UNABII WA 79

 

MIMI, YAHUVEH, NASEMA, “WATU MNAKOSA MWELEKEO!”

 

Imeandikwa/Imezungumzwa katika upako wa RUACH ha KODESH

kupitia Mtume Elisabeth (Elisheva) Sherrie Elijah

Agosti 2, 2005

              

                                       

 

Kama hunitii MIMI sasa na kama unaafikiana sasa na siku niliyoitenga kuwa Sabato YANGU Takatifu na kama hufikirii ni muhimu kutii Amri ZANGU zote, ni nini inayokufanya ufikiri ya kwamba utanitii katika Dhiki Kuu inayokaribia?  Kwa nini ni rahisi kusikia mafunzo ya kibinadamu wanapogeuza maneno yangu ili kuyalinganisha na hali yao ya dhambi? Hata ingawa Mwanangu YAHUSHUA ni pumziko lenu YEYE si siku yenu ya mapumziko. Mwananagu YAHUSHUA sio siku, na Amri Yangu ya nne inataja wazi kuizingatia Sabato YANGU ya mapumziko kama Siku Takatifu. Ni lipi kati ya haya msiofahamu? Ndiyo, pumzika katika YAHUSHUA kwa kuwa nira YAKE ni rahisi na mzigo WAKE ni mwepesi lakini haya hayana  uhusiano na Siku ya Sabato. Je, YAHUSHUA hakuizingatia Sabato?

 

Je, sikumtuma mwanangu YAHUSHUA awe mfano kwenu? Mnafahamu ni kwa nini niliitenga kando siku ya mapumziko? [Mwanzo 2:1-3] Hamfahamu ya kuwa Siku hii ya Sabato inapaswa kuwa baraka kwenu na wala si laana? Amri YANGU ya nne inasema wazi Siku YANGU ya Sabato izingatiwe kwa Utakatifu. Je, sheria nilioandika kwenye kidonge cha jiwe kwa kidole changu cha moto na kumpa Musa katika mlima wa Sayuni haisemi “Heshimu Siku YANGU ya Sabato na iweke kwa Utakatifu?” Tena nawauliza, tangu lini Mwanangu YAHUSHUA akawa Siku? Jiulizeni, kwa nini shetani alibadilisha siku ya Sabato iwe Jumapili kama haitatumika kwa mipango yake katika Dhiki Kuu?

 

Msiwasikilize wale wanaohubiri kinyume cha haya. Hapa ndipo ushindi upo. Imeandikwa katika Neno LANGU Takatifu ya kuwa MIMI, YAHUVEH siwezi kusema uongo. Mkinitii kuna baraka na ushindi kama inavyotajwa katika Kumbukumbu la Torati 28. Kuna laana kwa wale wasiotii. Soma na uzingatie yaliyoandikwa katika Kutoka 31:12-17. Sabato ya kweli itakuwa ishara  kati ya MIMI, YAHUVEH na watu WANGU, na itatumiwa kuwatambua wale wanaoniabudu na watakaonitumikia MIMI katika Dhiki Kuu. Je, utaniabudu MIMI, YAHUVEH na YAHUSHUA katika Sabato ya Kweli Ijumaa Jioni hadi Jumamosi Jioni? Au katika Dhiki Kuu utamtumikia na kumwabudu mwanaye shetani katika Siku ya Jumapili?

 

Kama huzingatii Sabato Yangu Takatifu sasa, ni nini inayokufanya ufikiri kuwa utaizingatia baadaye, katika Dhiki Kuu inayokaribia. Hili ndilo sababu nazungumza sasa kupitia huyu Ringmaiden WANGU aliyekadiriwa kuwa nabii kwa mataifa ili onyo hili liweze kuenea duniani kote. Je, hamjui kwamba wale wanaofunza kuwa haiwezekani kuwa mtiifu na mtakatifu KWANGU hutoa visingizio kwa ajili ya dhambi zao? MIMI, YAHUVEH, NASEMA, “WATU MNAKOSA MWELEKEO!” Jambo hili si wazi la kujadiliwa. Mtatenda yale MIMI, YAHUVEH nasema, au katika Dhiki Kuu mtalipa na roho zenu. Wale walioinuka na kusema “Nitakuwa hakimu wa Elisabeth, nitakuwa jury  wa Elisabeth” tubuni sasa au mtakaponiona nitawaambia , “Ondoka karibu NAMI wewe mtenda dhambi,” kwa kuwa MIMI ni YAHUVEH na sihusiki katika mjadiliano wowote. MIMI pekee ndiye hakimu, MIMI pekee ndiye jury.  MIMI pekee ndiye rifarii.

