UNABII 126

GHADHABU ZA MUNGU ZIPO KARIBU KUTUMWA HAPA DUNIANI. “MSIWADHURU WATOTO, BIBI ARUSI, WACHAGULIWA NA WATEULE WANGU!”

Imeandikwa/Imezungumzwa katika Upako wa ROHO MTAKATIFU (RUACH HA KODESH)

Kupitia Mtume na Nabii Elisheva Eliyahu

Ilipokewa Aprili 12 – Ilitolewa Julai 12, 2016

Huu ndio Unabii wa kwanza uliotoka katika muda halisi – na Nabii wote Ezra kutoka Israeli na Elisheva wakiwa pamoja. MUNGU YAHUVEH Alimpa Ezra upako mkuu kumlinda na kumfunika Elisheva, na kuukoroga Upako wa Kutabiri.

Yafuatayo ina mazungumzo yao yaliyo na baraka na upako, Tarehe Aprili 12, 2006, iliyosababisha Ndimi Takatifu za moto dhidi ya maadui wa YAH, na Unabii wa 126 kutoka. Mazungumzo haya yanaonyesha kuwa Manabii ni watu wa kawaida walio na furaha tele pia!

* * * * * * *

Yafuatayo ni Unabii ulivyokuja

na Nabii wote pamoja, Ezra na Elisheva, wakizungumza katika "Ndimi Takatifu," kama ROHO wa MUNGU Alivyowajalia kutamka (Matendo ya Mitume 2:3-4) kwa lugha za wanadamu na malaika (1 Wakorintho 13:1). Elisheva anazungumza katika ndimi Unabii ukitokea (1 Wakorintho 14:6). Ezra anaanza maombi na ndimi za maombezi (Warumi 8:26-27; 1 Wakorintho 14:15).

Inayo MAJINA ya KIEBRANIA ya MUNGU:

YAH/YAHU יה ni JINA TAKATIFU la MUNGU, kama vile “Alleluia” au “Hallelu YAH” הללויה ambayo humaanisha “Msifu YAH”: YAHUVEH/YAHWEH י-ה-ו-ה MUNGU BABA; YAHUSHUA/YAHSHUA יהושוע MWANA WA PEKEE WA MUNGU—(HA MASHIACH המשיח inamaanisha “MASIHI”; ELOHIM אלוהים INAMAANISHA “MUNGU.”)

Ufunuo wa “SH’KHINYAH GLORY” שכניה תפארהkama JINA la KIBINAFSI la RUACH HA KODESH רוח הקדש, (katika Kiiengereza “ROHO MTAKATIFU”) —upo kwenye tovuti hii.

(HA SH’KHINAH {SHEKINAH} ni Kiebrania inamaanisha UWEPO WA MUNGU.)

Zaidi ya hayo, ABBA YAH אבא יה humaanisha “BABA YAH” na IMMA YAH אמא יה humaanisha “MAMA YAH.”

Maandiko yaliyotajwa yametoka KJV au NKJV, isipokuwa pale palipotajwa vinginevyo. Bonyeza kwa upande wa kulia zile nambari za maelezo ya chini (footnote) kufungua ukurasa mwingine.

* * * * * * *

Maneno ya YAHUVEH kwa Elisheva Aliyosema yaongezwe mbele ya Unabii zote:

Nilikuonya kitambo Elisabeth [Elisheva], kutoita Huduma hii kwa jina la mwanamume au mwanamke. Hata kabla kuwepo na Huduma, Niliiweka ndani ya roho yako.

Kwa kuwa hakuna lolote lililofanyika kwa mikono yako. Hakuna lolote lililotoka kwenye kinywa chako.

Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUVEH Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUSHUA, MASIHI wako Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha RUACH HA KODESH, IMMAYAH wako Aliyeizalisha.

Kama ingekuwa tu kwa mkono wako, ingekuwa imefeli kitambo.

Ni kwa UPEPO WA SHKHINYAH GLORY unaovuma kote duniani, UPEPO TAKATIFU WA UAMSHO. Sio kwa pumzi yako, au ingekuwa imefeli.

‘‘Mimi ndimi BWANA YAHUVEH: hilo ndilo JINA LANGU! Sitampa mwingine UTUKUFU WANGU, wala sanamu SIFA ZANGU.” Isaya 42:8

(Unabii 105)

Katika mwezi wa Julai 2010, MUNGU YAHUVEH pia Alisema kuongezwe yafuatayo mbele ya Unabii zote kutoka Kitabu cha pili cha Mambo ya Nyakati:

Lakini waliwadhihaki Wajumbe wa MUNGU, na kuyadharau Maneno YAKE, na kuwacheka Manabii WAKE, hata ilipozidi Ghadhabu ya BWANA juu ya Watu WAKE, hata kusiwe na kuponya.”

2 Mambo ya Nyakati 36:16

Alafu, Julai 2016:

Ole kwa yeyote atakayethubutu kujaribu kuwadhuru— hawa wawili walio na upako. Mtajuta kuzaliwa kwenu. Msiwaguse masihi WANGU, msiwadhuru Manabii WANGU (Zaburi 105:15; 1 Mambo ya Nyakati 16:22). Ingekuwa ni heri kwenu kama MIMI, BABA YAHUVEH, Ningerarua ndimi zenu!

(Unabii wa 128)

Na kutoka Nabii Ezra:

Nawaonya nyote—nyote mnaokuja dhidi ya Huduma hii NA UNABII hizi na Elisheva na Mimi, Wahudumu wa Huduma ya Amightywind—Nawaonya nyote sasa, Msiwaguse Masihi wa YAH, msiwadhuru Manabii WAKE’ (Zaburi 105:15; 1 Mambo ya Nyakati 16:22) kabla Ghadhabu za Gongo la YAH zije juu yenu. Lakini kwa wale waliobarikiwa na wao ni baraka katika Huduma hii, na ni waaminifu, na wamepokea Unabii hizi, baraka tele zitakuja juu yenu—yote kulinda yale ambayo ni ya YAH katika JINA la YAHUSHUA.

