Unabii 37

Bariki na Ombeeni Amani ya Yerusalemu

Isaya 52:4-5 “Kwa maana hili ndilo Asemalo BWANA MWENYEZI, Hapo kwanza watu WANGU walishuka Misri kuishi; hatimaye, Ashuru wakawaonea. Basi sasa, nina nini hapa, Asema BWANA, kwa kuwa watu WANGU wamechukuliwa pasipo sababu? Nao wale wanaowatawala wanawadhihaki, Asema BWANA; na kila siku jina LANGU linatukanwa bila kikomo.”

Nitawabariki wale wanaobariki Yerusalemu, Nitawalaani wale wanaowalaani Yerusalemu! O Yerusalemu, O Yerusalemu! Binti WANGU Mpendwa Yerusalemu! Ewe taifa ndogo Israeli inayochukiwa na kutukanwa. Ninamtuma binti WANGU kuwaletea ujumbe wa Tumaini kwenu. Mnajua amri lakini sasa Ninamtumia kuwaletea Ahadi YANGU. MIMI YAHUVEH Nimewabariki na kuwaokoa kwa sababu ya YAHUSHUA, Mwana WANGU Mpendwa. MIMI pekee Nilimchagua Mwokozi wa binadamu wote kuzaliwa, kufunza kwa ishara, maajabu na miujiza na kuwapa upendo WANGU. Kwa sababu yenu Alikufa, Alifufuka kwa Utukufu, Alimshinda adui wa nafsi zenu na kuchukua kile ambacho shetani aliiba.

YAHUSHUA sasa yuaketi kwa mkono WANGU wa kulia kama mwombezi wenu wa pekee. YAHUSHUA, Damu Takatifu ya Mwana WANGU Mpendwa ilimwagika kwenye mchanga wa Yerusalemu ili dunia hii ipate kuokolewa. Ni kwa kupokea kufunikwa kwa Damu hii Takatifu na safi mtaokolewa. Hamna njia nyingine katika uwepo WANGU. Ondokeni na sherehe zenu, dhabihu, kufunga, maombi ya kurudia na siku spesheli zilizotengwa kumtukuza “MIMI NIKO” kama hamkubali Mwana WANGU Mpendwa YAHUSHUA, basi mnayoyazungumza na kufanya ni Bure! Nilitoa Tuzo LANGU la YAHUSHUA sio kwa dunia hii pekee, lakini kwanza Nilimtoa kwenu nyinyi. O taifa mpendwa Ninayoita Israeli. Damu YAKE Takatifu ilimwagwa sio kwa dunia hii pekee lakini kwanza ilimwagwa kwake Israeli. Damu YAKE iliyomwagwa inalia kutoka mchangani sasa na kuzungumza “Nilifanya haya kwenu nyinyi, mtanikataa MIMI milele? Je, mtalilaani JINA LANGU milele? Ni lini mtakaponiona MIMI kama dhabihu yenu ya pekee itakayopoza hasira za Baba YANGU tena?”

Ni lini mtakapoona kuwa Niliwaruhusu kuyafanya haya kwangu MIMI na siwalaumu?” O kwa siku ile ijayo mtakoponiita MIMI mpendwa wenu na kuheshimu JINA LANGU TAKATIFU! Ninawaonya haya; wanakondoo na dhabihu za wanyama hazitapoza hasira za Baba YANGU au hasira ZANGU tena. Ni kwa kunikubali MIMI, Mwana Mpendwa wa YAHUVEH. Niliweka maisha YANGU chini kwa kutaka, kwenye ardhi ya Yerusalemu kwenu nyinyi ili mwokolewe. Ni kwa kukubali tu kwamba MIMI YAHUSHUA Nimekaa kwenye mkono wa kulia wa YAHUVEH kama MFALME wa WAFALME na BWANA WA MABWANA, ndipo mtakapookolewa. Ni kwa kuita JINA LANGU YAHUSHUA MASIHI wakati wa dhiki kuu ijayo, ndipo mtakapookolewa. Ni kwa kupenda, kutii na kunitafuta MIMI ndipo mtakapoitwa Bibi Arusi WANGU Ninapowanyakua ili muwe kando YANGU. MIMI Ndiye mkombozi wa pekee wa dunia hii, hamna mwingine. Kwa hivyo sizungumzi tu kwa Yerusalemu lakini kwa dunia hii, jitayarisheni kwa kuwa yale yajayo hamtaepuka kama hamtaliita JINA la YAHUSHUA! Kumpenda Baba YANGU YAHUVEH haitoshi! Alinitoa MIMI kama dhabihu sio kwa watu WANGU Wayahudi tu, lakini kwa watu wa kila jamaa na lugha, Aliwapa Mwana WAKE wa kipekee kwa taifa hili ili muwe na kifuniko cha dhambi zenu, kwa wote wametenda dhambi na kupungukiwa na Utukufu wa YAHUVEH.

