Unabii 31

Pasaka Yako Ipo Mahala Imani Yako Ipo

Imepewa kwake Mtume Elisabeth Sherrie Elijah (Elisheva Eliyahu)

Machi 30, 1999

Haya maneno yanatoka kwenye Unabii wa 105, YAHUVEH alisema yaongezwe kwenye Unabii zote kutoka sasa: Nilikuonya kitambo Elisabeth [Elisheva], kutoita Huduma hii kwa jina la mwanamume au mwanamke. Hata kabla kuwepo na Huduma, Niliiweka ndani ya roho yako. Kwa kuwa hakuna lolote lililofanyika kwa mikono yako. Hakuna lolote lililotoka kwenye kinywa chako. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUVEH aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUSHUA, MASHIACH wako aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha RUACH HA KODESH, IMMAYAH wako aliyeizalisha. Kama ingekuwa tu kwa mkono wako, ingekuwa imefeli kitambo. Ni kwa UPEPO WA SHKHINYAH GLORY unaovuma kote duniani, UPEPO TAKATIFU WA UAMSHO. Sio kwa pumzi yako, au ingekuwa imefeli. (Isaya 42:8)

Katika mwezi wa Julai 2010, MUNGU YAHUVEH pia Alisema kuongezwe yafuatayo mbele ya Unabii zote kutoka Kitabu cha pili cha Mambo ya Nyakati:

2 Mambo ya Nyakati 36:16, “Lakini waliwadhihaki Wajumbe wa MUNGU, na kuyadharau Maneno YAKE, na kuwacheka Manabii WAKE, hata ilipozidi Ghadhabu ya BWANA juu ya Watu WAKE, hata kusiwe na kuponya.”

* * * * * * *

Hakika ameyachukua masikitiko yetu, amejitwika huzuni zetu, lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, amepigwa na Mungu, na kuteswa. Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, alichubuliwa kwa maovu yetu, adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.” Isaya 53:4-5

* * * * * * *

Nina haya dhidi yenu Marekani! Kiongozi wenu sio tu msambazaji wa usherati bali pia ni msambazaji wa vita. Mitaa yenu haijajawa na upotovu na mauaji ya kutosha, sasa lazima mpeleke haya katika taifa nyingine. Wasiozaliwa bado mwawachinja na huruma kidogo kushinda wanyama wenu mnaowaua kwa chakula! Mwawajali na kuwapenda wanyama kushinda watoto wanaoraruliwa na kuchomwa kila siku wakiwa hai.

Nina haya dhidi yenu Marekani. Mlikuwa taifa liliotengwa na mkono WANGU Mtakatifu kutukuza Bwana Mungu Mwenyezi ambaye Jina lake ni “MIMI NIKO.” Nyinyi ambao hapo awali mlisimamia Uungu sasa nyinyi ni ganda tupu tu. Mnamwaga ghadhabu zenu kwa taifa ambalo hamna haki yoyote kumwaga hukumu zenu juu yake. “MIMI NIKO” Ndiye Ninayo pekee haki hii kwa kuwa kisasi ni YANGU, asema Bwana. Je, wawezaje kutoa michepa machoni mwao wakati nyinyi mna ubao machoni mwenu? Kwanza toeni ubao machoni mwenu alafu saidia mwingine kuutoa mchepa.

Je, mwawezaje kulia dikteta wakati nyinyi mnao dikteta wenu? Marekani, Nimeamuru haya kutoka Mbinguni, msipoanguka chini kwa magoti na kukubali dhambi zenu kama Nilivyotoa onyo hapo awali kupitia huyu handmaiden Nitaizungumza tena kupitia kwake na pia kupitia manabii wengine. “Marekani TUBUNI kwa kuwa hamtawahi kushinda vita nyingine tena!” Mtavuna mnachopanda. Kipimo cha uharibifu na cha kifo unayomwaga, mtakunywa kutoka kwa kikombe CHANGU cha ghadhabu mpaka haitakuwepo tena. Marekani, hapo awali mlikuwa taifa ambalo liliaminika na kuheshimiwa lakini sasa nyinyi ni kejeli ya yote ambayo ni Takatifu. Watu wenu mbeleni walisimamia maadili na viongozi wenu pia, lakini sasa watu wenu na viongozi wenu wanajulikana kote duniani kama waovu na wasioaminika. Mnalinda wahalifu na mwataka kuwanyamazisha walio na haki.

