UNABII WA 79
MIMI, YAHUVEH, NAWAMBIENI, “WATU MNAKOSA MWELEKEO!”
(I, YAHUVEH, SAY, PEOPLE YOU ARE MISSING THE POINT)
Imeandikwa/Imezungumzwa katika upako wa RUACH ha KODESH
(ROHO MTAKATIFU) kupitia Mtume Elisabeth Sherrie Elijah Nikomia.
Agosti 2, 2005
* * * * * * *
Kama huwezi kunitii sasa na kama unaichukulia kimsaha siku nilioutenga kuwa Sabato Yangu Takatifu na kama hufikirii ni muhimu kutii kila Amri Yangu, ni nini inaokufanya kufikiri ya kwamba utanitii katika Dhiki Kuu inayokuja?
Kwa nini ni rahisi kusikia maadili ya kibinadamu wanapoigeuza maneno yangu ili kuilinganisha na hali yao ya dhambi? Hata ingawa Mwanangu YAHUSHUA ni pumziko wenu YEYE si siku yenu ya mapumziko. Mwananagu YAHUSHUA sio siku na Amri Yangu ya nne inataja wazi kuizingatia kwa utakatifu Sabato yangu ya mapumziko. Ni ipi katika hizi usipoifahamu? Ndiyo, pumzika katika YAHUSHUA kwa kuwa nira Yake ni laini na mzigo Wake ni nyepesi lakini haina uhusiano na Siku ya Sabato. Je YAHUSHUA hakuizingatia Sabato?
Je, sikumtuma mwanagu YAHUSHUA awe mfano kwenu? Je, mnafahamu kwa nini niliitenga siku ya mapumziko? [ Mwanzo 2:1-3]
Je, hamfahamu ya kuwa Siku hii ya Sabato inapaswa kuwa baraka kwenu na wala si laana? Amri Yangu ya nne inasema wazi Siku Yangu ya Sabato izingatiwe kwa Utakatifu. Je, sheria nilioandika kwenye kidonge cha jiwe kwa kidole changu kingaacho na kumkabidhi Musa katika mlima wa Sinai haisemi “ Huiheshimu Siku Yangu ya Sabato na kuiweka Takatifu?” Tena nawaulizeni ninyi, tangu lini Mwanangu YAHUSHUA ni Siku? Jiulizeni, kwa nini shetani alibadilisha siku ya Sabato iwe Jumapili kama sio itumike kwa ajili ya matakwa yake katika Dhiki Kuu?
Msiwasikilize wale wanaohubiri kinyume. Hapa ndipo ushindi upo. Imeandikwa katika Andiko Langu Takatifu ya kuwa MIMI, YAHUVEH
sisemi uongo. Mkinitii kuna baraka na ushindi kama inavyotajwa katika Kumbukumbu la Torati 28. Kuna laana kwa wale wasiotii. Usome na uzingatie yaliyoandikwa katika Kutoka 31:12-17. Sabato ya kweli ni ISHARA kati YANGU, YAHUVEH na Watu Wangu na itatumiwa kutambua ni nani anayeniabudu kwa kweli na nani atanitumikia MIMI katika Dhiki Kuu. Je, utaniabudu MIMI, YAHUVEH na YAHUSHUA katika Sabato ya Kweli Ijumaa Jioni hadi Jumamosi Jioni? Ama katika Dhiki Kuu utamtumikia na kumwabudu shetani katika Siku ya Jumapili?
Kama huzingatii Sabato Yangu Takatifu sasa, Ni nini inayokufanya ufikirie ya kuwa utaizingatia baadaye, katika Dhiki Kuu ambayo imekaribia mno. Hiyo ndiyo sababu sasa ninaongea kupitia huyu Mjakazi Wangu Atangazae ambaye ametawazwa kuwa nabii kwa mataifa ili onyo hii iweze kuenea ulimwenguni kote. Je, hujui kwamba wale wanaofundisha ya kuwa haiwezekani kuwa mtiifu na takatifu kwangu utengeneza visababu kwa ajili ya dhambi zao?
MIMI, YAHUVEH, NAWAMBIENI, “WATU MNAKOSA MWELEKEO!”
