Unabii 6

KWANZA MIMI HULIA, ALAFU MIMI HUKASIRIKA!

Ilipewa kwake Sherrie Elijah Mei 12, 1997


Katika ujumbe wa tarehe Mei 12, 1997 Saa 01:15:00 (EDT), KT Jerome aliandika: ninafurahia Wakristo kama wewe walio na ujasiri wa kuzungumza ukweli hata katika nyakati za mateso na/au upinzani.

Mpendwa Kelly,

Haujui jinsi nilivyohitaji kusikia ukiyasema maneno haya. Usiku uu huu, nilishambuliwa vikali. Hii ni mara ya tatu katika wiki hii na mashambulizi haya yanatoka kwa waumini wanaosema wanamtumikia YAHUSHUA. Usiku huu, naungama kwako kuwa nililia kwa sababu nilishambuliwa na nikaitwa nisiomcha mungu kwa sababu ya karama yangu, picha yangu, kwa sababu nina nywele nyeupe (blonde), na mimi hujipodoa. Iliniuma sana na nikalia na YAHUSHUA hakusema chochote kunifariji. Ilinifanya nihisi vibaya zaidi.

Alafu niliposema, “YAHUSHUA, kwani haujali kuwa ninaumia, nataka tu kuwa Baraka kwa watu wako, mbona wananishambulia hivi? Mbona upo kimya?” Sijui ni kwa nini ninakuambia haya; sikufikiria kuwa ningemwambia yeyote kwa sababu naona aibu. Ajabu, ninahisi upako unanijia kuzungumza haya maneno, nikakoma na kuanza kuomba katika RUACH ha KODESH (Roho Mtakatifu).

* * * * * * *

YAHUSHUA (YESU) alizungumza kwa Roho yangu na kusema, “Ndio Ninajali na sababu sizungumzi ni kwa sababu Ninalia nawe. Kwa sababu MIMI hukutuma kwa Watu WANGU kuwa Baraka na wengine wamekuona kama laana. Lakini MIMI, YAHUSHUA, pia Nimetumwa kama Baraka na ni wangapi wanaoniona MIMI kama laana? Ninalia nawe, na Ninakulilia, na kwa wote wanaojua bora, lakini bado huwashika wajumbe WANGU walio na upako, ingawa wameonywa. Ninalia kwa yote Watoto WANGU wanaojiita kwa JINA LANGU wanatendeana. Tamaa, wivu, kutoaminiana, mashtaka, kutopendana na chuki. Uongo mnazoambiana na wanaweka JINA LANGU kwa uongo huo ni kama Nimeizungumza MIMI. Ninalia, kwa kuwa moyo WANGU unavunjika, kwa kuwa kuna uchanga mwingi hata katika Wakristo waliokomaa.

Manabii wamekuwa pekee yao kwa muda mrefu sana. Wamekataliwa nyakati nyingi sana, sasa wanajua tu vile kukataliana na kutengana, ingawa hamu YANGU katika nyakati hizi za mwisho ni kwa nyinyi nyote kuungana pamoja katika JINA LANGU, katika umoja. Katika nyakati hizi za mwisho ugomvi huu na kugombana lazima uishe. Nyinyi, Mitume, Manabii, Walimu, Wainjilisti na Wachungaji WANGU lazima muwe pamoja. Nyinyi ni jeshi LANGU la nyakati za mwisho. Huduma zote za afisi tano, lazima mwache kutengana nyinyi wenyewe na mje pamoja katika upendo WANGU. Lazima mwache kuwekeana majeraha ya mauti kwenye Roho zenu. Lazima mwache kuwekeana majeraha ya mauti kwenye Roho zenu na mwanze kuyafunga majeraha ambayo mmeyasababisha kati yenu wenyewe. Ninalia kwa ajili yenu, kwa kuwa nyote mmeumizwa na mtu mwingine aliyesema kuwa wao ni wa Roho YANGU. Ndio, nyinyi, wengi wenu mmedanganyika, na ni nadra sana kama mtasema kuwa hamjawahi kudanganyika na adui aliyewajia akijificha kama kondoo lakini yeye ni mbwa mwitu anayemeza mifugo YANGU. Lakini hamwezi endelea kumezana. Sitayaruhusu.

