Unabii 36

MIMI Sio Mungu Wako Tu wa Jana, Leo, Lakini Wa Kesho, Hata Katika Wakati Wa Giza.

Agosti 10, 1999

Imezungumzwa kupitia chombo hiki cha udongo, mnyenyekevu, Mtume Elisabeth Sherrie Elijah (Elisheva Eliyahu). Niliamka na maneno haya kuanzia Saa 6:00 asubuhi.

Haya maneno yanatoka kwenye Unabii wa 105, YAHUVEH alisema yaongezwe kwenye Unabii zote kutoka sasa: Nilikuonya kitambo Elisabeth [Elisheva], kutoita Huduma hii kwa jina la mwanamume au mwanamke. Hata kabla kuwepo na Huduma, Niliiweka ndani ya roho yako. Kwa kuwa hakuna lolote lililofanyika kwa mikono yako. Hakuna lolote lililotoka kwenye kinywa chako. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUVEH aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUSHUA, MASHIACH wako aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha RUACH HA KODESH, IMMAYAH wako aliyeizalisha. Kama ingekuwa tu kwa mkono wako, ingekuwa imefeli kitambo. Ni kwa UPEPO WA SHKHINYAH GLORY unaovuma kote duniani, UPEPO TAKATIFU WA UAMSHO. Sio kwa pumzi yako, au ingekuwa imefeli. (Isaya 42:8)

Katika mwezi wa Julai 2010, MUNGU YAHUVEH pia Alisema kuongezwe yafuatayo mbele ya Unabii zote kutoka Kitabu cha pili cha Mambo ya Nyakati:

2 Mambo ya Nyakati 36:16, “Lakini waliwadhihaki Wajumbe wa MUNGU, na kuyadharau Maneno YAKE, na kuwacheka Manabii WAKE, hata ilipozidi Ghadhabu ya BWANA juu ya Watu WAKE, hata kusiwe na kuponya.”

* * * * * * *

O, Ninavyohuzunika na Ninavyoomboleza kwa yale ambayo yaja kwa wale walioamua kufuata njia ya uasi, wakikataa mamlaka YANGU na uwepo, wakikataa vile kuishi katika Utakatifu kama “MIMI NIKO” Nilivyo Mtakatifu. Nitaifunika ardhi hii na giza kuwaonyesha hasira ZANGU kwa dhambi zenu. Nitafunga macho YANGU wakati mambo mabaya yatakapowajia kutoka jehanamu kwa wale walioamua kutembea katika njia ya uasi na kutotii. Onyo hii haizungumzwi kwa maadui WANGU tu, lakini pia kwa Watoto WANGU kwa kuwa lazima waelewe wakati miguu yao itakapoenda kando na njia ya Utakatifu na waanze kutembea katika kutotii basi pia wao watajipata nje ya mwavuli WANGU wa usalama kutokana na dhoruba zijazo.

Ninazungumza mambo haya sasa kupitia handmaiden WANGU anayejua anawajibika kwa yale anayoyazungumza na asiyoyazungumza. Maneno haya yatathibitisha wale wanaosoma na kusikiza na mahala ambapo wamekuwa katika giza Nitamulika nuru YANGU ya thibitisho kuonyesha tena kuwa “MIMI NIKO” ni Mungu Mwenyezi ambaye ni Mungu wa Huruma na Upendo lakini “MIMI NIKO” pia ni MWENYEZI katika VITA kwa maadui WANGU. Kwa kweli kwa wale wanonijaribu MIMI watapata kuwa “MIMI NIKO” ni Mungu ambaye hatakajeliwa kamwe kwa hivyo jihadhirini siku hii!

Giza ijayo itakuwa ishara ya hasira ZANGU “MIMI NIKO” Ninapofunika macho YANGU kwa majanga, vita, ukame, kifo, uharibifu, tauni, ufukara, magonjwa yenu na orodha yaendelea. Waonye maadui WANGU kuwa wameleta aibu hii juu ya mataifa yao, juu yao wenyewe! Watoto, Bibi Arusi, Waliochaguliwa na Wateule WANGU hawapaswi kuogopa lakini wataomboleza na kuhuzunika NAMI wanapoona vitu hivi vikija juu ya wale waliochagua kutotumikia Mungu wanaomtumikia. Wataona haya juu ya wale wasio na alama ya ukombozi kwenye paji la uso. Damu ya YAHUSHUA ikifunika dhambi zao.