Hii haiko wazi kujadiliwa. Mtatenda yale MIMI YAHUVEH ninasema, ama katika wakati wa Dhiki Kuu mtalipa kwa roho zenu. Wale ambao wameinuka nakusema “ Nitakuwa hakimu wa Elizabeth, nitakuwa mwenye kumhukumu” tubuni sasa ama utaniona na nitakwambia, “Ondoka Kwangu wewe mtenda dhambi,” kwa kuwa MIMI ni YAHUVEH na sihusiki katika majadiliano yoyote. MIMI pekee ndiye Jaji, MIMI pekee ndiye hakimu. MIMI pekee ndiye mwamuzi.
Haya siyo maneno ya Elisabeth. Ninyi wahubiri na manabii wa uongo wa kutotii sheria, mnamshambulia; mnamsemea uongo kwa sababu ya Torati nilioandika kwa kidole changu. Mnafundisha kondoo Wangu na mwana kondoo Wangu ya kuwa MIMI sijali mtu akitenda dhambi. Okoka leo, kwa kuwa MIMI si MUNGU YAHUVEH ambaye amebadilika kwa vyovyote vile. Ninyi, mnaohukumu Elisabeth, toeni boriti katika macho yenu kabla hamjajaribu kukitoa kibanzi kutoka macho ya mtu mwingine. Mko wachafu katika dhambi, mko wachafu katika kutotii, mko wachafu katika kuvunja sheria na mko wachafu katika kiburi. Angukeni katika nyuzo zenu mbele YANGU, kwa kuwa MIMI Ndiye YAHUVEH niliyekuumba, MIMI wa Milele. Mnatubutu kumlaumu MWANANGU YAHUSHUA kama kisingizio kwa ajili ya dhambi zenu, mnatubutu kuikanyagia miguuni mwenu Damu yake, mkitoa visingizio kwa ajili ya dhambi zenu.
Angukeni katika nyuzo zenu kabla haijaenda mbali na isipatikane njia ya kurudi KWANGU. Msimhuzunishe RUACH ha KODESH (ROHO MTAKATIFU) WANGU. Mwanangu YAHUSHUA hakuja kubadilisha Sheria Zangu; Mwanangu YAHUSHUA alikuja kuikamilisha Sheria Zangu. Muwe na shukrani kwa kuwa siwaulizi mzifuate amri 613. Ninatarajia mzingatie amri kumi na mnarusha mkono juu na kusema, “Hayo ni mingi mno kwangu.” Mnaona ni heri msikilize mwanadamu anayeziandika tena Amri Zangu. Anawaambieni ya kuwa kuwaua watoto wachanga katika tumbo ya mama yao si dhambi. Wanahalalisha utoaji wa mimba. Wahubiri wanafundisha katika makanisa yenu, “Msiseme kinyume cha sheria hii.” Makanisa ya kidini wanaokutana siku ya Jumapili wamechukua hongo kutoka kwa serikali za ulimwengu huu; wameichukua roho ya uoga na kuivaa kama nguo. Wako wapi Wahudumu Wangu watakatifu wasiojichanganya na bado wanaongea kinyume dhidi ya dhambi? Amri zenu za kibinadamu huhalalisha yale niliyosema ni machukizo. Wanaita ndoa ya jinsia moja. Hata katika siku za Sodoma na Komora haikuweko dhambi kama hizi hataingawa machukizo za ushoga ilinawiri lakini hawakuita ndoa.
Msiamini uongo unaofundisha "Ukiokoka mara moja utakaa mwokovu kila mara." Msiamini ya kuwa kwa sababu YAHUSHUA alilipa deni katika Kalvari, sasa haijalishi hata ukitenda dhambi, ya kwamba unaweza kuninginia karibu iwezekanavyo na kilele cha Jehanamu mbali upendavyo kwa sababu ulisema ombi la kuokoka. Unafikiri huwezi kuweka matendo katika hilo ombi na bado unahakikishwa milango ya Mbinguni. Mbali nami enyi watendao maovu. Sitaki kusikia visingizio vyenu tena. Mueni Takatifu ama nitawaambia, “Watendao maovu, sikuwajua kamwe.”
MIMI, YAHUVEH, NAWAMBIENI, “WATU MNAKOSA MWELEKEO!”
