Unabii 33

Hofu, Hofu, Hofu! Kama Ilivyokuwa Wakati wa Hitler, Ndivyo Itakavyokuwa Tena!

Imeandikwa/Imezungumzwa katika upako wa RUACH ha KODESH kupitia Mtume Sherrie Elijah (Elisheva Sherrie Eliyahu)

Aprili 29, 1999

Haya maneno yanatoka kwenye Unabii wa 105, YAHUVEH alisema yaongezwe kwenye Unabii zote kutoka sasa: Nilikuonya kitambo Elisabeth [Elisheva], kutoita Huduma hii kwa jina la mwanamume au mwanamke. Hata kabla kuwepo na Huduma, Niliiweka ndani ya roho yako. Kwa kuwa hakuna lolote lililofanyika kwa mikono yako. Hakuna lolote lililotoka kwenye kinywa chako. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUVEH aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUSHUA, MASHIACH wako aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha RUACH HA KODESH, IMMAYAH wako aliyeizalisha. Kama ingekuwa tu kwa mkono wako, ingekuwa imefeli kitambo. Ni kwa UPEPO WA SHKHINYAH GLORY unaovuma kote duniani, UPEPO TAKATIFU WA UAMSHO. Sio kwa pumzi yako, au ingekuwa imefeli. (Isaya 42:8)

Katika mwezi wa Julai 2010, MUNGU YAHUVEH pia Alisema kuongezwe yafuatayo mbele ya Unabii zote kutoka Kitabu cha pili cha Mambo ya Nyakati:

2 Mambo ya Nyakati 36:16, “Lakini waliwadhihaki Wajumbe wa MUNGU, na kuyadharau Maneno YAKE, na kuwacheka Manabii WAKE, hata ilipozidi Ghadhabu ya BWANA juu ya Watu WAKE, hata kusiwe na kuponya.”

* * * * * * *

Popote mtakapoenda Nitawalinda. Chochote kitakachofanyika jua kuwa MIMI Niko nanyi, na Nitawalinda. Je, Bwana Arusi anaruhusu mabaya yoyote kuja kwa Bibi Arusi WAKE? Nyinyi ni Bibi Arusi WANGU na MIMI ni Bwana Arusi wenu. Ndio, Naja hivi karibuni lakini mpaka mtakaponiona MIMI msifikirie kuwa MIMI sitawafunika na kuwalinda Bibi Arusi WANGU. Je, si Neno LANGU linasema ingawa 1,000 wataanguka kando yako, ingawa waliofariki watakuzunguka, Nitakulinda (Zaburi 91:7)? Kumbukeni wakati Wanaisraeli na wakaazi wa Misri walipozungukwa na giza na nuru? Kumbukeni wakati wakaazi wa Misri walipokuwa na mapigo na Wanaisraeli hawakuwa nayo? Waliishi pamoja au sivyo? Lakini Wanaisraeli walikuwa wamelindwa. Kwa hivyo kama ilivyokuwa hapo awali, ndivyo itakavyokuwa tena.

HOFU KUU! HOFU KUU! HOFU KUU yaja kwa wale ambao wamezirusha Amri ZANGU usoni MWANGU na kutemea Torah YANGU na kulichafua Neno Takatifu na kulirarua.

HOFU KUU! HOFU KUU! HOFU KUU! HOFU KUU! HOFU KUU! HOFU KUU yaja juu ya wale waliokejeli Neno la YAHUVEH iliyozungumziwa vibaya na kuitwa takataka.

HOFU KUU! HOFU KUU! HOFU KUU! Nyinyi husema MIMI ni Mungu wa huruma na upendo na Ninapozungumza kwa kukemea au kwa sauti kali kupitia Manabii WANGU, mwasema “Huyo sio Baba wetu wa upendo na huruma.” Si MIMI husema, “MIMI huwaadhibu wale Niwapendao? Ni mzazi mgani anayemkanya mtoto wake bila kupaza sauti yake?” WAJINGA, WAJINGA, NYIE WAJINGA. Nitawapiga, Nitawapiga kwa kulia na kushoto, Nitawakanyaga. Lakini kwa niaba ya nafsi zenu, Nitamruhusu shetani kuua miili yenu, kwa sababu ya upendo WANGU na huruma, nililieni MIMI wakati huo unapofika, Nitaokoa nafsi zenu.