 

Haya sio maneno ya Elisabeth. Nyinyi wahubiri na manabii bandia wasiotii sheria, mnamshambulia; mnaomkashifu kwa sababu ya Torati niliyoiandika kwa kidole changu. Mnafunza kondoo WANGU na wana kondoo WANGU ya kuwa MIMI sijali mtu akitenda dhambi. Okoka leo, kwa kuwa MIMI YAHUVEH si MUNGU ambaye amebadilika kwa njia yoyote. Nyinyi, mnaomhukumu Elisabeth, toeni boriti katika jicho lenu kabla mjajaribu kutoa kibanzi kutoka jicho la mtu mwingine. Nyote wachafu katika dhambi, nyote wachafu katika uasi, nyote  wachafu katika kutotii na nyote wachafu katika kiburi. Angukeni kwa nyuso zenu mbele YANGU, kwa kuwa MIMI ni YAHUVEH Muumbaji wako, Anayeishi Milele. Mnathubutu kumlaumu Mwanangu YAHUSHUA kama kisingizio chenu ili kutenda dhambi, mnathubutu kuikanyagia Damu YAKE kwa miguu yenu, mkitoa visingizio kwa ajili ya dhambi zenu.

 

Angukeni kwa nyuso zenu mbele YANGU kabla hamjaenda mbali na hakuna njia ya kurudi KWANGU. Msimhuzunishe RUACH ha KODESH (ROHO MTAKATIFU) WANGU. Mwanangu YAHUSHUA hakuja kufuta Sheria ZANGU; Mwanangu YAHUSHUA alikuja kutimiza Sheria ZANGU. Mkuwe na shukrani kwa kuwa sijawalazimisha kuzingatia sheria 613. Nauliza mzingatie sheria kumi na mnarusha mikono juu na kusema, “Siwezani nazo.” Mnaona ni heri kumsikiliza mwanadamu anayezibadilisha sheria ZANGU. Wanawaambia ya kwamba kuwaua watoto katika tumbo la mama zao si dhambi. Wanahalalisha uavya mimba. Wahubiri hufunza katika kanisa zenu, “Msizungumze kinyume cha sheria hii.” Kanisa zilizopangwa wanaokutana siku ya Jumapili wamechukua hongo kutoka kwa serikali za dunia hii; wameichukua roho ya uoga na kuivaa kama nguo. Wapi wahubiri WANGU Watakatifu ambao hawajachanganyikiwa na bado wanaozungumza kuhusu kuepuka dhambi? Sheria zenu za kibinadamu huhalalisha yale niliyosema ni machukizo; wanaiita ndoa ya jinsia moja. Hata katika siku za Sodoma na Gomora hakuwa na dhambi kama hizi ingawa machukizo za ushoga zilikuwepo lakini hawakuthubutu kuziita ndoa.

 

Msiamini uongo zinazofunza "Ukisha okoka, huhitaji kuokolewa tena." Msiamini kwa sababu YAHUSHUA alilipa gharama pale Kalvari, sasa haijalishi unapotenda dhambi, kwa kuwa unaweza kuning’inia karibu iwezekanavyo na kilele cha Jehanamu vile upendavyo kwa sababu ulisema ombi la wokovu. Unafikiri si lazima utende vitendo na bado utahakikishwa kuingia milango ya Mbinguni, ondokeni karibu nami nyinyi watenda dhambi msiofuata sheria. Sitaki kusikia visingizio vyenu tena. Mkuwe Watakatifu au nitawaambia, “Watenda dhambi, MIMI sijawahi kuwajua.”

 

MIMI, YAHUVEH, NASEMA, “WATU MNAKOSA MWELEKEO!”