Mnabomu nchi ambayo afadhali huabudu Mungu. Hata Mungu wa wapagani ni heri kushinda kukosa kuwa na Mungu. Kwa kuwa hata taifa la wapagani linakubali kuwa wao si wakuu. Marekani, Nina haya dhidi yenu. Hamwabudu Mungu yeyote! Hampigi goti kwa Mungu yeyote ingawa fedha yenu husema, “Katika Mungu Twaamini” hamwamini Mungu yeyote. Nyinyi Marekani, mna umbo la Utakatifu lakini hamna Utakatifu ndani yenu. Marekani mtavuna mnachopanda.

Nyinyi mnaotuma wajumbe katika nchi zingine na Niwabariki hawa wajumbe na upako WANGU na ardhi za wapagani huja kujua YAHUSHUA kama Bwana na Mwokozi. Lakini nchi yenu hukejeli ujumbe huo. Si wote wanaofanya haya kwa kuwa Ninao watu. Ninao mabaki ambao hawatatingizika. Hawatapiga goti kwake shetani na mafunzo ya mpinga kristo lakini, ni wachache. O Nina huzuni, wengi wanapotea njia. Makundi wanasikiliza mafunzo ya moto mchafu, wakionyesha moto mchafu katika makanisa yao na hata kuomba maombi ya moto mchafu. Tokeni kati yao. Sikizeni sauti ya RUACH ha KODESH WANGU, mwajua sauti ya Mchungaji wenu Mzuri. Jaribu kila hatua na Neno la YAHUVEH. Jaribu kila Roho inayozungumza. Kwa wakati huu na msimu, manabii bandia wanafanana vizuri sana. Wanazungumza maneno wakisema yote yako sawa na baraka tu zipo mbele.

Ndio, kwa watoto WANGU Nitawalinda. Lakini kumbukeni Musa na mjifunze funzo la watoto wa Israeli. Mapigo hayakuja karibu na wale waliokuwa na imani kwangu MIMI, Mungu wa Abrahamu, Isaka na Yakobo. Lakini waliona mapigo yaliyowajia wengine. Ninamtuma Mwana WANGU Mpendwa YAHUSHUA, Masihi wenu, kuja kuwachukua Bibi Arusi WANGU. Je, si Niliwapa ishara katika Maandiko YANGU Matakatifu kuhusu ni nini mtakachongojea na kutazama? Hamjaona hivi vitu vikija kutendeka? Si Niliwaambia kwa kweli kuwa ukoo huu hautapita wanaoona vitu hivi bila Mwana wa Mungu, YAHUSHUA kurudi? Mbona hamniamini? Mbona asilimia 50 tu ya wanaoniamini na kunitumikia MIMI wanaamini kuwa Ninamtuma Mwana WANGU Mpendwa, YAHUSHUA kuwaokoa wale ambao hawataangukiwa na ghadhabu YANGU? Kwa wale wanaokataa kuamini katika Tumaini la Baraka hili, Nina ujumbe kwenu, YEYE hawajii nyinyi.

Kama vile hauwezi kuokolewa bila imani, kwa haya kuwa kweli, pia, hautahesabika kustahili kuwa Bibi Arusi wa YAHUSHUA kama hauna imani. Kama unaishi ni kama Mwana WANGU YAHUSHUA haji, unapangia miaka ijayo ukishughulika tu na vitu vya dunia na mali, basi Nina ujumbe kwako. Haupo katika orodha ya Bwana Arusi, wale walio Bibi Arusi WAKE. Sio wote wanaofaa kuwa Bibi Arusi wa YAHUSHUA. Wengine wanafaa kuwa Wageni. Hii haimanishi kuwa katika wakati fulani hautaokolewa. Inamaanisha kuwa mpaka utembee katika dunia inayofaa kwa ghadhabu YANGU ndipo mtakapoona mlichokosa, ndipo mtakaponirudia MIMI kwa njia mpya na imani mpya.

Alafu kuna wale wanaostahili kuwa Bibi Arusi WANGU (Naamini haya yanahusu imani ya 7th Day Adventist) na kumbe shetani amewadanganya kwa kuwafanya mfikirie mnanitumikia MIMI kwa kubaki katika Dhiki Kuu kubaki kuwahubiria watu. Imani yako inasema,”Nitabaki hapa na kukosa siku kuu ya harusi ili niwasaidie wengine!” Mahala imani yako ipo ndipo utakapokuwa wewe. Je, kwani hamfikirii kuwa Ninaweza kuwainua wengine wanaohitaji adhabu hii kuwafanya tayari kuenda Mbinguni? Kwani mwafikiri kuwa Nahitaji kumwacha Bibi Arusi WANGU mpendwa nyuma ambaye Nilisema kwa Maandiko YANGU Matakatifu omba ili uhesabike kustahili kuepuka ghadhabu zijayo. Lakini mwasema kuwa mmehesabika kustahili na mwafurahia kuachwa nyuma. Jihadharini, mahala imani yako ipo ndipo utakapokuwa wewe. Wengine watatembea katika wakati wa Dhiki Kuu kwa sababu wamechagua. Sio chaguo LANGU, lakini lao. Nitafanya watakavyoamini na kuwalinda imani yao itakavyoniruhusu MIMI kufanya. Mateso mengi yangu hayangefaa kama tu wangetubu sasa kwa kuzungumza haya na kufikiria haya.

