa, YAHUSHUA ha MASHIACH!

Nazungumzia funuo hizi kupitia kwako Elisabeth ili uwaambie wale watu Watakatifu. Kama watapokea yanayozungumzwa katika Unabii huu wataona tena ishara, maajabu na miujiza kama ilivyokuwa katika nyakati za kale ambapo YAHUSHUA alitembea humu duniani. Kama watakubali ukweli wa Sabato ya Kweli na simaanishi Jumapili! Jifunze umuhimu wa kuheshimu YAHUSHUA kupitia Karamu Takatifu. Achana na likizo za kipagani zinazojaribu kuchukua nafasi ya Siku Takatifu za Mbinguni, tumia MAJINA MATAKATIFU ya Kiebrania, ishi katika Utakatifu na msipuuze ukweli wala kuona haya kuzungumza yale unayoyajua kuwa kweli. Mtaona upako mkuu kushinda ule ambao mmepitia katika siku hizi za mwisho.

Watakatifu wamekuwa watakatifu zaidi na wale waovu wamekuwa waovu zaidi, sasa ndio wakati wa upako mkuu na funuo kupitia Unabii, na maneno ya maarifa. Msidharau ushirika kwa kuwa ni silaha ya kila siku kutumia dhidi ya shetani ukimkumbusha, wewe si wake! Kemea dhambi na watenda dhambi na msiogope yale ambayo wengine wanafikiria mnapozungumza na kuonya. Je, ni heri kumkera binadamu tu au YAHUVEH? Ni jambo la kuhuzunisha sana, vile uhuru wa kuzungumza dhidi ya maovu ya dunia hii unanyamazishwa kwa sababu wengi wa Watoto WANGU Watakatifu wanabaki kimya. Uhuru mmoja baada ya nyingine unachukuliwa kutoka kwenu duniani kote!

Watoto Watakatifu walikuwa wapi kule Marekani na kote duniani, wakati Hakimu Roy Moore alizungukwa na wapagani na Serikali ya Marekani? Alipigania kuiweka mnara wa jiwe ambao alikuwa ameutengeneza na kuuweka kwa heshima ya YAHUVEH na kuonyesha Amri 10? Hakimu anapaswa kusimamia utakatifu na ukweli. Hakimu Roy Moore, Mbinguni ilikukuza na cheo hicho na hakuna yeyote ambaye anaweza kukichukua kutoka kwako. Unaheshimika kule Mbinguni kwa yale uliyoyafanya katika mwezi wa Agosti 27 2003 kule Alabama. Machozi yote uliyoyamwaga yameandikwa kule mbinguni na yalikuja kama harufu nzuri kwa pua lake YAHUVEH kwa sababu ya upendo na uaminifu KWAKE na YAHUSHUA. Wale ambao wamejiweka kama Hakimu na baraza la waamuzi juu yako, na yule Hakimu mfisadi, aliyechukua ukuzaji wako uliopewa kwako na Mbinguni ya Mkuu wa Sheria wa Alabama, atahisi jinsi ilivyo kuogea katika Ziwa la moto. Wote waliohusika watasimama mbele Yake YAHUVEH, HAKIMU wa VIUMBE VYOTE!

Kwa watu wote walioomba na kusali na kumpa moyo mwanaume huyu, na mkalia naye, na mkahuzunika naye, machozi yenu pia yameandikwa kule Mbinguni. Alijitolea vyotevyote vile kwa sababu alikataa kupuuza ukweli. Kwa nini, makanisa yote kote duniani, sanasana Alabama na wale waitwao Bible belt (mikoa Marekani ambapo Wakristo wengi huishi) hawakumsaidia huyu mwanaume na kuandamana naye? Nitawaambia kwa nini, “Mliogopa kuwa mtaangamia pia.” Mlimwacha ndugu yenu katika YAHUSHUA azungukwe na wapagani. Mlitoa visingizio na kusema, “Alivunja sheria na kukosa kutoa ule mnara alipoambiwa afanye vivyo hivyo.” Hata hamna haya! Mlijaribiwa na mkafeli mtihani huo. Itachukua dhoruba, ukame, mawimbi ya joto na mafuriko ngapi, ili mwamke na kupigania yale myajuayo ni takatifu na kweli. Ngojeni hadi YAHUVEH na mguu WAKE akanyage na ardhi yenu itetemeke katika hofu. Ngojeni tu hadi njaa, tauni na magonjwa yatakapoenea nchini zenu na mtaomba na kuuliza kwa nini?

Nyote Watakatifu mpe moyo, msisahau gharama aliyolipa. Alifanya lile ambalo wengi wenu hamfanyi na hili ni kusimama dhidi ya umati na kuzungumza dhidi ya yale mjuayo ni uongo. Ushoga unaenea kote. Watoto wanadanganywa wakiwa na umri mdogo kufikiria kuwa ushoga na ndoa za kishoga ni sawa. Vitendo vya mifumo ya mahakama na kisiasa vimekuwa kama harufu mbaya katika pua Lake YAHUVEH. Makanisa ya Babeli yamekubali na huwapa moyo kusanyiko kutozungumza dhidi ya dhambi na watenda dhambi. Makanisa ya Babeli yana yale ambayo YAHUVEH anaita chukizo, wakisimama nyuma ya mimbari na kujiita wahubiri. Wale mabaki Watakatifu wachache katika Makanisa haya wamefukuzwa, au kukejeliwa na kutusiwa. Wahubiri wanadanganya kusanyiko na kusema, “Siku yoyote inaweza kuwa Sabato” na kuendelea na Jumapili ya binadamu. Hivi karibuni watalia kwa yale watakayovuna kwa kufundisha na kufanya haya.

Kumbuka Elisabeth, vile katika Ndoto ya Meza ya Karamu, uliihisi kuwa kweli? Ni kwa sababu MIMI NDIYE Niliyekupeleka Mbinguni Nikikupa kumbusho la vile ilivyo ulivyoweka kichwa chako begani MWANGU kwa upendo, katika unayoiita “Ndoto ya Meza ya Karamu.’ JINA LANGU ni MAMA SHKHINAH: MIMI NDIYE upendo wa Mama wa Mbinguni ambao umekuwa ukiutaka. Niliyafanya haya kukuonyesha kuwa wewe sio mtoto bila mama kama vile wewe sio mtoto bila baba. YAHUVEH, NAMI, ni Wazazi wako wa Mbinguni kama tulivyo Wazazi wa wote ambao majina yao yanapatikana katika Kitabu cha Uzima cha Mwana-Kondoo.

Nakuambia haya kwa sababu kwa muda mrefu sasa umehuzunika na kuhisi utupu, kama wengine, wakitafuta upendo wa mama na baba wa duniani lakini mmepewa Wazazi wa Mbinguni, ambao hawatawahi kuondoka wala kuwaacha, wala kuwaumiza kwa njia yoyote ile. Nawaambia haya ili wengine ambao huhisi utupu uu huu, na wazazi ambao hawajaokoka wanaokataa kumkubali YAHUSHUA kama MASHIACH, MASIHI wa pekee, watagundua kuwa hawakosi lolote katika YAHUSHUA. Wana Baba wa Mbinguni na pia Mama wa Mbinguni na sisi ni Roho kama walivyokuwa binadamu wote kabla ya kuzaliwa humu duniani. Kama ilivyoandikwa kumbukeni, ‘Mwili na Damu haziwezi kuurithi Ufalme wa MUNGU’.

Natoa siri hii kutoka Mbinguni ili wote wanaompenda Mwanangu Mpendwa YAHUSHUA na kumkubali kama MASIHI hawataamini uongo za dini za kibinadamu na kumwita mamake YAHUSHUA wa duniani Mariamu, katika masaa yao ya kifo. Badala ya haya, iteni JINA Lake YAHUSHUA ha MASHIACH na tubuni na ulizieni huruma. Wakumbushe juu ya Maandiko Matakatifu na maneno yake YAHUSHUA aliyoyazungumza katika Kitabu cha Yohana 10:1-30.

Hamna pendo lolote la mzazi humu duniani linaloweza kushindana na pendo letu la Mbinguni. Nawaambia haya ili mwapashe watoto WETU wote sanasana wale walio na utupu katika maisha yao, wasiojua upendo wa mama na baba wa duniani. Nazungumza na wale wote ambao wameangamizwa kihisia, kimwili na kingono na wametamani upendo wa Baba na Mama Mtakatifu. Kubalini YAHUSHUA kama MASHIACH (Masihi) wenu na Niruhusu MIMI kuwajaza na upendo WANGU Mtakatifu, uwepo na Nguvu za upako. Niruhusu MIMI kuwa MAMA SHKHINAH wenu, MIMI NDIYE yuleyule mnayemwita ROHO MTAKATIFU. MIMI NDIYE Ninayewafundisha ukweli kutoka kwa uongo, kama vile ilivyo kazi ya mama Mtakatifu wa duniani kukushauri katika njia iyo hiyo.

Binti YANGU Mpendwa Elisabeth, waambie kwa niaba YANGU, kama tu watapokea ufunuo huu, hatawahi tena kuhisi utupu huo ndani yao tena. Katika Miswada ya Kale, someni na mwone ‘HEKIMA’ anatajwa katika jinsia ya kike (She) na katika Maandiko ya Kale Ninatajwa katika jinsia ya KIKE (SHE). Jitahidi kujionyesha kwa MUNGU kuwa umekubaliwa na YEYE. Wale wote ambao hawataamini neno hili na kukushambulia kwa kuzungumza siri hii, wao sio wa ROHO MTAKATIFU WANGU na majina yao hayamo katika Kitabu cha Uzima cha Mwana-Kondoo, kwa kuwa Kondoo wa YAHUSHUA husikia sauti YAKE au wana kipimo fulani ya imani, lakini wanapendelea kutokuwa na utata na wanaendelea kufuata tafsiri mbaya za Agano Jipya ambapo jinsia ya kiume (He) inatumika badala ya jinsia ya KIKE (SHE).