Unaposikia mashtaka ya kukusanya na serikali ambazo hawajawahi kupima wataanza kupima, ambapo hata maji yatapewa ni kama tuzo kutoka kwa mwanadamu, basi mjue kuwa huu ndio mwanzo wa yale Niliyoyatabiri hapa. Wakati vita viko pande zote, na nchi yenu kuvamiwa jueni kuwa Nimewaonya wale ambao wanapaswa KUKIMBIA na kuwaambia WAKIMBIE wapi na kama watatii wako katika mwavuli wa usalama WANGU, wasipotii basi ingawa Ninawapenda na kuhuzunika juu yao, watateseka kwa njia ambazo hazikuhitajika. Muwe na hofu moja na hii ni kutosikia sauti YANGU.

Mtafute Mungu wa Abrahamu, Isaka na Yakobo, Mungu wa Israeli kama bado Naweza kupatikana. Sizungumzi kwa sauti ya juu kwa Roho zenu bali kwa sauti ndogo kwa wale wanaojali kuyaelekeza masikio yao KWANGU na kujaribu kusikia, watanisikia MIMI Nikizungumza. Je, ni muhimu kwako kujali kunikaribia MIMI Ninaoponong’ona maagizo YANGU kwako? Je, ni muhimu RUACH ha KODESH anaposema ufunge, ufunge ili uweze kunisikia MIMI vyema?

O Watoto WANGU, Ninavyotamani kuwashika mikononi MWANGU lakini mwakataa MIMI kuwagusa. Kwa kuwa mguso WANGU ni Takatifu na kwa MIMI kuwagusa inawathibitisha. Kwa hivyo inanilazimisha kuwagusa kwa njia ambayo sipendelei, kama Baba anayemchapa mtoto Mtanitii. Lakini wale wanaoniamini MIMI, wale wanaotamani mguso WANGU, Nitawafunika na kuwalinda. Nitawaweka mikononi MWANGU na kuwashughulikia kama mama anavyoshughulikia mtoto aliyeumia. Ninawaambia wapendwa WANGU, siku zijazo hazitakuwa kitu ya kuhofia bali tu uweke imani kwa Mungu unayeabudu, kumpenda, kumtumikia, na kujaribu kumtii. Sitawahi kuwaacha wala kuwabwaga! Msimwogope binadamu bali mwogope Mungu mnayemtumikia. Usiposikia sauti YANGU, hautapata maagizo yako.

Kama Lutu alivyokatazwa kuingia na malaika aliyemwonya asiingie, pia Nitakaposema mkimbie kutoka nchi ambayo mpo, basi MTII! Nitawatuma malaika waliofanana na wanaume na wanawake na watazungumza Maneno YANGU lakini msidanganyike. Kama Maneno haya hayatalainika na Neno la “MIMI NIKO”, kama RUACH ha KODESH hayupo ndani yao, basi msimsikize yeyote ambaye haniabudu, kunitumikia, kunipenda, na kuniweka MIMI kwanza kwa kila njia! Kwa kuwa adui atawatuma wale wanaofanana watakatifu na kuzungumza vitakatifu lakini myasikize maneno yao kwa makini. Je, wanakupa moyo kukaa katika imani, kuendelea kuishi kwa utakatifu, kufuata amri ZANGU za kale? Ambazo hazijawahi kupitwa na wakati kwa kuwa amri ZANGU, Torah YANGU haizeeki. Je, wanafunza injili nyingine inayosema kuwa kuna njia nyingine kufika Mbinguni na kuwa hauhitaji Damu ya Mwana WANGU YAHUSHUA kufika pale? Kama wanakuambia kufuata amri za binadamu na utupe amri ZANGU basi Ninawaambia haya, sijawatuma kukuongoza wala kukufunza kabisa.

