UNABII 118

JIHADHARINI, DHIKI KUU IMEKARIBIA MNO!


IMEANDIKWA/IMEZUNGUMZWA KATIKA UPAKO WA RUACH HA KODESH

KUPITIA MTUME ELISABETH SHERRIE ELIJAH (ELISHEVA ELIYAHU)

IMEPOKEWA FEBRUARI 19, 2010

ILITOLEWA JUNI 27, 2010

Kutoka Unabii 105, YAHUVEH Alisema ujumbe huu uwekwe katika kila unabiii kutoka sasa: Nilikuonya kitambo Elisabeth kutoita huduma hii kwa jina la mwanamume au mwanamke hata kabla kuwepo na huduma. Niliiweka ndani ya roho yako kwa kuwa hakuna lolote kwa haya lililofanyika kwa mkono wako au lililotoka kwenye kinywa chako. Ilitoka kwenye kinywa cha YAHUVEH Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye kinywa cha YAHUSHUA, MASIHI wako Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye kinywa cha RUACH ha KODESH, IMMAYAH wako Aliyeizalisha. Kama ingekuwa tu kwa mkono wako, ingekuwa imefeli kitambo. Ni kwa upepo wa SHKHINYAH GLORY unaovuma kote duniani, upepo Takatifu wa uamsho, sio kwa pumzi yako, au ingekuwa imefeli. (Isaya 42:8)

Katika mwezi wa Julai 2010, MUNGU YAHUVEH pia Alisema kuongezwe yafuatayo mbele ya Unabii zote kutoka Kitabu cha pili cha Mambo ya Nyakati:


2 Mambo ya Nyakati 36:16, “Lakini waliwadhihaki Wajumbe wa MUNGU, na kuyadharau Maneno YAKE, na kuwacheka Manabii WAKE, hata ilipozidi Ghadhabu ya BWANA juu ya Watu WAKE, hata kusiwe na kuponya.”


* * * * * * *

[Kwa wale wanaotafsiri unabii huu katika lugha tofauti, jina “Judas’” inatamkwa kama “Judases” katika Kiingereza.]

Neno la Unabii Unaanza:

[Elisabeth (Elisheva) anaanza kuomba katika Ndimi Takatifu]

"Imetosha, imetosha! Yudasi aliruhusiwa tu kutembea kati ya Mitume kwa muda fulani! Yeye, pia, hakuweza tena kucheza mchezo wa mnafiki kwa maana kuna waumini na kuna wafuasi.

Haitoshi kusema, 'Namwamini YAHUSHUA/YESU. Naamini kuwa kuna Mungu Mbinguni Anayeitwa YAHUVEH/YAHWEH. Naamini kuna ROHO MTAKATIFU, RUACH HA KODESH.' Swali ni hili, je, nyinyi mnatufuata SISI? Haitoshi tu kuamini!

Ninawafichua Mayudasi waliojificha. Ninawafichua wale wanaojiita Wakristo na sio! Ninafichua ni nani walio bibi arusi wa shetani! Bandia wamewazunguka nyinyi wote. Wanawapiga vita Bibi Arusi WANGU wa kweli! Bibi Arusi wa
YAHUSHUA MASIHI wapo katika vita dhidi ya bibi arusi wa shetani!

Mnataka kujua adui wenu hatari zaidi ni nani? Sio wapagani wanaokataa kukubali Jina LANGU. Ni Kanisa la Wanafiki!

Katika siku hii kelele inavyopigwa ulimwenguni wakati mmoja aitwaye Elton John ameinuka na kutangaza kwa watu wote, ‘Nadhani Yesu alikuwa na huruma, shoga mwenye akili zaidi na aliyeelewa matatizo ya binadamu. Yeye msalabani aliwasamehe wale waliomsulubisha na Yesu anataka tuwe na upendo na kusamehe. Sijui ni nini kinachofanya watu kuwa wakatili kwa sababu Bibilia inasema YESU alikuwa bila dhambi na hiyo inamaanisha ushoga umefutwa, kwa hivyo hauwezi kuwa dhambi.’ Ndivyo asemavyo Elton John.

Lakini MIMI YAHUVEH Nimechoka! Mtu huyu, Elton John, anathubutu kusema Maneno YANGU Matakatifu na kuyageuza! Na kusema kuwa YESU KRISTO wa Injili ni shoga?!

