Unabii 69

Kunakuja Wakati Wa Walinzi Kubadilishwa!”


Imepewa kwake Mtume Elisabeth Elijah (Elisheva Eliyahu)

Disemba 31, 2002

Imetolewa Januari 1, 2003


Haya maneno yanatoka kwenye Unabii wa 105, YAHUVEH Alisema yaongezwe kwenye Unabii zote kutoka sasa: Nilikuonya kitambo Elisabeth [Elisheva], kutoita Huduma hii kwa jina la mwanamume au mwanamke. Hata kabla kuwepo na Huduma, Niliiweka ndani ya roho yako. Kwa kuwa hakuna lolote lililofanyika kwa mikono yako. Hakuna lolote lililotoka kwenye kinywa chako. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUVEH Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUSHUA, MASHIACH wako Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha RUACH HA KODESH, IMMAYAH wako Aliyeizalisha. Kama ingekuwa tu kwa mkono wako, ingekuwa imefeli kitambo. Ni kwa UPEPO WA SHKHINYAH GLORY unaovuma kote duniani, UPEPO TAKATIFU WA UAMSHO. Sio kwa pumzi yako, au ingekuwa imefeli. (Isaya 42:8)

Katika mwezi wa Julai 2010, MUNGU YAHUVEH pia Alisema kuongezwe yafuatayo mbele ya Unabii zote kutoka Kitabu cha pili cha Mambo ya Nyakati:


2 Mambo ya Nyakati 36:16, “Lakini waliwadhihaki Wajumbe wa MUNGU, na kuyadharau Maneno YAKE, na kuwacheka Manabii WAKE, hata ilipozidi Ghadhabu ya BWANA juu ya Watu WAKE, hata kusiwe na kuponya.”

* * * * * * *


Tarehe 12/31/02 (timu ya Amightywind) tulikuwa tunaomba kwa majibu ya kibinafsi kwa maswali ambayo tuliyokuwa nayo. Kwa sababu hatufichi jumbe kutoka kwa Baba YAHUVEH wa Mbinguni au MASIHI YAHUSHUA tunatoa sehemu hii ambayo ni ya kibinafsi. Labda itamsaidia mtu mwingine.


Hata ninapokemewa na YAHUVEH kwa unyenyekevu tunakubali kuwa hata sisi tunafanya makosa na sisi sio bora zaidi kushinda watoto wengine wa YAHUVEH. Haya pia yapo katika kinaza sauti ili tunapoyaandika haya tunayaongeza pia kwa yale yaliyoandikwa. Tulijaribu kuyaweka haya kwenye mtandao tarehe 12/31/02 lakini tukajipata katika mashambulizi makali ya kiroho na sasa ndipo tunapopata nafasi ya kuitoa. YAHUVEH Alijua haya yatatendeka kwa hivyo lazima ilikuwa katika mpango wake.

* * * * * * *

(Neno la Kibinafsi) Watoto WANGU, Nileteeni MIMI swali moja kwanza alafu nyingine. Elisabeth [Elisheva] unakimbia katika hatua nyingi sana, katika pande zote tofauti. Je, miguu yako inaweza kuenda pande mbili tofauti au pande nne tofauti mara moja. Hii ndiyo sababu MIMI husisitiza chukua hatua moja alafu nyingine. Sawa [Ninacheka] tutauliza tena, “Ni swali gani unalotaka tuulize kwanza Baba”? [Nilikuwa nimeuliza wakati wa maombi na kuzungumza katika ndimi kuhusu maswali 4 au 5 ya kibinafsi] O Wow! [Bado ninacheka, tunafaa kutaka kujua tu hatua ifuatayo lakini mimi hutaka kujua ishirini, lakini ninajifunza.] [Nilianza kucheka na kuomba katika ndimi kama sijajua kuwa unabii ulikuwa unakuja] Mungu Baba YAHUVEH ni hatua gani inayofuata. Sawa, Ninatubu kwa kujaribu kutembea katika pande nyingi wakati mmoja. Ni hatua gani ifuatayo leo [Akiomba katika ndimi za Mbinguni] Ninasikia sehemu ya unabii unaojaribu kuzungumza na Baba pia ninasikia mahitaji yetu ya kibinafsi na nimechanganyikiwa kwa sababu sijui ni yapi wataka kuzungumza kwanza. Wanangoja kulisikia neno kutoka kwako Baba, sisi pia.” (Akiomba katika ndimi) Unabii wa 69 unatoka.