Ulimwengu huu utavuna yote ambayo imekuwa ikipanda kwa kipimo kamili. Nilimwonya mwovu Farao na Ninawaonya maadui WANGU tena. Niliwaonya Ninevah na wakasamehewa lakini mwishowe wakarudia maovu na Nililazimishwa kuangamiza yale ambayo Nilikuwa Nimepanga kuangamiza. Kwa kuwa najua nyoyo za waliolaumiwa. Wale kama Farao wanaoongea kwa unyonge na wataacha njia zao za uovu lakini baadaye huyarudia kwa pumzi ifuatayo kwa kunidanganya MIMI na Watu WANGU. Katika waliolaumiwa, hamna ukweli. Haijalishi Nitawafanyia nini lakini hawatanitumikia MIMI wala kuniabudu MIMI.

Nina ujumbe kwake binti YANGU mpendwa aliyepotea, Israeli. Mpendwa Israeli haufai kupeana yale ambayo Nimekupa MIMI. Umepeana mengi sana, Niliwaahidi ardhi iliyo na maziwa na asali. MIMI, Mungu wa Abrahamu, Isaka na Yakobo Niliahidi kubariki nchi yenu na uzuri na kufanikiwa, je sijafanya vivyo hivyo? Lakini viongozi wa nchi hii wako kama wanawake wanyonge wakijificha kwenye kona katika mikono ya mpenzi wao mhalifu. Israeli inaamini uongo wa mhalifu. Israeli huomba kwake Mungu “MIMI NIKO” na huuliza ukombozi lakini huonyesha kwa vitendo vyao kuwa hawaamini “MIMI NIKO” aweza na atalinda nchi hii ambapo siku moja hivi karibuni Mwana WANGU YAHUSHUA, ataiweka miguu YAKE katika Mlima wa Mizeituni. Israeli imekataa kuamini Mungu wa Abrahamu, Isaka na Yakobo tayari ameonyesha mapenzi YAKE kwa kuwatumia MASIHI wao, MKOMBOZI wao, YAHUSHUA ndilo Jina lake!

Watu WANGU wa Kiyahudi, Nilimtuma Mwana WANGU kama mmoja wenu, yeye sio Mwokozi pekee kwa Mataifa lakini kwenu nyinyi pia. Ombi LANGU ni Wayahudi wote na Mataifa wawe kitu kimoja katika YAHUSHUA. Je, mbona mwamngoja Masihi mwingine? Wakati Nimewapa mazuri YANGU. Shetani yuataka kuwadanganya na mazuri yake. Ninawatuma Manabii WANGU na Ninawatuma tena kuwaambia o binti YANGU mrembo na aliyepotea, sikilizeni maandiko yenu. Angalieni na macho mapya ya utambuzi kwa karamu na sherehe zenu. Msipende tu nusu YANGU, mpende kila kinachonihusu MIMI.

Nyinyi mnaosema kuwa Mungu wa Abrahamu, Isaka na Yakobo ni wenu na Nina mabaki wanaofanya hivi, kama katika sehemu nyingine za dunia, lakini lazima mkubali kila kinachonihusu MIMI. Kwa kuwa YAHUSHUA ni Mwana WANGU Mpendwa aliyeuwawa kama dhabihu ya mwana-kondoo kamili asiye na madoa, kwa wote ambao watakubali Damu Inayookoa iliyomwagwa pale Kalvari kwa kutoa dhambi. Damu YAKE ililowesha mchanga pale Kalvari lakini ilipokuwa ikimwagika kwenye ardhi pia ilifunika Yerusalemu na huruma. “Baba wasamehe kwa kuwa hawajui wanayofanya ni kwako pia.” Nimevumilia sana ewe mwana mpendwa uliyepotea, unaotaka kunifurahisha MIMI lakini hukataa tuzo LANGU pale Kalvari. Njia ya pekee pale Mbinguni ni kupitia YAHUSHUA; hamna jina lingine linaloweza kuokoa ila YAKE.

