Unabii 5

NYINYI NI HAZINA ZANGU ZA SIRI, NYINYI NI SILAHA ZANGU ZA SIRI.

Ilipewa kwake Mtume Sherrie Elijah Machi 14, 1997


Nilianza kuomba katika lugha za RUACH ha KODESH na kilichofuata, nilihisi kuwa YAHUVEH alikuwa ananipa upako na ujumbe ufuatayo ukaja. Ingawa nilidhani kuwa itakuwa ya Danieli pekee yake ikawa ya watu wengi. Mbarikiwe mkiyasoma haya na mwone kama RUACH ha KODESH hatawaonyesha, kuwa ujumbe huu ni wenu pia.

Kama wewe hutafuta uso WANGU daima na kuniuliza MIMI, “Utanitumia mimi lini?” Basi ujumbe huu ni wako. Kama mwaweza kusikia sauti YANGU katika unabii huu, basi nyinyi, Wana WANGU na Binti ZANGU, ujumbe huu ni wenu. Roho WANGU atathibitisha ndani yenu kama ujumbe huu ni wenu. Kwa kuwa utatoa ushahidi kwa roho yenu ndani yenu. Wote wengine watabaki viziwi na haya yatakuwa maneno tu kwao. Watashuku kama kwa kweli ni YAHUVEH anayeongea kupitia huyu Handmaiden. Mkiyahisi haya, basi bila shaka ujumbe huu si wenu.

* * * * * * *

Watoto WANGU Wapendwa, nyinyi ni kama hazina za siri, nyinyi ni kama podo za mishale za siri, wanapoona tu upinde. Nitawatumia kuzungumza kwa ujasiri na mtafanya yote ambayo dada yenu anafanya, kuonya juu ya hukumu ijayo. Nyinyi pia ni walinzi kwenye mnara. Tazameni ishara angani kama Eliyah alivyofanya, kwa kuwa mtaonywa na tena mtapasha onyo hizi kwa wengine. Watoto WANGU, Nimewapa upako wa kutumia karama Nilizowapa. Hamjakuwa na imani ya kufanya haya, vile Nilivyowapa upako wa kufanya haya. Lakini siku hii Niliyoikadiri, mmekutana na Handmaiden WANGU na karama zake na zenu zimekuwa moja. Mmezikoroga karama hizi ndani yenu nyote. Msifikiri kuwa haya hayakupangwa, kwa kuwa nyinyi nyote ni moja katika Roho WANGU.

Neno LANGU ndani yenu huchoma kama upanga mkali. Upanga wenye makali mawili utakata ndani sana. Kuna moto mwingi uliofungwa ndani ya mifupa yenu na hamjui ni nini mtafanya nayo. Anzeni kuyanena! Maneno YANGU hayawezi kurudi KWANGU tupu, lazima ifanye yote Niliyoiita ifanye. Nimekuambia mengi kwa siri na bado haujayatoa kwa wengine. Sasa ndio wakati uo huo wa kupiga mbiu na kuonya juu ya adhabu inayokaribia kwa wale wanaokejeli au kutojali. Lakini, wakati wa baraka kwa wale wanaonitii na kutafuta uso WANGU kwa unyenyekevu, wale wanaosikiza sauti YANGU na Kondoo WANGU hujua sauti YANGU na hawamjii mgeni yeyote. Hawa hawana chochote cha kuogopa.

