Unabii 42

JISALIMISHE!!!

Maadui Wangu Wekeni Silaha Zenu Chini!

Za Kiroho na Kimwili!

Imepewa kupitia Mtume Elisabeth Sherrie Elijah (Elisheva Eliyahu)

Disemba 18, 2000

Haya maneno yanatoka kwenye Unabii wa 105, YAHUVEH alisema yaongezwe kwenye Unabii zote kutoka sasa: Nilikuonya kitambo Elisabeth [Elisheva], kutoita Huduma hii kwa jina la mwanamume au mwanamke. Hata kabla kuwepo na Huduma, Niliiweka ndani ya roho yako. Kwa kuwa hakuna lolote lililofanyika kwa mikono yako. Hakuna lolote lililotoka kwenye kinywa chako. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUVEH aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUSHUA, MASHIACH wako aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha RUACH HA KODESH, IMMAYAH wako aliyeizalisha. Kama ingekuwa tu kwa mkono wako, ingekuwa imefeli kitambo. Ni kwa UPEPO WA SHKHINYAH GLORY unaovuma kote duniani, UPEPO TAKATIFU WA UAMSHO. Sio kwa pumzi yako, au ingekuwa imefeli. (Isaya 42:8)

Katika mwezi wa Julai 2010, MUNGU YAHUVEH pia Alisema kuongezwe yafuatayo mbele ya Unabii zote kutoka Kitabu cha pili cha Mambo ya Nyakati:

2 Mambo ya Nyakati 36:16, “Lakini waliwadhihaki Wajumbe wa MUNGU, na kuyadharau Maneno YAKE, na kuwacheka Manabii WAKE, hata ilipozidi Ghadhabu ya BWANA juu ya Watu WAKE, hata kusiwe na kuponya.”

* * * * * * *

O jisalimishe Ndivyo Asemavyo YAHUVEH. O jisalimishe, jisalimishe, jisalimishe. Tena Ninasema kwa maadui WANGU, maadui wanaozunguka Huduma hii ya Utume/Kinabii iliyo na upako, huyu binti WANGU Elisabeth Sherrie Elijah [Elisheva Eliyahu], maadui waliozunguka Huduma zingine za Utume/Kinabii zilizo na upako, Ninaizumgumza tena, wale waliozunguka Israeli, wale waliozunguka Yerusalemu, wekeni silaha zenu chini zote za kiroho na kimwili kabla MIMI ELOHIM Mkuu “MIMI NIKO” Nisababishe moto kuanguka kutoka Mbinguni na Nitawaangamiza nyote kabisa (Ezekieli 38:23-24).

HOFU, HOFU, HOFU, vilio na maombolezo, vifo na mazishi mengi mpaka hakutakuwa na nafasi ya kuwaweka makaburini. Mkono WANGU wa hukumu, ambayo hapo awali iliwapiga, itageuka kuwa ngumi na Nitawafinya. MIMI Elohim Mkuu “MIMI NIKO”, katika huruma YANGU, Naonya kila taifa, kila mtu, kila ukoo, kila ulimi, acheni Yerusalemu WANGU mpendwa. Damu ya waliouawa imelowa mchangani na hulia KWANGU MIMI. Damu ya waliouawa pale Israeli haijakuwa bure. Ninasikia vilio na maombolezo makuu, ya watu wanipendao MIMI, YAHUVEH. Ninasikia Jina LANGU likiitwa na wale wanaouawa.

Ni nchi gani, ni taifa gani iliyo na uaminifu, ni mkoa mgani, jimbo gani, kisiwa gani walio na upendo na uaminifu kama Israeli wanavyoonyesha wanapopigana kuiweka ardhi yao, ambayo Elohim Mkuu “MIMI NIKO” YAHUVEH Aliwapa baba zao kitambo? Ninazungumza kwa viongozi wa kiroho, kumbukeni Daudi na Goliathi? Daudi hakumkimbia Goliathi, lakini alikimbia kwake Goliathi, akijua ya kwamba vita ni VYANGU. Maadui sasa wanaleta miungu katika nchi yenu o Israeli, na kumbe wao si mungu hata. Wanawake na wanaume wa maadui wanaleta mafunzo yao ya uongo na kujaribu kuwachanganya watu wa Israeli katika mfano wa utumwa ambayo sijakadiri. Israeli, Ninazungumza kupitia binti huyu, kumbukeni nyinyi ni nchi ya maziwa na asali, nyinyi ni nchi Abrahamu alibariki, hamna chochote cha kuogopa, isipokuwa kuogopa kwenyewe.