Nilijaribu kukufanya ujawe na wivu na Nikawapa mataifa fahamu, wale ambao hawamtafuti MASIHI hata. Sasa Ninarudi kwenu kupitia huyu nabii na wengine Ninawatuma na hawasemi mmtupe YAHUSHUA. YEYE si MASIHI kwa Mataifa pekee lakini kwanza alitumwa kwa Wayahudi Ninaowapenda na hamwezi kuelewa. Je, si YAHUSHUA, alizaliwa kutoka kwake mwanamke Myahudi? Nyinyi Israeli hamfai kuogopa majitu nchini mwenu. Je, kwa nini mmesahau kuwa Nimeahidi kuwalinda wale ambao wametengwa na kukombolewa?

Nyinyi Israeli msipeane ardhi yenu ambayo sijawapa kupeana. Niliwapa hii ardhi kupitia baba zenu wa kale. Ardhi hii haiwezi kuchukuliwa lakini mwaweza na mmelazimishwa kufikiria kuwa majitu haya yatachukua ardhi hii na hawawezi kuchukua ambacho hampeani. Watu WANGU wanalilia “Pasaka kutoka kwake mwovu Farao tena.” Watu WANGU “MIMI NIKO” Ninamwongoza RUACH ha KODESH kuwafanya wale ambao wanaamini “MIMI NIKO” ni Mungu asiyebadilika na hubaki sawa na huwalinda wote wanaosema kilicho CHAKO ni changu, na kilicho changu ni CHAKO. Msiinamie mungu mwingine, Israeli! Israeli, msiinamie binadamu wapagani ambao sio mungu lakini ni vumbi ya kukanyagwa chini ya miguu yenu.

Msiyasikize maneno ya maadui inayosema tuongeze kipande kidogo tu cha ardhi, alafu wataenda na kuwaacha katika imani. Nimewaongoza Watoto WANGU katika Maandiko Matakatifu kuombea Amani ya Yerusalemu. Leo, kupitia nabii huyu, Ninazumgumza maneno haya tena. Msiwaamini wanaokuja kama majitu yanayotisha mtoto mdogo. Nyinyi sio watoto wadogo, Israeli. Nimemwaga upako WANGU kwenye ardhi yenu. Itumie kwa Utukufu wa “MIMI NIKO.” Ukuta wenu wa Hekalu uliolowa na machozi ipo mbele YANGU daima. Vilio vyenu hulia masikioni MWANGU. O Nina hamu ya kuwakumbatia mikononi MWANGU na kuwabembeleza na Nitafanya vivyo hivyo. Lakini msikatae tuzo LANGU Niliyowapa pale Kalvari, Jina LAKE ni YAHUSHUA. YEYE pekee Ndiye Wokovu wenu.

Msitamke tu maombi mnayoyazungumza Israeli, bali myaamini maombi mnayoyatamka. Msisherehekee tu Pasaka lakini mwamini kuwa ni Pasaka yenu. Haya pia ni ya watoto WANGU wote wapendwa wanaotaka kunifurahisha MIMI, wanaonitii MIMI, wanaonitumikia MIMI, wanaoniabudu MIMI, kuniweka MIMI Mungu mkuu “MIMI NIKO” na YAHUSHUA juu ya kila kitu. Ninatuma ujumbe huu na Nimeizungumza tayari kwa umati kupitia RUACH ha KODESH WANGU. Kama wataka ukombozi wa Pasaka kutoka kwa mikono ya maadui, lazima usherehekee na kuamini na kuwatia moyo wengine. Hii ni Pasaka yenu na mtapatikana kustahili kuepuka ghadhabu ya “MIMI NIKO” ijayo. Mapigo yatakupita na hayatakuguza, mapigo yote, kama wakati wa Musa itakuwa vivyo hivyo tena lakini mtakuwa na njia ya kuepuka. Mtakuwa na Pasaka tena. Damu ya YAHUSHUA ni Pasaka yako. Kama wayasoma haya, utawajibika kwa yale uyajuayo. Je, utayafanyia nini?

Pasaka ni ahadi yenu! Mungu wa Abrahamu, Isaka na Yakobo, Mungu mkuu “MIMI NIKO” Nitawakomboa tena katika njia ambazo hamfikiri kabisa kama tu mtaamini. Mahali imani yako ipo ndipo Pasaka yako ipo. Wale wanaoishi Marekani na Nimetabiri ghadhabu ijayo, haya ni kweli lakini kwa wale wanaomwamini “MIMI NIKO” na Pasaka, na kama Musa, Nitatoa njia ya kuepuka kwenu nyinyi, hamtaaibishwa kuwa mliamini. Nitathibitisha kuwa Mungu mkuu “MIMI NIKO” siwezi na sitawadanganya. Mahali imani yako ipo ndipo Pasaka yako ipo.

