Unabii 57

JIHADHARINI NA FARASI BANDIA!Imepewa kwake Mtume Elisabeth (Elisheva) Elijah anayelia kwa sauti kama Yona kwa taifa kama Ninawi. Ninawi walitubu kwa msimu, Marekani je? Au hii nchi yetu nzuri iliyobarikiwa na uzuri na hapo awali iliyosimamia utakatifu na uhuru, wataendelea katika njia isiyoenda popote na kujipata kama Ninawi na Sodoma na Gomora? Mimi sio mtume na nabii tu niliotumwa na onyo hili kwake Marekani lakini swali ni hili, ni nani anayesikiliza? Utafanya nini na onyo hili la kinabii? YAHUVEH daima huwatuma mitume na manabii kupiga mbiu ya toba, kurudi katika utakatifu kwake MUNGU wa Uumbaji na Wokovu. Kwa sababu ya upendo na huruma ya YAHUVEH YEYE Anatuonya kabla ya kutuma hukumu YAKE.

* * * * * * *

Juni 30, 2002, 11:00 Asubuhi

Watoto WANGU, mnaniuliza niwe na huruma kwake Marekani, lakini MIMI YAHUVEH Nauliza, “Ni wakati upi watoto WANGU watanionea huruma?” Nishasema, “Jihadharini na Farasi bandia.” Tena na tena Nimemwambia binti huyu anayetabiri “Jihadharini na Farasi bandia.” Marekani nyinyi ni huyo Farasi bandia. Mnakuja kama Baraka kwa Israeli, mnakuja kama mkono wa usaidizi kwake Israeli lakini nyuma ya migongo yenu mmebeba kisu kilicholowa damu kuiweka kwenye mgongo wa viongozi wa Israeli.

Marekani nyinyi ni huyo Farasi bandia, lakini mtalipa gharama ya haya kama hamtatubu. Yeyote atakayesaliti Israeli ananisaliti MIMI, YAHUVEH na anasaliti Mwana WANGU YAHUSHUA. Yeyote ambaye ni adui wa Israeli amejiweka kama adui wa MIMI, YAHUVEH, Muumba wa Israeli, pia Muumba wa Marekani, na MIMI, YAHUVEH Muumba wa ulimwengu. Kiongozi yeyote anayejigamba na kujifanya kama mungu na kusema “Nitaangamiza Israeli” akitingisha ngumi yake katika uso wa MIMI, YAHUVEH muumba. Marekani kwa kweli mtalipa. Marekani tayari mshaanza kuchomeka, mnachomeka na hasira ZANGU. Mnalilia Marekani kwa huruma, na bado mnataka hata kuliondoa JINA la MUNGU kutoka kwa akili za watoto.

Watoto WANGU mhakikishwe na haya, wale ambao ni WANGU wapo katika safina YANGU. Wale wanaosikia sauti YANGU, na kulia kwa huruma, kwa kuwa mnaogopa Nitawapiga Ninapowapiga wale wanaokataa kutii, msiwe na hofu. Nina mifuko kote duniani na mko salama katika mifuko YANGU, kwa kuwa ghadhabu ZANGU si kwa watoto WANGU. Nitakapogonga, MIMI, YAHUVEH, Ninajua ni nani Nitakayegonga, YAHUVEH Anajua ni yupi wa kugonga, mkono WANGU hulinda wale Ninaowalinda. Hakuna yeyote anayeweza kuwapokonya kutoka mikononi MWANGU. Hata nywele moja vichwani mwenu haitashikwa isipokuwa Nikiiruhusu, basi Watoto WANGU watakuwa kama Stefano wengine walioinua Paulo wengine, na makuu yatakuwa zawadi zao mbinguni. (Matendo ya Mitume 6-7)

Nina hasira Watoto WANGU, kwa kuwa mnalia kwa huruma kwake Marekani lakini kiongozi wa Marekani anajiona yeye kuwa mungu, yeye sio mungu. Ninasikia vilio vya watu WANGU kule Israeli, ndio, hata za wale ambao hawamtambui Mwana WANGU YAHUSHUA lakini wananililia MIMI. Watoto WANGU, wanaheshimu siku ZANGU za Sabato, wanazifuata karamu ZANGU za Kiyahudi na kutii Torah YANGU. Israeli inabeba damu ya YAHUSHUA na Yerusalemu inabeba damu ya YAHUSHUA, ingawa hawaikubali. Marekani nyinyi ndiyo Farasi bandia. MIMI, YAHUVEH na YAHUSHUA sasa tunatabiri kupitia Binti YANGU, MIMI, YAHUVEH Nitaigonga hiyo Farasi bandia na Nitakapoigonga haitawahi kuinuka tena. MIMI, YAHUVEH na YAHUSHUA tutakata kichwa cha huyo farasi. MIMI, YAHUVEH na YAHUSHUA tutaikata miguu ya farasi huyo. Nyinyi Marekani hamtaweza kusonga tena na wafanyibiashara watalia kutoka mbali, watakapoona Marekani ikichomeka kwa mbali. (Ufunuo 18)