Ninazungumza tena kutoka kwa Handmaiden WANGU kuwaambia kuwa MIMI silii pekee kwa yale yatakayowatendekea maadui wa Injili, lakini Ninawalilia nyinyi Watoto WANGU. Kwa kuwa jinsi mnavyotendeana si ya Roho YANGU ya upendo kabisa. Si Neno LANGU husema, “Kama mkipendana ninyi kwa ninyi, kwa njia hii, watu wote watajua kuwa ninyi ni wanafunzi Wangu?” Hamjagundua kwamba ni adui anayewajia na kusema viti hivi viovu ili kuwasababisha Mashujaa WANGU wapigane kati yao wenyewe na sio kuungana pamoja kupigana na adui, lakini wanafikiria kuwa wanaweza kufanya haya yote pekee yao. Si Neno LANGU husema, “MIMI huwafukuza maelfu?” Ni pepo wangapi zaidi watakaofukuzwa, mtakapoungana pamoja na sio dhidi yenu wenyewe? Hili ndilo jambo lililotenga jeshi la Gideoni. Ugomvi waliokuwa nao kati yao wenyewe. Hili ndilo jambo linalotenga jeshi nyingi. Nyote mpo katika Jeshi Kuu la ‘MIMI NIKO’. Nyinyi ndio kikosi cha nyakati hizi za mwisho Nilichokichagua mwenyewe. Ndio, adui amewadanganya, SONGENI MBELE!

Yuda alinisaliti MIMI. Je, MIMI huwatendea nyote kama Yuda? Hapana. Petero alinikataa MIMI, je, MIMI huwakataa? Hapana. Acheni haya sasa hivi. Mara moja tena Ninachagua kuzungumza na kusema kuwa mwisho upo karibu, kama tu mngeweza kuona jinsi kuja KWANGU upo karibu. Chochote ulichoitwa kufanya, ifanye sasa, na yote Niliyokupa. Kuna karama za kiroho zilizofungwa ndani yenu ambazo hamzijui. Mnafaa kukoroga karama za wengine na sio kukoroga hasira za wengine. Mnanikasirisha MIMI mnapofanya haya. Hamnipiganii MIMI, mnapigana dhidi YANGU. Kama nyinyi sio wa KWANGU mpo dhidi YANGU. Acheni kuhukumiana kwa sura. Lazima Nijirudie mara ngapi? Mbona hamsikizi? Mbona mnahisi kuwa nyinyi ni bora kushinda wengine kwa sababu ya rangi ya ngozi, au rangi, nguo, au sura?

Je, bado hamwelewi? Nitapambana nanyi hadi lini? Adui anawatenga hata kabla Niweze kuwaunga pamoja. Lakini msifikirie kuwa nyinyi hamwezi kubadilishwa. Kwa kuwa Nitawainua mashujaa wengine kuchukua nafasi yenu. Hii ndio nafasi yenu ya mwisho. TUBUNI! Sio nyote mlio na karama sawa. Nimewapa wachache Niliowachagua karama zisizo za kawaida. Msiwashike watu WANGU walio na upako na msiwaumize Manabii WANGU. Ndio, hukumu kinachozungumzwa, je, kinalingana na Neno Takatifu? Ipo katika muktadha au ipo nje ya muktadha? Mtajua. Lakini mwache kuwanyamazisha Manabii WANGU. Acheni kuwanyamazisha Mitume WANGU. Acheni kuwaambia watafeli kwa kuwa kazi ni kubwa, na lazima hawasikii kutoka kwa YAHUVEH na YAHUSHUA. Acheni kuniweka MIMI katika sanduku. Si MIMI NDIYE MUNGU wa yasiyowezekana? Kuna chochote ambacho ni ngumu KWANGU MIMI?