* * * * * * *

UNABII 69

Mnapoingia katika mwaka wa 2003 watu wenye dhihaka watawazunguka. Watasema “Wapi huyu YAHUSHUA ambaye mnasema yuaja?” lakini nina neno kwenu. Ninawakumbusha watu wenye dhihaka walivyomzunguka Nuhu. Haya mambo lazima yatakuja kutendeka. Ni njia YANGU ya kuwatenga makapi kutoka kwa ngano. Jaribu kunikejeli MIMI. Huu ndio ujumbe Ninaowapa maadui, kwa adui yeyote wenu ni adui WANGU. Adui ni mtu yeyote anayejiweka dhidi ya jumbe Ninazokupa, kwa kweli Nimekupa upako kama msemaji WANGU. Maadui wanapozungumza dhidi ya jumbe hizi zinazotoka Mbinguni, wanazungumza dhidi ya MIMI, YAHUVEH, na MWANA WANGU Mpendwa YAHUSHUA.

Usifikirie kuwa wanakukataa wewe Binti YANGU, kwa kuwa wananikataa MIMI. Kwa kuwa hata mnabii bandia huchukua jumbe hizi Ninazokupa na wanazisoma na kuzinakili kuzifanya ziwe ni kama maneno haya Ninayozungumza kwako yanatoka kwao. Usishangae Binti YANGU, kwa kuwa si shetani pia anajua ukweli hutoka mdomoni mwako na ni MIMI, YAHUVEH, Ninayeweka maneno haya mdomoni mwako. Bandia wanajitokeza na watu kudanganywa, ili wachukue maneno haya na kuyageuza katika yale ambayo sikutarajia.

Kunakuja wakati wa Walinzi Kubadilishwa. Haya ndiyo mtakayoyaona katika mwaka wa 2003. Kubadilishwa kwa Walinzi katika polisi wenu, katika serikali yenu, kisiasa na kiroho yaja, Kubadilishwa kwa Walinzi. Hawa ni Walinzi waovu wajao; watachukua kazi kutoka kwa wale Niliowaweka pale hapo awali. Wao ni wafanyikazi wa shetani watakaochukua uhuru wenu na kuwasababisha Watoto WANGU kulia KWANGU na kupiga mayowe kwa hofu, wengi watasema, “O YAHUVEH tunaweza kukupata wapi, O upako wa RUACH ha KODESH mbona hauzungumzi?” Mtanipata MIMI wapi Watoto WANGU kwa kuwa ni kanisa chache zimo na Roho WANGU ndani yao.

Nitawaambia ni wapi mtakaponipata MIMI; itakuwa kwa kibinafsi, MIMI na wewe. Jikaze na ushikilie pindo la vazi la YAHUSHUA, kwa kuwa wengi watapitia matopeni, wengi wenu mtapitia kwenye theluji ya barafu, wengi wenu watapitia joto la jua. Yale yaliyokuwa rahisi kwa wengi katika mwaka wa 2003 yatakuwa magumu. Watoto WANGU wengi wanaosikiza na kuitambua sauti YANGU kupitia huyu Binti YANGU lakini wanataka kutoa neno hapa na pale ili liwe vile wanavyofikiria, ni kama inaweza kuyazuia Maneno YANGU na kuyafanya tupu.Yale Nitakayoyatabiri yatakuja kutendeka! Waombezi WANGU wa kweli inukeni na ulizeni muda. Mliniuliza MIMI, “Mbona haya yalifanyika na Richard Eby, haya ndiyo maneno Ninayo ya kuzungumza kwa sasa. Richard alikuwa amechoka, afya yake ikizidi kupunguka. Richard alikuwa na hamu na alihuzunika kila siku akitaka kuuona mlango wa Mbinguni tena, kwa kuwa mnaona Watoto WANGU maombi yenu yamezuia kuja kwa YAHUSHUA. Sikuenda kinyume na alichotaka Richard, kwa kuwa aliniomba MIMI siku baada ya nyingine. Hakukuwa na kitu kingine ambacho alitaka kimweke hapa duniani, aliuona utukufu WANGU na aliutaka tena. Hata sio upendo wa familia na marafiki zake, hata sio kazi Niliyokadiri afanye, na hii ilikuwa kumngoja YAHUSHUA aje; hakutaka kuwekwa hapa.