O Marekani, Ninawalilia nyinyi mnavyojitayarisha kusherehekea siku yenu ya kuzaliwa. Mnasahau kuwa ni MIMI, YAHUVEH Niliowatenga kwa utukufu WANGU na YAHUSHUA. Nyinyi ni mtoto mchanga sana lakini mnatingisha ngumi zenu katika uso WANGU, mnamkataa yule aliyewaumba. Onyo hili sio la watoto WANGU wanaoniabudu MIMI katika ukweli na upendo na hujaribu kutii. Onyo hili ni la wale waliojiweka kama adui ZANGU. Jihadharini Marekani! Nyinyi ni kama Farasi bandia. Israeli amekuwa rafiki yenu, sasa mnamfanya kama adui anayechukiwa. Viongozi wenu huenda kusalimu mkono mmoja na kudunga kisu kilicholowa damu kwenye mgongo wa Israeli na mkono mwingine. Mnasema uongo kuhusu Israeli. Hamripoti ukweli. Mnawafanya watu WANGU Waebrania kukaa kama wagaidi. Mnakanyaga migongo yao na uchumi wao.

Mnatuma hofu kote duniani na kusema, “Msiende Israeli, sio salama kupatembelea” na kumbe maadui Palestine wanaochukia JINA LANGU, kwa dunia mnawainua kama mashujaa na haya mnatangaza kwa sauti ya juu. O Marekani, mnatoa ahadi hii kwa raia wa Palestine, kwa uongo mnasema, “Mimi Marekani nitawapa Israeli sanasana Yerusalemu kwa maadui wa MIMI, YAHUVEH.” Raia wa Palestine wamejiweka kama maadui wa YAHUVEH na YAHUSHUA. Raia wa Palestine wamewauwa watoto WANGU Waebrania. Raia wa Palestine wanajaribu kuiba mboni ya jicho LANGU. Kwa hivyo Marekani, kwa kuwasaidia mmejiletea ghadhabu ZANGU na Marekani hata jina lenu, MIMI YAHUVEH na YAHUSHUA sasa tunachukia. Nimekuwa na huruma mpaka sasa, kwa vilio vya watoto WANGU wa kweli wanaolia. Lakini watoto WANGU wa kweli lazima wajue haya, Niliposhikilia ghadhabu ZANGU kwa muda, hasira ZANGU MIMI, YAHUVEH na YAHUSHUA, zilizidi na Marekani mtalipia haya.

Kwa hivyo huu ndio ujumbe kwa watoto WANGU wapendwa, pakeni mafuta nyumba zenu tena, lilieni huruma kwa nyumba zenu na MIMI, YAHUVEH Nitawasikia watoto WANGU, tena. Tubuni watoto WANGU kwa nyumba zenu, kwa kuwa hamwezi kutubu kwa dhambi za Marekani. Kwa kuwa uvundo wa dhambi hizi umefika mbinguni na wote mbinguni wamefunga pua zao kwa kuwa hakuna taifa lingine lililofanya yale ambayo Marekani imefanya na kuwa hakuna taifa lingine lililobarikiwa kama Marekani ilivyobarikiwa. Mnataka kuondoa “Taifa moja chini ya MUNGU” basi mtakuwa na taifa moja chini ya miguu YANGU. Mimi YAHUVEH Nitawakanyaga, kwa kuwa mmeondoa huruma yenu, mmeondoa Neema ZANGU. Mnataka kuondoa “Katika MUNGU Tunaamini” kutoka kwa sarafu yenu alafu mtakachokuwa nacho ni “Katika (Marekani) Tunaamini”.

Nitawaonyesha ni nini kinachofanyikia taifa ambalo haliko chini ya ulinzi wa MUNGU YAHUVEH na YAHUSHUA, haitakuwa jambo la kufurahisha. Mtagundua Marekani, vile mlivyo wadogo sana katika nguvu zenu. Mnataka kuondoa “Katika MUNGU Tunaamini” alafu Marekani mlichobaki nacho ni “Katika sisi tunaamini.” Papo hapo mmetaja kuwa MIMI YAHUVEH, MUNGU Aliyewatenga Ameondoa huruma YANGU, mmeondoa ulinzi WANGU, kwa kuwa mnajiamini nyinyi wenyewe na kwa hivyo Marekani acheni dunia ione kinachofanyika mnapojiamini nyinyi wenyewe.