MIMI na BABA YANGU, pekee ni Takatifu na kamili. Kwa sababu ya kuanguka kwa Adamu na Hawa hakuna binadamu yeyote aliyeumbwa bila hitaji la Mwokozi na dhabihu YANGU ya Damu. Yerusalemu imebarikiwa sana kwa kuwa ni kwa mchanga huu Damu ya YAHUSHUA iliyo safi, Takatifu, inayoponya, kufufua, kukomboa, ilimwagwa pale chini Kalvari. Mwafikiria ni kwa nini shetani anachukia nchi hii sana? Mwafikiria ni kwa nini nchi hii inapigania uhai kutoka siku ya kuzaliwa? Mwafikiria ni kwa nini imejawa na vita na kila taifa inataka kuimiliki? Mwafikiria ni kwa nini Baba YANGU Ameibariki kushinda taifa lingine? Damu YANGU ilimwagwa na sasa italeta mbele hazina katika dunia hii zilizokuwa zimefichwa! Wale waovu watauma na kusaga meno yao wakijaribu kumiliki mali. Watagombana kati yao wenyewe kuwa ni nani atakayemshusha Israeli magotini na mali watakayopigania kupata. Lakini Baba YANGU huzungumza na kusema kwa maadui kuwa hawataendelea kugawanya na kumiliki taifa na watu Aliyewaita, kukadiri kuwa WAKE!

HAMTAFAULU kuibia watu Niliokadiri kuwa WANGU. Wanalipa gharama ya kubeba jina Myahudi na Nitailinda taifa hili liitwalo Israeli kwa njia ambazo mtu yeyote hajawahi kuota yawezekana. Nitamlinda yeyote aliye na upendo kwa Yerusalemu! Ingawa wanamkataa Mwana WANGU YAHUSHUA, sasa wakati waja ambapo jina la YAHUSHUA litaheshimiwa. Hili ndilo sababu sasa waovu wanajaribu kupitisha amri zitakazokataza jina hili kuzungumziwa wakitisha kuwaweka gerezani, kuwatesa au kifo. Shetani sasa ana mamlaka juu ya serikali ya taifa hili na mataifa kote duniani. Mwafaa kuheshimu serikali hizi kama wanavyoheshimu YAHUVEH na YAHUSHUA. Kwa kuwa serikali ipo kwenye mabega ya YAHUSHUA. Watu WANGU wanapaswa kutii MUNGU wanaomtumikia na sio Binadamu. Ombeni serikali za ufisadi zitashindwa na Watakatifu watajitokeza kuchukua yaliyoibwa.

Nchi ya Israeli imegawanywa kama nguo ZANGU, kuchezewa na kuuzwa kwa aliye na hela zaidi. Lakini MIMI YAHUSHUA Nitawarudishia Israeli yale ambayo wamenyanganywa na maadui wake watakimbia katika njia saba tofauti! O Ole kwa wale wanoinua mikono yao kwa mboni ya jicho LANGU kwa kuwa ingawa katika taifa hili JINA la YAHUSHUA linachukiwa, Nitawarudisha kumpenda kipenzi chao cha kwanza, na watagundua kuwa katika mateso yao, wao na YAHUSHUA ni Wapendwa WANGU na Mpendwa WANGU ni WANGU! Israeli watakosa maji kwa kuwa wanakosa Maji ya Uzima na Nitawatuma wengine, kuwaletea Maji ya Uzima na kwa wote watakaokunywa maji haya, kiu yao itazimwa sio tu kiroho lakini pia kimwili. Wale wanaomkataa Mwana WANGU YAHUSHUA, ndimi zao zitanyooka nje ya midomo yao kama aliye na kiu kwenye jangwa. Kama YAHUSHUA alivyokuwa na kiu, pia wale watakaokataa tuzo lake pale Kalvari watapata kiu. Je, ni wangapi watakaotoka kama yule mwanamke kwenye kisima? Je, ni wangapi watakaokuwa tayari kuwapa taifa la Israeli Maji YANGU ya Uzima? Kwa kuwa wana kiu na hawajui ni nini sababu ya kiu hii. Wanaitwa Nchi Takatifu lakini, ni mabaki wachache sana walio Takatifu mbele YANGU.

