Unabii wa 119

 

2011 Mwito wa Kutubu au Kufa, YAH Ana Nambari Yako!!!

 

Imeandikwa/Imezungumzwa katika upako wa RUACH ha KODESH

kupitia Mtume Elisabeth Sherrie Elijah Nikomia

Disemba 24, 2010

Ilitolewa Januari 1, 2011

 

 

(Kutoka Unabii wa 105, YAHUVEH alisema ujumbe huu uwekwe katika kila unabii kutoka sasa: Nilikuonya kitambo Elisabeth kutoita huduma hii kwa jina la mwanaume au mwanamke hata kabla kuwepo na huduma. Niliiweka ndani ya roho yako kwa kuwa hakuna lolote kwa haya lililofanyika kwa mkono wako au lililotoka kwenye kinywa chako. Ilitoka kwenye kinywa cha YAHUVEH aliyeizalisha. Ilitoka kwenye kinywa cha YAHUSHUA, MASHIACH wako aliyeizalisha. Ilitoka kwenye kinywa cha RUACH ha KODESH, IMMAYAH wako aliyeizalisha. Kama ingekuwa tu kwa mkono wako, ingekuwa imefeli kitambo. Ni kwa upepo wa SHKHINYAH GLORY inayovuma kote duniani, upepo Takatifu wa uamsho, sio kwa pumzi yako, au ingekuwa imefeli. (Isaya 42:8))

 

*******

 

Elisabeth aongea kwenye kinaza sauti:

 

Niliamka na nikasikia simu inalia, ikilia ring, ring, na nikasikia simu. Mara ya kwanza ilivyofanyika hivi ni jana na ilikuwa siku inayoitwa solstice ya baridi siku ya 22. Kwa hivyo nilisikia simu hiyo ikilia siku ya 22 Disemba. Na Niko alisema ya kwamba hakukuwa na simu yoyote iliyokuwa inalia.

 

 

 

 

Hata hivyo hapa ndipo nilipokuwa leo (23 Dis.) nilipoamshwa mara ya pili kwa sauti ya ring, ring, ring na wakati huu, salaaala, simu haikuacha kulia. Nilimwambia Niko simu yako inalia nilimwamsha na akasema kuwa simu yake hailii. Nikasema bado naisikia ikilia hata hivi nikikuongelesha wewe na ikalia, salaaala, mara nyingi hata nikiwa ninaongea ilikuwa bado inalia kutokatika.

 

 

Ilikuwa kweli sana na Niko alisema kuwa simu yangu iko humu ndani chumbani mwa kulala na sikuweza kuelewa haya alafu, salaaala, nikahisi kuwa ilikuwa kwenye ulimwengu wa kiroho, Mungu alikuwa anajaribu kuwasiliana nami. Kwa hivyo nilirudi kulala na nilipoamka nilikuwa nikimwambia Niko ya kuwa – mimi huwa naamka saa nne kamili asubuhi – na ninamwambia Niko kuhusu hio simu na kuomba kwa sauti ya juu, ninasema unajua haya yatakuwa mambo yasiyo ya kawaida duniani. Ninasikia kilio cha simu, ni nini, unalojaribu kuniambia mimi Baba wa Mbinguni? Alafu nikayasikia haya.

 

 

Ni kilio ambacho hamna yeyote anayetaka kujibu, na hili ndilo lililofanyika na kwa hivyo nikaanza kutubu na nikaanza…... ngoja nilisema, kilio ambacho hamna yeyote aliyejibu, na nikasema kwa hivyo ni kilio cha aina gani? Niliuliza, nimekufeli kwa njia yoyote na nikasikia ya kwamba ni kilio cha kutubu dhambi. O Abba YAH, Ndio, Ndio mimi ninatubu, pole sana kwa vile ninajua ya kuwa mimi sio kamili, ninajua mimi hufeli nyakati zingine. Nilikuwa ninajaribu kufikiria ni nini kibaya nilichokuwa nimefanya ambacho Mungu aliweza kusema ya kuwa sikuwa nimekitubu.

