Unabii 7

SHIKILIENI KWENYE UPINDO WA VAZI LANGU!

Ilipewa kwake Mtume Sherrie Elijah


* * * * * * *

Upindo wa vazi LANGU, haitoshi kamwe kuushika tu. Endeleeni kubisha kwenye mlango WANGU, alafu jibu itakapokosa kuja haraka, gongeni. Mtakapochoka, endeleeni kuuliza, kutafuta, na mtapata, lakini msikome hadi msikie kutoka Mbinguni.

Kwa kuwa Nimewaahidi, watoto WANGU, mkate na sio makombo ya dunia hii. Kwa kuwa mnaona hukumu imekuja kwenye nyumba ya YAHUVEH na sio rahisi kama kushika upindo WANGU, au kubisha kwa upole kwa majibu yenu, lazima mjitayarishe, inaweza kuchukua vita kupata Baraka zenu, kama Yakobo. Lakini inathibitisha imani yenu na inawafanya muwe na nguvu zaidi, inayotakikana katika nyakati hizi za mwisho. Kwa hivyo endeleeni kusema hatutaki makombo tena. Hamtakataliwa. Kwa kuwa nyinyi ni Bibi Arusi wa YAHUSHUA walionunuliwa na Damu.

Nitawajibu na kuwakomboa. MIMI sidanganyi. Kwa kuwa mmeahidiwa sio makombo ya dunia hii, lakini Mkate wa Maisha, mkate wa uponyaji wa watoto, wa ukombozi, wa mafanikio, maisha kwa wingi na yaliyojawa na utukufu. Kwa kuwa YAHUSHUA ha MASHIACH ni mkate wa maisha yenu na Ninataka kuona kama bado mtanisifu MIMI, na kushikilia imani yenu hata kama sitajibu saa iyo hiyo. MIMI daima sio MUNGU wa microwave. Ndio, Ninajua kuhusu microwave, je, mnadhani ni nani aliyewapa uvumbuzi huu?

Mnayo maandiko ya kusimamia, someni Mathayo 15:22-28 kuhusu imani ya mwanamke Mkananayo. Alikuwa anamwabudu YAHUSHUA, lakini YEYE alimpuuza, aliacha wanafunzi wake wamkemee, wakamwita mbwa, wakasema Baraka hii ilikuwa ya mtu mwingine sio yeye. Mnasema, “Kwa nini YAHUSHUA, mbona uliyafanya haya yote?” Kwa sababu katika siku hizi za mwisho, haya yote yatafanyika kwa wanafunzi WANGU waaminifu, haya yatafanywa na wengine katika JINA LANGU.

Mtatusiwa, kukataliwa, kuteswa, lakini mkiendelea kushikilia imani yenu, hata kama sitawaokoa saa iyo hiyo, basi kama mwanamke huyu mkananayo mtatuzwa. Kwa kuwa Nitaona jinsi imani yako ilivyo kuu. Kwa kuwa katika nyakati hizi za mwisho Ninawatayarisha Mwili WANGU katika njia hii, Nitakapokuja tena ni wangapi ambao watakuwa wameshikilia imani yao? Ni wangapi watakaogeuka watakapolia kwa maombi kwa hitaji fulani na Nisiwajibu papo hapo?

Lazima uwaeleze kuwa wanafaa kuwa tayari kupigana NAMI kwa Baraka zao kama Yakobo alivyofanya. Kwa kuwa Nina hamu ya kuwabariki. Ninataka tu kuwajaribu na kuona jinsi mnavyotaka Baraka hii. Je, bado mtaniabudu MIMI kama sitawajibu saa iyo hiyo? Sio adhabu YANGU inayosababisha haya, kwa kuwa mwanamke huyo alianguka na kuabudu kwenye miguu YANGU. NYOTE mnaabudu miguuni MWANGU. Lakini hukumu imeanza katika nyumba ya YAHUVEH na moja ya vitu Ninavyovijaribu sasa ni jinsi imani yenu ilivyo na nguvu?

Je, Nyinyi ni waaminifu, na mtanitegemea MIMI? Kama yule mwanamke Mkananayo, imani yenu na uaminifu wenu utatuzwa kwa kuwa mtaona mnachotamani, na tena zaidi sana na kwa wingi zaidi Nitawamwagia Baraka ZANGU kama ziwa lililofurika. Mtakuwa na furaha tele na Nitawabariki sana mtalazimishwa kuwapa wengine. Shikilieni kwenye upindo wa vazi LANGU. Msiuachilie. Endeleeni kubisha hadi mlango ufunguke kwa Baraka mlizoziulizia. Nitawajibu hatimaye. Msizitegemee akili zenu wenyewe, lakini katika njia zenu zote mnikiri MIMI,

NAMI Nitayanyoosha mapito yenu

Kumbukeni majaribio ya imani yenu ambayo ni ya thamani kushinda dhahabu. Wekeni macho yenu kwa Mwokozi wenu na sio kwenye vurugu la bara wala mawimbi yatakayowazamisha. Lakini Nipo hapa kuwaokoa nyinyi. Kwa kuwa MIMI ni Mwokozi wenu na mkombozi au sio? Sitawafeli wala kuwaacha. Ninajua shinikizo linalohitajika kuwekwa kwenye udongo kabla haujavunjika, moto Nitakayowaruhusu mpitie kabla hamjaangamizwa. Mawimbi ya kukata tamaa hayatawazamisha. Kwa kuwa sipo hapa tu kuokoa na kukomboa nafsi zenu, lakini pia akili, mwili na Roho. Niamini MIMI na mtayaona haya yakitendeka. Alafu kumbukeni ni nani aliyewakomboa, sio mwanaume wala mwanamke, bali MUNGU wenu aliyewaumba.