Mpenzi WANGU, usifikiri kuwa Ninasema hakuna yeyote kati yenu ambaye hatateseka, kwa katika dunia hii kuna machungu na mateso lakini Nimetuma njia ya kuepuka. Ninamtuma Mwana WANGU kama Nilivyowaahidi. Lakini, hii haimaanishi kuwa uketi tu na kutofanya lolote. Sasa ndio wakati wa kukusanya mavuno ya siku za mwisho kama bado kuna wakati. Tumia karatasi yako na plastiki kama mbegu kuleta Utukufu KWANGU. Hamasisha na maombi na msaada, huduma Ninazokuelekeza kuwaombea na kufanya kazi nao. Sio eti huduma hizi ziweke mali hapa duniani, kwa kuwa huduma hizi zitakazofanya hivi, Nitahakikisha mwenyewe kuwa ziwe mabua zitakazoangamia.

Kuleni mkate wa mateso inayoitwa matzoh. Msile tu kwa sababu ni ishara ya yale Wanaisraeli walikula walipokimbia kabla mkate haujavimba. Pia Ninataka mshiriki katika siku za mkate usio na chachu na kula mkate wa mateso kama kumbusho la YAHUSHUA na vile alivyolipa gharama kama mkate wa mateso. Aliteswa kwa ajili yenu. Mkate huo ni mgumu kwa sababu gharama aliyokulipia wewe haikuja kwa urahisi. Shiriki katika Meza ya BWANA kama YAHUSHUA alivyofanya. Fanyeni haya kwa kujikumbusha Damu ambayo YAHUSHUA Alimwaga ili tuokolewe na ule Mkate uliowekwa kwenye Damu, kwa YAHUSHUA Ndiye Mkate wa Maisha na Mwili wake ilitolewa kama dhabihu ili uweze kushiriki na “MIMI NIKO” na ondoleo la dhambi ili uwe na njia ya kuepuka kutoka moto wa jehanamu. Shetani hana chake kwa wale ambao kwa kweli ni WANGU.

Kila wakati ukiomba kumbuka kuwa sasa ndio wakati wa kuomba kuwa utapatikana kama anayestahili kuepuka ghadhabu zijazo hapa duniani. Ghadhabu ya “MIMI NIKO” sio tu hasira ndogo, imekuwa ikiongezeka na ni jambo la kuogopa sana kuanguka katika mikono ya Mungu Anayeishi. Lakini kwa Watoto, Bibi Arusi, Waliochaguliwa, na Wateule wasiwe na hofu. Nitawamwagia tu Baraka ZANGU na sio ghadhabu YANGU. Lieni kwa yale ambayo Marekani na marafiki zake wanaofanya sasa. Lieni kwa sababu hata wapagani huabudu mungu. Lieni kwa kuwa wengine ni ndugu na dada zenu katika YAHUSHUA, ambao mabomu zinawaangukia. Damu hii inayomwagwa na kisasi kutolewa na “MIMI NIKO” Ninatazama na Nimeiruhusu, kwa wale wanaoshiriki katika maneno haya, wanailetea nchi yao laana na wao wenyewe. Msishiriki katika vita hii na msiamini uongo inayosema, visingizio vinavyopewa. Serikali wana hoja zao na kumfurahisha Mungu Mkuu “MIMI NIKO” sio moja yao. Kuwaokoa waliokanyagwa sio moja ya sababu. Kujionyesha katika kiburi na kiburi ndio moja ya sababu. Ombeni viongozi wenu watatubu maovu haya kama wakati haujapita.

Andamana, zungumzeni dhidi ya vita hii. Marekani, mmeyaleta haya juu yenu kupitia kiburi na roho ya kutawala. Mmeyaleta yale yajayo kwa nchi ambayo Nimeilinda kwa Mkono WANGU hadi sasa. Vita havijaja kwenye mikoa yenu lakini yaja. Kwa ajili ya wapendwa WANGU Nitaushika mkono wa mwangamizaji kwa muda mfupi, o kwa muda mfupi sana. Mnatuma vita kwa nchi nyingine. Mtapata vita katika nchi yenu kwa kufanya vitu kwa kiburi. Mnazungumza dhidi ya nchi nyingine na bado hamsikii mwangwi wa yale mnayoyasema ikiwarudia katika masikio yenu. Kwa kuwa ni kwa maneno ambayo mnayoshtaki wengine ndio viongozi wenu hufanya wenyewe kawa siri.

Kila Mmarekani anafaa kushtuka kwa yale yanayofanywa. Viongozi wenu wote wa siasa na kiroho lazima watubu na kuyaacha yale wanayoyafanya. Kama Watu WANGU wanaojiita kwa Jina LANGU watanyenyekea na kuanguka kwa magoti na kutubu, Nitaiponya ardhi yao! Nitawasamehe. O lakini wana shingo ngumu na wakaidi, wakisema kuwa hawatendi dhambi na dunia nzima yaweza kuiona dhambi lakini wanasiasa wa Marekani na wale wanaofuata watendao maovu haya wanafanya vitu hivi.