 

 

Mimi huwa na wasiwasi sana kuhusu kitu hiki na Youtube, mimi huwa na wasiwasi kuwa roho yangu imekuwa wapi, baridi kuu hunikumba rohoni wakati mwingine. Watu hawa ni wanyama na imekuwa ikiendelea kwa muda kupita mwaka na mimi huwa na wasiwasi kuwa nyongo imeniingia kwa sababu Mungu amekubali na maadui wananikejeli na kucheka na wanasema, waona, yeye sio Nabii bado ninasimama hapa na bado niko hai na hakuna ambacho kimefanyika. Kwanza huyu Molly na mimi nilisoma kuwa mwanamke huyu alikuwa anakejeli kwenye akaunti yake bandia hata sijui jina lake. Siwajui watu hawa. Kwa hivyo nilipokuwa ninatubu na nilikuwa na wasiwasi kwa sababu ya kile nilichokuwa ninakiombea mara ya pili kabla sijarudi kulala, ni baraka ngapi zilizojitokeza na kufikia watu na ujumbe wa Wokovu na Unabii, lakini ninahisi ni kama nimejiumiza mwenyewe kwa njia fulani.

 

 

Kwa hivyo kweli hii Youtube imekuwa upanga wenye makali mawili, hata kama imekuwa baraka kubwa pia imeleta taabu, lakini nilipokuwa nikifikiria na kuomba kuhusu haya yote na kufikiri kuwa hii ndio sababu Mungu alikuwa amekasirika akisema kuwa hakuna ambaye ameshika simu, kilio cha kutubu.

 

 

Halafu nikamsikia YEYE akisema,

 

Neno la Unabii linaanza hapa:

 

“Sio wewe Elisabeth; sio wewe ninayezungumzia.” YEYE alisema, “Ni wale ambao hawajibu. Ni (wale walio ndani ya) dunia waliokataa kujibu kilio cha kutubu, wakijua kuwa Nimewapa onyo. Ni wale tu watakaohesabika ndio watakaoepuka Siku ya Dhiki Kuu. Ni wale wanaojua wanachofanya na kunikera MIMI na bado wanaendelea katika dhambi zao, wanaosema wana Roho Mtakatifu ndani yao lakini wanaendelea kwa dhambi zao, (wale) wanaotoa visingizio wakijua kuwa MIMI huona kila kitu wanachofanya iwe filamu za ngono au iwe ushoga, iwe pombe au iwe zini, usherati, ulevi, madawa za kulevya, laana, wanajua kuwa MIMI huona, wanajua wanafaa kuwa mfano, wanadai jina la Yesu Kristo, hata YAHUSHUA na kumbe MIMI niko mbali nao. Roho Mtakatifu hawezi kukaa katika Hema ya dhambi, lakini bado wao hunijaribu MIMI mara kwa mara.

 

 

 

Nilitoa mwito wa kutubu dhambi, ni wachache ambao wamesikia. Ni kama simu inayolia na kulia na hakuna anayejibu. Nilikuweka kwenye mtandao mbali na pana, MIMI Nilikuweka pale ili kuonyesha kuwa MIMI ni Mungu wa hukumu na pia huruma, MIMI sidanganyi. Lakini wanamtukana Nabii, wanasema kuwa huduma YANGU ni ya uovu, wananijaribu MIMI na wananikejeli na kusema, hakuna chochote kitakachotufanyikia, Elisabeth nenda mbali. Wanasema ni kwa neema yote imefanyika kwenye msalaba. Sasa ninaweza kufanya dhambi nitakavyo, waona, roho yangu haijapotea. Ni wewe, wewe unaoishi katika sheria, unafikiri kuwa ni lazima umtii Mungu huyu unayosema na sisi tunasema kuwa hakuna kitu kama dhambi imetolewa kabisa.

 

Wanakuchukia wewe (Elisabeth) kwa dhati: wanachukia wote wanaohubiri kuepukana na dhambi. Wanachukia wote wanoaonya. Wewe ulitoa mwito, MIMI nilikutuma kule Amightywind kuwaonya wale watu wanaojiita Wakristo kutubu dhambi zao. Nimesema mara kwa mara kwa mara. Ni wachache watakaosikia.

 

 

 

Nilituma Huduma ya Amightywind kwa YouTube na kile walichokufanyia wewe wananifanyia MIMI na bado wao hudai Jina LANGU Takatifu na kumbe MIMI niko mbali nao. Wao hutaja Maneno YANGU, wao huzitumia kama silaha kwako na watu wengine wote wanaowaonya kutubu na kutafuta uso wa YAHUSHUA kabla Hajawaondoa kabisa duniani kwa ghadhabu ZAKE.