HOFU KUU! HOFU KUU! HOFU KUU! HOFU KUU! HOFU KUU! HOFU KUU kama dunia hii haijawahi kuona. Lakini sikizeni, haya maneno Ninayowapa sio ya Bibi Arusi, Watoto, Waliochaguliwa na Wateule WANGU kuogopa. Sio ya wale wanaotii sauti YANGU na kuniogopa MIMI.

Ni hekima kumwogopa Bwana. Ni hekima kujaribu kuwa msafi. Ni hekima kuendelea kuishi katika Utakatifu na kukataa maovu. Chukueni Neno la Mungu na ishikeni usoni mwa wapagani na mseme, “Ndivyo Asemavyo Bwana.” Tazameni na mwone, vile nyumba ya jirani wako itakavyoharibiwa; mapigo, magonjwa, maafa, uharibifu na umaskini zaja na tazameni vile Nitakavyowaficha wale ambao ni WANGU. Ninafunika wale walioingia katika Pasaka YANGU. Wale ambao ni WANGU, walioingia katika Pasaka YANGU, mtaipita HOFU ya HUKUMU ZANGU zijazo.

Uharibifu mkuu waja. Dunia hii itatingika kwa hofu. Je, jua linaweza kuwaka zaidi ya nuru YANGU Ninavyokuja karibu na dunia? Lava itatiririka, haiwezi kushikilia ghadhabu ya YAHUVEH tena. O lakini mtaona malaika WANGU wakiwazunguka wale wanaonipenda MIMI, msiogope. Nyinyi ambao husikia sauti YANGU msiogope. Wakati wa kuenda utakapofika, mtajua. Si Nilifungua Bahari ya Shamu? Niliifanya hapo awali, na Nitaifanya tena. Kama mwovu farao na vikosi vyake walivyowakimbiza Watoto wa Israeli waliotaka tu kuwa huru na kuishi kwa Utakatifu na kuniabudu MIMI.

Watoto WANGU ndio Niliowalinda. Maadui wao waliangamizwa. Niliifanya hapo awali, na Nitaifanya tena. Wanaisraeli hawakutii na wakachelewa kuingia katika Ardhi Iliyoahidiwa kwa adhabu YANGU. Oneni uharibifu ukija kwake kahaba wa babeli. Mwamkumbuka Hitler? Kama Nilivyowaambia Manabii WANGU, jifunzeni kutoka kwa Hitler na mtaona yale yaliyokuwa hapo awali, yatakuwa tena katika siku zijazo.

O, O, O!!! Mito ya Damu itatiririka! Nyinyi mnaojiita Wakristo na midomo yenu iliyojaa na dhahabu. Hiyo dhahabu imetoka jehanamu! Dhahabu iliyotumwa kutoka jehanamu! Nyinyi ni WAJINGA, WAJINGA! Ili shetani achukue alichokupa. Si Hitler alivuta meno ya dhahabu kutoka kwa midomo ya Wayahudi? Shetani anakejeli na kucheka, kama alivyofanya hapo awali, atafanya tena. Wale wanaonijua MIMI, wale wanaonijua MIMI, jueni haya si ya KWANGU. Ninawaamuru kuwa wanyenyekevu. Je, mbona Niwaulize mringe na mdomo uliojaa dhahabu? Hii sio kiburi? Ninawachukia viongozi wanaofunza haya na kuwaongoza Watu WANGU katika upotovu. Mtajua na mtajua kuwa nyinyi viongozi waovu mtasimama mbele YANGU siku moja na kunisikia Nikisema, “Ondokeni KWANGU, ninyi watenda maovu. Sikuwajua kamwe! (Mathayo 7:23)”

Angukeni kwa nyuso zenu na TUBUNI! Ondoeni hiyo dhahabu kutoka midomoni mwenu kabla shetani hajaitoa kama vile Hitler alivyofanya, watafanya yaya haya tena. Mpinga kristo ataziita kambi ya mauaji. Hapo awali aliwaua wayahudi milioni 6, sasa itakuwa wakristo na wayahudi milioni 666. Umati utakuwa vuguvugu katika imani yao, lakini kabla maisha yao hayajachukuliwa, kuzimwa kama moto, watakuwa na moto wa upendo wa YAHUVEH. Yale ambayo hawana sasa, watakuwa nayo wakati huo. Si itakuwa rahisi zaidi kutoa akili, mwili, roho na nafsi yenu sasa kwa kunipa MIMI mapenzi yenu, kufanya mambo njia YANGU au mwataka kungoja kupitia HOFU ijayo?

