UNABII WA 1

HUKUMU HUANZA KATIKA NYUMBA YA YAHUVEH! 

Alipewa Rev. Sherrie Elijah Disemba 31, 1996. 

* * * * * * * 

Ni jambo la kuogopa na kutisha kuanguka kwenye mikono ya MUNGU aliye hai. Ghadhabu YANGU yaweza kuwa kuu kama pendo LANGU, lakini hakuna anayeongea kuhusu haya. Katika mwaka wa 1997, Nitajitokeza MIMI MWENYEWE si kama MUNGU wa Upendo pekee, lakini kwa wale wanaokejeli na kukana nguvu ZANGU, au wanaokataa Upendo WANGU, na hutafuta kuwapotosha mbali Kondoo WANGU…watatambua siku za Ananias na Sapphira tena. Hekima ni kuogopa YAHUVEH! Wengi wa kondoo WANGU hawanithamini MIMI. Wao hufanya vitu na hufikiria vimefunikwa na neema. Wao hufanya vitu wakijua kuwa si takatifu na vinanikera MIMI.

Lakini wao hufikiria MIMI NI kipofu na kiziwi. Mwaka wa 1997, Nitawaonyesha kuwa MIMI ni MUNGU wa moto na kitakachosimama njiani mwa Wahubiri WANGU kitachomwa kwa hasira YANGU. Wale ambao huthubutu kukomesha INJILI ya YAHUSHUA ha MASHIACH watateseka zaidi. Ninaijia kanisa isiyo na doa wala kunyazi na tena Nawaambia, wape onyo kanisa. Kanisa si Mchungaji, si mjengo. Kanisa ni watu, Kondoo WANGU. Nimechoshwa na binadamu kuziita huduma kwa majina yao; hawana haki yoyote kutenda hili chukizo. Hawakulipa gharama; hawana utakatifu wa kutosha kufanya hivi. MIMI, YAHUSHUA ha MASHIACH, nililipa gharama hii pale Kalvari.

Kama wana dhambi na wao si kamili, hawana haki yoyote kuita huduma kwa majina yao. MIMI pekee ndiye kamili na bila dhambi, si binadamu, “kwa wote wametenda dhambi na kupungukiwa na Utukufu wa YAHUVEH!” Wewe hauna dhambi mbele YANGU kwa sababu Damu YANGU huosha dhambi zako. Si kwa sababu hauna dhambi kwa kuwa kamili. Wewe ni mtenda dhambi aliyeokolewa kwa neema YANGU na huruma. Damu ya Kalvari huosha dhambi zako, kweli. Lakini huduma huniwakilisha MIMI, Baba yako YAHUVEH na huduma lazima ipewe jina la utakatifu, sio binadamu.

Tena, Natabiri kupitia kwako na kusema jihadharini. Wape onyo, kwa kuwa binadamu asiye kamili atakapoanguka (na ataanguka) huduma iliyo na jina lake itaanguka na kondoo watatawanyika hadi kwenye kambi la adui. Waambie, Handmaiden WANGU. Wape onyo. Msitende chukizo hili mbele ya macho YANGU kamwe. Kwa kuwa Nilisema, kuwa Mtakatifu kama Nilivyo Mtakatifu. Hata wale Manabii wanaojulikana na Wahubiri waliobeba upako WANGU wapo katika kiburi cha upumbavu na wanaita kile ambacho si chao…huduma zilizo na upako kwa majina yao. Kwa sababu ya haya, wataanguka. Nitakuwa papo hapo kuwainua baada ya kuwanyoosha.

Lakini wape onyo, ni kama mtoto anayepigwa, lakini alikuwa ameonywa wakati mwingi. MIMI, huwanyoosha wale Ninaowapenda. MIMI ni mwana kondoo kwa wale wanaokubali zawadi ya Damu YANGU kutoka pale Kalvari. MIMI ni SIMBA wa kabila ya Yuda kwa maadui WANGU. MIMI ni shujaa na si mwoga. Niligeuza shavu langu mara moja. Lakini nikija tena kwa maadui WANGU, Ninaleta ghadhabu YANGU. Ole wao wanaojiita adui WANGU na huthubutu kuharibu kazi nzuri ambazo Ninafanya kupitia watumishi WANGU. Simba hupasua na kurarua kabla hajala windo lake. Tai pia hufanya hivi, na huwakilisha Baba yako aliye Mbinguni. Utaona ghadhabu YANGU katika 1997. 