Ulimwengu, kwa chukizo hili nyinyi mtakunywa Pigo la Damu Nyeusi Inayochemka! Ulimwengu jitayarisheni! MIMI, YAHUVEH/YAHWEH, Ninasema hivi, Nimechoka!!!

Ugonjwa huu umekuwa upo ndani ya wale ambao ni mashoga na wasagaji, ugonjwa huu umekuwa ukisubiri muda WANGU ufike. Nyinyi mnaotoa visingizio kwa ajili ya mashoga, Nimewapa muda wa kutubu ...


Sitawaambia siku yenyewe, Sitawaambia mwezi, Sitawaambia hata mwaka ambapo ugonjwa huu utadhihirika wazi, lakini Nitawaambia haya sasa, Pigo la Damu Nyeusi Inayochemka imefika kwenye Ikulu, Ninawaambia hakuna yeyote atakayeepuka!

Yeyote awezaje kuthubutu kusema, haya Niliyoyatangaza MIMI katika Neno LANGU Takatifu ni chukizo, sasa mnathubutu kusema Mwanangu wa pekee YAHUSHUA MASIHI, Mwanakondoo kamilifu Aliyechinjwa bila doa, bila dosari ya dhambi, Alishiriki katika chukizo hili liitwalo ushoga, kejeli dhidi ya kile Nilichoumba wakati Nilipowaumba Adamu na Hawa.


Mayudasi wamefichuliwa mbele ya macho yenu, ndio, wale wanaonakili Maandiko na bado wanasababisha kupotea kwa wengi kwa kuwa hawafuati hata maneno ya Maandiko. Ole wao Mayudasi wanaosema, "Msiamini Bibilia. Msiamini Maandiko Matakatifu. Tupilieni mbali Torati, imeandikwa tu na mtu wa kawaida. Rarueni Andiko hili. Rarueni ukurasa huu. Rarueni sura hii.” Nitawaambia ni nini Nitakachorarua, Nilichorarua, Nilichofuta, ni majina yenu katika Kitabu cha Uzima cha Mwanakondoo!


MIMI, YAHUVEH/YAHWEH, Nasema, Nimechoka, vita vimekuwa vikiendelea kwa muda mrefu. Je, si Nilisema, 'Katika siku hizi kabla ya muda wa Taabu ya Yakobo, Dhiki Kuu, Mtakatifu atakuwa Mtakatifu zaidi na mwovu atakuwa mwovu zaidi?' (Unabii 90, "Ni nini Jina la RUACH ha KODESH? ")

Sasa wanathubutu kujiita ‘Wakristo’. Wanasema: ‘Msiwe na wasiwasi kwa kutenda dhambi. Ninawahakikishia Mbinguni hata hivyo’.

Na sasa huyu mpotovu, mtu mwovu na mwenye roho ya mpinga kristo, Elton John, anajaribu kuwashawishi wote walio katika jamii ya mashoga na wale wanaothubutu kujiita Wakristo, "Usiwe na wasiwasi. YESU KRISTO alikuwa mmoja wenu. Ushoga hauwezi kuwa dhambi kwa kuwa waona Yesu Kristo hakuwa na dhambi.” Na bado wananena kunihusu na hawajui hata Utakatifu wa Mwanangu YAHUSHUA, na wanazungumzia Maandiko YANGU Matakatifu na bado wanamtumikia shetani na yote yaliyo ndani mwao.

Mnajua Wapendwa WANGU, Bibi Arusi WANGU wa Mwanangu
YAHUSHUA MASIHI, Ninawaamini. Huwa Ninawaruhusu Mayudasi kuingia kati yenu, kama vile tu Yudasi Iskarioti aliruhusiwa kati. Je, hamfahamu, naye pia alikuwa na wafuasi wake, lakini Ninawaambia, kama vile Nilivyokuambia muda mrefu uliopita Elisabeth, ole kwa Mayudasi wanaotafuta kujiunga na Huduma hii. Walianza kwa kunywa maziwa na kula nyama ya kiroho na kisha wakasaliti yote waliyojua yalikuwa Takatifu. Kwa hivyo Ninawakataza kuomboleza Yudasi, kwa kuwa Mimi sifanyi hivyo!