* * * * * * *

Usuli: Elisheva alikuwa anahisi mashambulizi ya kiroho, mateso na unyanyasaji hata hakujua kama ataweza kutabiri tena. Ilichukua huyu Nabii aliye na upako kutoka Israeli aliyeinuliwa na MUNGU YAHUVEH kurekebisha na kuponya mabawa yaliyovunjwa ya kipepeo huyu Elisheva na kumwachilia katika ulimwengu wa kiroho. Yote katika Jina la YAHUSHUA MASIHI.

Shuhudia vile YAHUVEH Alikuwa Ameungunisha pamoja upako hizi mbili kama moja. Shuhudia vile Upako unavyobubujika kati yao. Shuhudia upendo YAHUSHUA Amewapa kwa kila mmoja.

Tunaomba msamaha kwa ugumu wowote wa kusikia sauti yake Elisheva. Unabii unaanza katika dakika 7.

Elisheva: Video hii ni ya kwanza katika muda halisi ya Unabii niliyopokea pamoja na Mtume, Nabii Ezra kutoka Israeli, aliyekuwa pale Tarehe Aprili 12, 2016. Hatukujua kuwa katika miezi miwili wakati wa Shavuot/Pentekoste Tarehe Juni 12, 2016, upendo wetu utaendelea kuinuka na kukua zaidi na mpendwa wangu Ezra atatangazwa kama kiongozi msaidizi wa Huduma ya Amightywind siku ile tulipotangaza kwa dunia yote juu ya upendo wetu. [VIUNGO VINAKUJA ]

Yeye sasa ndiye kifuniko kiume cha Huduma hii na mimi, na mpenzi wangu wa kweli, mpenzi wa maisha yangu. Alichukua nafasi ya yule aliyekataliwa ambaye sasa yeye ni fikra ya mbali tu. Ezra anatembea katika ofisi ya Mtume na Nabii na haogopi kazi ngumu katika Ufalme wa Mbinguni au kutoka kwa Upako!

Sasa sote tumefungwa nira kwa usawa katika uongozi na upendo, mahali ambapo kulikuwa na kiongozi bandia wa kiume hapo awali. Sote Ezra na mimi tunawaweka UTATU MTAKATIFU kwanza juu ya yote. Tunawashukuru wote wanaohimiza tangazo la uongozi mpya!

Leo, miezi mitatu baada ya kupokewa Aprili 12 2016, Unabii 126 umetolewa Julai 12 2016.

Machi 7 2016, katika siku niliyodhani kuwa siku mbaya ya maisha yangu, lakini ikawa siku yangu ya kwanza kuzungumza na Ezra. MUNGU MWENYEZI husema kuwa uhusiano wetu umekua katika miezi hii 4 kama inavyochukua wengine miaka 4, na haya tu ndiyo mwanzo! Tunashangaa, YAH Atafanya nini?

Unabii huu ulirekodiwa kwa mfano wa sauti tu. Haya ndiyo maandiko.

[ Ezra anaomba katika Ndimi Takatifu... ]

Kathrynyah: Sawa...

Ezra: Hallo, Hallo.

Kathrynyah: Ninafaa kumwambia [Elisheva] umevaa nini. 1

Ezra: O...

Kathrynyah: [Anacheka] O...

Ezra: Acha basi nivae nguo zangu.

Kathrynyah: Anasema, "Acha basi nivae nguo zangu"

anachekesha sana.

[ Kicheko ]

Kathrynyah: Amevaa shati rangi ya samawati.

Elisheva: O jana nilitaka kujua anafananaje kwa rangi ya samawati!

Kathrynyah: Rangi ya samawati isemayo U.S.A.

Elisheva: Lazima ulinisikia katika kiroho, kwa sababu nilikuwa ninashangaa tu... kumbuka jana? Nilisema, "Anafananaje kwa rangi ya samawati?"

Kathrynyah: Na ndivyo ilivyo. Sasa amevaa rangi ya samawati.

Basi, ndivyo ilivyo.

Elisheva: Najua, kwa hivyo utamwambia niliyosema atakaporudi.

Kathrynyah: Yupo hapa. Amekusikia.

Elisheva: Siwezi kumsikia. Zungumza nami.

Kathrynyah: O! Nimeangusha simu yangu! [Anacheka]

Ezra: Nina... Ninajaribu nisiwakatishekila ninapowasikia.

[ Kathrynyah anacheka ]

Elisheva: Na nipo pale najaribu kumwambia, "Hapana. Mtumie Ezra ujumbe kwenye sms. Nahitaji maombi.”

Kathrynyah: Nilituma!

Elisheva: Ilikuwa ni kama, "Siwezi kumwongelesha. Sina sauti!"

Ezra: Ndio...

Elisheva: Na nilipokuwa nasoma barua pepe yako, sauti yangu ilirudi mbele yake Kathrynyah.

Kathrynyah: Alivyokuwa anasoma barua pepe yako sauti yake ilirudi.

Ezra: Niliyokuwa nakuandikianiliyotaja kwenye barua pepe

sijawahi kumwambia mtu yeyote, hadi BWANA akakufunulia kuwa roho yako imechanganywa na roho yangu, na kama ni roho sawa, ni roho sawa.

Elisheva: Wewe una thamani. Hayo tu ndiyo nitakayosema.

Una thamani kwake YAH pia una thamani kwangu. SAWA?

Ezra: Asante, Asante. Wewe pia.

Kathrynyah: [Anarudia] Wewe pia.

Elisheva: Kitu kimoja tu ni, ulipomwachilia kipepeo wako kule2mabawa yake yamekatika sasa hivieh, kwa imani naamini nitapaa... waonaje?