Lakini watoto WANGU hawana lolote la kuogopa, wale wanaonipenda kweli, wanaoniabudu, wanaoniweka MIMI kwanza katika maisha yao. Nitafanya usafishaji katika hekalu hizi. Nitawaonyesha kuwa MIMI ni MUNGU wa kuogopwa sana. Bado MIMI ni MUNGU anayehitaji Utakatifu kutoka kwa Watoto WAKE. Sizungumzi kuhusu umbo la nje; hii ni ubatili na utakatifu ulioumbwa na binadamu. Utakatifu wa kweli hutoka ndani yako. Kunakucha na kushaanza vita vya kiraia kule Marekani.

Lakini, kusiwe na vita vya kiraia katika kanisa ZANGU. Kusiwe na ubaguzi, iwe umbo la nje au kirangi. Kwa kuwa Watoto WANGU wanapoonana, wanapaswa kuona NYEKUNDU pekee, DAMU YANGU! Acheni kugawa kanisa zenu kwa rangi. MIMI sioni rangi yoyote. MIMI ni rangi zote katika moja. Acheni kuhukumiana kwa umbo la nje. Kwa kuwa mahali roho ya ubaguzi ipo, RUACH ha KODESH (Roho Mtakatifu) WANGU hatabaki, hataishi. Badala YAKE, pepo mbaya zitaruhusiwa ndani. Mmepewa onyo.

Sherrie, (Elisabeth) haujajua ni nini utaandika kutoka neno moja hadi lingine. Wape unabii huu wale wote walio na masikio ya kusikia, wacha wale wengine wabaki viziwi. Ninaijia kanisa isiyo na doa wala kunyazi. Kinachonishikilia MIMI, ni kile kinachotakikana kunirudisha MIMI. Kanisa YANGU! Watu WANGU! Wachungaji WANGU! Wahubiri WANGU! Ninachukia kiburi! Ni moja ya dhambi 7 hatari, lakini bado wachungaji WANGU wanaobeba upako WANGU hufikiria wao ndio hujenga kanisa, kanisa ni zao na lazima wapate udhibiti wa kondoo. MIMI pekee ndiye Mchungaji Bora. Kazi yenu ni kuwa kidole kitakachowaelekeza KWANGU, YAHUSHUA.

Kiburi, kiburi kuu, imeingia katika hekalu Nilizozimwagia upako WANGU. Ni nani aliye na mkusanyiko kubwa, pesa zaidi? Haya hunikera MIMI. Ni nani anayeshinda roho nyingi? Wivu na tamaa ziko katika hekalu ZANGU. Haya hunikera MIMI. Mnasema, “YAHUSHUA yuaja lini tena?” Nasema, “Nimekuwa nikingoja kanisa, hekalu hizi, wajisafishe.” Acheni kuhojiana kati yenu wenyewe. Fichua mbwa mwitu ambao wamekuwa wakiwala Kondoo WANGU. Wapo nyuma ya mimbari na watu wote wanajali tu kanisa zao, hakuna yeyote anayewajali kondoo.

Nani anaweza kujenga hekalu kubwa? Nani anaweza kuwavutia zaidi wanahabari? Ni mwinjilisti yupi, nabii yupi, mchungaji yupi, kanisa ipi, aliye au iliyo nambari moja? Ninawaambia kupitia huyu Nabii, msikilize. Hukumu huanza katika nyumba ya YAHUVEH! Alafu nitakabiliana na wapagani. Haya hunikera MIMI. Nina hamu ya kuwakumbatia nyote mikononi MWANGU, na bado mnahojiana na kutusiana kwa sababu ya jinsia yenu. MIMI huchagua kumtumia yeyote Nitakayechagua kumtumia. Aliye mnyenyekevu kati ya wote Nitamtumia kwa njia hodari.