Mayudasi wanaokusaliti hapa duniani wanasaliti Bibi Arusi Watakatifu WANGU wote, hata wale wanaoishi miongoni mwa jamii zao wenyewe. Ni wangapi walio na Mayudasi katika jamii zao wenyewe? Ni wangapi walio katika jamii zilizofungiwa nira na wasioamini, hata wale wanaojiita WANGU? Wao (Mayudasi) walisaliti hapo awali katika vita na Lusifa kule Mbinguni. Je, mnafikiri Mimi Ninashangaa? Je, si Nilisema kwamba Ninaruhusu ngano na magugu kukua pamoja?
(Mathayo 13:30) Sasa Nimekuonyesha magugu leo hii na Ninakuambia haya, Nilikuambia uonye dunia ya kuwa Wakati wa Taabu ya Yakobo imekaribia mno, Dhiki Kuu.


Mwana WANGU Mpendwa (Mhudumu wa Vijana katika Amightywind), umetengeneza fundisho la kufichua uongo wa shetani unaohusiana na kunyakuliwa inayoitwa ‘Rapture’, na ni wachache mno wanaotaka kujua Ukweli. Kanisa la Wanafiki wanaona heri waamini uongo, 'ishi njia yoyote unayotaka, tenda dhambi njia yoyote unayotaka, inatosha tu kuwashawishi wengine kuwa wewe ni Mkristo, sio lazima kuyafuata yale unayoyaandika, unayoyasema, sio lazima kuwa mfano wa
YAHUSHUA MASIHI ni nani, imetosha tu kujifanya. Imetosha tu kusema, “Yesu akubariki”.

Ole wao hawa Mayudasi wanaowapoteza Kondoo na Wanakondoo WANGU, lakini mwaona majina ya Kondoo na Wanakondoo WANGU yameandikwa katika Kitabu cha Uzima cha Mwanakondoo na watarejea tena kwa MCHUNGAJI MWEMA YAHUSHUA
. Inaweza kuchukua kuteseka kwa njia ya moto wa mateso na uchungu usioelezeka katika wakati wa Taabu ya Yakobo, mnayoita Dhiki Kuu, lakini Kondoo na Wanakondoo WANGU watarudi KWANGU hata kama ni kwa pumzi yao ya mwisho. Imani yao itakuwa moto wakipitia moto wa mateso.

Jihadharini, nyinyi mlio vuguvugu, Nimeituma huduma hii kunena Maneno YANGU ili kuwapa onyo. Mimi Nimempaka mafuta Mtume WANGU kusema Maneno YANGU na kwa sababu yeye si mwanamume mwenye ndevu refu ya rangi ya kijivu, mnataka kumfukuza. Mnasema, ‘MUNGU hawezi hata kuzungumza kupitia mdomo wa mwanawamke huyu.’ Hamtaki kusikia. Mnaonyesha upumbavu wenu. Mnaonyesha jinsi mlivyo na masikio yanayowashwa.

Sababu kuu mnachukia Huduma hii ni kwa sababu ya hukumu
. Hamtaki kuambiwa ya kwamba Wakristo vuguvugu wataenda Jehanamu na hawa sio Wakristo, na kwamba mnafanya makosa wakati hamtii Amri Kumi. Mnataka tu kusema, 'YESU KRISTO Alinilipia gharama pale Kalvari.'

Ndio,
YAHUSHUA MASIHI Alilipa gharama kwa ajili yenu pale Kalvari, lakini mmemlipia gharama ipi? Je, kuwauliza kutii ni kuuliza kwingi? Mnapozaliwa mara ya pili na kujazwa na RUACH ha KODESH/ROHO MTAKATIFU, hamna sababu tena ya kutenda dhambi kwa maana RUACH ha KODESH Aliye ndani yenu Anayewakosoa mnapotenda dhambi. Kwa kweli mtakuwa na hamu ya kunitii MIMI, YAHUVEH/YAHWEH, kwa kila neno Nisemalo.

O wengi sana husema Ombi la Wokovu wakijigamba na kusema, 'Namwamini Yesu,' lakini ni wangapi wachache sana wanaofuata wanachodai kuamini? Mnachukia Huduma yoyote, mtu yeyote anayewakosoa
kwa ajili ya dhambi zenu.

Nuru na giza haziwezi kuenda pamoja.
(2 Wakorintho 6:14) Kwa mkono WANGU mwenyewe Neno LANGU limesema vivyo hivyo. YAHUSHUA MASIHI Alikuja na upanga unaotenganisha. (Mathayo 10:34) Kwa Maneno YANGU mwenyewe imenenwa na je, jibu lako ni lipi?