 

 

Wanasahau ya kwamba Nilikuwa yule Mwana Kondoo aliyechinjwa mara moja tu. Wanasahau kuwa Ninakuja na moto machoni MWANGU. Wanasahau ni ghadhabu ya Mwana Kondoo. Wanasahau kuwa dhambi MIMI huchukia. Wanatoa visingizio kufanya dhambi na wale watakaowajibika zaidi wale wanaotukana, dharau, chukia na kupaka uchafu Huduma hii Niliyoiita Amightywind.

 

Kwa hivyo Elisabeth Ninakuacha usikie simu ikilia, Ninataka uwaonye tena. Ni wachache sana walioshika simu ya kutubu na kuepuka dhambi. Ni wachache watakaookolewa wakati Siku ya Dhiki Kuu itakapoanza.

 

 

Haitoshi kusema tu tubu, lazima kuwe na vitendo vinavyotekeleza maneno hayo. Lazima kuwe na kurarua (rarua- kuharibu kabisa) na kuharibu kwa mavazi yako, lakini sio kwa njia ya kimwili. Nimesema tubu. Nimeiweka Huduma hii Takatifu hapo ndio wote duniani waone kama wamechagua pia na bado wengi wao wamefunga masikio yao na kupofua macho yao, wanasema sisi hatuoni, sisi hatukusikii na ni huduma ya Amightywind na wewe Nabii Elisabeth Elijah ndio tunaowachukia. Sisi ndio jamii ya Wakristo na hata useme nini, chukua Huduma yako ya Amightywind na chukua Unabii zako mbali kwa kuwa tutaendelea kwa dhambi zetu na utaona, bado tuko hai na haijalishi kama Huduma ya Amightywind tunaichukia kwa sababu Mungu wenu bado hajatuua. Mungu wenu hata hajatushika kwa hivyo huyo Mungu wenu sio Mungu wetu kwa sababu Mungu wetu anasema tunaweza kutenda dhambi. Mungu wetu asema tunaweza kukuchukia. Mungu wetu asema tunaweza haribu Amightywind. Mungu wetu asema wewe ni nabii bandia na hakuna haja ya kutubu dhambi zetu.

 

 

O, lakini nyinyi watu wajinga, wajinga huyu ni MIMI, YAHUSHUA, anayeongea kupitia chombo hiki cha udongo. Mmenijaribu MIMI na kunijaribu MIMI na kunijaribu MIMI na MIMI nimeitumia Huduma hii kwa mwito wa kutubu dhambi na bado mnasema ni shetani ambaye ametumwa. Mnasahau nilichoufanyia ule mti. Mnasahau kuwa ilikuwa MIMI, YAHUSHUA Niliyeulaani kwa sababu ulikataa kuzaa matunda mazuri. Mnasahau kwamba ulinyauka na kufa. Mnasahau kuna aliyelaumiwa ambaye MIMI Ninachukia. Ule mti unawakilisha wewe mwenye moyo mgumu kama jiwe, wewe unayetumia Maneno YANGU, wewe unayetumia Jina LANGU, wewe unayeiita Huduma hii ovu kwa sababu uliisikia neno tubu na epuka mbali na dhambi zako. Unachukia ya kwamba Nimenena na unamwita Nabii bandia kwa sababu unafikiri kuwa wewe unao ujuzi wote na bado MIMI Ninakuambia, wewe ni mjinga kwa vile maono yanapewa kwake huyu Nabii, lakini wewe unadhani unajua mambo yote. Bado, MIMI Ninakuita msomi mjinga wa bibilia kwa sababu unalitumia neno liuwalo tu na hamna roho katika yote unayosema na unaitumia Neno Takatifu na kusema ni Bibilia ya King James (KJV) pekee inayofaa, ondokeni mbali NAMI nyinyi nyote wengine, mmeiongezea vitabu vingine na hapana, hata hatutaziangalia.

 

 

 

Wajinga, wajinga nyinyi, MIMI ninatingiza kichwa changu nikiangalia maisha yenu. Nyinyi ndio msipotubu na kuepuka mbali na dhambi kwa uhakika, nyinyi ndio nitakaowaambia ondoka mbali na MIMI enyi wafanyakazi wa uovu kwa kuwa MIMI sijawahi kuwajua. Kwa sababu tu umesema ombi la wokovu, lazima pia vitendo vyako vitekeleze maneno yako, huwezi tu kusema kwamba unanipenda MIMI na ukose kunitii MIMI. Huu ni uongo kutoka kule Jehanamu. Huu ni uongo na kwa sababu Huduma hii ndiyo inayowaambia na pia kila Huduma nyingine inayotembea katika utakatifu WANGU na kukataa kuafikiana na dhambi na watenda dhambi. Nyinyi mnaojiita Wakristo hakuna utakatifu wowote ndani yenu na mnachukia yeyote ambaye huja kwenu na Roho ya Utakatifu na upako WANGU katika nyuso zao na jambo hili halijabadilika kutoka siku za kale. Mnachukia yeyote anayeongea Maneno YANGU, walio na upako na wajasiri na kwa hivyo nimempa Elisabeth ishara mnapokaribia kuingia mnayoita mwaka mwingine.  Kumekuwa na mwito wa kutubu na lo, ni wachache, wachache ambao wanasikiliza au hata kusikia simu hio ikilia.   