Ezra: Ndio, nili... Kwa kweli nili… Kwa kweli nilikuona akilini... Nilikuweka... Nilimweka yule kipepeo mikononi mwangu,

Kwa kweli nina...utaona kwenye video [niliyokutengenezea].

Nilimweka yule kipepeo mikononi mwangu na nilikuwa natengeneza [narekebisha]nikiweka mabawa yale [yaliyovunjwa] pamoja na nilikuwa natoa [anafanya sauti ya kuvuma]upepo mdogo, ili uweze kuutumia na kupaana nilikuwa nakuachilia.

Kathrynyah: Hayo ni mazuri.

Elisheva: Yenye thamani. Je, uliombea picha yangu pia?

Kathrynyah: Je, uliombea picha yake pia?

Ezra: Ndio, mimi huona picha yako kila wakati.

Elisheva: Ulichagua picha gani?

Kathrynyah: Gani?

Ezra: Ya mwisho aliyonitumia, hivi karibuni.

Elisheva: Sasa nina mwanamume anayezungumza maisha juu yangu na kuniachilia huru kupaa. [Anacheka kwa furaha]

Ezra: Hayo ni sawa.

[ Elisheva anacheka kwa furaha ]

Ezra: Je, si BWANA Alisema katika Unabii kwetu sisi, "Ezra, mfunze kupaa"?3

Elisheva: Ndio, ndio.

Kathrynyah: Asante kwa maombi yako ndugu mpendwa, Asante kwa kuwa hapo, vivyo hivyo.

Ezra: Acha niwaambie, nilikuwa niondoke leo na kila kitu kikacheleweshwa na sikuweza kuondoka.

Kathrynyah: O wow, MUNGU Alimchelewesha. Hakuweza kuondoka kwa hivyo alikuwa na wakati wa kuomba.

Elisheva: Kwa hayo, ninakupa sifa BABA YAHUVEH kwa sababu nilikuhitaji Ezra, nilikuhitaji [kuomba]!

Elisheva: Ndio BABA wa MBINGUNI, nani, ni nani huyu aliyetuma laana hiyo BABA? [Kwake Ezra] Waweza, waweza tu kuomba katika ROHO tafadhali?

Ezra: Ndio.

[ Kathrynyah anamfunga shetani katika JINA la YAHUSHUA na Ezra anaomba katika ndimi Takatifu… ]

Elisheva: Tunakungoja WEWE BABA YAH kuzungumza Neno sasa katika Kiingereza kupitia mpendwa, mpendwa WAKO Ezra. Wewe Ezra una thamani. Ni nini wataka kusema BABA YAHUVEH? Ni nini wataka kusema YAHUSHUA? Ni nini wataka kusema IMMAYAH?

BABA YAHUVEH kama Ulivyozungumza Neno, [zungumza tena] kupitia huu mdomo wangu wa udongona ulioweka upakona yalikuwa Maneno YAKO BABA YAHUVEH, MUUMBA wa vyote.

BABA ni nini wataka tujue? Ni nini BABA YAH?

[ Elisheva anaomba katika ndimi Takatifu... zinazozidi kuwa moto,

zimejawa na Ghadhabu zake YAH, mpaka YAH Anapozungumza ]

Elisheva: Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu... O! Amejawa na ghadhabu!

Unabii 126 Unaanza:

Aprili 12, 2016

Msiwaguse Manabii WANGU! Msiwaguse Masihi WANGU, wala msiwadhuru Manabii WANGU (1 Mambo ya Nyakati 16:22; Zaburi 105:15)! Yeye [Paul Hellem] ameziwasha Ghadhabu ZANGU!

MSIWADHURU BIBI-ARUSI WANGU! MIMI SIDHURU BIBI-ARUSI WANGU!4

OLE kwa yeyote atakayegusa hata nywele kwenye kichwa cha BIBI-ARUSI WANGU! Je, kwani hamjui? Ni Hasira ZANGU,

Ghadhabu ZANGU zinazowasha jehanamu! Siku hii moto umekuwa moto zaidi! Msiwadhuru Watoto, Bibi Arusi, Wachaguliwa na Wateule WANGU!

OLE kwa dunia hii! Kuyaita maovu yale ambayo Ninaita Takatifu! OLE KWA DUNIA HII! Ole! Ole! Ole! Muda sio mrefu sasa.5 Dunia hii itahisi Ghadhabu ZANGU! Na haitakuwa tu kukanyaga kwa BABA YAHUVEH lakini itakuwa ya MIMI YAHUSHUA na IMMAYAH!

Acheni kunijaribu! Acheni kujaribu Uvumilivu WANGUni mpaka wapi mtainama juu ya jehanamu na msianguke ndaniACHENI KUNIJARIBU MIMI!

Sizumgumzi onyo hili kwa Watoto, Bibi Arusi, Wachaguliwa, na Wateule WANGU Ninaowathaminiwale waliooshwa katika DAMU ILIYOMWAGWA, wale waliopokea ZAWADI YANGU pale Kalvari.

Nyinyi! Nyinyi! Nyinyi! Ninawakumbatia! Hamna chochote cha kuogopa.

Ninazungumza kwa maadui—waliolaumiwa (Timotheo 3:8; Tito 1:16),6 watoto wa shetani. Ninazungumza kwa wale vuguvugu wanaojiita "Mkristo," lakini hata HUCHAFUA Jina la KRISTO!

2 Timotheo 3:8 Vivyo hivyo watu hawa hupingana na ile kweli. Hawa ni watu wenye akili zilizopotoka, ambao wamekataliwa kwa mambo ya imani.

Tito 1:16 Wanadai kumjua MUNGU, lakini kwa matendo yao wanamkana. Hao watu ni chukizo, wasiotii, wasiofaa kwa jambo lolote jema.