Kama Marekani haitatubu “MIMI NIKO” Nitaangamiza ardhi yao, Nitaifanya iwe kejeli katika ardhi hii iliyoitwa hapo awali huru na shujaa. Kwa Watoto, Bibi Arusi, Waliochaguliwa na Wateule WANGU wanaosoma haya, msiwadhulumu Yerusalemu. Msiwadhulumu Israeli. Ombeni kwa amani ya Yerusalemu ili Niwabariki. Ombeeni mataifa ambao wametumiwa vita na NATO. Ombeni Watu WANGU na muwe na huzuni kuhusu yale yanayofanyika. Tena Siku ZANGU Takatifu zinachafuliwa na wapagani. Mimi sio Mungu wa kukujeliwa. Wale wote walio na hamu ya PASAKA kutoka kwa ghadhabu YANGU basi Ninawapa amri hii ambayo haijawahi kubadilika, tazama na ombeni kuwa PASAKA yenu ije. Jina LAKE ni YAHUSHUA ha MASHIACH na ombeni mtapatikana kustahili kuepuka ghadhabu YANGU na dhiki ijayo. Tayarisheni mkoba wa kusafiri kama utaihitaji kabla MASIHI wako hajaja kukuchukua. Kuna wale wanaosoma haya watakaotembea katika moto wa ghadhabu YANGU na dhiki. Wengine watafanya haya na Nitawalinda kwa njia ambazo hawawezi kufikiria.

Wengine watasoma haya na kumkejeli huyu handmaiden anayeleta ujumbe huu. Jihadharini, haya si maneno yake mnayoyakejeli kwa hivyo tena mjihadhari. Haya maneno mnayoyakejeli yatawarudia na kuwaandama kwa kuwa mnamkejeli Mungu Mkuu “MIMI NIKO,” sio maneno ya Sherrie Elijah [Elisheva Sherrie Eliyahu]. Kama yangekuwa yake yangekuwa hewa tu, lakini yakiwa Maneno YANGU ni maneno ya uzima na nguvu na Nitafanya Ninachozungumza. Ninawatuma Manabii WANGU na watume kutabiri kabla sijatuma Ghadhabu au baraka. Nyinyi ambao hukejeli mtaitambua ghadhabu YANGU ijayo. Yeye ameagizwa kuzungumza maneno YANGU hata kama yanapendeza masikio yenu au la. Yeye atawajibika kama atajishikilia na kupuuza ukweli kwa sababu ya hofu ya mtasema nini au wengine walio na mamlaka watasema nini. Manabii WANGU wote wanaonisikia Mungu Mkuu “MIMI NIKO” nyinyi wote mmepuuza ukweli na mwataka kuyazungumza tu maneno yanayowafurahisha masikio na ambayo yataleta huzuni mwingi wakati yale uliyoyazungumza hayatatendeka. Mwajali ni nini chama chenu cha Manabii kinachosema na sio Mungu Mkuu “MIMI NIKO” Anachosema. Mwajadiliana kati yenu na kutasfiri kwa hekima na ufunuo wenu, na sio hekima na ufunuo WANGU.

Jihadharini nyinyi mnaojiita Manabii WANGU na huwa hamzungumzi neno TUBU na geuka kutoka kwa dhambi. Jihadhari nyinyi mnaozungumzia maovu yajayo na hamwapi Watoto WANGU imani yoyote! “MIMI NIKO” sipo katika hizi unabii. Huwa kuna njia ya kuepuka kwa Watoto WANGU wapendwa, Bibi Arusi, Waliochaguliwa na Wateule. Nitatoa njia mahali ambapo hapatakuwa na njia. Kwa sababu hauyajui sasa, ni kama mwanadamu na tikiti ya kusafiri, hamhitaji tikiti hii mpaka ni wakati wa kuondoka. Hamhitaji hekima sasa hivi kwa kuwa Nikiwaambia Manabii WANGU njia ZANGU za kuepuka, basi mpendwa, adui pia atajua. Ninao WANGU ‘Waliofichwa’ na haya ndio yale mwahitaji kujua kwa wakati huu. Sio wote watakaoambiwa Kutoroka. Kama hautanisikia MIMI Nikiizungumza na kuithibitisha na kushuhudia ndani ya Roho yako, basi Nitakulinda papo hapo ulipo. Kama sijakwambia ni wapi utakapoenda sasa, basi Nitakuambia wakati wa kuondoka utakapokuja.