Je, si Neno LANGU lasema “walio vuguvugu” Nitakutapika utoke kinywani MWANGU (Ufunuo 3:16)? Mbona mkisoma Neno LANGU mwafikiria kuwa mtu yeyote anayejiita “Mkristo” atakutana NAMI angani (1 Wathesalonike 4:17)? Bibi Arusi Ninaowajia watakuwa tayari, wakitii na waaminifu, wananipenda MIMI kwa njia zote, akili, mwili, roho na nafsi, wakiwa wamejivaa bila doa wala kunyanzi. Je, ni Bibi Arusi mgani ambaye hufanya Bwana Arusi kungoja? Ni wageni ambao hukaa kwa muda. Bwana Arusi hawangoji Bibi Arusi WAKE; Bibi Arusi yupo tayari YEYE anapowasili. Kambi ya mauaji hayatakuwa yamejaa Bibi Arusi WANGU. Hakuna Bibi Arusi yeyote atakayepatikana kule. Lakini itakuwa imejazwa na wageni. Nina Bibi Arusi mmoja tu.

Mtakapochukuliwa na kuchungwa kama ng’ombe, mkiwa mmefinyana mmoja kwa mwingine, mahala ambapo hamwezi kusonga kwa upande wa kushoto au kulia, kama bado mko hai, dhahabu itavutwa kutoka midomoni mwenu. Dhahabu itavutwa kutoka midomoni mwenu. Dhahabu itavutwa kutoka midomoni mwenu na vito kutoka miili yenu. Haya ndiyo mtakayopata kwa kufuata mafunzo ya uongo, ishara na maajabu makuu. Nimemtuma huyu nabii kwenu kuwaonya. Shetani anawachezea; nyinyi ni chambo kwenye kulabu. Tazameni na mlie vile viongozi wa kiroho Niliowaamini wakiwashika Watu WANGU kama chambo kwenye kulabu juu ya mdomo wa jehanamu. Viongozi wa kiroho waovu wanajaza mifuko yao na dhahabu kama vile jehanamu inavyojaza midomo ya watu na dhahabu ili wale waovu waivute kama walivyowafanyia Wayahudi. Unachopanda ndicho utakachovuna.

Nyinyi mlio pale Israeli, mnaofuata haya tena, hamjajifunza kutotamani dhahabu ili ivutwe kutoka midomoni mwenu? Angukeni kwa nyuso zenu na TUBUNI leo! Kimbieni viongozi wanaowapotosha. Kwa wale ambao hawakufanya Karamu ya Pasaka, wasipojua la kufanya au kutotaka. Jifunzeni sasa. Mnahitaji Pasaka kutoka kwa hukumu YANGU. Ninawapa nafasi nyingine kwa sababu MIMI ni Mungu wa huruma na upendo. Nilizumgumza na huyu nabii katika ndoto kwa hivyo hamwezi kusema kuwa Mungu wenu hakuwaonya. MIMI, Niwaadhibu wale Niwapendao. Ndivyo ilivyokuwa hapo awali, ndivyo itakavyokuwa tena. Ni chaguo lako.

Je, mnataka kutii sasa hivi au mpitie adhabu YANGU au Niwakatae baadaye? Ndivyo ilivyokuwa hapo awali, ndivyo itakavyokuwa tena.

Kumbukumbu zake Sherrie (Elisheva Sherrie), “Nilikuwa na ndoto ambapo nilijiona nikiongoza Karamu ya Pasaka, vitu unavyohitaji si vingi. Niliona mkate usio na chachu (matzo), applesauce, horseradish, parsley, radish, sharubati ya mzabibu au mvinyo. Someni kujionyesha kuwa mmekubaliwa. Kuna maarifa mengi kwenye intaneti. Someni hadithi ya Musa, amini kuwa mtapitwa na hofu zijazo. Someni Unabii 31.)

* * * * * * *

Imeandikwa, Imezungumzwa. Imepewa katika upako wakati wa maombi kwa huyu mtoto, shujaa, bibi arusi na mtumishi wa YAHUVEH, YAHUSHUA na RUACH ha KODESH. Tarehe 4/29/99, Saa 7:13 usiku.

Tafadhali jisikie huru kunakili na kusambaza haya vile upendavyo. Ujumbe mzima. Wale ambao sipi ruhusa ni wale ambao watakejeli na kujilitea laana juu yao, wao wenyewe. Damu haipo tena mikononi mwangu. Mtume Elisabeth Sherrie Elijah (Elisheva Eliyahu).


* * * * * * *