Lakini kwa kweli Watoto WANGU, kuweni makini, andikeni chini kila kitu kwa siku ile alikufa na kuwa mbele ya uso WANGU pale Mbinguni, kuweni makini kwa yale yaliyokuwa yakifanyika duniani humu, kwa kuwa alikuwa kipimo cha joto, barometa, na shetani anajua haya, ndio sababu alijitokeza na kuringa kwa dunia kuwa anaweza kutengeneza mwanadamu (clone). Mnaona kuwa yale yaliyokuwa yanafanywa kwa siri kwa miaka mingi sasa ndipo yanapoonekana mbele ya masikio ya dunia. Mnajua Watoto WANGU kwa kweli hizi ni nyakati za mwisho wakati mwanadamu anasema, “Nimekuwa mungu” kwa kuwa hakuna yeyote ila Muumba mkuu MIMI, YAHUVEH, Naweza kuiweka roho na nafsi katika mwanadamu, kwa hivyo hivi ni viumbe visivyokuwa na nafsi, vilivyo chini ya ghadhabu ZANGU. Ni shetani aliyewapa maarifa hayo kunikejeli MIMI tena. Lakini Ninawaambia Watoto WANGU, hakuna chochote kinachoweza kufanyika ambacho sijakiruhusu.

Kwa wale wanaojaribu kunikejeli na kusema kuwa jehanamu haipo, kuwa ni fikra zao tu, hawatajipata jehanamu tu lakini wataogelea kwenye Ziwa la Moto. Kwa wale wanaokejeli kuja kwa pili kwa YAHUSHUA, Ninawaambia haya mara moja tu na sitawaambia haya tena, YEYE haji kwa Kanisa. Yeye haji kwa Kanisa zilizojipanga. Yeye anakuja kwa Bibi Arusi WAKE. Na sio yeyote ambaye anaitwa Bibi Arusi wa YAHUSHUA, je ni waaminifu, ni wa kweli, wana imani. Watachagua kumtii YEYE. Je, wanatembea katika utakatifu mbele YANGU. Jina LANGU lipo mdomoni mwao kila siku. Wanalia katika Jina la YAHUSHUA. Au wanazitupa amri ZANGU kumi chini, kuzikanyaga chini ya miguu yao mpaka zikawa vipande kwenye sakafu. Wanaambia watu waache kusikiza njia za kale kwa kuwa tunafanya vitu kwa njia mpya, tunafanya vitu tunavyotaka?

Hili ndilo ishara Watoto WANGU, Ninapowatenga, kwa kuwa wale ambao wana alama wana mhuri wa ulinzi WANGU. Malaika wanawajua kwa alama kwa mwaka huu wa 2003. Maovu yatawaangukia wale wanaojiita kwa Jina la Mwana WANGU na watashangaa ni kwa nini. Ni kwa sababu ya haya, kwa sababu mmejaribu kunikejeli, kwa sababu mnajaribu kurusha nje yale Niliyoyazungumza, kwa sababu mnamwangalia mjumbe na sio ujumbe. Mnamwona mwanamke tu, na kwa sababu hamwezi kuuangalia uso WANGU wa ghadhabu mnamrushia maneno yenu, lakini Ninataka mjue, hamna neno moja mliyozungumza ambalo halijafika masikioni MWANGU mlipomshambulia kwa hivyo pia mmenidunga kwa sindano machoni MWANGU, kwa hivyo mtakapolia kwa uchungu, sauti zenu Nitazichukia.