Mnawasikiliza watu hawa sasa na mnaketi makanisani mwenu mkiamini uongo kwamba Jumapili ni Sabato ama haijalishi ni siku gani ni Sabato. Mnaamini uongo unaofundishwa na Wahubiri na Rabbi ya kuwa hakuna upako kubwa katika Majina Matakatifu ya Kihebrania wa YAHUVEH na YAHUSHUA na RUACH ha KODESH, kwamba jina lolote lafaa. Wahubiri wanawaambia si muhimu kujifundisha Uyahudi wa MASIHI. Wanasema kama wewe si Myahudi haikuhusu. Wahubiri hawa waovu wanawafundisha kwamba wewe ni wa mataifa na hupaswi kuitii sheria iliyopewa Wana wa Israeli. Je, mlisahau ya kuwa mlipomkubali Mwanangu YAHUSHUA kama Masihi mlikuwa mmoja NAYE? (Warumi 11:16-21)
Mnashangaa, “iwapi nguvu ya upako wa kanisa la mwanzo iliyokuwa na ishara, kustaajabisha na miujiza?” Mnalia, “yako wapi matukio ya kimiujiza kama siku za hapo awali?” Rudini na mfanye yale kanisa la kwanza lilikuwa likifanya na mtayaona miujiza hayo tena. Kwa wale wasiokuwa na habari zaidi, nawaambieni mnatakiwa kutoa hesabu kwa yale tu umeyajua. Mnatakikana sasa kuwafundisha wengine ukweli haya. Lakini kwa wale wanaoijua ukweli na kutenda maovu, mtalipa kwa roho zenu.
MIMI, YAHUVEH, NAWAMBIENI, “WATU MNAKOSA MWELEKEO!”
Mnawatii sasa hawa viongozi waovu wa kiroho ambao wanatoa visingizio kwa ajili ya dhambi. Nini inaokufanya ufikiri ya kuwa katika Dhiki Kuu hautafanya hivyo tena na Mwana na Shetani? Nimewaambieni kupitia kwa unabii niliyoitoa kupitia Elisabeth ya kwamba Mwanangu YAHUSHUA yuaja kwa ajili ya Bibi arusi wake katika Rosh ha Shanah na itakuwa katika siku ya Sabato. Kama hufundishwi jinsi ya kuzingatia Sabato Yangu na Siku Zangu Takatifu, na kujifunza Majina Yetu Takatifu (angalia “kwa nini tunatumia Majina Ya Utakatifu”) na Torati Yangu kuitii, je, utajuaje jinsi ya kuheshimu Mimi na Mwanangu YAHUSHUA kama vile nivyoamuru. Utajuaje ni siku gani bila kujifunza na kujionyesha kwamba umekubaliwa ya kuwa Mimi, YAHUVEH, nimeitenganisha kuwa ni Sabato Yangu, Je, utakuaje tayari wakati YAHUSHUA atakaporudi?
MIMI, YAHUVEH, NAWAMBIENI, “WATU MNAKOSA MWELEKEO!”
Kama hamheshimu na kuzingatia Siku Zangu za Sherehe, je, mtajuaje Rosh Hashanah ni nini na inasheherekewa wakati gani? Na utakapoachwa nyuma utauliza “kwa nini?” Kwa hivyo ninaongea kupitia kwa Mjakazi Wangu Atangazae na kuwajulisheni kabla ya wakati wake ya kwamba Mimi, YAHUVEH ninatabiri kupitia kwa huyu Mjakazi Wangu Atangazae ambaye ni mmoja wa Bibi arusi wa Mwanangu YAHUSHUA.
Bibi arusi wa YAHUSHUA hawatabadilishwa tu na kupewa miili ya utukufu na kujazwa upako kana kwamba YAHUSHUA mwenyewe alikuwa anatembea ndani mwao, na pamoja nao, atawajaza upako ambao kwao hakutakuwa na jambo lisilowezekana. Na kwa siku arobaini Bibi arusi wa Mwanangu YAHUSHUA watapeana onyo, “Msichukue Alama ya Mnyama”. Watawaendea wale ninaowaita Wageni na wale ambao majina yao yako katika kitabu cha Uzima wa Mwana kondoo na watawaambia, “Msiwe wasiotii, na msiwe wakujichanganya hata ingawa mnaweza kupoteza maisha yenu ya kidunia.”
Tazama, ninamtumia Mjakazi Wangu Atangazae sasa, hata bila mwili wake wa utukufu, kama sauti iliayo ikitoa onyo mapema. Kwa kuwa nimemwita awe nabii kwa mataifa. Msichukue Alama ya Mnyama! Uabudu wa Jumapili na Alama ya Mnyama ina uhusiano. Jihadhari, utapoteza roho yako ukizingatia amri ya Kuabudu Jumapili katika Dhiki Kuu. Nitahitajika kuomba msamaha Sodoma na Komora niliyoharibu kwa moto na kiberiti nikiajilia vichukizo hivi viendelee zaidi vile vilivyo. Sitaomba msamaha Sodoma na Komora. Nitayaharibu na kukomesha yale yote Mimi, YAHUVEH ninayapuuza.