Je, nuru na giza zina uhusiano gani? Mwana WANGU YAHUSHUA na shetani wana uhusiano gani, maovu hayawezi kuelekeza mema. Viongozi wa kisiasa ni wafisadi na lazima mweze kutofautisha kamili kati ya mema na mabaya. Viongozi wenu wa kisiasa katika pande zote za siasa wamenisaliti MIMI. Shetani alikuwa mzabuni mkuu lakini Nitawaonyesha Ninayoyafikiria, kwa kuwa mchezo huu bado haujaisha. Ninayo mamlaka na Ninaongoza ingawa wanataka kudharau Uongozi WANGU. Hata nchi inayosema inaniabudu MIMI na uongozi hawajui “MIMI NIKO” ni nani, wala hawataki kunitumikia MIMI, wala hawataki kunitii MIMI.

Anapanga kuendelea kuikata nchi YANGU ni kama chombo cha kukata biskuti lakini Nitakuwa na msemo wa mwisho. Ninazungumza kwenye ukame, Ninazungumza kupitia upepo mkali unaovuma kote ardhini, Ninazungumza kupitia mitetemeko ya ardhi itakayoangusha mijengo mirefu na Ninazungumza kupitia mafuriko kwa kuwa machozi YANGU ni mvua kwa watoto WANGU waasi. Ninazungumza na moto wamwagika kwa hasira ZANGU. Mataifa yanayotaka kuwachinja watoto, kuuza sehemu za miili yao kwa mzabuni mkuu JIHADHARINI!

Siku moja hivi karibuni, mtamjibu Mungu wa Uumbaji. Mnayauza madawa na kutoa ujuzi wa upasuaji Nilizowapa kuokoa maisha na sasa mnayachukua maisha yasio na hatia. Enyi madaktari mtalipa kwa kutumia tuzo za maarifa Nimewapa kuwaua wasio na hatia. Nyoyo za watoto wasiotakwa zinarudi kwa Muumbaji wao na kurudi katika Mikono YANGU lakini ni nyinyi mtakaolipa kwa yale mnayoyatenda. Kwa mataifa yanayofanya vitu hivi, Nitafunga masikio YANGU wakati watakuwa wanachinjwa. Lakini tena hasira ZANGU hazitawashika wale ambao ni WANGU na huomboleza kwa ajili ya vitendo hivi vya unyama visivyojali ni nini haki au hatia.

Enyi wachungaji mtawajibika hivi karibuni. Wachungaji waovu wanaofanana watakatifu na hawawezi kupinga ushoga na kuavya mimba, inavyotapakaa kote sasa. Mnaogopa zaidi kupoteza hongo mlizozichukua. Nawaonya watu WANGU mtawajibika kwa kutoa fungu la kumi kwa huduma ambayo inaogopa zaidi kupoteza hongo za serikali kwa kufunga midomo yao wanavyoona usherati na maovu yakijaa ardhini. Kila kanisa lafaa kuinuka, kila mtu ajiitaye WANGU! Wakionya kuwa Bibilia yasema ushoga ni CHUKIZO kwake “MIMI NIKO”. Nimewaonya kwa Neno LANGU kuwa pepo hii itakuwa ya kuambukiza na lazima ishughulikiwe. Lakini, mlizungumza wakati mlipoona amri zinazolinda vitu Ninavyoviita chukizo zikipitishwa?

Wachungaji wote, viongozi wa kiroho, viongozi wa kisiasa ambao hawakuzungumza, sasa Ninawaita CHUKIZO kwake “MIMI NIKO!” Chukueni kujifanya kwenu kuwa watakatifu na chukueni kujifanya kwenu kwa ibada na Ninasema, “NENDENI MBALI NAMI!” Sitawasikiliza katika siku yenu ya msiba. Mtanijibu MIMI Nitakapowachukua Bibi Arusi WANGU wa kweli nyumbani kuwa NAMI, na nyinyi viongozi wa kiroho mtakaa kwenye shirika zenu na kuwaangalia na kujaribu kueleza kwa nini kanisa lao bado lipo kupitia Dhiki ijayo. Ni kwa sababu mmeuzwa kwa gharama, gharama ndogo itakayofanya mpoteze nafsi zenu msipoanza kuzungumza sasa! TUBUNI SASA! BADO WAKATI UPO! WAKATI MDOGO! O kama nyinyi mnaofikiria kuwa kuja kwa Mwana WANGU ni mbali mngeweza kuona vile ilivyo karibu, karibu kushinda pumzi yako unavyotoa pumzi baridi. Je, ni viongozi wangapi wa kiroho wanaoonya kuhusu haya? Je, ni wangapi wanaokubali kuwa yule Mungu aliyezungumza kupitia manabii katika nyakati za kale Ndiye huyu Mungu anayefanya hivi vitu tena?