Nyinyi mnaoishi katika kiburi na utukufu, umaarufu na mali, mnawadharau Manabii na Mitume WANGU, kwa kuwa matumbo yenu yana chakula, nguo nzuri zilizo migongoni mwenu, mna pesa nyingi na kuzidi, mmebarikiwa. Lakini mnaona hamjajua maana ya kuteseka. Lakini kwa mwaka wa 2003 mtajua. Itakuwa mwanzo wa mateso kwa wale ambao wanafikiria kuwa wako juu ya ghadhabu ZANGU. Ghadhabu ZANGU zitawaangukia. Sitajirudia tena, kuwaambia jinsi dunia hii itakavyotikisika kwa kuwa YAHUSHUA Anapokaribia tayari Nimetabiri kuwa dunia hii itatikisika kwa kuwa hata dunia hii hutikisika kwa hofu. O mwanamume na mwanamke mjinga. Hata wakati dunia hutikisika kwa hofu mnakejeli na kukataa kuwa MIMI Nipo hapa.

Mnategemea sayansi kama mungu. Mnategemea siasa kushughulikia mahitaji yenu. Kizazi hiki, Wajinga, Wajinga, Wajinga! Mnategema maarifa ya dunia hii na mnadharau Kitabu CHANGU kama kizee, kitabu kilichojawa na ukweli na maarifa, Kitabu ambacho Manabii walizungumzia. Ondokeni, Ondokeni, Ondokeni karibu NAMI, ondokeni karibu NAMI na ibada yenu ya kukufuru mnapojaza kanisa katika siku ya Jumapili na kuwafukuza wanaoabudu Sabato. Nitawaonyesha tena, kwa kweli hukumu huanza katika nyumba ya YAHUVEH. Tena YAHUSHUA Atawachapa wanaobadilisha fedha na kuwafukuza wakipitia mlangoni.

Sasa Nimewaonya juu ya ndoa zisizobarikiwa, lakini mnang’ang’ania wachumba wenu. Mkijua kuwa Jina LANGU na Jina la YAHUSHUA wanachukia. Kwa hivyo, wang’ang’anieni wachumba wenu. Fanyeni Nilichowakataza kufanya. Hamwoni Watoto WANGU, kuwa Nina mazuri zaidi inayowangoja. Yale ambayo MIMI sijaunganisha, yule ambaye jina lake halipo katika Kitabu cha Maisha cha Mwanakondoo. Yule ambaye unang’ang’ania kuwa bwana au bibi yako, watakuuza kwa mkandarasi mkuu katika nyakati zijazo za maovu. Hawa watakuwa Watoto WANGU ambao hawakutambua kuwa hawakuwa sawa mpaka watakapopoteza vichwa vyao.

Ni wangapi kati yenu mnaokimbia wito zenu na mtasikia huyu Mtume akizungumza na kusema, “Ninasimama nyuma ya huduma hii lakini fungu la kumi na sadaka zetu tutaziweka.” Je, hamtambui kuwa kuongea ni rahisi. Kama hamsaidii, mnamzuia, mkiyachukua maneno Ninayozungumza, na mtasimama mbele YANGU katika Siku ya Hukumu na Nitawauliza, “Je, mlimsaidia katika njia yoyote?”

Mapigo yaja na mkitegemea Serikali kwa ulinzi, mkitegemea madaktari kwa ulinzi, Nishawaambia kitakachotendeka. Hamna chochote kinachoweza kutendeka Watoto WANGU ambacho sijawaambia mitume na Manabii WANGU kwanza. Hata wale waovu juu ya mlima husikiza, ingawa hawanifuati MIMI, wanatikisika kwa hofu wakijua kuwa Ninazungumza siri ZANGU ambazo binadamu yeyote hajasema. Ni wangapi kati yenu mnaokimbia wito zenu? Ni wangapi kati yenu mnaowaacha wengine wa injili kuongea. Ni wangapi kati yenu mnaoyasoma haya au kusikiza, mpo nje kwa viwanja vya mavuno au mnasaidia kukusanya katika mavuno haya ya nyakati za mwisho.