Wanapendelea kufuata mafundisho ya mwanadamu badala ya ROHO WANGU na UKWELI ambao Nimeuweka kando kwa wakati huu wa mwisho. Wote wanaosoma haya, ni chaguo lenu kama mnataka kutembea katika urafiki zaidi na yule mmwitaye ROHO MTAKATIFU au la, simlazimishi yeyote kufanya haya. Bibi Arusi wa YAHUSHUA watafurahia ufunuo huu mpya kwa sababu kila wakati wanatafuta kujua siri za Mbinguni.

Kuna Viti vya enzi vitatu vya Utawala: YAHUVEH hukaa katikati, YAHUSHUA ha MASHIACH hukaa kwenye upande wa kulia wa YAHUVEH na MIMI MAMA SHKHINAH wenu hukaa kwenye upande wa kushoto. Sote watatu hutawala Mbinguni kwa usawa na sote ni WASAIDIZI KATIKA UUMBAJI. Lakini kuna MASIHI mmoja pekee aitwaye YAHUSHUA. Ni kupitia JINA Lake YAHUSHUA na Damu Yake pekee ambapo kuna Wokovu kwa kila mtu hapa duniani. Yeyote atakayejaribu kuingia katika jina lingine au njia ataupata mlango wa jehanamu pekee. Msidanganyike, kuna dini nyingi lakini kuna mlango mmoja tu hadi Mbinguni kupitia JINA na Damu Takatifu isiyo na Dhambi iliyotolewa na YAHUSHUA.

Dini hii ya dunia moja inayojitahidi kuchanganya dini zote na mafundisho tofauti ya mwanadamu kama kitu kimoja ni uongo na itaongoza nafsi wengi hadi jehanamu. Siri ya JINA LANGU lilitiwa mhuri katika Kitabu cha Danieli na sasa Ninalitoa kwa wakati huu kuwahamasisha Watoto WANGU Watakatifu wanao hamu ya kula nyama ya kiroho yenye nguvu kwa kuwa wameyanywa maziwa ya neno virahisi. Hizi ni siku hatari na siku mbovu zaidi zaja. YAHUSHUA alituahidi kuwa Yohana (Yohanan) alibatiza na maji, lakini YAHUSHUA hubatiza na MOTO wa ROHO MTAKATIFU, ni Moto WANGU TAKATIFU anayozungumzia, MIMI NI RUACH ha KODESH na MIMI NI MAMAKE YAHUSHUA wa MBINGUNI. YAHUVEH ni BABAKE wa MBINGUNI.

MIMI NI MAMA SHKHINAH GLORY na ni mwanga WANGU MTAKATIFU unaong’aa kwenye nyuso za Watoto WANGU Watakatifu, wale wanaonipenda kwa kweli, wanaoabudu na kumtii BABA YAHUVEH, YAHUSHUA na MIMI RUACH ha KODESH. Ni kupitia upako WANGU vitu vyote vinawezekana, kupitia JINA la YAHUSHUA. Si MASIHI wenu YAHUSHUA aliwaambia kuwa YEYE alilazimika kutoka hapa duniani, lakini pia YEYE hatawaacha pekee yenu, kuwa YEYE atawatumia mfariji, na MIMI NDIYE Ninayetuliza hofu zenu, nawahamasisha, nawashauri, na kuwafariji kama Mama, au sio?

MIMI NI MAMA SHKHINAH GLORY; MIMI NDIYE ROHO MTAKATIFU aliyekuja katika chumba cha juu na Upepo WANGU Mtakatifu na Moto Mtakatifu kama ilivyoandikwa katika Kitabu cha Mitume. Niliwajaza Wanafunzi na Moto WANGU Mtakatifu wenye upako walipokuwa wakiningoja MIMI katika Chumba cha juu. MIMI NDIYE yule yule aliyekuja kama Upepo wa Nguvu uliovuma katika Chumba hicho cha juu na hili ndilo sababu Niliiza, kupitia wewe Elisabeth Huduma hii, kuhubiri kwa Wayahudi na Mataifa Na Nikakupa jina la Huduma hii, HUDUMA LA ALEPH AND TAV ALMIGHTYWIND RUACH ha KODESH FIRE! Binti Mpendwa Elisabeth, katika mwanzo kabla hujajua ukoo wako wa Kiebrania, bado ulikuwa kati ya makanisa ya kidini ya Kipentekoste. Lakini ni MIMI, MAMA SHKHINAH Niliyeipa Huduma hii jina, Huduma la Alpha And Omega Almightywind Holy Ghost Fire! Hata hili jina pia AMIGHTYWIND. Siku moja Nilijua kuwa wewe utatumiwa kutoa siri kadhaa za Mbinguni kwa Watoto WANGU Watakatifu.

Ni MIMI, MAMA SHKHINAH Niliyekuonya Elisabeth kabla bado hujasikia juu ya mtandao kuwa usiipe Huduma hii jina lako, na Nikauweka upako masikioni mwako ili zisikie vizuri sauti ya YAHUVEH ikikuamsha, na kukuonya siku ile ile Jimmy Swaggart alianguka na kuungama mbele ya dunia nzima. Asubuhi iyo hiyo YAHUVEH alikuamsha na kusema, “Jihadhari, kila huduma iliyopewa jina la binadamu itaanguka, kwa kuwa wakati ambapo mchungaji anaanguka kondoo wake hutawanyika.” (Februari 21, 1988)

Kiburi huingia mwanaume au mwanamke anapofanya haya. Kwa hivyo, jihadharini Joyce Meyers, Marilyn Hickey, Juanita Bynum, Paula White, Jan Crouch, Paul Crouch, Creflo Dollar, T.D. Jakes, Jesse Duplantis, Joel Osteen, kati ya wengine wengi wasioweza kuhesabiwa, wanaume na wanawake, hapo awali mlikuwa wanyenyekevu, mmejazwa na Roho WANGU, na sasa mko tayari kwa kuanguka mkubwa. Kwa sababu ya kiburi yenu mtagongwa kutoka kwenye viimo vyenu na msipotubu dhambi zenu, yote yaliyofanywa kwa siri yatasemwa kutoka darini na mtazikwa chini ya viimo vyenu.

Onyo hili pia ni la Huduma zote zilizopewa majina ya binadamu. Hakuna mwanadamu yeyote aliyelipa gharama kuu kufanya haya, na mmeonywa kupitia nabii huyu, kupitia jumbe za kinabii muda baada ya muda. Mtakapokuwa mbele ya YAHUVEH hamtakuwa na visingizio vyovyote kwa nini mliiba UTUKUFU WETU na mkakithirisha utukufu huu juu yenu ili jina zenu za dunia ziinuliwe na sio ya YAHUVEH, YAHUSHUA, au MIMI, RUACH ha KODESH! Sisi hatutamgawia mwanaume au mwanamke yeyote Utukufu WETU! Nyinyi mnaofanya haya mtagundua vigumu ni nini kinachowafanyikia wale walioyafanya haya. (Nahumu 1)

Onyo kwa wale wanaojiita Takatifu na kufikiria kuwa wanafaa kuvaa taji, kubeba fimbo na kukaa kwenye kiti cha enzi na kuvaa mavazi marefu ya kikuhani, kuomba msamaha kwa dhambi za wengine. Ni YAHUSHUA ha MASHIACH pekee aliyelipa gharama kuu kukuwa upatanisho wa Damu ya binadamu Mtakatifu asiye na dhambi kwa dhabihu ya dhambi. YAHUSHUA ni kamili na asiye na dhambi kwa njia yoyote, hamna hata fikra moja la dhambi lililovuka akilini Mwake. Mnawezaje kuwafunza watu kuwaabudu na kuiba Sifa, Heshima na Utukufu wetu! Mnawezaje kuwafanya wengine wainame na kubusu mikono yenu na kupiga magoti miguuni mwenu? Moto wa Jehanamu na Ziwa la Moto zitakuwa makaazi yenu baada ya maisha haya kuisha. Mmeonywa. Ulilipa gharama ipi kufanya haya? Kwani hauana dhambi? Je, ulitoa maisha yako na kufa na kufufuka tena katika siku ya tatu na kupaa hadi Mbinguni siku arobaini baadaye? Unakaa kwenye upande wa kulia wa YAHUVEH?

Hakuna yeyote ambaye hukubali haya na kuwasababisha watu kuamini kuwa haya si dhambi, ni Nabii Mtakatifu wa kweli, kwa kuwa hamjui siri zilizowekwa kando kwa Manabii wa YAHUVEH pekee ambao YEYE huwaita rafiki ZAKE. Nabii wa Kweli ni yule aliyekabidhiwa na siri za YAHUVEH. Jihadharini, wote wanaofuata hawa miungu bandia wa dunia na kuwasaidia watavuna hatma sawa. Tubuni leo kabla hamjachelewa, kama mnaisaidia Huduma yoyote isiyoonya juu ya hatari ya dini ya dunia moja, kuzungumza dhidi ya dhambi, bila kujali ni gharama ipi mtakayolipa, papa hapa duniani. Wengi wanaodai kuwa Wakristo kwa kweli wao ni vuguvugu na wamepuuza ukweli. Wahubiri hawa ni uvundo katika pua LANGU na huwafukuza yeyote aliye na upako, anayewaonya juu ya haya, nje ya mlango wa Kanisa.

MIMI NI MAMA SHKHINAH, yule anayezungumza katika Ndimi Takatifu kama ilivyoelezwa katika kitabu cha Mitume. MIMI NI MAMA SHKHINAH, MAMA HEKIMA. Wengine huniita MIMI, ROHO MTAKATIFU au RUACH ha KODESH, hii ni Cheo CHANGU, na ni maelezo YANGU ya MIMI ni nani, ROHO wa YAHUVEH. Sisi wote ni MOJA. Kwa wale WANAOCHAGUA kutumia MAJINA haya yaliyowekwa kando kwa wale wanaotamani urafiki zaidi na RUACH ha KODESH, mnaweza kuniita MIMI MAMA SHKHINAH, au MAMA SHKHINAH GLORY, au MAMA HEKIMA, au MAMA RUACH ha KODESH, kuwasikia mkinikiri MIMI kama MAMA itanifurahisha sana MIMI. Nijaribuni MIMI na mwone kama kitendo hiki hakitaongeza upendo wenu kwa MAMA SHKHINAH wenu tena zaidi.