Mbona nyinyi huwashawishi kuwa watafeli, Ninapowaambia kuwa watafaulu? Acheni kuwakatisha tamaa wale ambao mnafaa kuwapa moyo. Kazi yao sio ngumu ya kutosha? Je, hawahisi unyanyasaji wa kutosha kutoka kwa adui? Lazima uje kutoka kwa wale wanaofaa kuwa na upendo, kuwahamasisha, kuwasaidia na kuombea mafanikio yao? MIMI sio mwandishi na mkamilishaji wa imani yao, imani yenu? Ningewaambia mfanye kitu, ingawa wengine wanawaambia kuwa haiwezekani. Ndipo mtakapojua kuwa Nimeyazungumza haya. Mara nyingine tena Nilimchukua Handmaiden huyu na Nikampa upako kuzungumza maneno ambayo Ninataka ayaseme. Yeye ni mdomo WANGU. Niliruhusu aumizwe ili aweze kunena maneno haya. Kumbukeni, si MIMI husema, “upako ukiwa mkuu, mateso yatakuwa makuu?” Lakini mateso hayatoki KWANGU, lakini kutoka kwa adui anayetaka kuwakatisha tamaa. Mateso haya huja kutoka midomoni mwa watumishi WANGU kwa wengine.

Nitaanza kuhukumu vikali kwa kuwa Hukumu huanza katika nyumba ya YAHUVEH na Nimewaonya hapo mbeleni mara nyingine tena. Nipo karibu kutoa wale Niliowakadiri na kuwaita lakini kwa sababu wanataka kuwaangamiza wale Niliowakadiri na kwa kujua na mawazo ya kupanga na habithi katika nyoyo zao (ingawa hawana shaka kuwa wanaongea kwa niaba YANGU) wametafuta uharibifu wao. Ninasema, “Maangamizi yatawajia wao wenyewe” na itarudi kwao wenyewe. Mmeonywa. Kwanza MIMI hulia, alafu MIMI hukasirika! Lakini hamtaki kumwona Kamanda Mkuu akiwa amekasirika. Niamini MIMI. Nilikuwa yule mwana-kondoo aliyeuawa kwa dunia mara moja tu. MIMI bado sio yule mwana-kondoo mpole na mvumilivu, lakini Naja kama simba kutoka kabila ya Yuda. Lazima Niipate Kanisa LANGU tayari bila doa wala kasoro… kuchelewa kote lazima uishe.

Fanyeni yote mnayojua kufanya na fanyeni kwa haraka. Wale uliowakosea, wafariji. Msiniletee MIMI sadaka, na dhabihu mpaka mtubu kwa dhambi wengi wenu mliotenda machoni MWANGU. Tubuni mbele YANGU na tubuni mbele ya kaka na dada zenu, mashujaa wenzenu wa YAHUSHUA ha MASHIACH. Mmeonywa. Msinifanye MIMI Nijirudie. ‘Mpendane,’ kwa haya mnathibitisha kuwa mnanipenda MIMI na mnathibitisha kuwa MNANIPENDA na kunitumikia MIMI juu ya yote. Msiniite MIMI Bwana kama hamnitii MIMI. Kwa kuwa Bwana ni Mkubwa wenu, kiongozi na utaniitaje MIMI Bwana kama haunitii MIMI? Mpendane; hii ndiyo Amri YANGU kwa kila mmoja wenu.

Simameni pamoja na mpiganie Utakatifu. Simameni pamoja na mpigane na uovu. Katika NGUVU ZANGU, katika NENO LANGU, katika JINA LANGU, na katika UPAKO WANGU, kupitia DAMU YANGU mtakuwa zaidi ya washindi kupitia YAHUSHUA ha MASHIACH bwana wenu. Lakini lazima mwungane pamoja. Hamna mwaminifu yeyote ambaye ni mnyororo, bali tu kiungo katika mnyororo wa dhahabu. Wengine ni minyororo mikubwa kushinda wengine, lakini bado mnahitajiana katika mnyororo huu, itakayomfunga slewfoot (shetani) na kumtupa katika ziwa la moto katika wakati wake uliopangwa. Kumbukeni, MIMI ni wa kwenu, Mbinguni yote husimama katika amri YANGU. Hamtafeli isipokuwa mtakapochagua kutosikiza maneno haya Niliyoyazungumza siku hii. Lakini hata hivyo MIMI sitafeli. Kwa kuwa MIMI sio MUNGU anayeweza kufeli, Nitawainua askari zaidi wa nyakati za mwisho kuchukua nafasi zenu. Hamtafeli kama mtayasikia maneno haya yaliyonenwa siku hii kupitia Handmaiden WANGU, Sherrie Elijah tarehe 5/12/97.