 

Bado hamuelewi? Bado hamuelewi? Njia ya pekee ya kuingia mbinguni ni kwa kuchukua simu hio. Ni lazima usikie simu hio ikilia. Ni lazima uujibu mwito huo wa kutubu na kuepuka mbali na dhambi, acheni kutunga visingizio kwa sababu hivi karibuni mtapata mmechelewa.

 

 

Uhukumu kali utakuja kwa wale ambao wametesa Huduma hii ambayo MIMI nimeiweka kwenye vyombo vya habari vilivyo na macho mengi na masikio nyingi na mmejua kuihusu na hamjaitetea na mmemchukia kwa sababu MIMI Nilisema kwa nguvu na uwazi TUBU, TUBU na muepuke mbali na dhambi zenu.

 

 

 

Mtachagua kadha wa kadha unabii hizi na kutumia akili yenu ya binadamu lakini MIMI Nimewaonya mara kwa mara ni kupitia Roho Mtakatifu pekee ndipo mtakapoelewa kuwa Maneno yaliyonenwa sio ya kutafasiriwa na akili ya binadamu. Kila Unabii bila kuzitenga zinasababisha watu kutubu dhambi. Zinasababisha watu kuja katika mikono YANGU ya upendo. Zinawaelekeza watu na kuwafunza Utakatifu. Haya sio Maneno ya mwanamke au mwanamume. MIMI hutumia chombo hiki cha udongo pekee, huyu mmoja ambaye mmechukia na kumtusi, mmesema tutakuangamiza, tutakuaibisha, tutaongea maneno yetu ya chuki kwa sababu tunaweza. Hata tutaiba na kulichafua jina la Huduma ya Amightywind kwa sababu unathubutu kutuita sisi watenda-dhambi na unathubutu kuonyesha dhambi zetu kwa sababu sisi hatuwezi kuvumilia Utakatifu ulio usoni mwako au nyuso za wafanya kazi wanaofanya kazi kando yako, kwa hivyo tunaambia kila mtu ili kuhakikisha kuwa wao pia wakuchukie na wasisikilize Unabii Takatifu kwa kuwa ni uongo na kwa hivyo mnawafunga macho enyi wanafiki na kwa hivyo mnawaziba masikio.

 

 

 

Enyi mliokataliwa, MIMI Nitawaonyesha ni nini MIMI hufanya kwa sababu ya chuki yenu. Hamna Roho Mtakatifu ndani yenu. Nyinyi ni watoto wake shetani na MIMI Nimekuwa mvumilivu nanyi kwa muda mrefu sana. MIMI Niliiweka Huduma hii ya Nafasi ya Mwisho kabla ya kuja kwa siku za taabu na kumbukeni, chochote mmemfanyia mmenifanyia MIMI pia. Mtasimama mbele YANGU katika Mahakama ya Sheria inayotoka mbinguni na mtasimama mbele ya uso WANGU na MIMI Nitakukumbusha maneno yako ya chuki na MIMI Nitasema, ondoka mbali NAMI wewe mfanyakazi wa uovu kwa kuwa MIMI sijawahi kukujua, MIMI sijawahi kukujua. Ni aidha Roho WANGU Mtakatifu alikuacha kitambo au hakuwa ndani yako hata.

 

 

Kwa hivyo Elisabeth, MIMI hukuwezesha kusikia simu ikilia. Nilikuacha usikie ni kwa muda gani imekuwa ikilia, ishara yake tu, mara nane. Kuna wale watakaoisikia na itakuwa kwao mwanzo mpya na kwa kweli watatubu na watajua kwa kweli kuwa Huduma ya Amightywind ni Takatifu na ni Huduma ambayo Mungu alituma.