 

Mnawasikiza watu hawa sasa na mnaketi kwenye kanisa zenu mkiamini uongo hizo ya kwamba Jumapili ni Sabato au haijalishi ni siku gani ndio Sabato. Mnaamini uongo zinazofunzwa na wahubiri na Rabbi wengine kuwa hakuna upako kubwa katika Majina Takatifu ya Kiebrania ya YAHUVEH na YAHUSHUA na RUACH ha KODESH, kwamba jina lolote lafaa. Wahubiri wanawaambia si muhimu kujua Uyahudi wa MASIHI. Wao husema kama wewe si Myahudi basi haikuhusu. Wahubiri hawa wasiofuata sheria hufunza ya kuwa kama wewe si Myahudi hupaswi kuitii sheria iliyopewa kwa Wana wa Israeli. Je, mlisahau ya kwamba mlipomkubali Mwanangu YAHUSHUA kama MASIHI mlikuwa kitu kimoja NAYE? (Warumi 11:16-21)

 

Mnashangaa, “Wapi nguvu ya upako wa kanisa la kwanza iliyokuwa na ishara, maajabu na miujiza?” Mnalia, “Yako wapi matukio ya kimiujiza kama siku za kale?” Rudini na mfanye yale ambayo kanisa la kwanza lilifanya na mtaziona miujiza hizo tena. Kwa wale wasiokuwa na habari, nawaambia hukumu utapewa kuhusu yale pekee unayoyajua. Sasa nawapa budi kuwafunza wengine ukweli huu pia, na mtapata hukumu kuzingatia haya. Lakini kwa wale wanaojua ukweli na bado hutenda maovu, mtalipa na roho zenu.

 

MIMI, YAHUVEH, NASEMA, “WATU MNAKOSA MWELEKEO!”

 

Mnawatii sasa hawa viongozi waovu wa kiroho wanaotoa visingizio kwa ajili ya dhambi. Ni nini inayokufanya ufikiri ya kuwa katika Dhiki Kuu hautafanya hivyo tena na mwanawe shetani? Niliwaambia katika unabii niliyoitoa kupitia Elisabeth ya kwamba Mwanangu YAHUSHUA yuaja kumchukua Bibi Arusi WAKE katika Rosh Ha Shanah na itakuwa katika siku ya Sabato. Kama haufunzwi jinsi ya kuzingatia Sabato YANGU na Siku ZANGU Takatifu, na kujifunza Majina YETU Takatifu (angalia “Kwa Nini Tunayatumia Majina Takatifu”) na Torati YANGU kuitii, utajuaje jinsi ya kuniheshimu MIMI na Mwanangu YAHUSHUA kama vile nilivyoamuru? Utajuaje ni siku gani, bila ya kusoma na kujionyesha ya kwamba umekubalika,  MIMI, YAHUVEH, nimeitenga kando iwe Sabato YANGU, je, utajitayarishaje YAHUSHUA atakaporudi?

 

MIMI, YAHUVEH, NASEMA, “WATU MNAKOSA MWELEKEO!”

 

Kama hamziheshimu na kuzizingatia Sherehe ZANGU Takatifu, je, mtajuaje Rosh Ha Shanah ni nini na huwa wakati gani? Alafu utakapoachwa nyuma utauliza “Kwa nini?” Ndipo sasa nazungumza kupitia Ringmaiden WANGU na kuwajulisha kabla ya wakati ya kwamba MIMI, YAHUVEH ninatabiri kupitia huyu Ringmaiden WANGU ambaye ni mmoja wa Bibi Arusi wa Mwanangu YAHUSHUA.

 

Bibi Arusi wa YAHUSHUA hawatabadilishwa tu na kupewa miili ya utukufu na kujazwa na upako kana kwamba YAHUSHUA mwenyewe  anatembea ndani mwao, na pamoja nao, atawajaza na upako wa ajabu hadi hakutakuwa na jambo lisilowezekana kwao. Na kwa siku 40 Bibi Arusi wa Mwanangu YAHUSHUA watapeana onyo, “Msichukue Alama ya Mnyama”. Watawaendea wale ninaowaita Wageni na wale ambao majina yao yapo katika kitabu cha Uzima wa Milele cha Wana Kondoo na watawaambia, “Msiwe wasiotii, msichanganyikiwe, ingawa itamaanisha kupoteza maisha yenu ya hapa duniani.”

 

Mnaona, ninamtumia huyu Ringmaiden sasa, hata bila mwili wake wa utukufu, kama sauti inayolia ikitoa onyo kabla ya wakati wake. Kwa kuwa nimemuita awe nabii kwa mataifa. Msichukue Alama ya Mnyama! Kuabudu katika siku la Jumapili na Alama ya Mnyama zina uhusiano. Jitahadhari, utapoteza roho yako ukizingatia sheria  ya kuabudu Jumapili katika Dhiki Kuu. Itabidi niombe msamaha kwa Sodoma na Gomora niliyoharibu kwa moto na kiberiti nikiacha vichukizo hivi vya duniani viendelee zaidi ya vile vilivyo sasa. Sitaomba msamaha kwa Sodoma na Gomora. Nitayaharibu na kukomesha yale yote MIMI, YAHUVEH nachukia.