Nachagua kutumia chombo hili kwa sababu yeye hufikiri ya kwamba yeye ndiye mdhaifu kati ya wote, lakini Nasema tena, Nitatumia wale wanyenyekevu na wapole, wale ambao hakuna yeyote hufikiria kuwa naweza kuwatumia, kwa nguvu YANGU hujitokeza bora kwa wale watu wadhaifu. Wengine hujua kuwa nguvu hii sio yao na hawajisifu. Kwa sababu wanajua ni upako WANGU pekee unaovunja kila nira, mnyororo, pingu na utumwa. Si kwa uwezo wako wala nguvu bali ni kwa Roho YANGU. Hivi ndivyo anavyosema YAHUSHUA, “Nilichagua kuja kama mtoto, mdhaifu kati ya wote kuwaonyesha, msiangalie umbo la nje, angalieni ndani. Upako haujui jinsia, rangi, umri.”

RUACH ha KODESH (Roho Mtakatifu) hutumia walio tayari, vyombo vya udongo walio watiifu, si wale wanaopiga kelele, “Nitumie mimi kwa sababu mimi ni mrembo, mimi ni mtakatifu kushinda wote.” Sitatumia wale wanaofikiria wao ni dhahabu; MIMI hutumia wale wanaojua wao ni vyombo vya udongo vilivyovunjika lakini wao ni shujaa hodari wa YAHUSHUA ha MASHIACH. Katika 1997, Nitawazindua wale walio na huduma zilizobaki katika unyenyekevu au wasiojulikana kwa umati. Wale ambao sikuwaita tu lakini waliochaguliwa, wamechaguliwa kwa sababu ya imani yao ambayo MIMI ndiye mwandishi na mkamilishaji. MIMI huwa sianzi kitu alafu kufeli. MIMI ni MUNGU wako asiyeweza kufeli.

Kuwa tayari, kwa katika 1997 nawaambia mali ya waovu itarudishwa kwenye mikono ya watakatifu kupitia JINA LANGU na Damu YANGU YAHUSHUA ha MASHIACH. Ni Kondoo WANGU watakaokuwa na mali na kazi. Watoto wa adui wataona haya na kusaga meno yao kwa hasira na wivu, lakini Nafanya hili kuonyesha kuwa neno LANGU sio uongo. Baraka za Kumbukumbu la Torati 28 bado zimewekewa Watoto WANGU na Ninawajua wote kwa jina na kwa nywele zilizo kichwani mwao.

Kuwa tayari, kwa sababu kwa Watoto WANGU, huu ndio kumwagwa mkuu wa RUACH ha KODESH (Roho Mtakatifu). Nitatumia wale wanaofikiria hawajulikani, si warembo, hawana elimu, wale wanaojua hawawezi kufanya chochote bila upako WANGU wa RUACH ha KODESH (Roho Mtakatifu). Wale waliotupwa, walionyanyaswa, waliopuuzwa, walioambiwa wakate tamaa, hakuna thamani.

Wale ambao hawajakuwa na fedha watamtegemea Mwenyezi MUNGU na nitawafungulia dirisha za mbinguni na kuwabariki zaidi hadi watalazimishwa kuwapatia wengine ili wao pia wabarikiwe zaidi. Na hili litakuwa jambo ambalo litatendeka mara kwa mara. Neno LANGU husema, “Mpenzi, naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo.”

Nitawaonyesha ya kwamba Neno LANGU haliwezi kurudi KWANGU tupu. Jihadharini nani unayemtupa kama asiye na thamani. Kwa kuwa ni mchungaji aliye na kundi ndogo, lakini husisitiza kuwa RUACH ha KODESH achukue udhibiti hata kama kondoo wengi hutoka na kuenda katika kanisa ambazo hazina ishara, maajabu, miujiza, kwa kuwa thibitisho ya RUACH ha KODESH haipo pia.

Jihadharini na kuwakana wainjilisti wasiojulikana katika macho yenu, na wanaotumia fedha zao kueneza injili ya kushinda roho. Jihadharini kukejeli, kuwatusi na kudharau Nabii anayekuja kwako na unabii na kwa sababu hautaki kuamini unabii huo kwa sababu wao ni jinsia tofauti au hawajulikani na wao sio maarufu. Jihadharini kuwakosea watoto wadogo Ninaowatayarisha kutabiri na ndio, kuwapa onyo wazee wasikilize sauti ya Mwenyezi MUNGU.