 

Kwa wale wote watakaonyenyekea na kuepukana na dhambi zao na akili, mwili, moyo na roho zao kwa kweli, watatubu kwelikweli. Kwa kweli, watatubu kwelikweli. Haya ndiyo maneno Ninayo ya kusema kwenu, jibu mwito huo, enyi Watakatifu wa kutubu, kila siku. Hata wewe Elisabeth, ulisema, ni nini ambayo sijajibu? Ni kwa njia gani ambayo sijatubu? O tafadhali nisamehe kwa njia yoyote ambayo mimi nimekufeli kwa kuwa mimi sio kamili. Nilikuambia, Elisabeth sio wewe, kwa sababu wewe husikia mwito WANGU na ulijibu simu YANGU na wale wote wengine ambao hufanya kazi kando yako na wale wote ambao wanajua kuwa Huduma ya Amightywind huongea ukweli na haijadanganya. Wamejibu mwito wa kutubu dhambi, lakini kuna wale ambao wanajua kuwa kuna ukweli kwenye Huduma hii na bado, wananijaribu MIMI na wanaamini kuwa imetosha tu kukujua. Wanaamini kuwa imetosha tu kusoma Unabii. Wanaamini kuwa MIMI siku zote Nitakuwa na huruma na hakutakuwa na matokeo ya dhambi. Hawa ndio MIMI Nitawapa hukumu kali zaidi kwa sababu hawaoni ya kwamba wanawajibika kwa dhambi Ninazozichukia.

 

Kwa hivyo waambie Binti YANGU, wanataka Neno jipya litokezee. Waambie Nilivyofurahia MIMI na wale ambao hujitahidi, ambao bali na kunitii MIMI kila siku, huamini na kuzungumza na kusambaza yale Maneno MIMI husema. Hawaogopi kumwudhi binadamu yeyote kwa kuwa nia yao pekee rohoni ni kinifurahisha MIMI YAHUSHUA, kwa kuwa wanajua zawadi zao zitatoka Mbinguni.

 

Kwa hivyo waambie Binti YANGU, wewe kuwa yule Eliyah wa Upya ambaye Nimempa upako na kazi ya kufanya.

 

Waambie Binti WANGU, hata kama watatema kwenye uso wako, wewe waonye Binti WANGU, hivi karibuni wataangamizwa.

 

 

Waambie Binti WANGU, o MIMI Naja tena. MIMI Naja tena, lakini wakati huu itakuwa Nikiwa na moto machoni MWANGU na siongei kuhusu Nitakapomchukua Bibi Arusi WANGU kuwa NAMI, Ninaongea kuhusu wale maadui ambao wako kama ule mti, Nitaulaumu na utanyauka na kufa kwa wote kuona.

 

 

Waambie Binti WANGU, kuwa yule Nabii mjasiri. Acha kushugulika na wanachosema wanawake na wanaume.

 

 

Wewe waambie Binti WANGU, wewe waambie kwa niaba YANGU kwa kuwa huo ndio mlio wa simu. Wewe una mwito wa kuwa Nabii. Uliijibu kitambo sana. MIMI sitakuacha ukose kuchukua simu hiyo. Ni mwito wa maisha yako ambao huwezi kuutoroka kwa sababu ni MIMI Nimekuita Binti WANGU kuonya binadamu wote kabla ya Siku Kuu ya Dhiki kufika, wakati wa Shida ya Yakobo. O na kwa wengi sana, sana, watakuwa wamechelewa.

 

 

Haya ndiyo Maneno Ninayo ya kusema. Tena maadui watakutumia kejeli na chuki.  Jua tu hivi, wao sio WANGU. Jua tu hivi, MIMI sijawatuma. Jua tu hivi, wao ni watoto wa shetani, bibi arusi wa shetani, waliokataliwa, wafanyakazi wa uovu na watalipa na roho zao na Jehanamu na Ziwa la Moto, hatima yao inawadia.