Hawa wahubiri wa uongo wanatoa visingizio kwa ajili ya dhambi na mmewasikiliza. Mnakuja kwa hii huduma kwa ajili ya chakula chenu cha kiroho, kuonja upako, kunywa maziwa ya kiroho na kula nyama ya kiroho, halafu ni wangapi kati yenu wanajichanganya na kwenda kwa Makanisa ya Jumapili. Mnaangukia miguuni mwa wachungaji wenu kwa uaminifu na hapo ndipo mnapeana fungu lenu la kumi na sadaka. Hamwezi kupata njia zote mbili. Mnapazwa kuamua ni siku gani niliyoamuru kuwa Sabato, kama nilivyoamuru ni siku ipi ni Sabato, hiyo ndiyo siku unapazwa kuniheshimu Mimi na kupumzika na kunikaribia zaidi.
MIMI, YAHUVEH, NAWAMBIENI, “WATU MNAKOSA MWELEKEO!”
Na hivyo ndivyo mwana wa shetani atakavyowalazimu wale waliojichanganya wamwabudu katika siku atakayoamuru.
MIMI, YAHUVEH, NAWAMBIENI, “WATU MNAKOSA MWELEKEO!”
Kama vile Mwanangu YAHUSHUA alipotamka na kusema “Kunyweni hii divai na kuleni hii mkate, fanyeni hivyo mkinikumbuka Mimi”. Katika Dhiki Kuu inaokuja hivi karibuni, je, hamjui ya kuwa mwana wa shetani atawaambia wale wote waliokubali Alama yake, “Fanyeni hivyo mkinikumbuka mimi?” Watakunywa damu ya wale waliouliwa kwa ajili ya imani yao wakitumia vikombe. Vitakuwa vimejazwa damu na kama wanyama wakunywao damu watakunywa damu haya. Na kama vile kwa hakika sahani ya ushirika upitishwa, kwa hakika, watapitisha sahani na mwana wa shetani atasema, “Fanyeni hivyo mkinikumbuka mimi” Nyama iliochomwa ya wale waliouliwa kwa ajili ya imani yao watakula. Watakejeli Meza ya Ushirika yangu na Bibi arusi wa YAHUSHUA. Kwa kweli watawadharau Bibi arusi wa YAHUSHUA kwa kuwa wanajua ya kwamba maombi ya wenye haki yalizuia mwana wa shetani hadi ilivyofika wakati Bibi arusi wa YAHUSHUA walipoitwa.
Maombi ya wenye haki kwafaa sana. Mimi, YAHUVEH nawaonya imeshaanza tayari. Kutakuwa na ushirikiano wa ngono katika makanisa ya Jumapili katika Dhiki Kuu. Itakuwa kupitia hayo mwana wa shetani atakejeli Bibi arusi wa YAHUSHUA. Kwa kuwa YAHUSHUA na Bibi arusi wake ni mmoja, na wale wote wanaomwabudu YAHUSHUA, wanaotii Mwanangu, ni mmoja, kwa sababu ni ungano wa kiroho kimwili, kiakili, kiroho na nafsi. Mwana wa shetani atakejeli katika Dhiki Kuu, kutakuwa na ushirikiano wa ngono katika makanisa ya Jumapili. Mwanzo wa upotovu kuu ni makanisa ya ushoga. Tena nawaambieni dhambi hiyo imeshaanza.
MIMI, YAHUVEH, NAWAMBIENI, “WATU MNAKOSA MWELEKEO!”