Lakini bado ni MIMI Nitakayejibu kilio chenu, kwa kuwa Ninajua ni nini mnachotaka hata kabla hamjauliza. Katika ulimwengu wa kiroho imemalizika, lakini inangoja wakati WANGU kamili kudhihirika katika ulimwengu wa kimwili. Imani yenu husaidia haya kuja. Si Neno LANGU husema, ni vigumu zaidi kumpendeza YAHUVEH bila imani? Mnanipendeza MIMI kwa kuonyesha imani yenu katika MUNGU anayewajali na kuwasikia na hujua yote.

Nyinyi huonyesha imani yenu mnapogundua kuwa hamwezi kujikomboa wenyewe, bali mnanihitaji MIMI, Mwokozi wenu kuwakomboa, na Nitafanya vivyo hivyo. Si MIMI NDIYE Bwana na Mwokozi wenu? MUNGU mnayemwabudu ni kiziwi? Hapana. Mkono WANGU ni mfupi usioweza kuwakomboa? Hapana. Imani yenu inajaribiwa? Ndio. Je, Nina hamu ya kuwabariki? Ndio. Mtakuwa kati ya wale watakaoshikilia kwenye upindo wa vazi LANGU, na huendelea kubisha? Je, mtakuwa mmoja ya wale watakaosimama na kungoja ukombozi WANGU na Baraka Nilizowaahidi? Ni chaguo lako. Nimezungumza siku hii kupitia huyu Handmaiden, ili mtaelewa kwa nini vitu vingine vilivyoahidiwa havijatendeka bado. Endeleeni kushikilia kwenye kipimo cha imani yenu Niliyowapa na ukombozi wenu utakuja hatimaye.

* * * * * * *


Ilipewa kwake Nabii Sherrie Elijah

Huu ndio Unabii mpya uliopewa kwangu kupasha na kuwalisha Kondoo wa YAHUVEH. Shikilieni kwenye upindo wa vazi lake. Ingawa nywele zangu ndefu nyeupe (blonde) zipo sakafuni katika uchafu anapopita kwenye umati, uso wangu unaangalia juu kwake, na sitamwachilia. Mnapopitia haya na nilifaa kusoma haya nilipoyasoma, kuyapokea ili niweze kuyapasha kwa wengine wanaotaka kujua ni kwa nini maombi yao hayajibiwi haraka.

YAHUVEH ni kiziwi? Hapana. Mkono wake ni mfupi kutufikia sisi? Hapana. Kama YAHUSHUA alivyosema, imani yetu inajaribiwa, sio jambo zuri au vipi? Lakini ni muhimu ili ikue. Mimi sasa hivi ni kama Yakobo anayepigana na MUNGU hadi anibariki na ukombozi alioniahidi. Lakini nimesimama papa hapa na kumwambia Bwana wangu YAHUSHUA kuwa sitakataliwa kwa kuwa ameniahidi hakuna makombo tena. Dunia hutupa makombo, lakini tumeahidiwa mkate wa maisha, mkate wa uponyaji wa watoto, wa ukombozi na mafanikio. Tumeahidiwa maisha na maisha kwa wingi zaidi. Mikono yangu imeumia kwa kugonga. Macho yangu ni hafifu kwa kulia. Lakini lazima tujikaze na kusonga mbele. YAHUSHUA atakaporudi atawapata wangapi bado wapo katika imani? Ninataka kuhesabiwa katika nambari hiyo, wewe je?

Katika Bwana, utumishi wake Mwokozi YAHUSHUA ha MASHIACH, chombo cha udongo kilichovunjika, mchungaji Sherrie Elijah. Kama bado haujajaribiwa na ombi uliyongoja kwa muda mrefu na haujaona ikija kutendeka, (Nimengoja miaka 21) basi hautaelewa ni nini ninachosema. Lakini nimetumwa kwa wale ambao hawajapata maombi yao kutimizwa katika ulimwengu wa kimwili, ingawa iliahidiwa katika ulimwengu wa kiroho. Ndivyo kwa sababu katika nyakati hizi za mwisho hata YAHUSHUA alisema, “Atapata imani atakaporudi?” Lazima niwaonye watu. Sasa lazima mwaonye watu. Ili waelewe na wasikate tamaa kwake YAHUSHUA na kukimbilia dunia kwa majibu au kukimbilia roho ya mpinga-kristo.