Canada, MIMI, YAHUVEH na YAHUSHUA Ninawapa onyo hili. Msifuate katika nyayo za dada yenu. Mnajiita Marekani Kaskazini, sasa mnabeba jina Ninalochukia, msipotubu na kuacha dhambi za Marekani, hatima ya Marekani itakuwa yenu. Mtashiriki nyote katika huzuni; mtashiriki nyote kwa ghadhabu ZANGU, msipofuata nyayo za YAHUVEH na YAHUSHUA. Njooni mjitenge sasa Canada, Wakristo wa Canada, anzeni kuombea Canada, kwa viongozi wenu wa siasa wameuza mikoa yenu kwa wazabuni wakuu. Katika Marekani kuna mikoa ambayo imejaribu kuachana na Marekani, kwa aibu walioihisi na kuna mkoa uliojaribu kujitenga kutoka Canada (Quebec) kwa aibu walioihisi. MIMI, YAHUVEH Ninawatambua wale waliojaribu kujitenga na MIMI, YAHUVEH Nitawatenga katika siku hiyo na ghadhabu ZANGU kamili hazitawaangukia siku hiyo.

O Marekani, Ninajua mipango yenu, viongozi wenu wa siasa wanataka kumbadilisha Arafat. Arafat ni mdogo wa maovu mawili. Kiongozi wa Palestine atakayekuja atafanya Arafat kukaa kama kijana wa shule. Atakuwa msaliti, atakuwa Yuda, atakuwa kama Yuda. Atawasaliti watu wake. Ni muda mfupi tu, alafu Arafat ataondolewa. Lakini ole wale watakaoshangilia kuondolewa kwa Arafat, kwa kuwa maovu makuu yaja. Kwa wale wanaofurahia wataomboleza. Wale wanaocheka sasa watakemewa. Viongozi wa siasa Marekani watalipa gharama kuu kwa kujaribu kuuza Israeli kwa mzabuni mkuu, yote kwa motisha zao wenyewe, yote kwa ulafi wao wenyewe.

Maovu makuu yaja, zaidi ya mnavyoota au kufikiria. Ole wake Marekani kwa kuwa mmecheza katika mkono wa shetani, mmejiingiza katika mipango ya mpinga-kristo, mmejiingiza katika mpango ulioandaliwa na mpinga-kristo ujao. Ni nyinyi Marekani Ninaowaagiza sasa. Nyinyi ni Farasi bandia na kwa haya mtalipa. Marekani furahieni ustawi wenu, furahieni anasa yenu, furahieni ulafi wenu, furahieni umaarufu wenu na furahieni bahati yenu, kwa kuwa itakuwa kwa muda mfupi tu. Watoto WANGU wa kweli wanaoishi Marekani, lazima mtubu mnavyojiita raia wa Marekani, msiache damu ya Marekani ipatikane mikononi mwenu.

* * * * * * *

Imezungumzwa na kuandikwa katika upako wa RUACH ha KODESH (Roho Mtakatifu) iliyopewa kwa huyu binti aliye Mtume na Nabii wa YAHUVEH na YAHUSHUA Tarehe Juni 30, 2002 Saa 11:00 Asubuhi. Kwa unyenyekevu, imepewa kwake Mtume binti Elisabeth (Elisheva) Elijah akiongea kwa simu na ndugu mwaminifu na msaidizi wa huduma hii anayeitwa Brian. Tulikuwa katika maombi wakati RUACH ha KODESH Aliponizuia kuomba kwa Kiingereza na kwa mshangao neno hili likaja. Tafadhali, Wakristo Marekani, tubuni na ombeeni nchi hii, iliyokuwa nchi ya walio huru, kabla wakati haujaisha. Tafadhali ombeeni amani ya Yerusalemu na pendeni ndugu na dada zetu wa Kiyahudi kwa kuwa sote tunamtumikia Mfalme wa Wayahudi, Masihi wetu na MUNGU ambalo jina ni YAHUSHUA.

Tafadhali ombeni na kuwaomba viongozi wetu kutoenda dhidi ya Israeli. Tunajua ya kwamba imani yetu ya Kikristo katika YAHUVEH na YAHUSHUA na maandiko ya Bibilia ni kweli, kwa kuwa Israeli haitawahi kuangamizwa. Israeli daima itasimama. Jihadharini Marekani na mataifa mengine kwa kuwa hamjapewa ahadi hii katika Maandiko Matakatifu. Kama Israeli ingeangamia basi tunachoamini ingekuwa uongo. Bibilia ni neno lililokuwa mwili kupitia YAHUSHUA, na YAHUSHUA siku moja ataukanyaga mlima wa Mizeituni kwa miguu yake miwili na kutawala Yerusalemu. Tunatarajia siku hiyo ijayo na tunasema “Njoo YAHUSHUA, njoo haraka, ndilo ombi letu! (Ufunuo 22:6-7, 12-13, 17, 20)

Tafadhali isome. YAHUSHUA ha MASHIACH wetu, anarudi. Je, utakuwa tayari?

* * * * * * *