 

Hawa wahubiri bandia hutoa visingizio ili kutenda dhambi na mmewasikiliza. Mnakuja kwa hii huduma kupata chakula chenu cha kiroho, kuonja upako, kunywa maziwa ya kiroho na kula nyama ya kiroho, halafu wangapi kati yenu wanachanganyikiwa na kuenda katika Kanisa za Jumapili. Mnaanguka kwenye miguu ya wachungaji wenu kwa uaminifu na ni hapo mnapotoa zaka na sadaka. Hamwezi kutegemea njia zote. Mnapaswa mjijulishe ni siku ipi niliyoamuru kuwa Sabato, kwa kuwa nimeamuru ni siku ipi ndio Sabato, siku ambayo mnapaswa kuniheshimu MIMI na kupumzika na kunikaribia zaidi.

 

MIMI, YAHUVEH, NASEMA, “WATU MNAKOSA MWELEKEO!”

 

Na kwa hivyo mwanawe shetani atawalazimu wote wale waliochanganyikiwa kumwabudu katika siku atakayoamuru.

 

MIMI, YAHUVEH, NASEMA, “WATU MNAKOSA MWELEKEO!”

 

Kama vile Mwanangu YAHUSHUA alinena na kusema “Munywe hii mvinyo na mle mkate huu, fanyeni hivi mkinikumbuka MIMI”. Katika Dhiki Kuu inayokuja hivi karibuni, hamjui ya kwamba mwanawe shetani atawaambia wale wote watakaokubali Alama yake, “Fanyeni hivi mkinikumbuka mimi.” Watakunywa damu ya mashahidi wakitumia vikombe. Vitakuwa vimejazwa damu na kama ‘vampires’, watakunywa damu hii. Na kama vile sahani ya ushirika hupitishwa, kwa uhakika, watapitisha sahani na mwanawe shetani atasema, “Fanyeni hivi mkinikumbuka mimi”. Nyama iliyochomwa ya mashahidi watakula. Watakejeli ushirika WANGU na Bibi Arusi wa YAHUSHUA. Kwa kweli watawachukia Bibi Arusi wa YAHUSHUA kwa sababu wanajua ya kwamba ni maombi ya wale watakatifu yaliyomzuia mwanawe shetani hadi ilivyofika wakati wa kuwaita Bibi Arusi wa YAHUSHUA wajitokeze.

 

Maombi ya wale watakatifu yafaa sana. MIMI, YAHUVEH, nawaonya ishaanza tayari. Kutakuwa na ushirikiano wa ngono katika Kanisa za Jumapili katika Dhiki Kuu. Hivi ndivyo mwanawe shetani atawakejeli Bibi Arusi wa YAHUSHUA. Kwa kuwa YAHUSHUA na Bibi Arusi WAKE ni kitu kimoja, na wote wanaomwabudu YAHUSHUA, wanaotii Mwanangu, ni kitu kimoja, kwa sababu hii ni uungano takatifu wa kimwili, kiakili, na kiroho. Mwanawe shetani atakejeli katika Dhiki Kuu, kutakuwa na ushirikiano wa ngono katika Kanisa za Jumapili. Mwanzo wa huu udanganyifu kuu ni Kanisa za ushoga. Tena nasema dhambi hizi zimeshaanza.

 

MIMI, YAHUVEH, NASEMA, “WATU MNAKOSA MWELEKEO!”

 

Hivi ndivyo ninavyotumia hii huduma, nikitenganisha kondoo mbali na mbuzi, nikitenganisha ngano mbali na magugu. Wale ambao majina yao yaliandikwa katika Kitabu cha Uzima cha Mwana Kondoo kabla ya kuumbwa kwa dunia hii, ni majina ya hawa ambayo yatabaki katika Kitabu cha Uzima cha Mwana Kondoo, hawatamwabudu mwanawe shetani na watakataa Alama ya Mnyama. Hata kama unasikia au kusoma haya sasa na unaendelea kuchanganyikiwa sasa, katika Dhiki Kuu utaizingatia na kuiheshimu Sabato ya kweli ambayo ni Ijumaa Jioni hadi Jumamosi Jioni hata kama itamaanisha maisha yako na utauliwa kama mshahidi. Majina yenu yote yalishaandikwa kwa kuwa nilishafahamu kabla haujazaliwa hapa duniani ni nini utakachotenda. Kama hautasikia sasa, utasikia baadaye. Wale wanaosoma na kusikia ujumbe huu na kusaga meno yao kwa hasira kwa Ringmaiden WANGU, vilevile pia mtasaga meno yenu kwa hasira na kunitingizia ngumi zenu kwangu MIMI, YAHUVEH muumbaji wenu katika Dhiki Kuu, laana na mapigo yakiwaangukia moja baada ya nyingine na bado hamtatubu dhambi zenu. Kwa kuwa katika siku hiyo, kama jina lako lipo katika Kitabu cha Uzima cha Mwana Kondoo, Nitalifuta jina lako. [Ufunuo wa Yohana 3:5]