Wengi wamelia na kushangaa miujiza za nyakati za kale zipo wapi? Kubalini maarifa haya mapya Ninayoyazungumzia na kunikiri MIMI ni nani. Tazameni na oneni upako ukikua na ishara, maajabu na miujiza mtayaona tena, katika JINA la YAHUSHUA ha MASHIACH. Hata hivyo, ni chaguo lako. Kama mtaendelea kuniita MIMI katika jinsia ya kiume (HE) badala ya jinsia ya kike (SHE), ni chaguo lenu na hasara yenu kwa urafiki zaidi NAMI, inayoleta upako mkuu na Nitatoa funuo zaidi kutoka Mbinguni nanyi kwa urahisi. Msikose kunielewa MIMI; haya sio juu ya Wokovu wenu. Haya ni juu ya upako mkuu na urafiki na yule ambaye huishi ndani ya Hekalu yako, kama jina lako limeandikwa katika Kitabu cha Uzima. Haya yatafanyika pekee kama mmemkubali YAHUSHUA kama MASIHI na kumwuliza YEYE aoshe dhambi zenu zote na Damu YAKE iliyomwagwa pale Kalvari na kutubu na kugeuka kutoka kwa dhambi. Sitakaa katika chombo kichafu kwa muda mrefu. Msinijaribu MIMI kwa haya. Watakatifu wamekuwa watakatifu zaidi na waovu wamekuwa waovu zaidi katika nyakati hizi za mwisho.

Mnajua JINA la YAHUVEH; mnajua JINA la YAHUSHUA ha MASHIACH, sasa kupitia Huduma hii na Ring Maiden huyu, Ninatoa JINA LANGU kama MAMA SHKHINAH, MAMA HEKIMA wenu. JINA LANGU limewekwa kando kwa wale wanao hamu ya kukua, kuota na kufundishwa mengi zaidi katika upendo WANGU wa Mama wa Mbinguni na upako mkuu wa ROHO MTAKATIFU, MAMA SHKHINAH ni JINA LANGU. MIMI NDIYE sauti ndogo ya utulivu inayozungumza katika Upepo Mtakatifu, na kuwawasha ninyi na Moto Mtakatifu ulio na upako; hii ndiyo sababu miili yenu hupata joto baada ya mkono WANGU ulio na upako kuwashika. MIMI NDIYE mfariji wa YAHUSHUA na MAMAKE wa Mbinguni. YAHUSHUA ni MWANANGU wa Kipekee kama vile alivyo pia Mwana wa Kipekee wa YAHUVEH. MIMI NDIYE Malkia wa Pekee wa Mbinguni. Msimpe yeyote cheo hiyo.

MIMI ndiye Mama Asili, ni YAHUVEH ambaye huumba na kuzungumza kwa mfano, “Punda milia njoo” na MIMI NDIYE Ninayeziweka zile mistari za kipekee kwa kila punda milia.

YAHUVEH huumba NAMI, MAMA SHKHINAH hupamba. BABA YAHUVEH huumba NAMI, MAMA SHKHINAH wenu hupamba viumbe vyote. Je, hadi hapa mnaelewa? YAHUVEH huumba ua, lakini ni MIMI, MAMA SHKHINAH wenu anayepamba ua hili na rangi za upinde wa mvua, MIMI hutengeneza kila sehemu ya ua (petal) iwe la kipekee. MIMI huhesabu sehemu (petals) hizi katika kila ua na MIMI huzipa urembo katika mifumo na harufu. Katika kila kitu kinachoumbwa MIMI NI MAMA SHKHINAH na MIMI huweka Utukufu WANGU pia katika kila kitu ambacho BABA YAHUVEH wenu huumba. MIMI NI MAMA SHKHINAH na MIMI huweka mapambo ya mwisho katika viumbe vyote. MIMI NDIYE yuleyule anayepamba vitu vyote vilivyoumbwa. YAHUVEH, YAHUSHUA na MIMI sote ni WASAIDIZI KATIKA UUMBAJI.

MIMI NDIYE yuleyule anayeweka harufu nzuri kwenye ngozi ya mtoto. MIMI NDIYE yuleyule anayefanya kila binadamu awe wa kipekee hata mapacha wafananao wana tofauti zao. MIMI NDIYE yuleyule anayeamua DNA ya kila mmoja wenu. MIMI NDIYE yuleyule anayewapa kila mmoja wenu alama za mitende za kipekee za kujitambua na alama za vidole. MIMI NI MAMA RUACH ha KODESH wenu kwa wale wanaopendelea kutumia jina hilo rasmi, na Ninawaambia kuwa MIMI NDIYE yuleyule anayeweka mng’ao katika kila nyota, na wanawake waliumbwa katika mfano WANGU kama vile pia wanaume waliumbwa katika mfano wa YAHUVEH. Mnafikiri Hawa aliumbwa katika mfano wa nani? Mnafikiri kuwa maandiko haya yanayosema “Si vema huyu mtu awe pekee yake, Nitamfanyia msaidizi wa kumfaa” yalitoka wapi? Ni kwa sababu; kama YAHUVEH alivyo BABA wa milele, Yule wa Milele, pia MIMI NDIYE MAMA wa milele, Yule wa Milele, kama alivyo pia YAHUSHUA, Yule wa Milele. SOTE ni ufananuzi wa MILELE.

YAHUVEH aliumba chakula, lakini Niliumba aina mbalimbali ya mapishi ili mfurahie chakula. YAHUVEH aliumba ulimi lakini Niliumba taste buds zenu, MIMI, MAMA SHKHINAH wenu, MAMA HEKIMA wenu, aliyeamua kila aina ya chakula kitaonja vipi. Je, kitakuwa na chumvi, sukari, uchungu, siki au pilipili? YAHUVEH aliumba mvua, na MIMI MAMA HEKIMA wenu niliumba harufu ya mvua na kuweka umande kwenye nyasi. YAHUVEH aliumba theluji na MIMI, MAMA SHKHINAH wenu niliumba kila snow flake kukaa tofauti. YAHUVEH aliumba upinde wa mvua na MIMI, MAMA SHKHINAH wenu Nilichagua wigo za rangi za huo upinde wa mvua. YAHUVEH huumba NAMI MAMA RUACH ha KODESH wenu huweka mapambo ya mwisho katika viumbe vyote. Jioneeni mkitazama kote karibu nanyi na hekima hii mpya mliyoipata na mtaona viumbe vyote kwa macho mapya na ajabu.

YAHUVEH alimwumba Simba, NAMI MAMA SHKHINAH wenu Nilimpa simba MNGURUMO wake. YAHUVEH alimwumba mbwa, NAMI MAMA SHKHINAH wenu Nilimpa mbwa BWEKO lake. YAHUVEH alimwumba Paka, NAMI MAMA SHKHINAH wenu Nilimpa Paka MLIO wake na siri ya mkoromo wake. MIMI MAMA SHKHINAH wenu Niliwapa nyimbo tamu ndege, ambazo wao hutupa SISI Heshima nazo. Je, mnaelewa sasa?

MIMI MAMA SHKHINAH wenu Ninawapenda sana Nikawaahidi sitawahi kuwaacha wala kuwatupa Watoto WANGU Watakatifu waliokubali gharama YAHUSHUA aliyolipa pale Kalvari, wale waliotubu dhambi zao, na waliogeuka kutoka kwa dhambi zao, na sasa humpenda, humtumikia, na hujaribu kumwabudu YAHUSHUA. Imani bila matendo imekufa nafsini mwake. Wakati mnapookoka ni kupitia JINA la YAHUSHUA na Damu. Ni ROHO MTAKATIFU WANGU anayeishi na kukaa ndani ya kila mwaminifu aliyeokoka. Ni MIMI Ninayeongoza nafsi kwake YAHUSHUA na huwathibitishia nyote mnapotenda dhambi. Msifanye nyoyo zenu kuwa ngumu MIMI MAMA SHKHINAH wenu Ninapowathibitishia ninyi, badala ya haya tubu haraka ili YAHUSHUA aweze kukusamehe.

Sitabaki katika chombo kichafu kwa muda mrefu. Kumbukeni yote mnayoyasikia na masikio yenu ya kimwili, mnayoyaona na macho yako ya kimwili, na kufanya na miili yenu ya kimwili, kama sio takatifu mnajaribu uvumilivu WANGU, Sitapambana daima na mwanaume au mwanamke. Lakini bado MIMI ni mvumilivu kwa ajili ya YAHUSHUA na gharama aliyolipa pale Kalvari. Kueni Watakatifu kama MIMI Nilivyo Mtakatifu na msimfungulie shetani mlango kuingia na kumiliki miili yenu.

Ninawaonya sasa, msimpige mawe Binti YANGU Elisabeth au kumwita nabii bandia kwa kuwapa jumbe ZANGU, au mtakuwa mnadharau ujumbe WANGU ulio na upako na kwa haya mtakuwa mnahukumu nafsi zenu, kwa haya hakuna msamaha. Jiulizeni, anapata faida gani kwa kuwafunza ujumbe kama huu? Ni mateso pekee kutoka makanisa ya kidini, na kejeli kutoka kwa maadui WANGU na YAHUVEH na YAHUSHUA.