Tokeni katika kiburi. Kwa sababu hawa ndio Ninaowatuma. Mkiwakosea, mnamkosea MUNGU aliyewatuma. Wao ni Wajumbe WANGU, kwa hivyo msimpige mawe mjumbe. Ni hawa wasiojulikana Ninaowainua, kupitia wasiojulikana Nitawatumia kufanya ishara, maajabu na miujiza YANGU, na kwa kuwa mdomo wa YAHUVEH. Kwa kuwa hao sio wasiojulikana. Bali tu katika macho ya wenye kiburi. Ninawajali MIMI kwa kuwa Ninaweza na Nitawatumia kwa uhodari kwa Sifa, Heshima na Utukufu WANGU. Kwa kuwa hawataiba haya kutoka KWANGU kama wengine walivyojaribu.

Hamkujenga hizi huduma zilizofanikiwa. Ilikuwa kwenye nguvu na upako wa RUACH ha KODESH fanaka ilikotoka. Acheni kuchukua Utukufu WANGU. Wewe sio mponyaji, mkombozi; ni Mwenyezi YAHUVEH pekee anayekomboa. Ujumbe kwa kanisa ya 1997 ni kuwa mnyenyekevu mbele ya YAHUVEH. Huu ujumbe ni wa Manabii, Wainjilisti na Wachungaji. Hamna nguvu yoyote bila upako WANGU. MIMI ni MUNGU aliye na wivu. Toa jina ya binadamu kutoka kwa huduma ZANGU. Mmepewa onyo. Pea sifa, utambuzi kwa yule pekee aliye na haki kuita huduma kwa jina lake, Bwana na Mwokozi wako, yule unayetangaza kumtumikia na kumwabudu. Mimi huwa sishiriki Utukufu WANGU na binadamu yeyote.

Kuna funzo la uongo linaloenezwa katika nyakati hizi za mwisho kwenye kanisa ZANGU ambapo upako WANGU umemwagwa. Roho ya kiburi na dini imeeneza uongo ambao wachungaji wanasema ni ‘Sisi’ pekee tulio na mamlaka ya kusema ni nani anaweza kuomba na nani hawezi kuomba. Mmekatazwa kuombeana bila ruhusa. Hata Mwenyezi YAHUVEH, Muumbaji wa Mbinguni na dunia hawezi kunena jambo kama hilo.

Neno LANGU linasema wazi, “Mwombeane.” Mimi sina upendeleo. Kwa hivyo, kwa nini ningeruhusu jambo kama hili. Wafukuze hawa wachungaji bandia nje ya nyumba YANGU. Waambie unajua Neno la YAHUVEH. Acheni kuamini na keneza uongo huu. Ndio, kuna watu watakaojaribu na kukulaani badala ya kukubariki, lakini hizo laana zitarudi kwenye kichwa cha yule anayetuma hizo laana zikiwa zimefichwa kama maombi. Roho ya ibada ya uovu anayetafuta kuwaangamiza Kondoo WANGU itarudi pale aliyeituma yupo.

RUACH ha KODESH anaweza kabisa kuwalinda wale wanaoombewa. Acheni kujaribu kufanya kile ambacho hamtakikani kufanya. Hii ni kazi ya RUACH ha KODESH. Hii ni kazi ya Mchungaji Bora na MIMI pekee ndiye Mchungaji Bora; Ninaweza kuwalinda wote walio WANGU. Toa boriti machoni mwako kabla hujahukumu kuwa mtu fulani hafai kumwombea mwingine. Hukumu huanza katika nyumba ya YAHUVEH. Nitafanya usafishaji kwa njia hodari katika 1997, kabla sijawahukumu wapagani. Dhambi ni dhambi. Ukosefu wa utakatifu bado ni kutokuwa na utakatifu. MIMI sio MUNGU anayebadilika na nyakati ZENU. MIMI niko sawa jana, leo na milele.

Kwa sababu wachungaji wanakataa kuwa na ujasiri wa kusimama na kusema tubu na neno la YAHUVEH husema hii ni dhambi. Wanaogopa kupoteza hali ya msamaha wa kodi, na huruhusu serikali kuwanyamazisha kwa sababu ya kuogopa. Sasa watakuwa na mtu wa kuogopa, MIMI YAHUSHUA. Kwa sababu mlibaki kimya, na hamkuzungumza na kusema tubu au moto wa Jehanamu utakuchoma. Kitu kimoja ambacho nyinyi wachungaji na wahubiri mliogopa kitawapata ghafla. Hamtakuwa na hali ya msamaha wa kodi. Nitairuhusu serikali kuichukua tena ndio mtazungumza bila kuogopa, kuwa dhambi ni nini. Hili litakuwa ishara ya kwamba unabii huu umetoka KWANGU kwa kuwa mtaliona jambo hili likija kutendeka. Kukuza haitoki kwingine ila pale kaskazini ambapo ni Mbinguni.