 

Kwa wale wote wanaoshangaa ni kwa nini Elisabeth amejiletea haya yote, ni kwa sababu ninaitumia hii huduma  kutenganisha ngano mbali na magugu. Utakapoyasikia haya, utajua kama wewe ni ngano au magugu. Je, wewe ni magugu  yanayoharibiwa tu kwa hasira ZANGU, kwa moto WANGU unaoteketeza? Ijapokuwa ninamtumia sasa kuwatangazia Bibi Arusi, kama sauti inayowatangazia wanawali watano wenye busara, msichanganyikiwe, mkuwe tayari, kwa kuwa Bwana Arusi yuaja kumchukua Bibi Arusi WAKE wakati wa Rosh Ha Shanah na Sabato. Bibi Arusi wa YAHUSHUA mpige magoti mbele YANGU. Mbaki watakatifu na wanyenyekevu. Ombeni ya kwamba mtakubalika kuwa Bibi Arusi wa Mwanangu YAHUSHUA wanaolinganishwa na wanawali watano wenye busara. Hili ndilo unyakuzi wa kwanza unaofahamika kama Unyakuaji.

 

Wageni, ombeni ya kwamba mtakuwa katika unyakuzi wa pili ili mkuwe wageni katika Karamu ya Arusi ya Mwana Kondoo [Ufunuo wa Yohana 19:9]. Wageni wanalinganishwa na wanawali watano wapumbavu wanaoambiwa ya kuwa Bwana Arusi atarudi tena baada ya Bibi Arusi kunyakuliwa. Kwa hivyo mkae tayari kwa sababu hamjui siku wala saa. [Mathayo 25:12] Itakapofika wakati wa Mwanangu YAHUSHUA kuja kunyakua wanawali watano wapumbavu, watakuwa wenye busara.

 

MIMI, YAHUVEH, NASEMA, “WATU MNAKOSA MWELEKEO!”

 

Je, mnataka kujua ni nini inayokutenga kando ili uwe Bibi Arusi wa YAHUSHUA au Mgeni? Nawaambia sasa; ni kwa kiasi gani unavyoitamani, ni jinsi utakavyojionyesha kwa Utakatifu, upendo na kutii. Ni kwa kiasi gani upo tayari kujitolea ili kuwa Bibi arusi wa YAHUSHUA, ukiyafanya yote jinsi atakavyo na sio vile wewe utakavyo. Ukimtukuza kwa yale yote ufanyayo. Bibi Arusi anajua ya kwamba anapaswa kuzingatia Siku ZANGU Takatifu. Bibi Arusi anajua hapaswi kuchanganyikiwa kwa yale anayoyajua kuwa ni kweli; ni mshupavu kwa kuzungumza ukweli. Hili ndilo jambo linalomtenga kando na wote. Ushirika ni kumbusho la agano la arusi na YAHUSHUA. Bibi Arusi wa YAHUSHUA wanatumia MAJINA YETU Tatakatifu ya YAHUVEH na YAHUSHUA. Haijalishi inavyoandikwa kwa kuwa ninazijua nyoyo zenu na kwamba hazina aibu.

 

Ni kwa kiasi gani unatamani kuwa Bibi arusi wa YAHUSHUA, ni kwa kiasi gani unayo shauku kwake YAHUSHUA? Unafanya yapi kuonyesha ya kuwa MIMI, YAHUVEH na YAHUSHUA ni nambari moja katika upendo wako na maisha yako na kwa yote ufanyayo? Haya ndiyo yanayokutenga kando kama Bibi arusi wa YAHUSHUA. Kwa kuwa nawaambia siri hii: Shauku kuu na uzito wa upendo wako kwa YAHUSHUA ni ushuhuda kwa wote wanaotazama. Hii ndiyo alama ya Bibi Arusi wa YAHUSHUA. Wanahisi ya kwamba hawawezi kunifanyia ya kutosha MIMI. Sasa mnazijua siri. Mnaona, Wapendwa WANGU, hii si kitu mnayoweza kunificha kwa kuwa ninajua ni nani kwa kweli, anayetamani kweli kulipa gharama ili kuwa Bibi Arusi wa YAHUSHUA kwa sababu sitamwita yeyote Bibi Arusi wa YAHUSHUA asiyekuwa na shauku hii. Kila siku Bibi Arusi wa YAHUSHUA huomba, “Nifanye niwe Mtakatifu KWAKO hata zaidi.” Bibi Arusi wa YAHUSHUA ni mnyenyekevu na Mtakatifu mbele YANGU.