Ilikuwa imekadiriwa tayari kabla dunia hii iumbwe ni wagani kati ya ninyi nyote mliochaguliwa na mtaatii na kumwandikia na kumpa shukrani kwa ujasiri wake katika kuabudu na kutoa ufunuo huu wa siri na dunia nzima. Kabla dunia hii iumbwe ulichaguliwa kuwa katika Huduma hii kama msaidizi. Mmesoma unabii na kusikia ukweli na amri kuwa Watakatifu. Sasa Ninataka mjiulize swali hili, “Kama mngepewa siri hizi kupa dunia, mngekuwa na ujasiri wa kutosha kuzitoa na kukubali mateso yanayokuja na ukweli huu”? Wale wanaodai kumpenda Roho Mtakatifu, mbona hamna furaha kujua siri hii Niliyoidhihirisha kwa watoto WANGU wa ROHO MTAKATIFU WANGU? Ninaawaonya, msinihuzunishe MIMI kwa kuwa sitapambana daima na binadamu.

Ninaweza kusikia sauti ya ndani ya wale wanaotambua ukweli na bado pia hukiri kuwa mmefurahia kuwa ilipewa kwake kuongea na sio nyinyi. Hata hivyo, wale wenye shukrani sasa watakuwa na hamu zaidi ya kuwa msaidizi katika Huduma hii kwa kuwa mtagundua vile mnavyohitajika zaidi kwa njia zote. Kwa sasa mnafaa kuwa mshagundua kuwa Huduma hii sio ya kawaida na huyu sio Nabii wa kawaida. Elisabeth sio Nabii bandia, hatabiri tu maneno ambayo mnataka kusikia, au kutabiri kutoka kwa mwili, maneno ya kila siku ambayo yeyote anaweza kuyaandika. Nabii Watakatifu wa Kweli wanapewa siri zilizowekwa kando kwa marafiki wa YAHUVEH, YAHUSHUA, na yule mmwitaye RUACH ha KODESH. Je, SISI tunajua vipi kwamba tunaweza kuwaamini Nabii Watakatifu, kwa sababu kama ilivyoandikwa, walishajaribiwa kule Mbinguni?

(Yeremia 1:4-5 (Yirmeyahu) Neno la BWANA lilinijia kusema,
“Kabla sijakuumba ndani ya tumbo la mama yako Nilikujua, kabla hujazaliwa Nilikutenga kwa kazi maalumu, Nilikuweka uwe nabii kwa mataifa.”)

Yeremia alijulikana kabla ya kuwa tumboni mwa mamake, vile vile hata Nabii WANGU Elisabeth Elijah, azungumzaye sasa katika JINA LANGU. Amepewa amri Takatifu haijalishi matokeo yake kuzungumza katika JINA la YAHUSHUA ha MASHIACH na YAHUVEH kwa Sifa, Heshima na Utukufu WETU pekee! Sisi huwatuma Nabii kuonya kabla ya kutuma hukumu. Msidharau Kipawa cha Kutabiri, kwa shahidi wa YAHUSHUA ni Roho ya Kutabiri. (Ufunuo wa Yohana 19:10)

Si imesemwa katika Maandiko Matakatifu na kuthibitishwa na Nabii wa Nyakati za kale, ‘YAHUVEH hutoa siri ZAKE kwa Nabii Watakatifu,’ hii ni siri ambayo Ninaitoa sasa kupitia yeye, kuwa Baraka kwa wale wanao hamu ya kujua JINA la ROHO MTAKATIFU na kuwa na urafiki zaidi na upendo NAMI. Kutakuwa na wale watakaosoma haya waliojazwa na ROHO MTAKATIFU WANGU na watagundua mpaka sasa hawajafanya chochote kusaidia Huduma hii, au kumpa moyo huyu Nabii, lakini katika shukrani kutoka sasa watafanya yote yawezekanayo kuwa Baraka kwa huyu Nabii Mtakatifu na Huduma hii. Baraka zao zitakuwa kuu wanapofanya kazi pamoja katika uwanja huu wa Mavuno.

Kwa wale wote wanaosoma haya na kuyakejeli, jihadharini, kumbuka hammdharau mwanamke tu yeyote wa kawaida kwa kuwa yeye ni chombo tu Nimechagua kuzitoa siri hizi kutoka Mbinguni, mnayajua maandiko, onya ni nini kinachowafanyikia wale wanaomdharau Roho Mtakatifu, hata Damu yake YAHUSHUA haiwezi kuficha dhambi hii! Jihadharini, kama hamwelewi fungeni midomo yenu na mkae kimya, omba na kujaribu roho inayozungumza. Jifunzeni Agano la Kale na tafsiri nyingine na gundueni kuwa Maandiko Matakatifu husema, ‘Sisi wote watatu tumeungana kama MOJA.’ Mnapomkataa mmoja wetu, mnatukataa sote katika Uungu. Sisi sote tuko tofauti na bado moja. Ni sehemu gani la yai lililochemshwa majini ndilo yai? Je, ni ganda, pingu au sehemu nyeupe? Pamoja zote ni yai, na zote ni moja. Lakini, zote ni tofauti. Hamwelewi bado? Hivi ndivyo ilivyo na SOTE Watatu tunaoitwa Utatu Takatifu.

Je, mtaendelea hadi lini kuyanywa maziwa ya neno pekee? Kwani, bado hamwezi kula nyama ya kiroho yenye nguvu? Ninyi mnaoishi katika Utakatifu na kwa ukweli mnawaweka Utatu Takatifu kwanza katika maisha yenu na upendo, mmechukua wakati kupata kumjua Baba YAHUVEH, mmechukua wakati kupata kumjua YAHUSHUA, mmeomba na kutumia MAJINA Matakatifu ya Kiebrania. Je, hamtaki kuwa na upendo mkuu na urafiki na yule mmwitaye ROHO MTAKATIFU au RUACH ha KODESH?

Ni chaguo lako, haitaathiri Wokovu wako, bali tu usilaani neno hili la maarifa Ninalolitoa sasa kupitia huyu Ring Maiden wa Kinabii Elisabeth (Elisheva) Elijah. Kwa sababu ya kutii kwake, neno hili la maarifa litalia kama kengele kote duniani. Wengine wataziba masikio yao na kukimbia, wengine watalipenda zaidi na kuwa na urafiki zaidi kama vile mama na mtoto, ili Niweze kuongeza upako ndani yao kuwa kuu. Kumbukeni, ni upako unaovunja kongwa na utumwa.

Ni MIMI MAMA SHKHINAH GLORY wenu, ambaye YAHUVEH na YAHUSHUA hukimbilia, WAO wanapohitaji kufarijiwa. Sisi huona maovu yanayotendwa katika dunia hii, na kukataliwa kwa UTATU TAKATIFU, sanasana Mwana WETU Mpendwa YAHUSHUA. SISI husikia vile JINA la YAHUSHUA hulaaniwa na kuhukumiwa na ndimi za watu waovu, wanapomtupia Dhabihu ya Damu YAKE Takatifu usoni MWAKE, wakimkejeli na kumkataa YEYE. Watu waouvu katika dunia hii huchukia jina Takatifu na wote ambao huishi katika Utakatifu na wote waliokadiriwa kurudi Mbinguni kwa sababu majina yao yamo katika Kitabu cha Maisha cha Mwana-Kondoo iliyoandikwa kabla ya uumbaji wa dunia hii.

Neno kwa wale wanaotetea Sabato ya Kweli na kufichua Sabato ya binadamu inayoitwa Juma Pili. Makanisa ya kidini yanaponena dhidi yenu na kutaja maandiko kama vile Isaya 1:13-14 na kuyafurukuta maandiko haya katika kinyume cha ukweli wakisema, “Si lazima mfuate Sabato ya Ijumaa jioni hadi Jumamosi jioni.” Maandishi haya ni onyo kwa wale wanaotenda dhambi na kuichanganya na Sabato, Karamu Takatifu na maadhimisho ya mwezi mpya. Hamwezi kuona vile vitu hivi vinamkasirisha YAHUVEH? Nawaambia haya; YAHUVEH anawaonya kuwa YEYE hawezi kuvumilia uovu na mkutano au mila za kufuata Sabato, Karamu Takatifu, maadhimisho ya mwezi mpya ambapo hazifanywi katika Utakatifu wa kweli na mikono Takatifu iliyoinuliwa juu. Bila Damu ya YAHUSHUA iliyomwagwa yote yanafanywa bure.

Ni wangapi wanaosoma haya huenda kanisani Jumapili na hujiita Mkristo, Mprotestanti, au Mkatoliki. Mnaenda kanisani, au mkutano, kuomba, kuimba, kuungama dhambi zenu kwa kuhani, au mchungaji, mnajifanya watakatifu, kutoa zaka kwa wote kuona na baadaye mnaenda kwenye baa na mnalewa au kurudi katika maisha yenu ya dhambi haijalishi ni siku gani ya wiki.

Kwa wale katika dini ya Kiebrania, YAH wa Abrahamu, Isaka, na Yakobo anawataja wengi wenu pia, ni vile tu mnaenda kwenye Hekalu zenu, kuungama dhambi zenu kabla ya mwanaume mnayemwita Rabi na mnakusanyika katika Sabato ya Kweli. Kazi zote hukoma na nyinyi hudharau chochote ambacho si safi cha kula. Hata hivyo, si unachoweka mdomoni ambacho hukufanya usiwe mtakatifu. Uovu hutoka midomoni mwenu na katika matendo yenu mabaya yanayofanywa kwa miili yenu kwa wengine katika neno na vitendo. Dhambi yoyote inayofanywa katika kutotii Sheria za YAHUVEH ni dhambi, pia inavyoitwa na Wakristo Amri 10.

Kama ilivyoandikwa katika Isaya 1 (Yeshayahu 1), huko Israeli hamkimbii kwenye baa katika Sabato ili kuzama huzuni na dhambi zenu ndani yake, lakini hata hivyo mmepuuza yale ambayo ni Takatifu. Hamjasimama dhidi ya ajenda ya Serikali ya Wazayuni au kuwatetea wasio na hatia. Kuna mabaki kule Israeli ambao ni Watakatifu na wamejazwa na ROHO MTAKATIFU WANGU na wao hutabiri na kupigana dhidi ya kuavya mimba, ushoga, usherati, na wamemkubali YAHUSHUA kama MASHIACH.