Nitamtuma binti huyu Ninayemtumia kutabiri sasa na kikombe cha Maji YANGU ya Uzima. Atakuwa na upako na wengine atakaokuwa nao wanaomtangulia kwa njia ambazo dunia hii haijaona bado, anapowalisha walio na njaa na kuwapa maji ya uzima wale wanao kiu ya utakatifu. Je, utakuwa mmojawapo wa watakaomsaidia? Au utakuwa mmojawapo wa watakaomzuia? Kila mmoja anayesoma haya anafaa kukumbuka kuwa isipokuwa kwa taifa hili ndogo liitwalo Israeli, mwokozi wenu angezaliwa, kuhubiri, kufa na kufufuka wapi? Ilikuwa kwa sababu yenu nyinyi na nyinyi pekee Israeli inalipa gharama hii. Kwa kuwa shetani anachukia Yerusalemu na Israeli na chuki isiyoeleweka! Anamleta mpinga kristo kuongoza na kutawala Yerusalemu. Jihadharini, kwa wale wote wasiomkubali MUNGU wa kweli Anayeishi wataanguka katika nguvu za utawala mwovu ujao. Wale wanaomtafuta Mwana WANGU YAHUSHUA, watakuwa na chakula na maji iliyofichwa wakati watakapoihitaji. Watoto WANGU watapata hazina, mkate kutoka mbinguni uliofichwa wakati watakapouhitaji. Msitizame dunia hii iliyojawa na ufisadi kuwashughulikia nyinyi, lakini tazameni MUNGU wa Abrahamu, Isaka na Yakobo na mkumbuke vile daima MIMI huwa na Musa anayeenda mbele ya watu WANGU kuwaongoza kutoka kwa utumwa, kama ilivyokuwa hapo awali Nitayafanya tena. Miujiza ambayo hatujaona, nyinyi mlio wa YAHUSHUA na YAHUVEH mtaona!

Msinizuie MIMI, Msinishuku MIMI, amini tu JINA la Mwana WANGU YAHUSHUA ha MASHIACH na nililieni MIMI na miujiza na baraka sitawanyima. Kama tu mwaweza kuamini kwa imani. Nina ufunuo kwa nyinyi mnaojiita “Mataifa”, kama nyinyi ni waaminifu, mnampenda, kumwabudu na kumkubali YAHUSHUA kama BWANA na MWOKOZI basi nyinyi mmepandikizwa na NYINYI NI WAYAHUDI TU KAMA MWANA WANGU YAHUSHUA ALIVYO. Hakuna Myahudi na Taifa tena. Hakuna tena kuita karamu, KARAMU za WAYAHUDI na Siku Takatifu, siku hizi na Sabato ni zenu pia! Nina ufunuo kwa wale “Wayahudi” wa damu Nisikilizeni MIMI! Mnamkataa YAHUSHUA kwa kuwa mwafikiria yeye ni wa Mataifa lakini YAHUSHUA alizaliwa kutoka kwa binti Myahudi na YAHUSHUA ni MYAHUDI! O Israeli, JINA LANGU ni “MIMI NIKO!” Nimewabariki! Msimlaani YEYE tena kwa kuwa “MIMI NIKO” sio nusu YAKE, SOTE ni moja! Wale wanaomlaani, kumkataa Mwana WANGU Mpendwa YAHUSHUA, wanalaani, na kunikataa MUNGU mkuu “MIMI NIKO”. Kwa haya hakuna msamaha wa dhambi, mmejichimbia shimo jehanamu mtakapoishi.

Wale wanaomkataa RUACH ha KODESH WANGU HUMKATAA Baba na Mwana kwa kuwa hakuna vile yeyote anaweza kuokolewa kama si RUACH ha KODESH WANGU kumvuta katika maarifa ya upendo kuwa, ni YAHUSHUA pekee anayeokoa na kuingia Mbinguni hakuna njia nyingine, hakuna JINA lingine Takatifu. Ninamjia Bibi Arusi WANGU kuwa NAMI kando YANGU! Lakini lazima mnitamani MIMI sio kwa hofu lakini kwa UPENDO mkuu! Hofu ni kinyume cha imani. Hofu hainiletei heshima, ni imani yenu, kuwa YAHUSHUA atawashughulikia wote ambao ni WAKE, haya ndiyo yanayoniletea heshima. Kwa sababu Bibi Arusi WANGU wamekuwa katika hofu na hawajanililia kwa imani na upendo, ndiyo sababu bado sijaja. Ninamjia Bibi Arusi mwenye moyo, uaminifu na misukumo misafi, sio kiburi au ukosefu wa amani kuwa Nitawatunza. Haya kwa mfano ndiyo sababu Bibi Arusi WANGU hawapo kando YANGU.

Nitafute MIMI, Jifunze juu YANGU, Nitamani MIMI, Nitii MIMI, zaidi kila siku. Njooni chini ya mabawa ya Baba YANGU kama vifaranga na mtaniona MIMI. Jueni kwamba hakuna yoyote yanayoweza kufanyika kama Baba YANGU hajayakadiri. Atatoa njia ya kuepuka katika siku hiyo ya uovu wakati ambapo yote yatakaa ni kama yamekwisha. Tazameni juu kwa sababu ukombozi wenu wakaribia. Tazameni juu na mnione Nikija kwenye anga. Kazeni masikio yenu na msiogope, mtasikia tarumbeta ya waliokombolewa, na macho yenu mtaona Utukufu WANGU kama tu mwaweza kuamini.

Imezungumzwa, imeandikwa kupitia huyu Binti wa YAHUVEH na YAHUSHUA katika upako wa RUACH ha KODESH. Saa 7:00 asubuhi, Tarehe 10/19/99. Mtume Elisabeth (Elisheva) Elijah

www.amightywind.com www.almightywind.com


* * * * * * *