Wale ambao hawataki kuachana na jamii zao walipofungiwa nira na wasioamini, ili wasikusaliti katika Dhiki Kuu, jibu lako ni, 'Mtaje yeye nabii bandia
. Rarua Maneno haya kutoka kwenye Bibilia. Yapuuze. Yafute'. Hilo ndilo jibu lako. 'Potosha wengine.' Hakuna kitu kilichobadilika!

Roho ile ile ya Mafarisayo waliowapiga mawe Watakatifu WANGU, Bibi Arusi wa YAHUSHUA, wanaoishi maisha yao kila siku kunipendeza MIMI, hawadai kuwa wakamilifu na wanaponikosea MIMI bila kusudia, wanatubu haraka na machozi machoni mwao na wanasema, "O tafadhali nisaidie nisitende dhambi hii tena.” Kuna aina nyingi za dhambi, hata Nabii huyu Ninayemtumia kuzungumza Ujumbe huu sasa, anapambana na dhambi ya kuasharisha. Ni wangapi kati yenu mnaojikwaa kwa dhambii hii? Mnajua mnachofaa kufanya, lakini mnafanya hivyo kwa wakati wenu. O mnajua Ninachotaka mfanye na sizungumzi juu ya Amri Kumi sasa. Inaweza kuwa ni kitu kidogo sana, lakini hamfanyi. Kuna aina nyingi za dhambi.

Hakuna aliye mkamilifu, kila mtu ni kazi inayoendelea lakini MIMI Ninawaambia, wakati utakapofika kuja kuwachukua Bibi Arusi wa YAHUSHUA itakuwa wakati gredi zenu za mbinguni zipo katika kiwango cha juu, wakati kila siku mnajitahidi kunitii MIMI kwa kila njia, wakati mtakapofanya miili yenu dhabihu iliyo hai, wakati mtakapojua Sheria ya kwanza ya Torati, (Amri ya kwanza - Usiwe na Miungu mingine ila MIMI) na hamtawahi kwa ajili ya mke/mume au mpendwa kuivunja hata kama itamaanisha mwisho wa ndoa zenu. Mnatambua kuwa hakuna anayekuja kabla yake YAHUVEH /YAHWEH, YAHUSHUA na RUACH ha KODESH.

Ndoa zilizo na nguvu na zilizobarikiwa zaidi zitakuwa za wanaozingatia Amri ya Kwanza na wote wawili watakuwa ‘sio sawa’ katika upendo na kutii kwake YAHUSHUA, yaani wote wawili watakuwa wanampenda YAHUSHUA zaidi ya vile wanaopendana au mtu mwingine. YAHUSHUA ni Mpenzi wa maisha yao, nafsi na roho na Ninaposema ‘sio sawa’
je, si hivyo ndivyo ipasavyo kuwa wakati mnapompenda YAHUSHUA juu ya yote? Uko hapa duniani kwa muda mfupi sana. Hii ni pumzi moja tu katika maisha yako. Tunaongea kuhusu milele Mbinguni.

O Bibi Arusi Mpendwa WANGU, Bibi Arusi Mpendwa wa YAHUSHUA MASIHI, nisikilizeni MIMI, msiruhusu chochote kiwe cha muhimu zaidi kuliko YULE Anayesababisha moyo wako kupiga, YULE Anayepumua uhai kupitia kwako. O Mpendwa WANGU, hakuna yeyote anayeweza kukupenda kama vile MIMI, YAHUVEH/YAHWEH, Ninavyokupenda. Je, yule unayemwita Mpendwa wako, mke/mume wako, anajua idadi ya nywele kichwani mwako? (YAHUVEH/YAHWEH Analia kupitia Elisabeth [Elisheva] Alivyokuwa Anasema haya, Aliposema jinsi YEYE Anavyopenda Bibi Arusi WAKE.) Usiruhusu MIMI, YAHUVEH/YAHWEH na YAHUSHUA kuwa mwisho mdomoni mwako.

O, enyi Wakristo vuguvugu, wale YAHUSHUA Atakaowatema nje kama matapiko kutoka kinywani MWAKE, hii ndiyo sababu upendo wenu umekuwa baridi. Mmeweka vipenzi vingi mbele YETU, tamaa yenu ya kidunia, tamaa za kimwili, mbele YETU, ndio, hata wale wanaojiita WANGU na kuthubutu kujiita Wakristo! Na mnashangaa kwa nini hamwezi kutenganisha kati ya Ukweli na uongo, lakini mnawapiga mawe Watakatifu na Huduma hii inayozungumza kama vile kwa hakika Stefano alipigwa mawe.
(Matendo ya Mitume 7:59) Ninazungumza na wale Wakristo vuguvugu, sio lazima mbaki kuwa matapiko! Chaguo ni lenu!