 

 

Usiyaweke maneno hayo ya chuki, nipe MIMI. Ninayaweza, wewe hauyawezi. Haya sio yenu enyi Watakatifu kushughulikia, maneno haya ya chuki ni ya kwangu MIMI. Hizi kejeli, matusi yanayosemwa ni ya kwangu MIMI. Hawawezi kuona ule Upako na Utakatifu Niliouweka juu yenu WOTE ambao ni WANGU sanasana Bibi Arusi WANGU wanaokazana kila siku kunitii MIMI na hunitumikia MIMI na kuniabudu MIMI na kuniita MIMI MWENYEZI MUNGU na BWANA, KIONGOZI wa maisha yao, MKUBWA, MWOKOZI, wao hunikiri MIMI. Hawa ndio Bibi Arusi WANGU. Wao huchukua matusi, huchukua chuki, wanalaumiwa, wanapakwa matope, wanaongelewa maovu. Hawa ndio Bibi Arusi WANGU na o Nitawachukua kwa haraka kuwa karibu NAMI. Mnajijua. Mnakubali ukweli unaojitokeza. Mnajijua. Mnayafahamu matunda mazuri yaliyomo kwenye Huduma hii ya Amightywind kwa vile upepo mkuu unaenea kote duniani. Na sasa Ninaipeleka kote katika lugha nyingi tofauti na kuna zingine zaidi zinazokuja.

 

Mnajijua o Bibi Arusi WANGU Ninaowathamini. Je mnajuaje? Kwa sababu mmechukiwa, mmetukanwa, mmedharauliwa, mmetupwa mbali kama waovu. Bali kila mfanyalo ni kunifurahisha MIMI kwa kila njia na kuwaambia watenda-dhambi kutubu na kuepuka na dhambi na mmetukanwa kwa sababu ya hayo. Mnajijua, lakini hamwongei tu kuhusu Utakatifu, mnaishi maisha ya Utakatifu na hata hamfikirii kutenda dhambi kabla ya kuifanya. Nyinyi ndio Bibi Arusi WANGU. Nyinyi ndio Matunda YANGU ya Kwanza. Nyinyi ni wachache Ninapoangalia duniani humu, lakini nyinyi ndio Bibi Arusi WANGU na ni nyinyi Ninaowapenda na kuwathamini. Maadui wenu ni maadui WANGU, kama vile Esau Ninawachukia.

 

 

Wewe chukua maneno haya Elisabeth, wewe waonye ya kuwa simu inalia. Nimekutuma kama Nabii kwao kuwaambia. Ni wangapi wamesikia na hata hivyo wamekataa kukubali ya kuwa wameisikia. Kwa hivyo Ninakuambia, o Nabii WANGU, waambie watubu dhambi, waambie Nilichokuwezesha usikie na kutakuwa na wale watakaotubu dhambi na kuepukana na dhambi zao. Na ukiwaambia kuwa simu inalia, watasikia. Watasikia na watasamehewa na kama namba 8 inavyosema (Vilio 8 kwa simu) tutakuwa na mwanzo mpya kwa sababu Nina Nabii aliye tayari kukejeliwa na kuchukiwa kwa ajili ya jina LANGU akitoa kilio kuu, jibu mwito huu wa kutubu dhambi, simu inalia kutoka Mbinguni, kwa kuwa Ninawapenda sana kuwaonya kupitia Eliyah WANGU wa Upya, hata jina lako Eliyah linachukiwa. Kumbuka tu ile Roho ya Jezebel ilimfukuza Eliyah wa Kitambo na je unatarajia jambo lipi lingine? Je, Nabii Mtakatifu yeyote anaweza tarajia jambo lipi lingine? Je, Bibi Arusi wa YAHUSHUA anaweza tarajia jambo lipi lingine? Kwa sababu kama wangenikubali MIMI, kama wote wangenikubali MIMI kwa upendo wangekuwa pia wanakukubali, lakini ukiangalia dunia hii na hata MIMI hutuma baridi kunyeshea nyoyo za mawe na bado hawatubu, bado hawaepuki. Wanasema kuwa MIMI tu ni Mungu wa upendo na huruma na MIMI siwashtaki kuhusu dhambi, lakini wataona hiyo ndiyo sababu kutakuwa na kile kinachoitwa Siku ya Dhiki Kuu.

 

Asante Elisabeth kwa kujibu mwito kwa kuwa ungekuwa unaishi katika dhambi hatya haungesikia simu hii ikilia, lakini ulisikia na ililia mara 8 kwa sababu wengi, wengi watakasikiza na hii itakuwa kwao mwanzo mpya.”

 

 

Imezungumzwa katika Upako wa RUACH ha KODESH 

kwake Mtume Elisabeth (Elisheva) Sherrie Elijah

Nikiwaudhi wengi, na baraka kwa wengine. Mtoto, Shujaa, Bibi Arusi wa YAHUSHUA ha MASHIACH/YESU KRISTO

 

 

Contact AmightyWind

 

www.amightywind.com

www.almightywind.com