Ndio, Nitakuwa na watakaouawa kwa kweli kama damu yake Stefano ilimwagwa chini kulikuwa pale na mwanamume aliyesimama aitwaye Sauli, ambaye Nilibadilisha jina lake kuwa Paulo. Wakati damu ya Stefano ilipomwangukia yeye, aliposhika koti lake, upako wa Stefano ukamjia Sauli ambaye akawa Paulo. Kwa hivyo Ninayoyasema Ninaposema haya ni damu ya wanaouawa sio bure. Inainua Stefano wengine, Sauli wengine wanaokuwa Paulo. Kwa wale wapendwa WANGU Ninaowaamini waliojawa na upako WANGU wanaonitafuta MIMI kila siku na kuomba, 2003 itakuwa na Baraka kwenu Ninapoichoma takataka kutoka kwenu. Kwa kuwa imani yenu Watoto WANGU ina thamani kuu kushinda dhahabu. Jifunzeni kunisifu MIMI Watoto WANGU, katika yote maishani.

Ninasikia maombi ya wale wanaokuja KWANGU na moyo wa asante. Haya ndiyo maombi yanayonifurahisha MIMI sana. Kama ilivyokuwa katika nyakati za Musa hawa ndio Watoto Nitakaowashughulikia na kuwalisha. Kwa hivyo ujumbe huu si wa wale wanaokejeli. Ujumbe huu si wa kila mtu, ni kwa wale tu walio na masikio ya kiroho kusikia; ni kwa wale tu walio na macho ya kiroho kuona na wataosikia hata sauti YANGU Nikizungumza.

Ninatuma neno hili hadi Israeli, Ninatuma Mtume huyu kwenu kuwaambia, jihadharini na wale wanaokuja kama rafiki, mkono wao umo ndani ya mfuko wako, wanakuibia. Na mkono ule mwingine wana kisu na wanasema, “Fanya ninachokuambia ufanye” lakini Ninawakumbusha Israeli, kama tu mtamlilia Mungu wa Abrahamu, Isaka na Yakobo, MIMI, YAHUVEH. Kama tu mtaacha kusikiza hawa rabi wanaokuambia msizungumze Jina LANGU Takatifu. Kwa kuwa Nina watu WANGU walio na upako walio pale Yerusalemu waliojawa na RUACH ha KODESH WANGU. Wamemkubali YAHUSHUA kama MASIHI na wananiita na kuniomba MIMI. Hii ndiyo sababu Israeli hawajaangamia mpaka sasa. Kwa kuwa ingawa Israeli mlikuwa mboni la jicho LANGU, sasa nyinyi pia mna mdudu ndani.

Israeli dunia hii haiwezi kamwe kuwaona katika Utakatifu. Kwa kuwa mna utoaji wa mimba, mna mashoga, mna picha uchi, hakuna dhambi ambayo haijapenya Israeli ndani. Mafarisayo sasa ndio wanaoongoza serikali yenu na bado hata hawana umbo la utakatifu. Nitawahukumu katika mwaka wa 2003 mikoa, mataifa ambayo yanafanana na Sodoma na Gomora KWANGU. Hata sitayazungumzia yale yatakayotendeka katika mwaka wa 2004, kwa kuwa mkifikiria kuwa hukumu YANGU ilianguka mwaka wa 2002 na dunia haiwezi kupumua kwa mwaka wa 2003, maneno haya yatakuwa ya hofu sana hata mtume huyu ataogopa kuzungumza.