Ufunuo wa Yohana 3:16 Hivyo kwa kuwa u uvuguvugu, kwamba wewe si baridi wala si moto, Nitakutapika utoke Kinywani MWANGU.

Mnachukua Amri ZANGU Kumi na mnazifinya kama mpira mkononi na kisha mnasema, "Hizi ni takataka tu. Yote yalikwisha pale msalabani wa Kalvari. Waona, nafsi yangu haitapotea. Alilipa gharama! Sasa, naweza kutenda dhambi nitakavyo. Hakuna sheria zozote. YAHUSHUA tunayemwita 'Yesu Kristo' ni wa upendo tu! Yeye ni wa upendo tu! YEYE hatatutupa ndani ya jehanamu!"

O! O o o, enyi wapumbavu, watu wapumbavu!

Kuna gharama ya kulipakwa wote wanaokanyagia DAMU ya YAHUSHUA chini ya miguu yao. Kuna gharama ya kulipakwa laana, kwa chuki, kwa uongo na kashfa ambayo mmemtumia Nabii huyu na kwa Amightywind. Kuna gharama ya kulipa!

Ni heri mtubu!

Kwa wengine wenu haitawezekana. Mtasikia ujumbe huu na mtamrudishia chuki zaidi!

LAKINI NINA NABII! Na atazumgumza kwa ujasiri! Kwa hivyo, hamwezi kusema kuwa hamkuonywa! Manabii WANGU wa kweli watazungumza. Hamtawanyamazisha.

Na Ezra, Nimekuita. Wewe pia utayachukua Maneno YANGU. Na hapo awali ulipowaacha kwa unyenyekevu na machozi machoni mwako, NITAWEKA MOTO PALE!ambapo haikuwa hapo awali.

Kwa kuwa Niliunganisha Upako hizi mbili pamoja. Na hakuna yeyote atakayezitenganisha. Na haijalishi kama yeyote anaelewa.

Ninajua ni nini Niliyoweka ndani ya mwanamke na mwanamume huyu.

Nyinyi tu zungumzeni Maneno YANGU! Hilo tu ndilo jukumu lenu. Sio jukumu lenu watafanya nini nayo! Nyinyi tu zungumzeni Maneno YANGUyaliyomo kwenye Unabii, yaliyofungwa katika Kitabu [Siri za ROHO MTAKATIFU (RUACH HA KODESH)].

Wale na macho ya kweli ya kuona watazifungua Kweli hizi katika Kitabu hichokupitia IMMAYAH. Atawapa hekima. Atawapa Ufunuo kwa wote wanaotafuta na wanao hamu ya kusikia kutoka KWANGU.

MIMI NIKO AMBAYE NIKO!

Na siombi msamaha kwa mwanamke au mwanamume yeyote!

Itafanywa kwa njia YANGU!

Na ninaonya dunia hii!

Kwa uasi wenu, mtalipa.

Wale wanaopokea Maneno ya Kweli ya Huduma hiiwametengwa kando7—na watalindwa na kubarikiwa. Kwa kuwa mwaona, sio maneno ya mwanamke au mwanamume. Lakini yametoka Mbinguni!

Mjihadhari kwa kila laana, kila fingo, kila ibada, kila pepo mliojaribu kutumamjihadhari nyinyi mnaofanya uchawiitarudi KWENU mara milioni! Nimesema, itarudi KWENU mara milioni. Lakini haitakuwa hapa duniani pekee, pia itakuwa vivyo hivyo kule jehanamu—jehanamu ikiunganishwa na Ziwa la Moto!

Ni heri ufunge mdomo wakoni heri ukimbie mbali kama haupendi Maneno Ninayosema!

O, O, O! O, O! Kwa Watoto, Bibi Arusi, Wachaguliwa na Wateule WANGU! O, O, O! Kwa Bibi Arusi WANGU, wathaminiwa WANGU, wathaminiwa, Bibi Arusi mrembomuda sio mrefu kabla MIMI, YAHUSHUA, sijaja kuwachukua muwe Karibu NAMI. Shikilieni kwenye Upindo wa Vazi LANGU!

SHIKILIENI NA HATA MSITHUBUTU KUACHILIA!

Wakati mwingine mtafikiria kuwa lazima mpigane NAMI kwa baraka zenu lakini haya husaidia imani yenu kukua! Sitawapungukia, Sitawaacha! Lieni tu katika JINA LANGU! Kwa kuwa Ninawapenda na upendo ambao hamwezi kuanza kufahamu! Na tuzo zenu zinawangoja papa hapa Mbinguni!

Kathrynyah: Sifa kwake YAHUSHUA!

Unabii Unaendelea:

O NINAWAPENDA! NINAWAPENDA! NINAWAPENDA! NINAWAPENDA! Nyinyi ndio sababu Nilienda Kalvariili mrudi KWANGU! Wale woteNizungumzao nao sasakatika Kitabu cha Uzima cha Mwana-kondoo, nyinyi ndio sababu Nilienda Kalvari!

Hakuna chochote kizuri ambacho Nitawazuia kupata—mnaposhikilia na kutorudi nyumaNina hamu ya kuwabariki!

Na nyinyi mnaofanya kazi katika shamba la mavuno, nyinyi mnaofanya kazi hapa AmightywindSHIKILIENI! Hata msithubutu kuachilia! Kwa kuwa mnafanya kazi ya upendo kwa BABA YAHUVEH, MIMI, YAHUSHUA na IMMAYAH.

Na Nimefurahishwa sana sana sana na waombezi, "Wakanyaga Pepo wa YAHUSHUA." Na kuna wengi zaidi ya wale ambao majina yao yanajulikana. Kwa kuwa wapo kote dunianimashujaa 500,000 kwenye ukuta huo kama Nilivyotabiri zamani! Na wao ndio mashujaa wenye nguvu! Katika kila jamaa na lugha!