 

MIMI, YAHUVEH, NASEMA, “WATU MNAKOSA MWELEKEO!”

 

Kuwa mwaminifu KWANGU sasa hivi. Msiwe tu wasikilizaji wa Neno LANGU bali mkuwe watendaji wa Neno LANGU Takatifu. Mkuwe watakatifu kama MIMI nilivyo Mtakatifu, kwa kuwa ingawa mpo katika dunia hii, hamfai kuiga tabia za dunia hii. Msiwaruhusu wahubiri wasiotii sheria kuwapotosha kondoo na wana kondoo WANGU, kwa kuwa wote wanapaswa kuimarisha wokovu wao wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka. Kwa kuwa imani bila matendo imekufa. Mwanangu YAHUSHUA ashatenda sehemu yake pale Kalvari. Sasa MIMI, YAHUVEH, nawaambia, "Tenda sehemu yako." Jitahidi kutii. Usiwaze awali kuhusu kutenda dhambi, usitoe visingizio kwa ajili ya kutenda dhambi, usipokee maneno ya wahubiri wanaofunza kutotii sheria. Kwa kuwa MIMI, YAHUVEH, nawaambia, "Kwa nini mnamwita Mwanangu YAHUSHUA Bwana na hamtii?” MIMI, YAHUVEH, nasema, usipotubu jinsi unavyokataa kutii, "Ondoka karibu NAMI, ewe mtenda dhambi" katika siku ya hukumu kwa kuwa MIMI sitakuruhusu ukejeli Damu Takatifu ya YAHUSHUA.

 

Nyinyi mnaojiita wahubiri mnaotoa visingizio ili watu wangu watende dhambi. Tubuni leo kwa kuwapotosha kondoo WANGU na wana kondoo WANGU. Au moto wa pumzi YANGU inayochoma kama majivu kwenye Upepo kali nitawapulizia mbali. MIMI, YAHUVEH, nasema kama haupendi maneno haya yaliyosemwa kupitia Ringmaiden WANGU Elisabeth, basi utavuna matokeo yako. Kwa sababu nakataa kujadili. Kuna jaji mmoja tu, kuna jury mmoja tu, na MIMI, YAHUVEH, ndiye rifarii wa pekee. Kama haupendi ujumbe huu wa unabii, usiyapeleke kwake Elisabeth. Bali uniletee MIMI, YAHUVEH, kwa kuwa yeye ni Mjumbe WANGU mtakatifu tu.

 

 

Kwa hivyo imezungumzwa, kwa hivyo imeandikwa katika 8/2/05 saa 4:00 asubuhi, ilipewa kwa na kuzungumzwa kupitia Ringmaiden wa YAHUVEH na YAHUSHUA kwa Sifa, Heshima na Utukufu WAO.

 

Nabaki nikiwa handmaiden mnyenyekevu, Mtume Elisabeth (Elisheva) Elijah

 

* * * * * * *

 

Katika 8/1/05 Elisabeth alisikia mara kwa mara "MIMI,YAHUVEH, NAKUAMBIA ELISABETH, WAAMBIE WATU, WATU MNAKOSA MWELEKEO!" Katika 8/2/05 Elisabeth alipokuwa anamwambia Msimamizi wa Tofuti, upako mzito ulimjia na akaanza kuongea kwa Ndimi Takatifu. Alikuwa kwa simu na Msimamizi wa Tofuti hakuwa na kinaza sauti na hakukuwa na namna ya kurekodi Ndimi Takatifu, ndipo akaanza kuyaandika Maneno haya Takatifu kwa mkono.

 

Tofuti:

 

www.amightywind.com

www.almightywind.com

 

Anwani la kutuma Barua:

 

Almightywind

Sanduku La Posta, 40007

Upper Hutt

New Zealand 5018

 

Contact AmightyWind