Nitafuteni MIMI kama bado Naweza kupatikana. MIMI sio Mungu wa kukejeliwa! Mtaona katika siku zijazo. Nitazungumza kupitia huyu handmaiden anayewalisha kama watoto, kijiko kwa kijiko, kwa vile wengi wenu bado hamwezi kumeza nyama au mmechagua vivyo hivyo. Nitawapa vipande vidogo kula, sio vipande vikubwa kwa kuwa mmekosa mengi na mmejinyonga, au kuitema kwa kuwa haikupendeza kusikiza. Wengine wanaotamani mengine zaidi kwa kuwa wamekula nyama Ninasema rudini na msome tena Niliyoyazungumza, hata huyu handmaiden Nimemwongoza kufanya yaya haya. Ninawaambia NYOTE mmekosa kitu fulani na mnapomtafuta RUACH ha KODESH WANGU mtaona ni nini mmekosa.

Ninawaacha na maneno haya, “Je, mmefanya yote mwezayo kumsaidia handmaiden huyu katika huduma hii Niliyoiweka kwenye mabega yake? Mmechukua kweli hizi Nilizozizungumza na kama sahani ya mapochopocho kuwapa wengine kula? Au ulikula pekee yako na kuzisahau? Nimezungumza yale yatakayotokea mara kwa mara kupitia kwake. Sasa mtaona yale Niliyoyazungumzia yakitendeka. Kwa wale na masikio ya kiroho ya kusikia na macho ya kiroho ya kuona watajua nini ijayo, cha kufanya, cha kutarajia, kwa wale wanaochagua kubaki viziwi na vipofu mtaendelea kukejeli, mtaendelea kutafuta usalama na haitapatikana.”

Nimesema kwa uwazi, “Je, anayeamini na asiye amini wana uhusiano gani?” Vitu vya dunia hii vinaharibu visipoandamana na utakatifu. Tena Ninasema mnitafute MIMI kama bado mwaweza kunisikia MIMI. Nitafuteni MIMI katika Neno LANGU. Mpate kujua “MIMI NIKO” ni nani. Tafuteni RUACH ha KODESH WANGU na mpate kujua YAHUSHUA ni nani. YEYE anawajia Bibi Arusi WAKE. Je, wewe ni Bibi Arusi au mgeni wa Bibi Arusi? Wewe ni mmoja wa wale walioalikwa na ukakataa mwaliko na kuitupa? Kuna zaidi ya moja ya kuja kwa Mwana WANGU lakini kuna pokezi MOJA PEKEE ya HARUSI. BIBI ARUSI MMOJA, WEWE NI YUPI? Kumbukeni, “MIMI NIKO” tayari Najua yupi amemkubali YAHUSHUA kama Bwana NA masihi! “MIMI NIKO” tayari Najua kwa kuwa ilikuwa imeandikwa katika Kitabu cha Maisha cha Mwana-Kondoo kabla ya dunia kuumbwa. Najua ni chaguo gani utachukua kabla haujaichagua. MIMI nipo kote, najua yote na naona yote.