Nimetuma Huduma hii na Huduma nyingine na watu binafsi ambao ni sehemu ya Bibi Arusi Takatifu wa YAHUSHUA MASIHI kuwaonya! Nimemtuma huyu Eliya WANGU Mpya na sijali kama mnapenda kusikia haya au la, lakini Nilimtumia Eliya WANGU Mpya kuizaa Huduma hii na hiyo ilianza Marekani na sasa iko duniani kote, kuonya, kukemea , na kutia moyo. MIMI sineni tu baraka bali MIMI, YAHUVEH/YAHWEH, hunena laana pia. Imetosha! Sitaomba Sodoma na Gomora msamaha!


Dunia hii imekuwa Sodoma na Gomora katika macho YANGU. Aibu kwenu! Aibu kwenu enyi msiowatetea Watakatifu wanaonena onyo hizi!

Kwa hivyo, Wapendwa WANGU, leo hii Nimemfichua Yudasi. Mtaona Mayudasi wakija na kuenda. Ole wao wanaofuata Mayudasi kwa kuwa yenu itakuwa hatima sawa! Ole wake mtu yeyote anayesema ya kwamba kuchukua ushirika katika kumbukumbu ya yale MWANANGU YAHUSHUA Alilipa, kutoa mwili wake na Damu kwa ajili ya dhambi zao, ni
kula nyama ya binadamu (cannibalism) au kunywa damu ya binadamu (vampirism)! Ole! Ole! Ole! Ole! Ole! Hii ni kufuru, na kejeli kuu dhidi ya sadaka yake YAHUSHUA.

(Tulimjua mtu huyu kwa takriban miaka mitatu. Mtu huyu alikuwa msaidizi mwaminifu na tulimchukulia kama sehemu ya familia ya YAHUSHUA. Mtu huyu alienda kwenye tovuti kwa intaneti isemayo kwamba kuchukua ushirika ni kula nyama ya binadamu (cannibalism) na kunywa damu ya binadamu (vampirism) na cha kuhuzunisha ni kwamba, mtu huyu aliamini uongo huu wa shetani. Kwa hivyo Yudasi huyu aliwatumia wengine barua pepe na kujaribu kuwafanya kuamini uongo huu, mtu huyu hata alijaribu kumshawishi Elisabeth kuhusu uongo huu. Mtu huyu sasa ni Yudasi na atapata hatima sawa kama Yudasi.)

Tangu lini! Tangu lini! Unapoomba kwamba uwe mmoja na YAHUSHUA katika akili, mwili, roho, na nafsi na kuomba msamaha wa dhambi zako, na Damu YAKE hukusafisha uwe msafi, tangu lini haya yakawa mabaya? Ni nani anayethubutu kusema uongo kama huo?! Ni nani anayethubutu kuamini uongo kama huo?!
RUACH ha KODESH/ROHO MTAKATIFU hayumo ndani mwao! Una ujuzi wa kichwa na sio ujuzi wa moyo. Ushirika ni muhimu, na ni silaha dhidi ya adui.

Nyinyi mnaosema, 'Ushirika si muhimu', maneno ya mwisho ya YAHUSHUA Alipokuwa Ameketi pamoja na wanafunzi WAKE yalikuwa, 'Huu ni MWILI WANGU, fanyeni hivyo kwa Ukumbusho WANGU.
(Mathayo 26:26-28, Marko.14 :22-24, Luka. 22: 17-20, 1 Wakorintho 11: 22-30) Tangu lini hii ni dhambi!? Ni nani, isipokuwa shetani anayeweza kusema hivyo!? Ni nani anayethubutu kusema hivyo!? Hili ni tusi kubwa mno kwa kuwa mmekejeli Damu ya MWANANGU! Mnaita maovu yale Niliyoita kamili! Hili ni tusi kubwa mno na tena nyinyi waongo mnajaribu kumpotosha Nabii WANGU Ninayemtumia kuzungumza, na kuwaambia wengine uongo huu. Ushirika ni silaha kuu mno dhidi ya shetani na nyinyi mmeiita uovu ushirika huu, na kile Nilichozungumza ni kizuri, nyinyi mmeita kibaya?