Ingawa kifo kimewazunguka na uwaambie, haitawadhuru wale ambao ni WANGU na kama wao ni shahidi, damu humwagika ardhini ili kuwaleta Paulo wengine ambaye mbeleni aliitwa Shaul na kuwazaa Stefano wengine. Nyinyi ni kama Stefano; nyinyi ni silaha ZANGU za siri Nilizozificha. Tena Ninasema, mnajua sauti YANGU na mmepata thibitisho usiku huu kutoka kwa mmoja wa Manabii WANGU. Mtatumika na mnatumika kwa njia kuu kwa wale ambao mshawagusa. Msidharau mwanzo mdogo kwa kuwa hata mti mkuu wa mwaloni ulitoka kwa mbegu ndogo. Nyinyi ni kama mti mkuu wa mwaloni wa utakatifu, utakatifu WANGU. Hamjajazwa na kiburi, wala sitairuhusu, kwa kuwa Nitawagonga kutoka kwenye kiimo chenu mkithubutu kuyajaribu haya. Mmebaki wanyenyekevu mbele YANGU, na Ninawapenda sana, kwa kuwa Ninawaona mkisoma hadi masaa ya usiku, Ninahisi upweke wenu na kushangaa ni wapi mnapotoka.

Nyayo za Watakatifu zimekadiriwa na YAHUVEH. Endeleeni kufuata nyayo ZANGU na kuelekeza wengine KWANGU. Fuateni nyayo ZANGU na kuelekeza wengine kwa mti wa Kalvari. Fuateni nyayo ZANGU na kuelekeza wengine kwenye milango ya Mbinguni. Nimewafundisha, sio binadamu. Nimewakadiri, sio binadamu. Nyinyi ni hazina ZANGU za siri, silaha ZANGU za siri, na Nitaanza kuwatumia kwa njia kuu katika hizi nyakati za mwisho, na msidangayike, hizi ni nyakati za mwisho. Lakini sio mwisho kwa Watoto WANGU, kwao ni mwanzo mpya wa ajabu.

Kurudi nyumbani kutatendeka na angalieni Watoto WANGU wote waliokusanyika kwenye meza ya karamu. Ndio, Wana WANGU na Binti ZANGU, mtakusanyika kwenye meza hiyo ya karamu hivi karibuni, kushinda mnachojua au kufikiria. Kwanza, anzeni kukusanya mavuno, kwa kuwa ni kuu na wafanyakazi ni wachache. Kejeli zinazidi Ninavyosikia wachungaji ambao mbeleni walihubiri Injili YANGU sasa wanahubiri injili yao. Wao hujiita miungu. Nitathibitisha kwao MUNGU YAHUVEH ni nani. Watajuta kwa kuyafunza haya kwa kuwa wengi wamepotea kwa sababu ya uongo huu. Wengi wamefariki na walishangaa kuwa hawakukutana NAMI; kwa sababu ni mwovu ambaye wao huona. Lakini msidanganyike kwa kuwa MIMI huwa sikejeliwi vivyo hivyo. Uongo mwingi unatajwa na hao waongozi wa kiroho ambao hapo mbeleni mliwaamini. Watajibu kwa yote wajuayo. Walihubiri uasi na kuibandika kama injili. Ninawaambia, watalipa kwa njia kuu. Kwa kuwa wao huniita MIMI Baba na hata hawafahamu MIMI ni nani. Lakini, sio nyinyi Wana WANGU na Binti ZANGU. Sio wale wanaoitambua sauti YANGU kwenye jumbe za kinabii Nilizompa Handmaiden WANGU.

Kondoo WANGU watajua sauti YANGU. Ingawa sauti ya mgeni watakayoisikia yaweza kutoka kwa mchungaji anayeheshimiwa, au kiongozi wa kiroho, mahali hapo kitambo wangewaamini, sasa hawawezi kamwe. Msimtegemee binadamu bali tu YAHUSHUA pekee kama kiongozi wenu wa kiroho. Je, wanachosema hawa viongozi wa kiroho inalingana na Neno Takatifu la YAHUVEH au wameichukua na kuibadilisha katika mfano wa binadamu? Lazima mmtegemee RUACH ha KODESH na yeye atawaongoza katika ukweli, na kuwapa macho na masikio ya kiroho ya kusikia. Mwamini kiongozi hadi RUACH ha KODESH atakaposema ni mwisho. Huduma nyingi zinaanguka mbele ya macho yenu. Ni mwanzo wa mwaka tu na yale Niliyoyatabiri yametendeka, na nyingi zaidi zitaanguka kabla mwaka huu haujaisha. Msihuzunike juu ya huduma au wachungaji walioanguka kwa kuwa walionywa.