Giza iliyopo tayari kushuka katika sehemu mbalimbali za ardhi hii itaachilia pepo katika kila upande. Kupatwa ujao angani pia ni ishara kuwa maovu hupigana na mema. Shetani, YAHUSHUA na malaika WANGU wanapigana na Nimeiweka ishara hiyo angani. Kuna mengi ya kuhofia yaliyo katika ulimwengu wa kiroho hata wale wasionitambua MIMI kama Mungu Mwenyezi na kuinamia miungu wengine wanajua kuwa kupatwa huu sio kama nyingine. Shetani ataweka katika akili za binadamu fikra ya kushinda, na kupora, kuiba, kuharibu katika njia kuu.

Shetani ataiachilia pepo ya vita juu ya Watoto WANGU kwa njia kuu. Mmeonywa. Msiseme kuwa “MIMI NIKO” hakuwaonya. Msiogope, Niiteni MIMI na Nitawaokoa na MKONO WANGU MKUU! Lakini Nitawalinda wale waliofunikwa na Damu ya Mwana WANGU iliyomwagika. Kuna rehema moja tu ya dhambi, Damu moja iliyo Takatifu na safi inayoweza kuosha harufu ya dhambi kabisa. Hakuna yeyote aliye kamili; wote lazima wafunikwe katika Damu Takatifu inayookoa ya YAHUSHUA, njia ya pekee ya kufika kwenye kiti cha enzi CHANGU cha neema. Miezi ijayo itazidi kuwa mbaya katika macho ya dunia lakini kwa watoto WANGU wanaolala kwenye kipaji cha mkono WANGU Nitawaficha na kuwalinda na mkono WANGU mwingine.

Usijitahidi wala kuwa na wasiwasi, usijisumbue kwa neno lolote, usitegemee akili zako mwenyewe lakini katika njia zako zote nikiri MIMI, omba kwangu MIMI, nitafute MIMI, nipende MIMI, nitii MIMI na sitawakasirisha waaminifu WANGU wanaoyafanya haya. Jificheni chini ya mabawa YANGU hadi maovu haya yapite. Wekeni Damu ya YAHUSHUA kwenye akili, miili, roho na nafsi zenu. Iwekeni kwenye milango na dirisha zenu ili pepo zisiweze kuiingia. Zungumzeni kwa imani alafu shikeni pindo la vazi la YAHUSHUA, vazi la utakatifu na msiiachilie. Giza iliyoko ndani ya nafsi ya binadamu itawakilishwa kwenye kupatwa, giza ya dhambi inayofunika ardhi, giza ambako nuru YANGU haikaribishwi. O Nitahuzunika kwa yale Nitakayoyafanya, lakini ilikadiriwa hapo awali, ilitajwa hapo awali, mmeonywa kama mnasoma NENO LANGU.

Kama ilivyokuwa katika wakati wa LUTU, Nipo karibu kuharibu taifa ambayo imejawa na dhambi, uasi, mauaji, wizi, upotoshaji, usherati na kiburi. Amri nyingi zinazotengenezwa sasa Marekani zimewekwa kumheshimu mpinga-kristo na sio YAHUSHUA (Yesu Kristo). Hamjui lakini Marekani ni kama mvuke mbaya kwenye pua LANGU. Pia viongozi wenu wa kisiasa. Viongozi wenu wa kisiasa wanaojaribu kufanya mazuri, huwa wananyamazishwa au kutishwa na hujipata wakifanya vitu vibaya. Huyu SIO kiongozi. Mbinguni yote inafunga mapua yao kwa harufu ya dhambi ambayo shetani anaiweka mbele ya uso WANGU kila siku. Baba zenu wa kale wanatazama na wanajua nini Nitakayofanya kwa taifa hii kama vile mtoto anavyochafua suruali yake na ni lazima nimbadilishe lakini Nitawapaka uchafu huu usoni kwa kuwa mmenikasirisha MIMI.

Hamna aibu! Ninazungumza kwa viongozi wenu wa kisiasa wanaopitisha amri zinazotakikana kuwaongoza Watu WANGU lakini wanawafunza watu kuchafua suruali zao pia na kukosa kuaibika. Niliwafunza kupitia Amri ZANGU, Torah YANGU iliwekwa kuongoza mataifa yenu na ni taifa gani hapa duniani ambayo itatumia amri hizo kuwaongoza watu? Duniani kote, hata taifa ile inayoinua Jina LANGU, na kujifanya kuwa WANGU, Israeli HAINITII MIMI! Lazima watanitii MIMI kwa njia ambayo imenenwa na manabii wao! NITAYAFANYA YOTE AMBAYO NIMEAHIDI KUYAFANYA! OLE! OLE! OLE! KWA MATAIFA NITAKAKOACHILIA HASIRA ZANGU!