Kwa kuwa neno la mdomo limechukua Huduma hii kote duniani. Na itazidi kuwa vivyo hivyo, siku zinazofuata mnapowafikia8 watu ambao hamkuweza kuwafikia hapo awali!

Kwa kuwa BIBI ARUSI WA ISRAELI wanalia! Kuna BIBI ARUSI KULE LEBANON! Kuna Bibi Arusi! Kuna Bibi Arusi! Kuna Bibi Arusiwanaonililia MIMI, wanaotembea katika Utakatifu mbele YANGU katika sehemu nyingi kote dunianina wengine hata hamjawafikia, wanaowangoja.

Haya ndiyo Maneno Ninayo ya kusema kama, Ezra, alivyosababisha Unabii huu mpya kutoka siku hii. Hii ndiyo sababu shetani alijaribu kumwua Nabii huyu leo hiihakutaka Unabii huu utoke kwa mdomo wa binti YANGU Ringmaiden WANGU.

Kwa hivyo Ezra, endelea kuyafanya yale ambayo uliitwa kufanya.

Kwa kuwa sasa hamna mmoja tu, lakina kuna wawili.

Na kuna wengi walio njiani!

Kuna wale wafasiri Waebrania! Endeeleni kutazama mkiwatafuta. Kwa kuwa Kitabu hiki kinafaa kuwa katika lugha ya Kiebrania, kama Nilivyotabiri itakavyokuwa katika lugha ya Kiasia!

Endeleeni kuwatazama wale wote wanaopokea Kitabu hiki kama Ukweli kule Israeli, wale wote wanaoweza kuzungumza katika lugha ya Kiebrania na wanajua [lugha ya] Kiiengereza vizuri. Watasimama nanyi. Itawapendeza sana kuwasaidia. Nawaita wote waje leo hii.

Ninajua majina yenu tayari. Ninayazungumza katika ulimwengu wa kiroho na Ninawaita.

Hongera, hongera, hongera binti YANGU mwaminifu. Hongera, hongera mwanangu mwaminifu!

Endeleeni tu katika njia iyo hiyo. Endeleeni kwenye mwendo uo huo. Kwa kuwa tukio mpya limeanza. Endeleeni kunililia MIMI. Endeleeni kuulizia Hekima! Na Nitawaongoza kwa uaminifu, upako na Nitawapa Hekima zaidi kwa wingi.

Lakini, ole, ole, ole, ole, OLE kwa maadui wenu! Ninazumgumza nanyi maadui. Ole, ole, ole, ole kwa kila mtu anayesimama dhidi ya Watoto, Bibi Arusi, Wachaguliwa na Wateule WANGU!

Na kwa kila mtu mwingine anayesikia haya na kusema, "O! Sitaki kuwa adui wa YAH,"

basi tubuni haraka!

Kwa sababu GHADHABU YANGU kwa dunia hii ipo karibu kutumwa!

Pigeni magoti na mlilieni YAHUSHUA kabla wakati haujaisha! Tubuni! Tubuni! Tubuni! Kubalini ZAWADI YAKE pale Kalvari ili DAMU YA YAHUSHUA ILIYOMWAGWA Aweze kuwa MASIHI wenuna Atawalinda na kuwasamehe na kuwakomboa nyote.

Haya ndiyo Maneno Ninayo ya kusema shetani anapokasirika kwa ghadhabu akijaribu kumnyamazisha Nabii huyu tena. Lakini, Ninamwezesha kuzungumza kwa sauti ya juu zaidi! Hamwezi kuwanyamazisha Manabii WANGU!

O maadui WANGU, kumbukeni haya.

Nabii ni rafiki YANGU! Chochote mtakachowatendea, ni kama mmenitendea MIMI.

Na MIMI NI YAHUVEH!

Siku hii hamjasikia tu kutoka KWANGU, BABA YAHUVEH, lakini pia mmesikia kutoka kwa MWANANGU, YAHUSHUA! Je, sasa mtafanya nini na Maneno Niliyozungumza kwenu? Yote yamezungumzwa kwa sababu ya IMMAYAH. Je, mtafanya nini?

Kwa kuwa sasa mtawajibika kwa Maneno yaliyozungumzwa.

Mwisho wa Neno.

Elisheva: [Anapumua] Ni hayo tu.

Kathrynyah: Sifa kwake YAHUVEH! Sifa kwake YAHUSHUA! Sifa kwake IMMAYAH!

Ezra: Asante! Amina.

[ Elisheva anacheka ]

Kathrynyah: Asante BABA!

Elisheva: Naomba umeyapata hayo Ezra, umeyapata?

Ezra: Umesema nini?

Kathrynyah: Umeyasikia hayo?

Ezra: Ndio. [Anacheka]

Kathrynyah: Ndio.

Ezra: [Anacheka] Sifa kwake MUNGU.

Elisheva: [Anacheka] BABA ninakushukuru na ninakusifu kitu kizuri kimetendeka leo. Wow, huu ni Unabii mpya. Aprili 12, 2016. Huu ni Unabii mpya.

Kathrynyah: Sifa kwake YAHUVEH! Sifa kwake YAHUSHUA! Sifa kwake IMMAYAH!

Elisheva: Na yote ni kwa sababu mwanamume alikujaambaye sasa yuko Israeli.

Kathrynyah: [Anarudia] Yote ni kwa sababu mwanamume alikujaambaye yuko Israeli sasa.

Ezra: Wow, maajabu, maajabu!

Elisheva: Waona, mimi husikiasiwezi kueleza karama hii inavyofanya kazi. Siwezi kuieleza. Ni kwamba... wakati mwingine YEYE ata... Kuna mengi sana ambayo yote huja kwangu mara moja. Hamna namna ya kuieleza.

Lakini Ezra aliukoroga Upakona tulingoja na tukangoja na tukangoja Neno lije. Alizungumza katika ndimi Takatifu, tukaenda mbele ya Kiti cha enzi na nikasema, "Ni nini unachotaka kusema YAHUVEH?" Na tukangoja na tukangoja na Ezra akaomba katika ndimi tena.