Kwa hivyo wapendwa WANGU, Nina ujumbe huu kwenu. Chukueni hatua moja kwanza alafu nyingine, kwa kuwa mwaka wa 2003 sanasana, haya tu ndiyo mnayoweza kuyashughulikia. Nisikilizeni MIMI, sikieni Maneno YANGU, jifunzeni kunitafuta MIMI nyinyi wenyewe. Maneno haya Ninayoyazungumza kupitia huyu binti Nitayathibitisha tena. Je, kuna yeyote anayetazama vile vitu hutendeka kwa haraka baada ya maneno haya kuzungumzwa kutoka mdomo huu. Ni kwa sababu sio maneno ya mwanamke tu; ni Mungu Mkuu “MIMI NIKO!”

Tena Ninasema, hamtajuana kwa majina yenu. Hamtajali mambo ya zamani ya mwingine. Mtatambua familia yenu ya kweli ya YAHUVEH na YAHUSHUA kwa upako ambao umo ndani. Sanasana kwa Mitume na Manabii Ninazungumza, Nimewatenga nyie kuyatega masikio yenu KWANGU, masaa 24 kwa siku mkiniuliza MIMI, “O Mungu Baba YAHUVEH ni maneno yapi unayotaka kusema?” Mmefanya miili yenu kuwa Hekalu ya Dhabihu. Mmekuwa tayari kuteswa kwa ajili ya Mwana WANGU YAHUSHUA. Msifikirie kuwa siwajali, sanasana kwa vile mlivyojitolea. Makuu, makuu, makuu yatakuwa thawabu zenu Mbinguni, lakini sitasahau kuwabariki hapa duniani. Hakuna chochote ambacho mmekitoa ambacho sitawarudishia mara 7 lakini ni kweli Watoto WANGU kuwa inakuja na mateso wakati watu wenye dhihaka, wale wanaohatarisha maisha yenu mtawaona.

Nimempa upako huyu anayezungumza. Watajua mahali watakapoenda na yale ya kufanya, sanasana katika mwaka wa 2003. Sitawaacha wapotezwe; itakuwa tu kama katika ndoto ya Elisabeth [Elisheva]. (Angalia Ndoto ya Kombora) (Nilikuwa na ndoto miaka iliyopita kuwa tulikuwa tunaoongoza umati wa magari kwenye barabara, magari mengi yasiyoweza kuhesabiwa, tulipata ufunuo juzi kuhusu ndoto lakini sasa sio wakati wa kuutoa.) (Angalia Ndoto ya Meteor)

Kwa ukweli umezungumzwa kutoka huduma hii. Ukweli huu ndio utakaookoa, kwa ukweli huja katika Jina la YAHUSHUA. Kwa wale ambao hunakili unabii hizi na kujifanya ni kama ni MIMI, YAHUVEH, Niliyezungumza kupitia mdomo wako, lazima utalipa gharama ya upako aliyolipa, Nitaiongeza mara elfu mia moja. Kwa kuwa umeiba kitu na haukulipa gharama, kama Nilivyomwambia Binti YANGU, upako ukiwa mkuu basi mateso yatakuwa makuu.Kwa hivyo Watoto WANGU mnapoingia katika mwaka wa 2003 wale Ninaowaita kwa kweli Watoto WANGU Wapendwa, Watoto, Bibi Arusi, Waliochaguliwa na Wateule, endeleeni kuniangalia MIMI. Endeleeni kuyasikia Maneno YANGU. Endeleeni kutii na kuamini na imani yenu itawafanya muwe wazima, imani yenu mnapoendelea kukua kiroho itanifurahisha MIMI. Iteni Jina LANGU mnapohisi ardhi inatetemeka na kutikisika. Iteni Jina la YAHUSHUA (wengine wanamwita YESU) Jina la pekee linaloweza kuokoa. Nikumbusheni MIMI Zaburi 91 ili mapigo yasije karibu na makao yenu; ficheni Neno LANGU ndani ya nyoyo zenu, ndio isiwe tu Kitabu lakini iwe sehemu ya mwili yenu. Ninawapenda nyie wapendwa WANGU. Bibi Arusi jitayarisheni kwa kuwa Bwana Arusi wenu yuaja. Wale wanaohisi hawawezi kulipa gharama ya Bibi Arusi, lakini wao humwona na kulia. Ni ukweli Watoto WANGU kuwa kuna Bibi Arusi mmoja tu. Kutii ni bora zaidi kushinda dhabihu.