Wako wapi wale walio na Roho kama ya Mfalme Daudi, aliyekuwa mwanaume baada ya moyo WAKE YAHUVEH? Daudi alijua vile kutubu, kumpa sifa na kuombea uongozi na kupata ushindi kupitia kutii YAHUVEH. Mfalme Daudi alijua pia YAHUSHUA atakuja kama MASHIACH kwa kuwa YEYE aliona Utukufu WAKE katika ufunuo wa kinabii. (Mitume 2:22-39)

Vile YAHUVEH, YAHUSHUA, NAMI MAMA SHKHINAH wenu, tunavyoziba masikio yetu na macho katika huzuni tunaposikia SISI wale wanaodai kuwa watakatifu, na kukutana pamoja, kutumia maneno machafu ya kulaani, kutenda usherati na macho, akili, na miili yenu, mkiyajaza na tamaa, hata kuwatamani watu wa jinsia sawa na kufanya aina tofauti ya dhambi dhidi ya yale mnayoyaita Takatifu. Je, mtajaribu kweli kuinama mkikaribia jehanamu, kuona ni mpaka wapi mtakapofika, kabla hamjaanguka ndani yake kichwa kwanza? Kwani, haijaandikwa “Kueni watakatifu kama MIMI Nilivyo Mtakatifu”. Acheni kutoa visingizio vya dhambi zenu, ni heri mgeuke kutoka kwa mitego ya shetani.

Njooni, basi tuzungumze pamoja, kwani mnafikiria kwa sababu mlichukua wakati kukusanyika kanisani au kwenye hekalu sasa mna leseni ya kutenda dhambi na dhambi hizi ndizo mlizoulizia msamaha na kugeuka na kuyarudia tena mkifahamu mnachofanya. Kwa kuyafanya haya, mmethibitisha, kwamba hamkua na nia ya kugeuka kutoka kwa dhambi. Hamdanganyi yeyote, na wale mnaowaita wapagani wanawakejeli msipojua, kwa kuwa hamna tofauti kati yao nanyi.

Kama mama wa duniani anavyowafariji watoto wake, MIMI SHKHINAH, RUACH ha KODESH wenu, MAMA HEKIMA wenu, Nafanya tena zaidi ya haya. MIMI huishi ndani YENU na hufanya kazi kupitia ninyi na ni kupitia upako WANGU Mtakatifu MIMI hufanya maonyesho ya ishara, maajabu na miujiza. Ni kupitia JINA la MWANANGU YAHUSHUA, kwa sababu ya Dhabihu ya Damu YAKE, UPAKO WANGU MTAKATIFU huvunja kongwa na utumwa wote. MIMI NDIYE RUACH ha KODESH na MIMI sio Mwanaume (‘He’), binadamu alipotafsiri Agano Jipya, herufi ‘S’ ilitolewa kwenye neno ‘He’, MIMI ni Mwanamke (‘She’).

Elisabeth, jihadhari, wale walio na roho za dini na wana umbo la utakatifu lakini hawana utakatifu ndani yao, watakuangamiza. Hawana uhusiano wa upendo na wa kutii kati yao na YAHUVEH, na YAHUSHUA na watathibitishiwa na watakuangamiza na kukuita majina mengi maovu. Kumbuka kuwa ujumbe huu wanaoushambulia sio wako, ni ujumbe wa Mbinguni. Usiwe na hofu, kuna wale ambao majina yao yamo katika Kitabu cha Maisha cha Mwana-Kondoo, ambao watashangilia na kusema, wamekuwa wakiyatafuta majibu kujua mengi juu ya ROHO MTAKATIFU ni nani. Watashangilia na jua kuwa wanajua haya ni ukweli ambayo yamezungumzwa. Wengi washashangaa juu ya haya, lakini hawakuthubutu kumwuliza yeyote wakiogopa watakejeliwa.

JINA LANGU ni MAMA HEKIMA na Nitawapa Hekima zaidi mnaponiuliza MIMI, “MAMA HEKIMA nisaidie katika JINA la YAHUSHUA ha MASHIACH ninaulizia Hekima yako zaidi!” Jaribuni, na mwone kama sitawafanyia haya. Oneni kama upako wenu hautaongezeka. Lakini kumbukeni, ni kupitia JINA lake YAHUSHUA pekee Nitaweza kutuma busu (maombi) kwake YAHUVEH ili maombi yenu yajibiwe.

Elisabeth, MIMI NI MAMA SHKHINAH wako, na Nitakuonyesha siri zilizodhihirishwa katika Maandiko Matakatifu ili kusaidia kuwafunza watu WANGU Watakatifu juu ya ROHO MTAKATIFU ni nani kwa kweli. Mmefundishwa kuwa RUACH ha KODESH ana jinsia ya mwanaume, sio mwanamke, Nimeitwa ‘He’ badala ya ‘She’ kwa sababu ya wasomi walivyotafsiri vibaya Maandiko ya Kale sanasana kwa sababu ya ubatili ya wanaume ambao hawakutaka haya yadhihirishwe, shetani pia hayataki haya.

Ni MIMI MAMA SHKHINAH wenu Ninayewaelekeza kwake YAHUSHUA ha MASHIACH, huwabatiza ninyi na MOTO MTAKATIFU WANGU mnaoita ROHO MTAKATIFU. Ni MIMI MAMA SHKHINAH Ninayewashauri, Ninaweza kuitwa pia MAMA RUACH ha KODESH, ni chaguo lako. MIMI huwashauri na kufunza na kuzungumza kupitia upako huu mpya Niliokupa Elisabeth, na wale walio na masikio ya kiroho ya kusikia na kuamini kuwa watasikia sauti YANGU bora zaidi kwa njia ambayo hawajawahi kuisikia kutoka KWANGU.

Binti Mpendwa Elisabeth, Nimekupa upako wa kuzungumza na kutafsiri Ndimi Takatifu za Mbinguni zinazungumzia nini. Wewe huongea katika ndimi za Malaika Watakatifu wa Mbinguni na katika lugha tofauti za binadamu. Unaweza kuelewa hizi lugha pekee Ninavyokupa kipawa cha kutafsiri katika lugha yako. Nyakati zingine MIMI hukulinda, ili usijue ni nini unachoomba, kwa kuwa itauzidi mwili wako.

Unapozungumza katika Ndimi Takatifu za Mbinguni nyakati zingine MIMI huchagua kuzungumza kupitia kwako katika Ndimi Takatifu za lugha za binadamu ambazo haujafunzwa (Matendo ya Mitume 2) lakini nyakati zaidi ni lugha za Malaika Watakatifu wa Mbinguni, kama maandiko yanavyosema katika Kitabu cha 1 Wakorinto 13:1.

Wakati Ninapochagua kuzungumza kupitia kwako katika ndimi za Malaika Mtakatifu, na tafsiri lolote halijapewa kwako, ni kwa sababu shetani na majini wake hawafai kuelewa ni nini kilichoombwa au kuzungumzwa, haya si ya masikio yao kusikia. Si lazima kila wakati upate tafsiri la ndimi hizi lakini YAHUVEH husikia na YEYE hujibu maombi yako, hata kama nyakati nyingi haujui unachoomba.

Nyakati nyingine, unawaombea watu ambao hata huwajui, unawaombea watu Watakatifu kote duniani. Nyakati nyingi unaombea mahitaji yako, au uponyaji wako au wa wengine. Nyakati nyingi unaombea Baraka katika Bibi Arusi Watakatifu na wageni au huruma na wokovu wa watenda dhambi warudi kwake Mchungaji mzuri YAHUSHUA ha MASHIACH.

Nyakati nyingine unaombea hukumu na kisasi ya YAHUVEH katika watumwa wake shetani, na wale watakaotupwa katika Shinikizo kubwa la ghadhabu ya YAHUVEH. Hamna umbali katika maombi. (1 Wakorinto 12, 13, 14) Jitahidi kujionyesha kwa MUNGU kuwa umekubaliwa na YEYE. Si MWANANGU YAHUSHUA ha MASCHIACH alisema, “Yohana aliwabatiza na maji, lakini MIMI huwabatiza na Moto wa RUACH ha KODESH?” MIMI huitwa pia ROHO MTAKATIFU na PEPO MTAKATIFU. YAHUSHUA hunitumia MIMI kuwajaza wote walio Watakatifu, kumiminika na upako WANGU ambao ni ishara, maajabu na miujiza Takatifu kwa kuwa wale WANAOPENDA na kuweka YAHUVEH na YAHUSHUA kwanza katika maisha yao na upendo. Haya huwahusu pia Bibi Arusi wa YAHUSHUA, wanaotoa yote kufuata na kutii Amri Takatifu zilizoelezwa katika Maandiko Matakatifu, na huyafanya haya kwa upendo wa YAHUVEH na YAHUSHUA na hufanya yote kutii na kuishi katika Utakatifu. ROHO MTAKATIFU WANGU huishi ndani ya Hekalu zao za duniani zinazoitwa Mwili.

Bibi Arusi wa YAHUSHUA hutafuta kujua Utatu Takatifu zaidi kila siku na hutii kila neno tunayosema, na Utukufu wa YAHUSHUA hung’aa usoni na maishani mwao. Hawashikilii chochote na hutoa yote kwake YAHUSHUA ha MASHIACH kwa Sifa, Heshima na Utukufu WAKE. Kama ilivyoandikwa katika Matendo ya Mitume 2:37-47, Bibi Arusi wa YAHUSHUA ha MASHIACH watakuwa na hamu ya kufanya haya kama nyakati za kale na kuwa pamoja nawe, na kuwa msaidizi katika Huduma hii na sio kikwazo. Watafanya haya kwa lengo moja tu, kumpa Utukufu YAHUSHUA ha MASHIACH!