Na alafu tukangoja... na nikasema [akilini], "O! Hakutakuwa na Neno lolote utakalosema? Na WEWE NDIWE Uliyeniambia niombe, Ukaniambia nimwambie Ezra aombe [katika ndimi] na bila shaka, tunajua yaliyotendeka

Sikujua lolote, kama kawaida. Alafu alipozungumza, Alikuwa amekasirika.

Ezra: Ndio.

Elisheva: …na yule [Paul Hellem] aliyeniumiza leo vibaya. Na...

Ezra: Wow.

Elisheva: Ningependa kuyasema haya. Ndio... Ole kwa maadui zetu.

Kathrynyah: Amina.

Elisheva: Ni hayo tu.

Ezra: Amina.

Elisheva: Ole kwa wale...

Ezra: Wow.

Elisheva: Mtajibu kwa kila neno mliosema. Mtajibu mbele yake MUNGU WA VIUMBE. Hamnijui mimi. Hamjui chochote kunihusu mimi. Na bado mmeyasema... Mmeiweka sura yangu... na mkaiweka kwenye video ya mapenzi machafu... mnathubutu kufanya mambo kama haya? Kumchukua muigizaji wa mambo ya mapenzi machafu na kusema ni mimi? Hamwezi hata kufahamu

Unabii Unaendelea:9

Hamwezi hata kufahamuBABA YAH Anasema sasaMATESO! ... yanayowangoja. Nyinyi mnaothubutu kusema, na kutengeneza video hizi, kuwa mimi ni "mtume wa kanisa la shetani"... hamwezi hata kuanza kufahamuBABA YAH Ananiambiamateso ambayo yanawangoja kwa sababu, kila neno mlilozungumza, lilienda mbele ya Kiti cha Enzi cha Mbinguni.

Elisheva: Na BABA YAH, YAHUSHUA na IMMAYAH...

Ezra: Wow.

Elisheva: WAO wanajua, kwa miaka 30 mimi nimekuwa WAO. WAO wanajua.

Ezra: Amina.

Elisheva: Na ole kwenu. Ole, ole, ole! Jamani!10

Nina matumaini, ombi langu nina ninayasema haya mbele ya dunia nzimaninataka kujua wakati mateso haya yanapoanza. Ninataka kujua.

Sitaki kuyatazama kwa muda mrefu, lakini ilikuwa tu kama Lazaro na yule tajiri. Alimwona yule tajiri akiomba maji, tone tu kwenye ulimi. Ninataka kujua BABA YAH Atawatendea nini.

Kwa sababu nyinyi... Mnafikiria mlipata ushindi. Mnafikiria mliniaibisha.

Lakini mwajua nini? Hakuna chochote mnachoweza kufanya ambacho BABA YAH wangu hajawaruhusu kufanya. Na hayo yalikuwa kwa hukumu yenu wenyewe. Mlijichimbia kiwango chenu hadi chini, shimoni mwa jehanamu [hadi pale] mtakaposhuka.

Kathrynyah: Amina.

Elisheva: Kwa hivyo nyinyi watu mnaotaka kuendelea kutengeneza video hizi, kuendelea kukashifu jina langu, kuendelea kuongea maovu haya dhidi ya Huduma hii... Nyinyi ni wapumbavu.

Kathrynyah: Amina. [Anacheka]

Elisheva: Mngekimbia tu.

Ezra: Ndio.

Elisheva: Na kwa nyote mnaosikia haya, na mtakasirika, ni heri mnyamaze.

Kathrynyah: Amina!

Elisheva: Ni heri mkimbie.

Ezra: Amina.

Elisheva: Kwa sababu BABA YAH wangu hataki michezo. Anajua nani ni WAKE, na jina la nani limeandikwa katika Kitabu cha Uzima cha MWANA-KONDOO, hadi Mbinguni.

Kathrynyah: Amina.

Elisheva: Na haya ndiyo maneno ninayo ya kusema...

Ezra: Amina.

Elisheva: Aprili 12, 2016.

Kathrynyah: Amina.

Elisheva: YAHUSHUA yupo njiani.

Ezra: Wow.

Elisheva: Yupo njiani.

Ezra: Wow.

Elisheva: [Anaomba katika ndimi Takatifu] Hallelu YAH—BABA YAH! Asante kwa kunipa nguvu siku hii. [Anacheka] O, ndio... Asante kwa kunipa nguvu siku hii. Asante, asante kwa mwanamume huyu wa YAH uliyemleta kwetu kutusaidia kwa njia ambayo mtu mwingine hajawahi kutusaidia hapo awali, kama hamu yangu ilivyo kuwafikia Israeli.

Ezra: Amina.

Elisheva: Na watu Waebrania, Wayahudi walio kote duniani, lakini hatutayaacha hapo... Hatutayaacha hapo.

Ezra: Ndio, wow...

Elisheva: Hii ni Huduma ya Kimataifa na tunawapenda watu wote, jamaa na lugha...

Ezra: Sifa kwake MUNGU.

Elisheva: ambao majina yao yameandikwa katika Kitabu cha Uzima cha MWANA-KONDOO, na YAHUSHUA hatampoteza hata mmoja.

Ezra: Amina.

Elisheva: [Anacheka kwa furaha] Huu ni Unabii wetu wa kwanza pamoja.

Kathrynyah: Anasema, "Huu ni Unabii wetu wa kwanza pamoja."

Ezra: O... [Anacheka]

Elisheva: Ni baada ya kumwachilia yule kipepeo huru.

Kathrynyah: [Anarudia] Ni baada ya kumwachilia yule kipepeo huru!

Ezra anacheka: Yu huru kweli!

[ Elisheva anacheka ]

Kathrynyah: [Anarudia] Yu huru kweli!