Kama katika wakati wa Lutu na Musa, itakuwa vivyo hivyo tena, “MIMI NIKO” Nitatuma Pasaka yako. Usiache machweo ipite bila kuomba kuwa Pasaka yako ya kweli, YAHUSHUA, aje. Shirikini katika siku hii sio kwa lazima lakini fanya uwezavyo. Jifunzeni na kujionyesha mmekubalika ili mjue mtafanya nini leo hii. Je, Ninauliza mengi Nikiwauliza msile mkate bila chachu kwa siku 8? Kukula mkate wa Mateso kukukumbusha yule aliyelipa gharama kama Mkate wa Mateso kukuletea Pasaka yako.

Nilipanga kuwa Wanaisraeli hawatakuwa na muda wa mkate kuvimba. Nilipanga kwa kuwa hawakujua lakini haikuwa makosa kuwa Niliwafanya watoroke ili mambo haya yatendeke. Kwa kuwa tena Wayahudi walikula na kutoa Mkate wa Mateso kwanza inayoitwa Matzoh na sasa Ninawapa maarifa haya ambayo walipewa, kwa kuwa ni YAHUSHUA ambaye alikuwa yuaja, ilipewa kama kumbusho. YAHUSHUA ni Pasaka kwa wote, Wayahudi na Mataifa. Hakukuwa na hamna Dhabihu nyingine kamili ya Mwana-kondoo inayoweza kuchinjwa kwa ondoleo la dhambi, ikiziosha kabisa ni kama haikuwa ila moja tu. Jina LAKE ni YAHUSHUA ha MASHIACH, Jina LAKE ni WOKOVU! YEYE pekee Ndiye Pasaka. Sherehekeeni na kujifunza maana sawa ya Pasaka iliyokuwa na Pasaka ijayo.

Heshimu Siku za Sabato, pia Siku Kuu Takatifu, Aprili 1, Aprili 2. Heshimu Siku za Sabato zote zilizokuwa kutoka Ijumaa machweo hadi Jumamosi machweo… sio Jumapili kama wengi wenu mnavyonikumbuka MIMI Jumapili na kuishi kama shetani kutoka Ijumaa hadi Jumamosi machweo mkijihusisha katika mambo ya dunia kwa siku ambazo zimetengwa kwa Sabato yetu. Ombeni kwa Pasaka kutokana na ghadhabu zijazo katika dunia hii. Ombeni kuwa mtapatikana kustahili na hizi bakuli na mlio wa ghadhabu ZANGU zitawapita na mtapatikana kustahili kuepuka na haya. Kwa kuwa “MIMI NIKO” ni Mungu ambaye hawezi na hatawahi kudanganya, Natabiri yajayo kupitia Manabii WANGU ili yeyote asiseme kuwa “MIMI NIKO” hakuwaonya watu.

Ukifika ule upande mwingine, je, itakuwa Mbinguni au Jehanamu na laana? Pasaka yenu ikija, je, utanyakuliwa au utakuwepo kwenye Dhiki Kuu kama dunia hii haijawahi kujua wala haitawahi kujua tena. Je, mtafanya nini na ujumbe huu wa kinabii kutoka kwake “MIMI NIKO”? Je, utaupita na kusahau ukiuita ujinga? Au utajitayarisha kwa Pasaka yako aitwaye YAHUSHUA ha MASHIACH. Ombeni leo kuwa wote wanaosoma haya na hawajui vile kuwa bila doa wala kunyanzi. Andikieni huyu Mchungaji. Atakukaribisha kwake Kondoo wa kweli wa Pasaka aliyeuwawa na kufufuka tena kutoka mauti katika siku ya 3. Aliyeweka maisha yake chini kwako wewe ili uokolewe kwa dhambi zako kuoshwa na Damu kamili ya Pasaka wa kweli, kondoo wa Mungu asiye na dhambi, Mwana wake “MIMI NIKO” aitwaye YAHUSHUA ha MASHIACH. YEYE pekee ni MASIHI wako kwa wale waliokubali tuzo yake “MIMI NIKO” tuzo ya Pasaka pale Kalvari.

Kwa wale wanaompenda, kumtumikia, na hujaribu sana kutii amri za “MIMI NIKO”, wakijua wakikosa wanayo kondoo wa Pasaka ambaye Damu yake ilimwagwa pale Kalvari kwa dhambi zenu, na pia mwajua kuwa hamfai kunijaribu MIMI na kutenda dhambi kimaksudi kwa sababu mwafikiria mwaweza. “MIMI NIKO” sitakejeliwa na kila mtu lazima atimize wokovu wake kwa kuogopa na kutetemeka kwa kuwa “MIMI NIKO” pekee Ndiye Ninayejua moyo wako wa kweli na hoja na nia. Sasa Nimezungumza. Je, mtafanya nini na Pasaka yenu? Kwa wengi wenu mnaosoma haya hakutakuwa na chanzo nyingine ya kusherehekea Pasaka. Ni wakati wa kuamua, ni chaguo lako. Jihadharini, tayari Ninajua mlichochagua. Je, mtaniheshimu MIMI kwa hii Pasaka?