Ni MIMI ninayemkuza mmoja na kumwondoa mwingine. Wengi wataondolewa katika 1997 waliotengeneza faida wakiuza zawadi za RUACH ha KODESH. Hazikuwa zenu kuuza. Wale waliongia katika huduma hii na kufikiria kwamba hii ni njia ya kupata mali haraka, na huduma zingine zilizojulikana sasa wamekuwa na tamaa zaidi. Watatubu au kuanguka. Mtayaona haya yakija kutendeka. Wahubiri walio katika dhambi ya siri, kama miaka zilizopita watafichuliwa na kuaibishwa ili ulimwengu wote uone. Kwa kuwa roho iliyo katika kiongozi mtakatifu ni roho iliyo katika mkusanyiko. Lazima Nifanye haya yote kwa uwazi na kuwakemea wale wanaohubiri Neno la YAHUVEH, ingali hawaniogopi MIMI, wanaofikiria kuwa Nimekuwa kipofu kwa ajili ya matendo yao mazuri. Sio kwa matendo mazuri utaenda mbinguni, kabla ya binadamu yeyote ajisifu. Kwa wale wanaopewa mengi, mengi yanahitajika kutoka kwao.

Wachungaji, Wainjilisti, manabii, Wahubiri, Watoto WANGU… mtawajibika kwa yale yote mnayoyajua. Kadhaa wanajua mengi zaidi ya wengine, lakini wanawajibika zaidi kwa sababu wanajua bora kuliko kunikosea MIMI. Katika 1997 tafuteni ndani yenu wenyewe na kutojali maisha ya uovu na roho za kiburi na uasi. Kwa sababu MIMI ni MUNGU anayejua, huona na husikia yote. Wale wanaojiita Kondoo WANGU na wahubiri watawajibika kwa yale yote wanayojua ni Utakatifu ilhali wao hutenda yale yasiyo takatifu.

Wale wachungaji wanaojifanya kupenda na kuwajali kondoo, lakini hawawajali tena, wataondolewa. Kama walijiingiza kwa sababu ya tamaa, watajua umaskini. Hukumu itaanza katika nyumba ya YAHUVEH katika 1997 kwa njia hodari na kama wewe, uliye mtakatifu haujaokolewa kabisa, basi yule mpagani anafaa kuogopa tena zaidi. Jaribu Roho inayooongea na utaona ni sauti ya RUACH ha KODESH anayeongea kupitia Nabii huyu kukemea, kuwabariki na kuwajenga wale watakatifu wa YAHUVEH na kupiga mlipuko wa tarumbeta ya adhabu kwa maadui wa injili ya YAHUSHUA ha MASHIACH.

Msiwaguze wale WANGU walio na upako, pia msiwadhuru Manabii WANGU. Msimpige mawe huyu mjumbe kwa kuwapa ujumbe WANGU. Kwa sababu madhara itamjia yule atakayenena neno dhidi ya Mjumbe WANGU. Nijaribu MIMI na uone kama MIMI ni MUNGU wa moto unaochoma. Moto wa Jehanamu ni hasira YANGU iliyowaka. Usiache iwake dhidi yako.

Nakili haya na uwape wale wote walio na masikio ya kusikiliza. Wacha wote wengine wabaki viziwi. Ingawa hawaamini, haimaanishi ya kwamba sitafanya yale niliyoyazungumzia, itakuja kutendeka. Ezekiel 3:17-21 husema wape neno na wasiposikiliza, damu haitakuwa mikononi mwako. Usipowapa onyo na kupitisha unabii huu, basi watakufa katika dhambi yao lakini damu yao itakuwa mikononi mwako. MIMI hutuma manabii wangu kuwapa onyo kabla adhabu haijafika. MIMI hutuma Manabii WANGU kusema baraka inakuja kabla baraka haijafika.

 

* * * * * * *

Ilipewa siku hii ya 12/31/96 kwake Rev. Sherrie Elijah kama hajaitarajia alipokuwa anamwandikia mwingine kuwapa asante kwa maombi yao.

www.amightywind.com 
www.almightywind.com 

Contact AmightyWind