Richard Eby hakudanganya. Alichoka na dhambi za dunia hii. Atapewa thawabu kwa miaka yote aliyoishi lakini hakumaliza kazi Niliyomtuma kufanya. Msiweke imani yenu katika mwanamke au mwanamume yeyote, lakini katika MIMI, YAHUVEH na YAHUSHUA pekee simama. Wekeni imani yenu kwa maneno, maneno YANGU katika Vitabu Vitakatifu, hivi ndivyo mtakavyojua YAHUSHUA Anarudi. Mwanadamu anaweza kufeli hata Nikimrudisha kufanya kazi fulani. Waona Watoto WANGU, Nilimruhusu kufeli, kutomaliza kazi hiyo. Kuwafunza nyote funzo, je imani yenu bado itabaki? Kwa wale kama Binti YANGU aliyeomba kuwa Richard Eby afufuke tena, hakuchagua kurudi duniani.

Mmepata onyo; yeye alikuwa kipimo cha joto na barometa katika siku iyo hiyo alikufa. Mnapotazama Sodoma na Gomora wakizungumza, mlipoona maovu yakiinuka. Anzeni kuhesabu sasa hadi Dhiki Kuu. Adhabu kwa maadui WANGU na wako, ingawa wanadhani hao ni vichwa, kwa kweli wao ni chini ya mikia. Kunakuja kubadilishwa kwa walinzi Watoto WANGU, wale walioshikilia vyeo kwa muda mrefu, wale walioandika amri zenu sasa watajipata bila kazi. Huzunikeni na kupiga mayowe Watoto WANGU, mnapoona kubadilishwa kwa walinzi. Kwa wale ambao walikuwa Watakatifu watabadilishwa na wale ambao ni waovu. Wale ambao mngewaamini, mfanyikazi wa benki, polisi, mwanaposta, walinzi wanabadilika. Madaktari wenu, walinzi wanabadilika. Serikali zenu, walinzi wanabadilika. Viongozi wenu wa kiroho, jihadharini na kubadilishwa kwa walinzi.

O lakini mnaona o maadui WANGU. Jihadharini na kubadilka kwa Walinzi WANGU. Ninawaweka wale na upako mkuu. Wale ambao ni wanyenyekevu mbele ya uso WANGU. Hawa ndio wapendwa WANGU Niliowaficha kwa siri; wanajua vile vya kuona Maneno YANGU na uso WANGU. Wanasimama katika pengo, wanalia katika Jina la YAHUSHUA. Kwa maadui WANGU kote duniani, jihadhari na kubadilika kwa Walinzi WANGU. Kwa kuwa wamekuwa watakatifu zaidi. Wamezidi kuwa wenye bidii na ujasiri. Watahubiri Utakatifu na watakemea dunia hii. Kwa hivyo jihadhari na kubadilishwa kwa Walinzi WANGU waliojivaa katika Vazi kamili la Vita (Waefeso 6) wasiokuja kwenu katika jina lao lakini huja katika Jina la YAHUVEH na YAHUSHUA. Wale wasiobeba silaha za vita za mwili, lakini kubadilishwa kwa Walinzi WANGU wana silaha za kiroho ambazo hazijajulikana.

Wako na ghala ya silaha yote ya Mbinguni na kile tu wanachotakikana kufanya tu ni kuniita MIMI katika Jina la YAHUSHUA. Wataaibisha kubadilishwa kwenu kwa Walinzi. Kwa hivyo jaribuni kunikejeli MIMI. Nyinyi waovu mnapobadilisha Walinzi wenu, MIMI pia Nimebadilisha Walinzi WANGU. Ni wale ambao hautatarajia, wanyonge wa wanaume, wanawake na hata Watoto. Ninazungumza nao sio tu kwa unabii zinazokuja kutendeka lakini pia katika ndoto na maono. Karama hizi zitazidi kukua na nguvu zaidi Ninapobadilisha Walinzi WANGU Ninaowainua na pia kuwashusha.