Tangulieni kila vita kama ilivyofanywa hapo awali na waimbaji, nyimbo za kusifu, kuabudu na maombi. Je, hamwamini maneno yaliyomo kwenye Torah? Israeli, nyinyi ni taifa ambalo dunia haielewi, mnachukiwa na kutukanwa, mnachukiwa bila sababu. Kwa kuwa mnatamani amani na bado hamjawahi kuwa na amani. Mnapeana ardhi na nyumba ambazo zijawaambia mpeane, ili kuwe na amani. Je, hamjui ya kwamba mkizidi kuwapa, ndipo watakapotaka zaidi? Hamjui ya kwamba hamwezi kufurahisha roho ya ulafi? Niangalieni MIMI o Israeli, tena, kwa kuwa Elohim Mkuu “MIMI NIKO” YAHUVEH Ndiye mkombozi wenu.

Sherehe ya Hanukkah yaja, kwa wale wanaofuata sherehe hii, tarajia miujiza tena kwa kuwa MIMI ni Nuru itakayomulika njia yako kwenye giza. Wafunike viongozi wenu katika maombi kwa sababu wanatafutwa na shetani kama chembe za mchanga. Mlidanganywa na viongozi wenu mliowaamini kutoka kwa wale wadogo kwa wakubwa kwa faida mbaya ambayo haitaweza kununua nafsi zenu. Fungeni na kuomba, ili Mapenzi YANGU kamili yatimizwe kwa kuwa Nimejawa na hasira kwa sababu ya mauaji, kudanganya na uongo unaofanywa.

Ninawaamrisha nyote mwombee amani ya Yerusalemu. Mkidhani ya kwamba ni kubaya sasa hivi, mauaji yameanza tu, lakini msiogope kwa kuwa Baba yenu Elohim YAHUVEH anaona na kusikia. Amri YANGU ya mwisho ni kubariki wao wanaokubariki o Israeli, msiwakatae wale wanaowapenda Israeli, Yerusalemu, au watu WANGU Niliowachagua. Nitawabariki wote wanaokubariki o Israeli! MIMI Elohim Mkuu “MIMI NIKO” Nitawalaani wote wanaowalaani Israeli.

Onyo kwa maadui WANGU, kumbukeni punda wa Balaam. Msiwe kama Balaam (Hesabu 22-24). Ninafanya zaidi, Ninazungumza kupitia huyu Mtume na kuwaonya uharibifu utakaowafanyia wengine yatawarudia mara saba zaidi. Baraka mtakazowapa Israeli na watu WANGU Wayahudi zitawarudia mara saba zaidi. Baraka au laana, amueni, Kumbukumbu la Torati 28 haidanganyi. Imezungumzwa, imeandikwa Disemba 18, 2000. Saa 2:53 mchana na kwa kweli katika wakati WANGU haya yatatendeka.

Nikiwakera wengine, na kuwafunulia wengine. Imepewa kwake mtoto, shujaa, bibi arusi WANGU, Elisabeth Sherrie Elijah (Elisheva Eliyahu)

* * * * * * *

Nukuu binafsi kutoka kwake Mtume Elisabeth Elijah (Elisheva Eliyahu)

Kama unabii huu umekupa moyo au kukubariki, tafadhali tuma barua pepe au niandikie kwenye anwani inayofuata na tafadhali nikumbuke kwa maombi. Usaidizi wowote kwa kutupa moyo au kwa hela inakaribishwa. (Elijah [katika Kiebrania, Eliyahu]) ni jina langu na sioni haya kuwa mimi nina damu ya Kiyahudi ndani yangu).


* * * * * * *