Wale walio na masikio ya kiroho ya kusikia watasikiza, wote wengine watabaki viziwi. Ndivyo ilivyosemwa na kurekodiwa katika siku hii. Baraka au laana zitakuja njiani mwenu, inategemea na kile mtakachofanya na unabii huu siku hii. Tubuni sasa Watoto WANGU kabla wakati haujapita.

* * * * * * *


Ilipewa kwake Nabii Sherrie Elijah tarehe 5/12/1997

Kelly, wewe ndiwe wa kwanza kuyapokea haya. Ni kwa sababu ulimtii RUACH ha KODESH na kuniandikia na kunifariji mimi bila kujua kuwa nilikuwa ninahitaji kufarijiwa. Huu ndio unabii wa sita ambao RUACH ha KODESH ameuandika kupitia kwangu tangu tarehe 12/31/96. Unabii zingine zinaweza kupatikana katika mtandao wangu kwa YAHUSHUA pale http://almightywind.com au http://amightywind.com. Kanisa la Alpha & Omega Almightywind Holy Ghost Fire.

Tafadhali someni haya na mniambie kama mnasikia sauti ya RUACH ha KODESH humo ndani. Nimeshangazwa. Nilikuwa nimefunga tangu tarehe 9 na 11 na labda ndiyo sababu ujumbe huu ulikuja. Sijui… Asanteni kwa kujibu haraka na tafadhali YAHUSHUA acha watu wasikize sauti yako na si yangu. Kama huyu ni wewe kwa kweli acha Kelly awe wa kwanza kuhisi upako mkuu. Bariki moyo huyu mpendwa aliyesikiza sauti yako, akaniandikia neno la kunipa moyo ingawa hakunijua mimi, lakini alikutii ili upako huu uweze kuja. Mbariki sana na ninaomba watu walioumizana makusudi, wakikatishana tamaa, watatubu kwa uwazi kwako na kati yao wenyewe. Katika jina lako YAHUSHUA ninauliza. Ninawasamehe wale walionishambulia vikali bila sababu yoyote, na ninaihesabu kama furaha ulivyoleta kitu kizuri kutoka kwake. Nasi tunajua ya kuwa katika mambo yote YAHUVEH hutenda kazi pamoja na wote wampendao, katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi Lake. Ninakupenda YAHUSHUA. Ninakupenda mpendwa Kelly kwa kutii YAHUSHUA. Ninataka kuiweka barua pepe yako ilivyo, ili wengine waweze kuona kuwa haya hayakutungwa. Je, naweza kuitumia ilivyo? Tafadhali usione haya kwa kuwa YAHUVEH alikutumia kukoroga karama zilizomo ndani yangu. YAHUSHUA atakubariki vikuu kwa kuwa umembariki handmaiden huyu asubuhi hii mapema saa 3:35 (central time).

Nukuu Binafsi pamoja na Unabii huu #6:

Ninahisi nikiongozwa tena kuuliza kwa vile haya yatawafikia waaminifu wengi duniani kwa muda mfupi, tafadhali ninamtafuta nabii mwingine wa YAHUVEH aliye hai, jina la kwanza ni Nikomia, labda katika sehemu ya Canada, anayezungumza kifaransa vizuri. YAHUVEH amenipa jina hili na kusema kuwa yeye ana umuhimu mkuu kwa huduma hii niliyomo. Tafadhali nitumie barua pepe kama mnamjua mtu yeyote na jina hili. Kwa kweli YAHUSHUA atawabariki vikuu. Imani bila matendo imekufa kwa hivyo ninaendelea kuuliza; tafadhali semeni ombi nimpate haraka kwa Utukufu wa YAHUSHUA ha MASHIACH!

Kusema ombi hilo tu katika RUACH ha KODESH litakuwa Baraka kwa huyu mtumishi na sina shaka kuwa mtabarikiwa kutoka kwa yule ambaye baraka zote hutoka. Tafadhali mtakaponakili unabii huu pasha pia hii nukuu binafsi. Asanteni. Ninangoja muujiza kutoka kwa MUNGU asiyeweza kudanganya.