Jihadharini Kanisa walioonywa, Kubadilishwa kwa walinzi kumekuja na wanakaa katika viti vyenu na wanawauliza kuhusu maovu ndani yenu, kutotii ndani yenu. MIMI ni yuleyule YAHUVEH na sibadiliki kamwe, sio kwa yeyote. Maneno YANGU hayatarudi KWANGU tupu, sio kwa yeyote. Kwa sababu Binti YANGU aliomba na kulia na kuomba mbele YANGU aliposikia kuhusu kifo cha Richard Eby, kwa sababu wengi wenu mmeandika na kuuliza na wengi zaidi wanataka kuandika na kuuliza “Je, Dkt. Richard Eby alinidanganya?” Hapana, hakufanya hivyo. Dhambi yake tu ilikuwa hakuwa mtulivu na alikuwa na uchovu, lakini sikumlaumu.

* * * * * * *

Imezungumzwa siku hii ya Disemba 31, siku ya mwisho wa mwaka wa 2002. YAHUVEH na YAHUSHUA tafadhali tuhurumie tunapoenda katika mwaka wa 2003.

Nikiwasaidia wengine, kuwakera wengine katika Jina la YAHUSHUA ha MASHIACH. Ninabaki Dada yenu Mtume Elisabeth Elijah (Elisheva Eliyahu).

Iliisha Saa 6:45 Asubuhi.

Mwisho wa unabii, maelezo yanafuata

* * * * * * *

Niliamka Saa 5:00 Alfajiri na YAHUVEH Akaniambia nitafute uso WAKE, nije mbele ya kiti CHAKE cha enzi na kuomba. Nilipoanza kufanya hivyo, na nikasema “Lazima niombe katika ndimi kwa hivyo nitaenda sebuleni”. Nilianza kuomba…

Hii ndiyo sababu neno hili lilitoka nilipokuwa ninaomba na nikachukua orodha ya vitu kwa maombi kama kuhitaji RV, ambayo itakuwa ya kusafiri, ambayo tunaamini kwa amani tutaipata, na pia mahitaji yetu yote ya kibinafsi, na nilikuwa ninauliza maswali mengi wakati mmoja. Kama mnavyoona nilikemewa mbele ya dunia mzima. Kwa sababu kitu cha kwanza neno hili lilikuwa litoke. YAHUVEH Akatuambia hilo ndilo jambo la kwanza tulilopaswa kuuliza. Kwa ukweli ninawaambia kuwa hatukujua kuwa neno hili lilikuwa linakuja. Tulijua ujumbe mwingine unakuja kwa sababu jana Disemba 30 vita vya kishetani vilivyokuja dhidi yangu vilikuwa vikali zaidi. Lakini kama mnavyoweza kuona vita ni vya YAHUVEH na YAHUSHUA na Ushindi ni wetu. Kwa sababu leo neno lipya lilikuja, kutupa moyo, kukemea na nina matumaini, kujenga imani katika wale wanaohitaji imani, na kwa wale wanaohitaji kutubu na kutafuta uhusiano wa karibu zaidi na kutembea na YAHUVEH na YAHUSHUA kama wakati haujaisha, na wapoteze vichwa vyao.Tafadhali nakili haya na kuwaonya wengine na kutuma haya kwa mitandao mingine na tafadhali mtuweke kwa maombi. Tafadhali fikirieni kwa maombi kama mnafaa kuwa wasaidizi wa huduma hii ambapo sote tutapata thawabu sawa.

Upendo na Baraka katika Jina la YAHUSHUA,

Mtume Elisabeth Elijah (Elisheva Eliyahu)


Wasiliana Nasi

* * * * * * *