Kwa uhakika kama mlivyokufuru YAHUSHUA MASIHI na pia MIMI, YAHUVEH/YAHWEH, Niliyemtuma MWANANGU wa pekee kutoa mwili WAKE na Damu kwa ajili yenu, mmemtukana RUACH ha KODESH. Mmewakufuru wote WATATU! Niliwaambia. Niliwaonya, 'Jihadharini na wakati ambapo maovu yatasemekana ni mema na mema yatasemekana ni maovu.'
(Isaya 5:20)

MIMI daima huwatuma Manabii WANGU kunena Maneno YANGU. Maandiko Matakatifu hayakunenwa na mwanadamu. Hamna tofauti kama Ninavyozungumza MIMI kupitia chombo hiki cha udongo sasa. Ni MIMI, YAHUVEH/
YAHWEH, Niliyeweka Maneno hayo ndani yao ili wayaandike. Maneno haya Safi yaliharibiwa na waandishi na wafasiri mbalimbali.


Nawaonya msitegemee tu Bibilia ya Mfalme James kwa kuwa Mfalme James anachomeka Jehanamu. Alitoa vitabu na maneno ambayo hakutaka yajumuishwe
kama vile kwa uhakika wanavyofanya leo na kusema, "Maandiko haya na Sheria za Torati hazina maana tena. Hii haiambatani na fikra yangu ya Mungu ni nani. YEYE hapaswi kulaani. YEYE Alimtuma MWANAWE wa pekee kulipa gharama pale Kalvari, kuteseka na kufa kwa binafsi yangu, kwa hivyo sasa ninaweza kufanya chochote nitakacho, haijalishi MUNGU tena. YEYE hajali nitendalo kwa sababu YEYE Alimtuma MWANAWE wa pekee kulipa gharama. Sheria ilipigiliwa misumari msalabani, kwa hivyo ninaweza kufanya chochote nitakacho. Amri ya Nne, ninasema, siku yoyote yafaa kama Sabato, YESU KRISTO, YAHUSHUA MASIHI, Alisema YEYE ni BWANA wa Sabato, haijalishi tena kwa sababu walitupilia mbali siku hiyo.'

Waongo! Waongo! Waongo! Je, mnafikiri Ningepoteza muda WANGU kuchukua kidole CHANGU mwenyewe na kuandika juu ya tembe ya mawe na kumpa Musa na kutetea wana wa Israeli na kuwaamrisha waniheshimu siku ya Sabato kwa kupumzika?! Kwa kupumzika?! Sio kwa kufanya kazi bali kwa kupumzika?! Waongo!


Nyinyi mnaodai kwamba nyinyi ni Wakristo na huweka video hizi
kuhusu kwa nini Wakristo, ‘hawapaswi tena kuhangaishwa na Sabato, haijalishi ni siku gani, haijalishi, Kanisa la Kikatoliki imeibadilisha.’

Waongo! Kama hamtatubu mtajipata katika Ziwa la Moto! Mimi sitacheza michezo! Dhiki kuu, Wakati wa Taabu ya Yakobo, ipo karibu nanyi mno, wakati wa maombolezo, kilio, wa mateso makuu, zaidi ya dunia hii imewahi kujua!

Mnafikiri ni nini hufanya Jehanamu kuwa moto? Moto huzidi tu kuwa moto zaidi! Ni hasira, chuki na ghadabu ZANGU MIMI, YAHUVEH!


Nataka Bibi Arusi WANGU nyumbani! Ninataka Bibi Arusi wa YAHUSHUA nyumbani! Bibi Arusi WAKE ni Bibi Arusi WANGU. Ninawataka nyumbani.

Ninatazama huu mfereji wa maji taka uitwayo dunia. Kinyesi kipo kila mahali na Ninaona wanaong’aa katika kinyesi hiki, wale ambao ni Bibi Arusi wa YAHUSHUA MASIHI na wote Watakatifu, hapa na pale. Ni kana kwamba wao wamefunikwa chini ya kinyesi na o ni kinyesi kingi! Harufu mbaya sana ipo kwenye kinyesi, katika wale wanaojiita ‘Makanisa ya Kikristo’! Hukumu! Hukumu! Hukumu imekuja kwa ile mnayoita ‘Nyumba ya BWANA’!!