Mhuzunike juu ya wale kondoo waliodanganyika na sasa wameacha kuniamini MIMI. Mhuzunike juu ya kondoo wanavyoenda katika pango la mbwa mwitu, kwa sababu hata kama wamevaa barakoa ya kondoo, watawala. Watawala kwa sababu tena kondoo wametawanyika katika kambi la maadui kwa sababu ya masikio yao yanayowasha. Chungeni masikio yenu Watoto WANGU. Chungeni macho yenu. Msidanganyike na yale ulimi huzungumza hata ingawa yanasikika kuwa nyororo kama asali; tambueni ni Roho ya aina gani inayozungumza. Tambueni na macho yenu, je, inalingana na Neno la YAHUVEH? Je, wanafikiria, ah ha, sasa nimesoma sana, nina ufunuo mpya na ufunuo huo hauwaleti nyote karibu nami, lakini huwasababisha nyote kuenda mbali NAMI. Kiongozi wa kiroho wa kweli atawaleta nyote karibu, akiwaonya, akiwapa moyo na kuwaimarisha. Kiongozi wa kiroho wa kweli hajajazwa na kiburi.

Wanajua kuwa wao si Mungu, hata yule mdogo. Wanajua wao ni nani; wameumbwa katika mfano WANGU kuumanisha kuwa wana pua, macho na masikio. Jamani; jiangalieni kwenye kioo, mnajua picha ni nini. Msiwaruhusu hawa walimu wapumbavu kuwapoteza. Nyote ni watoto Niliowakubali kuwa WANGU, Nina tu Mwana mmoja wa Kipekee, au sio? Lakini hata kama nyote ni watoto Niliowakubali kuwa WANGU, Ninawapenda kama Ninavyompenda Mwana WANGU wa Kipekee. Ambieni wengine juu ya yale Niliyoyazungumza usiku huu kwa sababu, ingawa ulianza kama ujumbe wa mtu mmoja yakawa pia maneno ya wengi. MIMI ni YAHUVEH, MUNGU wenu na MIMI sipotezi chochote. Hata mazungumzo haya yalikuwa yamekadiriwa. Kukutana kwenu ulikuwa umekadiriwa.

Ninawaambia sasa YAHUSHUA anawajia Bibi Arusi WAKE, na wasiomtarajia YEYE wataachwa NYUMA! Wale wasioishi kama anarudi siku yoyote ile, wataachwa NYUMA! Endeleeni katika shughuli ZANGU na mfanyeni kazi Niliyowaita mfanye. Haijalishi kama wanaamini, acheni yaya haya kati yao na MIMI. Kama katika siku zake Nuhu hawakuamini. Kama katika siku zake Lutu hawakuamini lakini msidanganyike, sauti katika Unabii hizi huzungumza kwa Watoto WANGU na MIMI sitaruhusu wadanganyike, isipokuwa watakapochagua haya wenyewe.

Ninapotuma ishara zaidi za ghadhabu YANGU, hasira dhidi ya Manabii wanaozungumza jumbe hizi itazidi. Lakini jueni haya, MIMI huwatuma Manabii daima kuonya kwa sababu ya upendo WANGU na huruma. MIMI sitaki yeyote ateseke wala kuangamia au kuteseka katika laana ya milele. Kwa hivyo, pigeni mbiu tena, wale walio na masikio ya kiroho ya kusikia wataisikia sauti YANGU vizuri na wengine wote watabaki viziwi na vipofu. Ni chaguo lao sio lenu.

* * * * * * *


Ilipewa kwake chombo hiki cha udongo 3/14/97. Njoo YAHUSHUA, njoo!
Mtume Sherrie Elijah