UNABII WA 3

JIHADHARI NA WAPELELEZI WA SHETANI WALIO KATIKA MAKANISA!

Alipewa Rev. Sherrie Elijah
Januari 17, 1997

* * * * * * *

Wapelelezi ndilo jina ambalo watumishi wa shetani huwaita. Roho ya ibada ya uovu imejitokeza katika kanisa za injili kamili kwa sababu ya wapelelezi hawa. Lakini ukiwaona utawajua, kwa kuwa MIMI YAHUVEH ninawapatia, Kanisa Kweli ya YAHUSHUA ha MASHIACH (Yesu Kristo) macho mapya ya kuona, masikio mapya ya kusikia, mdomo jasiri ya kuongea na mikono mpya ya kuwafukuza nje. Kwa kuwa hizi ni mikono ZANGU, Nimeutokeza mkono WANGU wa kulia, mkono wa Utakatifu na kama Mwana WANGU alivyowafukuza waovu kutoka kwenye Nyumba ya YAHUVEH ndivyo itakavyotendeka tena.

Mwaka huu wachungaji waovu, wapelelezi, watafariki wanapohubiri. Kwa kuwa wanahubiri Neno LANGU kunikejeli MIMI. Lakini hawanijui MIMI, Neno lililofanywa kuwa mwili. Shetani anajua Neno, msidanganywe, na je, Ana hofu ya kutosha ili aache uovu wake, Hapana, na hawa wapelelezi pia hawaogopi kwa kuwa wameuza roho zao kwa shetani na watavuna uharibifu waliyopanda. Wengine wao ni wainjilisti, ingawa wanasema kuwa wanaelekeza roho kwake Yesu Kristo, ni Yesu tofauti wanaowaelekeza kwake, kwenye miguu ya mpinga kristo.

Watu basi huanza kumwabudu kiongozi na hii ndiyo ishara yenu. Wao huacha kunitafuta MIMI na sheria ZANGU na Neno na hutafuta neno kutoka kwa binadamu tu. Hawajali kuhusu kumkera Mwenyezi YAHUVEH ‘MIMI NIKO’ Mkuu na wa pekee lakini wao hujali kuhusu kumkera mchungaji wao aliye mpelelezi wa shetani, kuleta kuchanganyikiwa, kukata tamaa, uasi, uharibifu, umaskini, uongo, roho za udanganyifu na kuiba imani kidogo ambayo Kondoo WANGU walikuwa nayo hapo awali.

Watakapoanguka katika nguvu wakati mpelelezi anawaombea, hawaanguki kwenye miguu ya YAHUSHUA lakini kwenye miguu ya mpinga kristo na hata hawaelewi kuwa walikuwa wananitafuta MIMI, na kuwa roho ya kuthibiti akili yao imewafanya wanamtafuta mchungaji mwingine, mchungaji mwovu anayetesa kondoo wake na huwachinja akijua kuwa wataunga wapelelezi kwa kuwa wametolewa kama dhabihu kwake shetani. Jambo hili linaweza kuonekana kama jambo la kigeni lakini linatendeka katika Mkutano wa kanisa za Mungu, na kanisa za Kipentekoste na katika mstari kuu wa kanisa zote.

Lakini Nitawaonyesha kuwa YAHUSHUA ndiye Mchungaji Bora na mwaka huu Ninakuja kuwaokoa Kondoo WANGU. Kuwafukuza mbwa mwitu nje ya kanisa ZANGU, na Nitawatumia nyinyi kufanya hili. Kama nilivyomwaga Maji YANGU ya Uhai na Mvinyo Mpya. Shetani amemwaga siki bandia niliyoikataa, roho ya fugufugu, kuwa na umbo la utakatifu lakini hamna utakatifu ndani.

Nina huzuni kwa vile Watoto WANGU na wateule WANGU wanavyodanganywa. Mimi ni MUNGU aliyejazwa na huruma kwa wale ambao ni WANGU, lakini kwa sababu wanapotezwa na masikio inayowashwa kusikia yale tu ambayo wanataka kusikia, wameelekezwa kichinjioni. Ninainua jeshi hodari ya Gideon kuwachukua Kondoo WANGU katika upako mpya ambao wengine wenu mshaona.

Mnaposoma unabii hizi zawadi nilizowapatia zitaamsha zawadi za mwingine zilizotoka kwa RUACH ha KODESH (Roho Mtakatifu), hadi shahada ya juu. Sasa wale walio na roho za kiakili na mantiki, hii itakuwa kama Mvinyo uliozeeka na Mvinyo Mpya zikijaribu kuchanganyana. Hii injili ya YAHUSHUA ni rahisi sana hadi mtoto anaweza kuelewa ni vipi atakavyookolewa.

Msiyafanye magumu yale niliyoyafanya yawe rahisi. Sababu ikiwa MIMI sikupangia jehanamu iwe ya binadamu, ilitengenezwa kwa sababu ya shetani na malaika wake waovu. Nilikutengenezea njia ya kuepuka haya, yeye ndiye njia ya PEKEE ya kuepuka haya, ukweli wa pekee, maisha na njia kuenda Mbinguni na mikononi MWANGU inayowangoja, Nikiwa na hamu ya kuwakusanya kama kuku anavyowakusanya vifaranga wake.

Sitaki yeyote aangamie au ahukumiwe kama aliye na hatia, tafadhali wape onyo. Piga mlipuko wa tarumbeta kuwa upako Niliyokupatia. Kama vile mama au baba anavyowapatia onyo kabla ya kuwanyoosha watoto wake, MIMI kwa huruma WANGU usio na mwisho na upendo nasema wape onyo. Kwa kuwa Nitakavyoachilia hasira YANGU itakuwa vigumu sana kunituliza MIMI.

Kama unawapatia onyo, ingawa walimkejeli Musa, alitii na kuwapa onyo. Wakati ardhi itakavyotingizwa kote ni Watoto WANGU wa Kweli watakaosikia sauti YANGU na kujua RUACH ha KODESH WANGU, na wamefunikwa katika Damu ya Mwana WANGU iliyomwagwa pale kalvari, na kuita JINA la YAHUSHUA ha MASHIACH, YAHSHUA MASIHI, katika lugha yoyote unayoongea. Anajua JINA LAKE na ni Roho ipi inayotaja JINA LAKE.

Ni hawa tu watakaookolewa. Ita jina la YAHUSHUA ha MASHIACH na wewe na nyumba yako itakayoita JINA la YAHUSHUA wataokolewa. Sikiza kwa kuwa tena; bila yeye kutarajia Nimeandika Maneno YANGU kupitia Handmaiden WANGU, Nabii WANGU, Mtoto WANGU, Shujaa na Bibi arusi wa YAHUSHUA.

Sherrie Elijah (Elisabeth) tena hakujua ya kwamba Nitamtumia kupiga mlipuko wa tarumbeta hii pamoja na wengine niliowapachika kote ulimwenguni katika sehemu tofauti ya ulimwengu. Sikia onyo la mlipuko wa tarumbeta, kabla vita iendelee MIMI hutuma mlipuko wa tarumbeta.

Wape onyo, na utakuwa unafanya kazi yako. Wale wote wanaopokea haya pia wana kazi ya kuwapa onyo wale walio na masikio ya kusikia na kusikiliza, na ndio kwa wale wanaochagua kubaki viziwi. Kwa hivyo hawataweza kusema kuwa hawakupewa onyo.

* * * * * * *

Alipewa Rev. Sherrie Elijah katika 1/17/1997 

Contact AmightyWind