Elisheva: Ilikuwa Unabii wangu wa kwanza tangu nilipofikiria sitawahi kutabiri tena.

Kathrynyah: Wewe husema hivyo kila wakati, pole lakini [Anacheka] wewe huwa wasema hivyo.

Elisheva: [Anacheka] Wasema ukweli. Mimi hufanya hivyo... lakini, sio kila wakati. Lakini ilikuwa baada ya wewe kuyarekebisha mabawa yangu na kuniachilia huru [kuwa nitabiri tena]. Asante BABA YAH, asante kwa kunionyesha.

Maono

Kathrynyah: ...alafu ukaanza kuomba na nikaona [katika maono] kuwa nyinyi wawili mna vijiti vya baseball na mlikuwa mmeviweka pamoja, ni kama mnajitayarisha kuvitumia. Wajua unavyoweka panga pamoja, alafu waanza kupigana, hivyo.

Elisheva: lakini kijiti cha baseball?! [Anacheka]

Kathrynyah: Nafikiria, uwagonge [maadui] kwenye vichwa.

Elisheva: [Anacheka] SAWA!

Kathrynyah: Na MUNGU Alipozungumza moto ndani ya Ezra niliona moto kwenye mkono wake, kama uliinua mkono wako na kulikuwa na moto mwisho wake, wajua kama, mwali wa moto. Hayo ndiyo niliyoyaona.

Elisheva: Wow, sifa kwake YAH. Waona utakachopata, unavyovaa rangi ya samawati!?

Kathrynyah: [Anarudia] Waona utakachopata unavyovaa rangi ya samawati?

Ezra: Ndio. [Anacheka]

[ Elisheva anacheka ]

Kathrynyah: Mambo haya yahusu rangi. Ninacheza tu kidogo BABA YAHUVEH. WEWE wajua hivyo.

Elisheva: Haiya.

Ezra: Ndio. [Anacheka]

Elisheva: Huu ndio mwanzo tu wa mimi na wewe tunapokuja pamoja katika Upako.

Ezra: Ndio, kwa kweli.

Kathrynyah: Poa!

Elisheva: Wakati shetani anapofikiria atanivunja, [anasikia kutoka Mbinguni] BABA YAH Alisema, “Kitu cha pekee nilichofanya leo ni kukunjwa.!” BABA YAH Alisema, “Kitu cha pekee nilichofanya leo ni kukunjwa.!” Hayo tu. Sababu la kukunjwa kwangu leo na sio kuvunjika, ni kwa sababukulikuwa na mwanamume [Ezra] aliye na Gongo na yeye ndiye nusu nyingine yangu ya Upako.

Kathrynyah: Amina!

Ezra: [Kwa nguvu] Amina!

Elisheva: Na haya ndiyo ninayo ya kusema. Na jehanamu nzima inatetemeka sasa hivi.

Kathrynyah: Vizuri!

Ezra: Hayo ni kweli.

Elisheva: shetani alishindwa.

Kathrynyah: Katika JINA la YAHUSHUA MASIHI, vizuri!

Ezra: Mwambie nampa tano [high five]. "Nipe tano."11

Kathrynyah: Anakupa tano, mpe tano. [Anacheka]

Elisheva: Je, mbona sio busu kwenye shavu?

Kathrynyah: [Anarudia] Je, mbona sio busu kwenye shavu? [Anacheka]

Ezra: Haiya.

Kathrynyah: Haiya, anaweka shavu lake kwenye skrini.

Elisheva: [Anacheka] Sitaki kuufurukuta mkono wako!

Kathrynyah: Hapana, anataka kupa tano!

Ezra: Umekuwa ukiifurukuta, nakuambia. [Kwa mchezo]

Kathrynyah: Hapana, anataka kupa tano!

Elisheva: Tano ni nini? O! Nipe tano! [Anacheka]

Kathrynyah: Sawa. Ameelewa sasa!

Elisheva: Nimeweka mkono wangu juu. Mikono yetu yenye upako imeunganishwa.

Kathrynyah: Ameweka mkono wake juu kwa ‘tano’. AnasemaSawa, ameelewa sasa. Sasa ameelewa...

Elisheva: Sasa mikono yetu yenye upako imeunganishwa.

Kathrynyah: Amina!

Ezra: Kumbuka tu, na ghasia/majaribio haya uliyoyapitia, kitu kizuri kilikuwa chaja. Siku ya ushindi.

Elisheva: Amina.

Kathrynyah: Alikuwa anapenda kusema, "Niko tano na niko hai!"

Elisheva: Sasa tuna wengi kushinda hao! Tuna Ezra! Wajua! Na yeye yupo pale juu [kiroho]! [Anacheka]

Kathrynyah: Shujaa.

Ezra: Sasa naelewa kwa nini siku yangu nzima ilicheleweshwa na sikuweza kufika kule na... ilikuwa kwa sababu hiyo, kabisa.

Elisheva: Asante kwa kuwa hapa kwa niaba yangu.

Ezra: O, karibu.

Elisheva: Na BABA asante kwa kumweka hapa kwa niaba yangu. Kwa sababu ungeondokahaungekuwa hapa leo kwa niaba yangu. Na Neno hili halingetoka.

Ezra: Kama nilivyosema, kila kitu tufanyacho kilikadiriwa "hapo awali."12

Elisheva: Amina. Amina, amina, amina. Kwa hivyo sasa... umeshuhudia Unabii wa kwanza nawe. [Anacheka]

Kathrynyah: Alisema [hapo mbeleni] kuwa tumengoja muda mrefu kwa Unabii mwingine na anazo Unabii ambazo hazijatolewa bado

Elisheva: —kwa sababu yake [Paul Hellem].

Ezra: BasiNdiyo hayo. Haiya.

Kathrynyah: Kwa sababu ya 'butt-head'.