Hivi ndivyo ninavyotumia hii huduma, nikitenganisha kondoo na mbuzi, nikitenganisha ngano na magugu. Wale majina yao yaliandikwa katika Kitabu cha Uzima cha Mwana-kondoo kabla ya kuumbwa kwa hii dunia, hawa ndio majina yao yatabaki katika Kitabu cha Uzima cha Mwana-kondoo, hawatamwabudu mwana wa shetani na watakataa Alama ya Mnyama. Hata kama unasikia au kusoma hii sasa na unaendelea kujichanganya sasa, katika Dhiki Kuu utazingatia na kuheshimu Sabato ya kweli ambayo ni Ijumaa Jioni hadi Jumamosi Jioni hata kama itakugharimu maisha yako na utauliwa kwa ajili ya imani yako. Majina yenu yote yalishaandikwa kwa kuwa nilishafahamu kabla hauchazaliwa hapa duniani ni nini utakachotenda. Kama hautasikia sasa, utasikia baadaye. Wale wanaosoma na kusikia hii habari na kusaga meno yao kwa hasira katika Mjakazi Wangu Atangazae vilevile utasaga meno yako kwa hasira na kunitingizia mkono uliokunjika MIMI, YAHUVEH muumbaji wako, katika Dhiki Kuu wakati ambapo laana na matukio ya kustaajabisha utakapokujia moja baada ya nyingine na hata hivyo hautatubu dhambi zako. Kwa kuwa katika siku hiyo, kama jina lako liko katika Kitabu cha Uzima cha Mwana kondoo, Nitalifuta jina lako. [Ufunuo wa Yohana 3:5]
Na kwa wale wote wanaoshangaa kwa nini Elisabeth alijiwekea hili juu yake, ni kwa sababu ninaitumia hii huduma kutenganisha ngano na magugu. Utakapoyasikia haya, utajua kama wewe ni ngano au magugu. Je, wewe ni magugu tu yanayoharibiwa na hasira zangu, moto wangu unaoteketeza? Ijapokuwa ninamtumia sasa awalilie Bibi arusi, kama sauti iliapo kwa wanawali watano wenye busara, msijichanganye, muwe tayari, kwa kuwa Bwana-arusi anakujia Bibi arusi wake wakati wa Rosh Hashanah na Sabato. Bibi arusi wa YAHUSHUA muwe katika magoti yenu mbele yangu. Kaeni watakatifu na wanyenyekefu. Ombeni ya kuwa mtakubalika kuwa Bibi arusi wa Mwanangu YAHUSHUA wanaolinganishwa na wanawali watano wenye busara. Hii ndio unyakuzi wa kwanza unaofahamika kama Rapcha.
Wageni, ombeni ya kuwa mtakuwa katika unyakuzi wa pili ili muwe wageni katika Karamu ya Arusi ya Mwana kondoo [Ufunuo 19:9]. Wageni wanalinganishwa na wanawali watano wenye busara walioambiwa ya kuwa Bwana arusi atarudi tena baada ya Bibi arusi kunyakuliwa. Kwa hivyo kesheni kwa sababu hamwijui siku wala saa. [Mathayo 25:12] Itakapofika wakati wa Mwanangu YAHUSHUA kuja kunyakua wanawali watano wapumbavu, watakuwa wenye busara.
MIMI, YAHUVEH, NAWAMBIENI, “WATU MNAKOSA MWELEKEO!”
Je, mnataka kujua ni nini inaokutenga kando uwe Bibi arusi wa YAHUSHUA ama Mgeni? Nawambieni sasa; ni jinsi unavyotamani, ni jinsi unavyoonyesha kwa Utakatifu, upendo na kutii. Je, ni jinsi gani unavyoweza kujitolea uwe Bibi arusi wa YAHUSHUA, ukiyafanya yote jinsi atakayo na sio vile utakayo? Ukimtukusa kwa yote ufanyayo. Bibi arusi anajua ya kuwa anapazwa kuzingatia Siku Zangu Takatifu. Bibi arusi anajua hapazwi kujichanganya kwa yale anayoyajua kuwa ni ukweli; anakuwa shupavu kwa kuongea ukweli. Haya ndiyo yanayomtenga kando. Meza ya YAHUSHUA (Komunion) ni ukumbusho wa agano ya arusi na YAHUSHUA. Bibi arusi wa YAHUSHUA wanatumia Majina Yetu Matakatifu ya YAHUVEH na YAHUSHUA. Haijalishi jinsi ya kutamka kwa kuwa ninayajua mioyo yenu na hayana aibu.