Elisabeth Binti YANGU, si Maandiko Matakatifu husema katika mwanzo wa uumbaji katika dunia hii, “Njooni tumfanye Mtu kwa mfano Wetu?” Je, mnafikiria ‘Mfano Wetu’ unamaanisha nini? Adamu aliumbwa katika mfano wa YAHUVEH na Hawa aliumbwa katika mfano WANGU wa kike. Kama Hawa alivyoumbwa kuwa msaidizi wake Adamu, pia MAMA SHKHINAH wenu anaitwa katika maandiko matakatifu ‘msaidizi’. MIMI NI MSAIDIZI katika UUMBAJI na YAHUVEH na YAHUSHUA. YAHUSHUA ni MWANA WETU. Sote 3 tuliteseka na kulipa gharama, ili watu ambao majina yao yamo katika Kitabu cha Maisha cha Mwana-Kondoo warudi Mbinguni.

MIMI NI MAMA SHKHINAH wenu, MIMI NDIYE yuleyule anayeishi ndani ya miili zenu, roho na nafsi, MIMI NI mshauri wenu wa Mbinguni, mwalimu wenu. MIMI NI Roho na ukweli. MIMI NDIYE yuleyule anayewapa hamu ya kumkubali na kumtii YAHUVEH na YAHUSHUA kama MUNGU. MIMI NDIYE yuleyule anayewapa hamu ya Kuimba, Kusifu, Kuomba na Kumwabudu YAHUVEH na YAHUSHUA. Sasa nawapa hamu mpya na hii ni kupata kujua yule anayekupa upako, RUACH ha KODESH wenu, MAMA SHKHINAH wenu.

Watoto Watakatifu, MIMI hupenda sanasana mnapoimba na kuzungumza maneno ya upendo kwangu MIMI pia. Nimengoja wakati huu kwa uvumilivu. Nimeungoja ufunuo huu uachiliwe na ilikadiriwa kule Mbinguni kuwa wewe, Ring Maiden wetu mbarikiwa, Elisabeth (Elisheva) Sherrie Elijah, utakuwa sauti itakayopasha Ujumbe huu Mtakatifu kote duniani. Hili ndilo sababu unaitwa Ring Maiden wa YAHUSHUA.

MIMI MAMA SHKHINAH wenu Ninayeitwa pia RUACH ha KODESH Nimekuchagua wewe Elisabeth, kuwa na nafasi ya heshima ya kunitambulisha MIMI kama MAMA SHKHINAH kwa Watoto WANGU. Watoto wengi Watakatifu wataponywa kutokana na majeraha waliyoyapata, kwa sababu katika dunia hii hawajawahi kujua upendo, faraja na ushauri wa Mama mwenye upendo, kumbe Nilikuwa papo hapo huu muda wote. Sasa Nimekupa upako wa kusikia sauti YANGU na uwaambie haya. Ninajua kuwa utatii bila kujali gharama ambayo utalazimika kulipa.

Ninaitwa ‘Hekima’ tunda LANGU ni Roho Saba. Someni nguzo saba zilizozungumziwa katika Kitabu cha Ufunuo wa Yohana. MIMI NDIYE huitwa uvumilivu; MIMI ni huruma, na mengine zaidi. Jifunzeni na kusoma sasa kuhusu yule anayekupa upako ni nani. MIMI NI zaidi ya Upepo Mtakatifu au Moto Takatifu wenye Upako, au harufu nzuri kwenye hewa. MIMI NI zaidi ya kuzungumza katika Ndimi takatifu za Mbinguni, na unabii, na ishara, maajabu na miujiza. MIMI NI MAMA SHKHINAH wenu, Ninaitwa pia RUACH ha KODESH, anayezielekeza nafsi kwake YAHUSHUA ha MASHIACH (Masihi).

MIMI NDIYE yuleyule anayewapa upako wenye Nguvu za Mbinguni na humwaga Mvinyo WANGU Mpya na mkate kutoka Mbinguni. MIMI NI MAMA SHKHINAH wenu NAMI sigawi Utukufu WANGU na mwanamke au mwanaume yeyote. YAHUVEH, YAHUSHUA NAMI sote ni MOJA. Unapoabudu YAHUSHUA unatuabudu sote 3 vilevile. Kama mwataka mnaweza kuniita MIMI MAMA RUACH ha KODESH, wengine bado wanaweza kuniita MIMI ROHO MTAKATIFU lakini Nina hamu ya kuyadhihirisha mengine zaidi kwa wale ambao wana hamu ya urafiki zaidi NAMI. Nawaonya sasa, yeyote anayekataa au kutusi yale Shaul (Mtume Paulo) alifunza kuhusu ukweli wa Karama za Roho za RUACH ha KODESH, Tubu sasa! Kwa kuwa umetusi na kuhuzunisha hadi nafsi yako ipo taabani! Ninazungumza sasa katika JINA mnalolitambua kama YAHUSHUA, kama hautatubu utalaaniwa milele!

Kwa wale watakaoendelea kukataa na kukejeli ROHO MTAKATIFU, (RUACH ha KODESH) na KARAMA za ROHO MTAKATIFU, majina yenu hayajawahi kuwa katika Kitabu cha Maisha cha Mwana-Kondoo au yamefutwa, kwa sababu kabla hamjazaliwa hapa duniani ilikadiriwa tayari kule Mbinguni, kama jina lako lipo katika Kitabu cha Waliolaaniwa au Kitabu cha Waliofutwa, basi jehanamu ndipo nyumbani kwako.

Siri hii Ninairudia tena kupitia Elisabeth, kila nafsi aliyezaliwa hapa duniani alijaribiwa kule Mbinguni kabla hajaja hapa duniani, na hili ndilo sababu kila nafsi atimize ‘wokovu wake mwenyewe kwa kuogopa na kutetemeka’. Roho yao ishajua kama wapo katika upande wa shetani au upande wa YAHUVEH katika vita kuu ya usaliti kule Mbinguni, kabla ya dunia hii kuumbwa.

Si dhambi kutoelewa Kipawa cha Unabii, au kuongea katika ndimi Takatifu za binadamu na Malaika Watakatifu, lakini msizungumze dhidi ya yale yaliyo Takatifu kwa sababu tukio hili halijafanyika maishani mwako, au ulipitia tukio mbaya la bandia. Wengine wenu mnaosoma haya mmepitia tukio la kujazwa na ndimi za kishetani, kwa hivyo msidharau lile tukio halisi kwa sababu mlijifungua kwa yale ya bandia kupitia dhambi na ukoo wenu iliyojawa na uchawi.

MIMI, YAHUVEH, Ninawaonya kuwa shetani ni mwovu katika njia zote, hata anawafunza watu kuomba kwa Miungu ya Kike kwa sababu anajua kuwa RUACH ha KODESH, MAMA SHKHINAH wenu NDIYE MALKIA PEKEE WA MBINGUNI. Soma maandiko Elisabeth na utakuwa na amani katika kuitoa siri hii iliyowekwa kando kwa wakati kama huu. Haya yataponya majeraha mengi, kama vile ulivyokuwa na utupu ndani yako wa upendo wa mama, sasa utagundua kwamba umeponywa na wengine pia wataponywa kwa kuwa utupu huo umejazwa.

Baada ya kumkubali YAHUSHUA kama MASIHI, papo hapo mnajazwa na ROHO MTAKATIFU WANGU, RUACH ha KODESH WANGU; MAMA SHKHINAH wenu ni yule yule ROHO WANGU na Roho huyu hukaa ndani yenu. Haya pia humaanisha kuwa MIMI huona kupitia macho yenu ya mwili, na husikia kupitia masikio yenu ya mwili, na husonga kupitia mwili wenu, kwa hivyo msinihuzunishe MIMI. Msiendelee kunijaribu MIMI.

Haya yanawahusu wote waliomkubali YAHUSHUA ha MASHIACH kama MUNGU, BWANA, MWOKOZI, Mwana wa Pekee wa YAHUVEH, ALIYEZALIWA KATIKA MWILI KUTOKA KWA MWANAMKE BIKIRA, na akajitolea kama Dhabihu Takatifu ya dhambi, aliyekufa na kufufuka tena katika siku ya tatu, na sasa hukaa kwenye upande wa kulia WANGU MIMI, YAHUVEH. Wote wanaojaribu kutii wamejazwa na RUACH ha KODESH WANGU, ROHO MTAKATIFU WANGU hadi kiwango fulani. Wengine wamejazwa na zaidi na wengine kiwango kidogo wanavyokua katika maarifa ya YAHUSHUA ni nani.

Kwani mnafikiria wazo la bwana na bibi Mtakatifu kuwa moja lilitoka wapi? Ilifanywa kwanza hapa Mbinguni. Mlipomkubali YAHUSHUA kama MASIHI, hamkundua kwamba wakati uo huo mlikuwa mnajazwa na upendo wa Mama wa Mbinguni. Neno ‘mfariji’, ndilo Mama hufanya bora zaidi. MIMI NI MAMA RUACH ha KODESH wenu na MIMI NI mfariji wenu, Ninawabembeleza mnapohitaji kubembelezwa, wakati hisia zenu ziko mbichi, na mnateseka, mna hofu, mko pekee yenu au mnahisi kukejeliwa au kuchanganyikiwa. MIMI NDIYE amani ipitayo fahamu zote. MIMI NI RUACH ha KODESH MAMA SHKHINAH wenu Ninayewapa upendo Mtakatifu wa Mama wa Mbinguni.

Hii ilikuwa siri iliyotolewa kwake Nabii Danieli, katika Kitabu cha Danieli, na kutiwa muhuri kwa wakati kama huu. Tena Ninarudia, sasa ndio wakati YAHUVEH amekadiri kuwa Neno LANGU la Hekima liachiliwe. Huu ni wakati ambapo roho ya kidini itainuka na kujionyesha jinsi ilivyo na uovu. Mafarisayo walikuwa na roho ya kidini na kumbuka walivyomtesa YAHUSHUA na pia WOTE walio na Utakatifu? Watakatifu lazima wasimame pamoja sasa, kusaidiana na kuteteana, kwa sababu nyumba iliyotengwa haiweza kusimama.