Imezungumzwa, imeandikwa siku hii ya Machi 30, 1999 Saa 4:26 Alfajiri, kupitia Handmaiden WANGU Sherrie Elijah [Elisheva Sherrie Eliyahu], katika upako WANGU wa RUACH ha KODESH utakaovunja pingu zote na utumwa.

* * * * * * *

Ujumbe kutoka kwake Mtume Sherrie Elijah (Elisheva Sherrie Eliyahu). Tafadhali jisikie huru kuwapa moyo na kutuma ujumbe huu kwa wengine kuwafunza na kuwapa moyo, pia kuwaonya. Nimezungumza na kuandika ujumbe huu uliokuwa umefungwa kama moto ndani ya mifupa yangu ikingoja wakati na msimu. Pasaka hii ninatafuta ukombozi kutoka kwa Mafarao Waovu waliojaribu kuniangamiza na huduma hii na pia shirika hili la wapendwa. Ninatarajia kukombolewa kutoka kwa pingu zote na utumwa.

Ninasherehekea Pasaka kwa mara yangu ya kwanza kama wengi wenu mlivyoongozwa na RUACH ha KODESH. Mwaka huu wa 1999 tulioupitia umekuwa mwaka usioeleweka. Lakini kwa kukumbuka na kusherehekea siku za mkate usio na chachu na Pasaka tunaweza kuamini kuwa tunaye Mungu YAHUVEH na YAHUSHUA. Ninataka maovu yapite na yasiniguze wala wapendwa wangu, huduma na wote walio sehemu ya shirika hili. Tafadhali tuandikie na utujulishe wataka ukombozi kutokana na nini Pasaka hii. Ukikubali, tutaweka mahitaji yako mbele ya wengine ili wakuombee pia. Sote tunahitaji ukombozi kutoka kwa kitu au mtu.

Kwa huduma hii pia ninatarajia Pasaka ya uhuru kutoka kwa vifungo vya deni. Tunafanya kazi kuiweka tovuti nyingine ISP yake ikitoka Israeli. Hii ni tendo la imani kuu na kazi iliyo na gharama kubwa sana. Nimepewa amri kufanya vivi hivi kwa sababu ‘nguvu zilizo’ zitakapotaka kuninyamazisha mimi katika sehemu moja, tutaendelea kuzungumza kutoka sehemu nyingine ya dunia. “MIMI NIKO” amenipa amri kufanya haya hata ingawa binadamu wanaweza kuifikiria ujinga Nikimtii Mungu na sio bindamu. Yeyote atakayeongozwa na RUACH ha KODESH kunisaidia katika tendo hili la imani, tafadhali tuma barua pepe au niandikie. Sasa tunazo tovuti Canada, Marekani, na hivi karibuni Israeli. Nyingine baada ya hapa, Bwana akichukua muda kuja, itakuwa Afrika. Tafadhali jisikieni huru kuchukua kopi na kusambaza ujumbe huu kwa wote wanaohitaji kusikia ukweli itakayowaweka huru. Kile nitakachouliza ni haya tu, msiondoe au kubadilisha sehemu yoyote, fikisha ujumbe wote ilivyo hata sehemu hii ya mwisho ninayoiandika. Simpi mtu yeyote ruhusa ya kusambaza ujumbe huu Mtakatifu wa Kinabii kama ni kwa kunikejeli mimi au ujumbe huu.

Ninanyenyekea kwa kutumiwa tena kufikisha jumbe za MUNGU Mwenyezi kutoka Mbinguni. Kuwa Nabii ni tuzo na pia wakati mwingine inaweza kuwa kama laana kwa kuwa tunaogopa kama hatukumsikia MUNGU vizuri? Je, nilizungumza yote Mungu alitaka niseme? Naomba msamaha sasa ninapokosea, ninajaribu sana iwezekanavyo kusikia yale YAHUVEH anayozungumza kupitia RUACH ha KODESH ndani mwangu. Lazima nifikishe jumbe na nisipuuze ukweli kwa kuruhusu roho ya kuogopa kuingia.

Chombo cha Udongo lakini Shujaa Mkuu wa YAHUSHUA, Mtume Elisabeth Sherrie Elijah (Elisheva Eliyahu)* * * * * * *