Ni jinsi gani unaotamani kuwa Bibi arusi wa YAHUSHUA, ni shauku ipi unao kwa YAHUSHUA? Ni jinsi gani unaoonyesha ya kuwa MIMI, YAHUVEH na YAHUSHUA ni wa kwanza kwa upendo wako na kwa maisha yako na kwa chochote ufanyacho? Haya ndiyo yanayokutenga kando kama Bibi arusi wa YAHUSHUA. Kwa kuwa nawaambieni siri: Ni shauku kuu na uzito wa upendo wako kwa YAHUSHUA inaodhihirika kwa wote. Hii ndiyo alama ya Bibi arusi wa YAHUSHUA. Wanahisi kana kwamba hawanifanyii ya kutosha. Sasa mnaijua siri. Mnaona, Wapendwa Wangu, hakuna unachoweza kunificha kwa kuwa najua ni nani kweli, anayetamani kwa kweli kulipa gharama kuwa Bibi arusi wa YAHUSHUA kwa kuwa sitamwita yeyote Bibi arusi wa YAHUSHUA asipokuwa na hii shauku. Kila siku Bibi arusi wa YAHUSHUA anaomba, “Unifanye niwe Mtakatifu KWAKO hata zaidi.” Bibi arusi wa YAHUSHUA ni mnyenyekevu na Mtakatifu mbele YANGU.
MIMI, YAHUVEH, NAWAMBIENI, “WATU MNAKOSA MWELEKEO!”
Endelea kuwa mwaminifu kwangu. Msiwe wasikiaji tu wa Neno Langu bali muwe watendaji wa Neno Langu Takatifu. Muwe watakatifu kwa kuwa MIMI ni mtakatifu kwa kuwa hata ingawa mko katika hii dunia, ninyi msiwe na tabia ya kidunia. Msiwaruhusu wahubiri waovu wapotoshe Kondoo wangu na Wana Kondoo wangu, kwa kuwa wote wanapaswa kuimarisha wokovu wao wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka. Kwa kuwa imani pasipo matendo imekufa. Mwanangu YAHUSHUA ametenda sehemu yake katika Kalvari. Sasa MIMI YAHUVEH nawambieni, "Tenda sehemu yako." Jitahidi kutii. Usiwaze awali kuhusu kutenda dhambi, usitoe visababu kwa ajili ya kutenda dhambi, usipokee maneno ya wahubiri wanaohubiri kutokutii sheria. Kwa kuwa MIMI YAHUVEH nawambieni, "Kwa nini mnamwita Mwanangu YAHUSHUA Bwana na hamtii Yeye?” MIMI, YAHUVEH nakwambia usipookoka kwa njia usiotii, "Ondokeni Kwangu, enyi watenda maovu" katika siku ya hukumu kwa kuwa sitakuruhusu ukejeli Damu Takatifu ya YAHUSHUA.
Nyinyi mnaojiita wahubiri mnaowatengenezea watu wangu visingizio vya kutenda dhambi. Okokeni leo kwa kupotosha Kondoo Wangu na wana kondoo Wangu. Ama moto Wangu wa pumzi inayoharibu kama takataka katika upepo kali itakupulizia mbali. MIMI YAHUVEH asema kama hauyapendi maneno haya niliyoyasema kupitia kwa Mjakazi Wangu Atangazae Elisabeth, basi utavuna matokeo yake. Kwa kuwa nakataa kujadili. Kuna jaji moja tu, kuna hakimu moja tu, na MIMI YAHUVEH ndiye mwamuzi pekee. Kama hauyapendi haya, usimpelekee Elisabeth. Bali uniletee MIMI YAHUVEH. Yeye tu (Elisabeth) ndiye mzungumzaji WANGU niliyempaka mafuta.
Kwa hivyo imezungumzwa, kwa hivyo imeandikwa katika 8/2/05 saa 4:00 asubuhi imepeanwa na kuzungumzwa kupitia kwa Mjakazi huyu Atangazaye wa YAHUVEH na YAHUSHUA kwa sifa, heshima na utukufu wao.
Ninabaki kuwa mjakazi mnyenyekevu, Mtume Elisabeth Elijah Nikomia
* * * * * * *
Katika 8/1/05 Elisabeth alisikia mara kwa mara "MiMi YAHUVEH NINAKWAMBIA ELISABETH, UWAMBIE WATU, WATU MNAKOSA MWELEKEO!" Katika 8/2/05 Elisabeth alipokuwa anamweleza Msimamizi wa Tofuti, upako mzito ulimjia na akaanza kuongea kwa Ndimi Takatifu. Alikuwa kwa simu na Msimamizi wa Tofuti hakuwa na kinaza sauti na hakukuwa na namna ya kurekodi Ndimi Takatifu, ndipo akaanza kuyaandika Maneno haya Matakatifu kwa mkono.
Anwani la kutuma Barua:
Amightywind
P.O. Box 40007
Upper Hutt
New Zealand 5018
Barua pepe:
revholyfire@yahoo.co.uk
nikomia2k@hotmail.com
Tofuti:
www.amightywind.com
www.almightywind.com