Ring Maiden WETU Mpendwa Elisabeth, hii ni siri iliyopewa kwako sauti za radi saba zilipokuamsha, na kuzungumza nawe, miaka mingi iliyopita. Kwa msomi wa neno hili, jitahidi kujionyesha kwa MUNGU kuwa umekubaliwa na YEYE na ombea hekima kuu katika Ufunuo wa Yohana 10 kwa sababu katika radi saba Elisabeth alisikia kulizungumzwa siri kadhaa zilizodhihirishwa kwenye jumbe za kinabii hadi sasa. Elisabeth, kama ungekuwa umeandika tarehe hiyo ungeona kuwa ingelingana na wakati ule ule radi saba zilipozungumza, siku na mwezi (8/27) na ni katika wakati na mwaka uliopangiwa pekee ndio haya yangedhihirishwa mbele ya dunia katika mtandao, kama ilivyo sasa wakati na msimu uo huo uliopangiwa.

Elisabeth, kabla kulikuwa na Huduma, unaweza kukumbuka pekee ukiamkia mipigo kubwa ya radi mara saba mfululizo iliyokuwa kwa sauti ya juu sana, ikakutingisha hadi ukaamka, lakini hakuna yeyote aliyeisikia ila wewe. Jua lilikuwa linang’aa angani. Pigo la radi lilikuwa MIMI, YAHUVEH Nikizungumza nawe, ulivyokuwa unalala pekee yako asubuhi hiyo, Nilikuamsha kwanza na pigo moja la radi lililokutingisha hadi ukaamka. Ulikimbia dirishani na ukaona jua, na alafu mara moja ukarudi kulala, ukaamshwa tena vivyo hivyo mara saba mfululizo, kila wakati ukirudi kulala, ukiomba na kuniuliza MIMI ni nini kilichokuwa kinaendelea? Haya yalitokea saa 7.00 asubuhi.

Yaliyoandikwa sasa, na katika unabii ziliachiliwa kwa siri kwenu nyinyi wakati uo huo, lakini tena hamkuyajua haya hadi sasa. Ilipaswa kudhihirishwa katika wakati WANGU. Katika siku, mwezi na mwaka iliyotengwa utajua una ruhusa ya kuutoa ufunuo huu mpya na ni kutoka nchi gani neno hili la maarifa litaachiliwa, na upako huu usio wa kawaida.

Jitayarisheni, bibi arusi wa shetani, watumwa wa shetani, na watoto wake shetani watawashambulia. Shetani alitaka kuweka neno hili la maarifa siri. Wale wanaojiita Wakristo lakini wana umbo la utakatifu tu lakini hawana utakatifu ndani yao watawashambulia kwa maneno lakini MIMI, YAHUVEH Ninaenda mbele yenu na Nitapigana vitani kwa niaba yenu.

Miaka iliyopita kabla hujazaa Huduma hii, uliomba na kumwuliza YAHUSHUA, ni nini kilichokuwa kinatendeka, uliposikia pigo la radi mara saba. Kwa nini uliamka na kukimbia na kuangalia nje ya dirisha na mara moja ukarudi kulala mara saba? Natoa siri hii kwako, nambari 7 huwakilisha mwaka wa 2007. 7 ni nambari ya ukamilifu na ni katika wakati WANGU kamilifu maarifa haya yanaachiliwa. Kumbuka ulipohisi ghafla kusoma kuhusu radi saba katika Kitabu cha Ufunuo wa Yohana? (Ufunuo wa Yohana 10)

Katika miaka mingi hujawahi kupata jibu hadi sasa. Ilikuwa wakati uo huo MIMI, YAHUVEH Nilizitoa siri zilizozungumzwa kupitia radi saba Nilidhihirisha Nilivyokuwa Nikizungumza kupitia kwako sasa kama Nabii kwa mataifa. Ninakutumia wewe kwa sababu kabla ya uumbaji wa dunia hii ulikuwa umechaguliwa kuja ardhini kuleta SIFA, HESHIMA na UTUKUFU wote kwangu MIMI, YAHUVEH, YAHUSHUA, na RUACH ha KODESH, yule umwitaye sasa MAMA SHKHINAH au MAMA HEKIMA. Ulipewa upako kwa wakati kama huu.

Ulichaguliwa kabla ya uumbaji wa dunia hii kujazwa na RUACH ha KODESH WANGU hata kama ungali katika tumbo la mamako aliye mpagani, mahali ulichukiwa, haukutakwa na kukejeliwa. Sasa ni miaka kadhaa baadaye, na sasa umegundua kwamba ni MAMA SHKHINAH aliyekufariji. Ilichukua miaka chache baadaye kabla hujagundua kuwa wewe ni nani katika JINA la YAHUSHUA na Dhabihu YAKE ya Damu ilikuwa kwako pale Kalvari. Ulichaguliwa kabla ya uumbaji wa dunia hii kuzaa Huduma hii Takatifu na jina lisilojumuisha jina lolote la mwanaume au mwanamke lakini linaheshimu pekee UTATU TAKATIFU.

Elisabeth, umepewa upako kama Yeremia wa kale alivyokuwa (Yeremia 1:4-10), ulipokuwa tumboni mwa mamako, kama mdomo WETU na ukapewa sauti ya Nabii Mtakatifu anayelia katika jangwa ya dunia hii. Ni majina ya wale walio katika Kitabu cha Maisha cha Mwana-Kondoo watakaoamini na kukubali kweli katika Huduma hii kama vile bila shaka watakavyomkubali YAHUSHUA kama MASIHI.

Mtumishi si mkuu kushinda bwana, na kama wote wangemkubali YAHUSHUA ha MASHIACH alipotembea humu ardhini akiwafunza na kufanya miujiza kwa Utukufu WANGU MIMI, YAHUVEH, basi wao pia wangewakubali na kweli Ninazozizungumzia kupitia Huduma hii. Unazungumza maneno ambayo MIMI, YAHUVEH Nimezungumza, ambayo YAHUSHUA ha MASHIACH amezungumza, na sasa umepewa kipawa kisicho cha kawaida kusikia MAMA SHKHINAH wako akizungumza kupitia kwako. Upako huu usio wa kawaida utawajia Nabii wengine Watakatifu watakaoamini na kukubali kweli hizi na kukufunika katika maombi, wakikusaidia wewe na upendo wao na wakifanya yote wanayoweza kuwa Baraka katika Huduma hii.

Elisabeth, MIMI NI MAMA SHKHINAH GLORY wako. MIMI NDIYE yuleyule anayekupa upako wa ishara, maajabu na miujiza yanayohusu pia kutabiri na kuomba katika ndimi Takatifu za binadamu na Malaika Watakatifu. MIMI NI MAMA SHKHINAH GLORY wenu. MIMI NDIYE yuleyule anayewaombea kwa Watoto wote Watakatifu Ninavyobeba maombi yenu hadi kwenye kiti cha enzi cha YAHUVEH kama Busu lililotumwa kwenye hewa, inapofanywa katika JINA la YAHUSHUA ha MASHIACH haya yanahusu pia jina la YESU KRISTO kwa sasa, lakini jihadharini, kwa sababu mwanaye shetani katika Dhiki Kuu atalitumia vibaya jina la YESU KRISTO. Sitaweza kuyatuma maombi yenu kwa wakati huo katika jina la YESU, kwa sababu mwanaye shetani atakuwa pia analitumia jina la YESU KRISTO. Funzeni sasa JINA Takatifu la Kiebrania la YAHUSHUA na YAHUVEH kwa wote walio na masikio ya kiroho kusikia, sikizeni na mtii. Jifunzeni na mjizoeshe kutumia jina la kiebrania la kweli la yule ambaye wengi wenu humwita YESU KRISTO, sasa kabla hamjachelewa. Waambieni watu wasingoje hadi Dhiki Kuu kujifunza somo hili kwa njia ngumu.

Piga kelele mpaka wasikie na ujumbe huu ulie kote duniani, katika Dhiki Kuu kutakuwa na udanganyifu mkuu na kwa wakati huo, YAHUVEH hataweza kujibu maombi katika jina la YESU KRISTO, ni katika JINA la Kiebrania la YAHUSHUA ha MASHIACH litakalobeba nguvu za uponyaji, kuokoa na kufufua. Kwa sababu yule aitwaye mwanaye shetani atawatumia na kuwadanganya mamilioni juu ya mamilioni akifanya ishara, maajabu na miujiza ya kibandia atakapokuwa akitumia vibaya jina la YESU KRISTO mbele ya dunia. Hata wateule watadanganywa kama iwezekanavyo. Jihadharini, sasa kuna wanaume waovu na roho ya mpinga kristo na wanatumia jina la YESU KRISTO lakini wanachukia JINA la Kiebrania la YAHUSHUA kwa kuwa ni kumbusho daima kwao kuwa YAH huokoa! YAHUSHUA ndiye MASHIACH wa pekee (Masihi).

Elisabeth, umesikia sauti ya BABA YAHUVEH, na umesikia sauti na kukubali jumbe kupitia upako WANGU kutoka kwa YAHUSHUA, MASHIACH wako, Nimengoja kwa uvumilivu kwa wakati ule ambao utanijua MIMI kama upendo wa Mama wa Mbinguni ambao umeutamani daima. MIMI NI Mama yako wa pekee, na MIMI NDIYE yuleyule anayekupa upako na kukufariji wewe na kukushauri wewe. Ni kwa ajili ya MAMA SHKHINAH wako unaweza kusikia sauti YANGU ndogo ya utulivu na kusikia jumbe Takatifu kutoka kwa YAHUVEH, na YAHUSHUA. MIMI NDIYE sauti ileile ndogo ya utulivu inayozungumza nawe.