Elisheva: Ndio.

Ezra: Hakika.

Elisheva: Kwa sababu...

Kathrynyah: Siwezi kufikiria jina mbaya ambayo linamfaa [Paul Hellem].

Elisheva: [Anacheka] Hata mimi siwezi.

Ezra: Nilifikiria 'cheese-head' ni nzuri.

[Rekodi imekatika, lakini wanawake wote wawili wasema kuwa maneno haya sio mabaya ya kutosha kwa yule mlaumiwa Paul Hellem!]

Elisheva: Nahitaji kuona sura yako. Nahitaji kumwona mwanamume wangu kule kwenye rangi ya samawati, Rangi hiyo yenye upako! Ilikoroga Upako!

Ezra: O, SAWA.

Kathrynyah: Ilikoroga Upako.

Elisheva: Ilikoroga Upako....

Ezra: Je, mlijua, mlijua, nitamalizia na haya, ukilichukua jina "Yerusalemu"ukilichukua jina "Yerusalemu," U.S.A. [Marekani] ipo katikati ya "Yerusalemu".

Kathrynyah: Ndio.

Elisheva: Ndio, najua.

Ezra: U.S.A. ilibarikiwa tu kwa sababu ya Yerusalemu. Kwa sababu ya Israeli.

Kathrynyah: Ndio...

Elisheva: Ninaamini hayo...

Ezra: Na sasa wanawaacha Israeli.

Elisheva: Wao ni maadui na bado hawataki kukubali kuwa wao ni maadui. "Jihadharini na Farasi la Troy" (Unabii 57). Unazo Unabii kwa Israeli [Alizozizungumza YAH]. Sikuweza kuwafikia na Unabii hizo, unawezakuwaonya.

Ezra: Ndio.

Elisheva: Na utakapofika Marekani waonye huko pia.

Ezra: Ndio, kwa kweli.

Elisheva: Kuna Unabii nyingi za Marekani. Sawa?

Ezra: Ndio, ndio!

Elisheva: Basi, nitakuachilia sasa. Na...

Elisheva: Yale ninayoweza kufanya ni kusema asante. Sina mengine ya kusema.

Ezra: SAWA.

Kathrynyah: YAHUVEH akubariki!

Elisheva: YAHUSHUA akubariki.

Ezra: Kwaheri!

Kathrynyah: Kwaheri!

Ezra: Asante.

Mwisho wa Rekodi.

Imezungumzwa, imeandikwa katika JINA LA YAHUSHUA, Aprili 12, 2016

Mtume, Nabii Elisheva Eliyahu

1

Elisheva aliunga simu hii ya video kupitia simu ya Kathrynyah—na hakuweza kuiona video, na alikuwa anataka kujua Ezra amevaa nini siku hiyo. Hii ndiyo sababu Kathrynyah alikuwa anarudia maneno ya wote wawili—kwa sababu hawakuweza kusikizana wakati wote.

2

Elisheva ndiye kipepeo: “Ninamleta mwanamke ambaye ni laini, nyeti, dhaifu, wa kihisia kama kipepeo aliye na mabawa iliyovunjwa, raruliwa, kuungana na mwanamume aliye na UPAKO WA ROHO MTAKATIFU WANGU wa kuzungumza Uponyaji, Upendo, Huruma, Amani & Kicheko, na katika Upako WANGU, ataitengeneza mabawa yake iliyoraruka—ili aweze kupaa, juu, kwenye anga—na nyimbo za upako Nitakazompa kuimba.” (Mfupa wa Mfupa, Mwili wa Mwili Nakupa” Unabii – Shairi).

3

Angalia footnote ya awali; pia inaeleza Maneno ya kibinafsi ya Unabii

4

Aliyekataliwa Paul Hellem alikuwa amemshambulia Elisheva kwa miaka mingi— hadi YAH Akachoka! “Bibi Arusi wa YAHUSHUA” ni kikundi cha walioitwa na waaminifu waliosafishwa kutii amri ya kumweka YAH kwanza katika upendo na maisha yao, juu ya yote (Isaya 54:5).

5

Maneno mengine inayomaanisha “nitafanya” na pia yanaweza kuongeza uchangamfu au uharaka

6

[Reprobate] Aliyekataliwa inawezwa kuelezwa kama mtu ambaye amekataliwa na MUNGU bila matumaini ya wokovu (Yeremia 6:26-30; Waebrania 6:4-8), waliomkufuru ROHO MTAKATIFU (Mathayo 12:31; Waebrania 10:26-31), ambayo ni dhambi isiyoweza kusamehewa (Luka 12:10) na lazima watalaaniwa (Warumi 9:22). “Reprobrate” inaweza kutumika kama kivumishi kuelezea uhusiano wa namna hii.

7

Maana mbili – Kweli katika Huduma hii na watu wanaoikubali wametengwa, spesheli, Watakatifu kwake YAH.

8

Mnawafikia” katika tenzi ya wakati uliopo—YAHUVEH Anazungumza katika kuwepo, akiwafika wale ambao hawajafikiwa.

9

Elisheva, anazungumza kama Nabii, na anao upako hadi maneno ya YAH yanachanganyika na yake. Hamna hata neno moja “linaloanguka chini” (1 Samueli 3:19)

10

Man!” Tamshi la Kimarekani la uchangamfu au kukasirishwa.

11

Kuugonga mkono wako kwa mkono wa mwingine— ishara ya furaha, sherehe au salamu

12

Angalia Unabii 71, Kilichofumbwa Sasa Kimefunuliwa! — “Ni nafsi tu kabla ya kuumbwa kwa dunia hii, walio waaminifu kwa MIMI, YAHUVEH & YAHUSHUA wakati ule ule, ndio watakaotukubali, kutupenda, na kutii [MIMI] na kupinga maovu na kupigana naye shetani na chukizo zote sasa.”

* * * * * * *