Kwa ajili ya wateule, Nitafupisha muda wa OLE lakini Nitayafanya yanayotakikana. Vita vinavyoongezeka Angani, pia vita vya mema na maovu yanaongezeka duniani. Ninawatenga kondoo WANGU na mbuzi, giza na nuru. Haitakuwa jambo la kufurahisha kwenu Watoto, Bibi Arusi, Waliochaguliwa na Wateule WANGU kwa mbuzi wengine mmewapenda na kutamani kushiriki nao na kuishi na hata kuwaoa. Siwaamuru kuwapa talaka lakini Ninawauliza kuweka mahusiano haya madhabahuni, niambieni kuwa mwatamani MIMI Niwaokoe, haijalishi vile Nitakavyowashughulikia, kufanya itakikanavyo. Msifanye mzaha. Niambieni MIMI kuwa mwatamani MAPENZI YANGU katika mahusiano haya na mniulize MIMI kutoa yote ambayo sitaki maishani mwenu.

Kwa aibu YANGU mmetoa visingizio kwa upendo vuguvugu kwangu MIMI. Mmetoa visingizio kwa kukosa hamu ya kunitii MIMI au kuishi maisha matakatifu au kujifunza juu YANGU au kunitumikia MIMI. Sikubali visingizio VYOVYOTE! Nimewaambia kuwa hamfai kuwa na ushirika na giza mara kwa mara katika neno LANGU. Mnapaswa kuwa mfano wa utakatifu WANGU lakini wengi sasa huvuta mabega yao na hawajali maovu yaliyoko ardhini.

Wananiambia MIMI Niwaokoe wale walio na nafsi za mbuzi wanaoishi gizani, wasiotaka kuwa kondoo lakini hawataki kukemea marafiki zao, familia, mpendwa, au watoto kwa hofu kuwa watawakera. Watoto WANGU wanang’ang’ana kuogopa majibu ya wapendwa wao na sio MIMI. Watoto WANGU wanaelewa ni aidha wawe kero kwao sasa hivi au wawe kero kwao milele wakichomeka jehanamu. Thubutu kuwa kero katika Jina la YAHUSHUA. Wengine watakerwa; wengine wataelimishwa, yote katika Jina la YAHUSHUA ha MASHIACH! Mnawajibika sasa kwa yote mnayoyajua. Je, mtafanya nini na maarifa haya?

* * * * * * *

Kama ilivyozungumzwa, imeandikwa tarehe 8/10/99 imeachwa kwa huyu handmaiden Mtume Sherrie Elijah (Elisheva Sherrie Eliyahu) anayethubutu kukera katika Jina la YAHUSHUA ha MASHIACH. Naomba kuwa hautakerwa bure lakini utaelimishwa kwa niaba ya nafsi zetu. Naamini kuwa neno hili imenenwa yote kwa yaliyozungumzwa kwangu kupitia upako wa RUACH ha KODESH. Naomba kuwa nimesikia kila neno vile Mungu alivyotaka lizungumzwe.

P.S. TAFADHALI nisaidie kuweka unabii huu katika mikono ya wengine ambao watawapa wengine. Tafadhali tuma kwenye mitandao nyingine ambayo wanaweza kunisaidia kufanya haya niliyoitwa kufanya. Zungumzeni Unabii hizi za Bwana YAHUSHUA kwa kuwa muda ni mfupi, mfupi sana. Tazameni juu kwa kuwa ukombozi wetu wakaribia! Tembeeni katika IMANI na sio kwa kuona au hofu! Mengi ni majaribio ya watakatifu lakini Bwana wangu atanitoa kwa zote! Simameni katika neno LAKE Takatifu; msimwache Tumaini wenu wa Baraka!

* * * * * * *