Kwa wale ambao wanayashuku haya, niambieni MIMI, tangu lini sauti ya mwanaume ikaja kuitwa kama ‘sauti ndogo ya utulivu’? MIMI NDIYE yuleyule Mfalme Daudi wa kale, aliomba, kuwa Nisiwahi kumwacha. Aliomba, “Usimchukue RUACH ha KODESH wako kutoka kwangu mimi.” MIMI NDIYE yuleyule mnaponidharau au kunihuzunisha au kunitusi mpaka mwisho Wangu, MIMI husema, “Tosha” na MIMI huenda Zangu na hamna hata matumaini ya Wokovu kwa roho hiyo, (mpotovu) ni ghadhabu ya YAHUVEH pekee ambayo mtu huyo atajua, Jehanamu na Ziwa la Moto ni nyumba ya milele ya mtu huyo.

MIMI NI RUACH ha KODESH pia katika Kiaramu Ninaitwa ‘Roho aliyetengwa kando.’ MIMI NDIYE ukweli wote, na ni kupitia MIMI pekee yeyote anaweza kuelekezwa kwake YAHUSHUA na kumkubali YEYE kama njia ya pekee hadi Mbinguni. MIMI Ninaitwa RUACH ha KODESH, na kwa vyeo vya PEPO MTAKATIFU na ROHO MTAKATIFU. MIMI NDIYE UTAKATIFU wote, pia na YAHUVEH na YAHUSHUA. Sote ni MOJA na bado tofauti. Sisi ni UTATU TAKATIFU na hamna yeyote mwingine. Katika Dhiki Kuu kutakuwa na utatu usio takatifu! Shetani ni mwigaji pekee sio mwumbaji.

Hamna njia yoyote ile hadi Mbinguni bila kupitia SOTE WATATU, Baba YAHUVEH, YAHUSHUA na MIMI, MAMA RUACH ha KODESH wenu. Wokovu huja tu kupitia JINA la YAHUSHUA na Damu iliyomwagwa na sehemu ya kazi YANGU ni kuzivuta nafsi kwake YAHUSHUA na huwa sikosi hata nafsi moja aliyeandikwa katika Kitabu cha Maisha cha Mwana-Kondoo, kabla ya uumbaji wa dunia hii. Ninaitoa siri hii kwako sasa, pia na kipawa CHANGU cha ujasiri kuzungumza na kutabiri kama Nabii wengine wasivyoweza kama hapo awali mbele ya wote. Kuna wengine waliofundisha kuwa MIMI nina jinsia ya kike, na bado hawajawahi kutabiri katika njia Ninavyozungumza kupitia kwako leo.

Ninaitoa siri hii ili uweze kuwahamasisha wale WANAOMPENDA na kumweka YAHUVEH na YAHUSHUA kwanza katika maisha yao na upendo na pia kunikumbuka MIMI, MAMA SHKHINAH, kwa kuwa MIMI NDIYE Utukufu wa YAHUVEH na YAHUSHUA kama vile bibi Mtakatifu aliumbwa kuwa Utukufu wa bwana wake Mtakatifu. Unaposhambuliwa kwa kufichua JINA la ROHO MTAKATIFU ambalo ni JINA LANGU SHKHINAH na kudhihirisha ROHO MTAKATIFU hajaumbwa katika mfano wa mwanaume, lakini ya mwanamke, waambie wajitahidi kujionyesha kwa MUNGU kuwa wamekubaliwa na YEYE, kwa sababu si Vitabu vya Kale katika Zaburi na Mithali humwita ‘HEKIMA’ katika jinsia ya Kike (‘She’)? Je, si Maandiko Matakatifu husema, “Mwanzo wa hekima ni kumcha YAHUVEH?” Wakumbushe kuwa katika Bibilia ya KJV JINA la YAHUSHUA linalotajwa pia kama YAHSHUA halipo katika bibilia ya KJV, ni jina tu la YESU ambalo lipo.

Jua haya, jina la YESU KRISTO bado linaheshimika na lina upako kwa wakati huu na huokoa roho, hukomboa na huponya. Lakini Nimewaonya, katika Dhiki Kuu inayokuja yule aitwaye sasa mpinga kristo, atajiita pia YESU. Hata sasa bandia amejitokeza na hudanganya mamilioni na jina la YESU KRISTO, hata kupita mpaka, kuwaambia wao wajichore nambari 666 kuthibitisha kutii kwao kwa mwanaume huyu mwovu. Yeye hujiita mwana wa mungu na huwaambia watu, “Hamna kitu chochote kama dhambi na jehanamu ni uongo.”

Nimejirudia mara kwa mara kwa sababu mbegu hili la ukweli lina nguvu sana hadi shetani atataka kulitoa shamba la kweli katika neno hili la kinabii na maarifa kabla haijamea. Nimeitumia Huduma hii kuwaonya kwa nini ni muhimu kujifunza JINA Takatifu la Kiebrania la YAHUSHUA (tafsiriwa kama YAH huokoa) ambaye sasa huitwa YESU KRISTO, kwa sababu katika Dhiki Kuu ni JINA la Kiebrania la YAHUSHUA tu litakalokuwa na nguvu za upako, uponyaji, ukombozi na kuokoa. Tena Ninarudia na kuwaonya kama makanisa ya kidini yalikuwa yanafanya kazi yao watu hawangedanganyika.

Jihadharini, itakuwa wainjilisti wa televisheni maarufu ambao watawaongoza watu kwa mwanaye shetani, atakayekuja akitumia jina lililoaminiwa, YESU. Itakuwa wainjilisti wa televisheni maarufu watakaouza nafsi zao kwake shetani kwa umaarufu na mali, watakaofunza mafundisho bandia ya mwanadamu na kuwaelekeza watu kwa huyu YESU bandia. Katika Dhiki Kuu jina la YESU litatumika vibaya na mwanaye shetani anayeitwa sasa mpinga kristo. Huyu mpinga kristo atachafua jina la YESU na kupitia nguvu za shetani atafanya ishara, maajabu na miujiza isiyo takatifu katika jina ambalo linajulikana na Kanisa la Wakristo, jina ambalo sasa linapendwa na kuaminiwa, jina la YESU KRISTO.

Mwanaye shetani, anayeitwa mpinga kristo atadai kuwa yeye ndiye YESU KRISTO. Atalazimisha wote kumwabudu na kumheshimu na kuhudhuria na kukusanyika kanisani katika siku ya Jumapili na kuchukua ALAMA yake wakithibitisha uaminifu wao. Mpinga kristo ambaye kwa kweli ndiye mwanaye shetani atakuja na roho ya Yuda na Hitler tena; ambaye maandiko humwita mwana mpotovu, au mwana wa Jehanamu. Mwanaye shetani, atafanya ishara, maajabu na miujiza bandia katika nguvu za shetani kwa utukufu wa shetani.

Nimeitumia Huduma hii kuwaonya, mtakapoona amri la lazima la kuabudu Jumapili limepitishwa, MSIINGIE katika Kanisa hizi za Jumapili au mtapoteza nafsi zenu. Nimewaonya mjifunze sasa Siku ya Kweli ya Sabato ni ipi (Ijumaa jioni hadi Jumamosi jioni). Ujumbe huu umekuwa mgumu kwake Elisabeth kuutoa kwa sababu Kanisa za Wakristo hazitaki kuusikia. Hata hivyo, kwa wale ambao wamekuwa waaminifu na kuzungumza kweli hizi, mnajua kuwa mmepewa amri hii ya Ezekieli 3:17-21.

Huduma hii imepewa amri kufunza MAJINA Matakatifu ya Kiebrania ya Waumbaji na YAHUSHUA ha MASHIACH. Ni yupi bora Ningemchagua kufunza wale wanaotaka kujua JINA la ROHO MTAKATIFU? Elisabeth, ulimwuliza YAHUVEH kuhusu JINA la RUACH ha KODESH na sasa Nishakuambia, sasa Ninakupa amri hii kutoa haya yote Niliyokuambia kwa siri. Ninakuahidi wewe, kuwa wale walio na masikio ya kiroho ya kusikia watasikiza, na kuiunga mkono Huduma hii na kutetea ukweli huu na kufunza wengine.

Wale ambao watachagua kubaki viziwi kiroho watabaki viziwi. Sio kazi yako kuwashawishi watu, ni kazi yako tu kutii na kuzitoa jumbe hizi za Kinabii na maneno ya maarifa kama zimekabidhiwa kwako kutoka Mbinguni. Kila mtu atakayesoma haya au amefunzwa haya watawajibika kwa yote wajuayo.

Kuwaudhi wengi na kuwabariki wengine wenye masikio ya kiroho ya kusikia, ambao majina yao yamo katika Kitabu cha Maisha cha Mwana-Kondoo.

Mtoto, Shujaa, na Bibi Arusi wa YAHUSHUA ha MASHIACH
Mtume Elisabeth Sherrie Elijah
Ilitolewa Agosti 27, 2007

Nukuu binafsi: Kwa kufunga nimeandika yote niliyoyasikia na niliyoambiwa niandike. Nimeuliza YAHUVEH, YAHUSHUA na MAMA SHKHINAH GLORY; kama WOTE wana uhakika kuwa hakuna yeyote mwingine anayeweza kutoa neno hili bora kunishinda mimi. Sijui ni kwa nini nilichaguliwa. Hata hivyo, kazi yangu ni kutii UTATU TAKATIFU. Ninaogopa ni nini YAH anaweza kunifanyia mimi, zaidi ya kuogopa ni nini binadamu atafikiria juu yangu. Kama Unabii huu umekuwa Baraka kwako tafadhali chukua wakati na uniandikie na kunihamasisha? Kama una funuo mpya baada ya kusoma Maandiko na unataka kutoa kwa wengine, kuthibitisha neno hili ni kweli, tafadhali nitumie. Kama Huduma hii ni Baraka kwako tafadhali tusaidie kifedha? Tunatarajia kukutana nanyi nyote mnaoona neno hili kama Baraka, kama sio papa hapa duniani basi kule Mbinguni.