Wakati Makanisa ya Kikristo ya Ikabodi yanapoacha kuhubiri dhidi ya dhambi kama vile kuavya mimba, usherati na ndoa za jinsia moja, mnaporuhusu dhambi nyuma ya mimbari, mnaporuhusu mashoga kuhubiri nyuma ya mimbari na kujisifu juu ya dhambi zao, mlipokoma kuwakemea wenye dhambi, Ikabodi iliwekwa kwenye milango yenu na
RUACH ha KODESH/ROHO MTAKATIFU WANGU Alitolewa! (1 Samueli 4:21)

Mnaimba nyimbo zenu na kukusanyika siku ya Jumapili lakini MIMI sipo! O, baadhi ya Watu WANGU wapo pale lakini uwepo WANGU wa kweli, upako wa
RUACH ha KODESH WANGU, haukaribishwi pale. Mnatumia hisia zenu na kujifurahisha na nyimbo lakini Manabii WANGU wa kweli hawaruhusiwi kunena.

SISI haturuhusiwi huko. Ninaposema, ‘SISI’ Ninamaanisha uwepo haswa wa YAHUVEH/YAHWEH, YAHUSHUA, na
RUACH ha KODESH. Uwepo WETU HAUPO pale la sivyo wote wangeanguka chini nyusoni mwao!

Watatubu kwa ajili ya Marekani lakini je, wataonya wengine dhidi ya dhambi waliomo ndani? Hii ni kejeli. Je, wataka kujua kwa nini nguvu ya Upako, si kama vile ilivyokuwa katika Kanisa la Kwanza? Angalia na mwone kile Ninachoona MIMI. Uvundo ni zaidi ya vile MIMI, YAHUVEH/
YAHWEH, Ninaweza kustahimili.

Wapagani huangalia wale wanaoitwa Wakristo na kusema, "Hakuna tofauti kati yako na mimi '
. Elton John husema, 'Hakuna tofauti kati yako na mimi. Ninaweza kuandika upya Maandiko pia. Watu wanasema, 'Tupeni nje Amri ya Nne,’ kwa hivyo ninaweza kusema, 'YESU KRISTO ni shoga,' hakuna tofauti.'

Lakini tazama, MIMI Niliinua Huduma hii inayokataa visingizio vya dhambi, Huduma ya Aleph na Tav (Alfa na Omega) Almightywind (pia huitwa Amightywind)
RUACH ha KODESH Wildfire!

Huduma YANGU ya Amightywind ni upepo mkubwa wa kasi uvumao ulimwenguni na shetani hawezi kuusimamisha! Basi, anafanya kila mtu amtazame tu mwanamke huyu (Elisabeth
Elijah [Elisheva Eliyahu]).

Wale wanaomjua na kumpenda wanaweza kutofautisha kati yake na wakati MIMI, YAHUVEH/
YAHWEH, Ninapozungumza. Lakini sio mwanamke tu anayezungumza. MIMI ni YAHUVEH/YAHWEH na Ninawaambia Huduma hii huwaita Bibi Arusi wa kweli wa YAHUSHUA MASIHI wajitokeze kwa sababu mnawahitaji wengine. Nyinyi wote mnashambuliwa. Nyinyi ni kama mnyama aliyejeruhiwa anayelamba majeraha yake mwenyewe kwa sababu hamwezi kumwamini mtu yeyote kwa hivyo MIMI, YAHUVEH/YAHWEH, Nimeweka kundi hili pamoja na Nikatumia chombo hiki kinachozungumza kuizaa katika ulimwengu wa kimwili, MIMI YAHUVEH Nilikuwa tayari Nimeizalisha katika ulimwengu wa Kiroho na ni wale Wakanyaga Mapepo wa YAHUSHUA (YDS, Mashujaa Watakatifu wa Sala).


Mtaona Mayudasi wakija na kuenda, chaguo ni lao. Niliwaambia, 'Si kila mtu anatosha kuwa Bibi Arusi wa YAHUSHUA MASIHI, ni wale tu watakaobaki waaminifu hadi mwisho. Mtajua Bibi Arusi ni nani.

Wapendwa WANGU, Ninawakataza kulia chozi lingine kwa ajili ya Yudasi mwingine! Ninawakataza kulia! Badala ya haya, angalieni Mitume wote na wafuasi wa kweli wa YAHUSHUA wanaokataa visingizio vya dhambi! Kanisa la Wanafiki hukataa kuniweka MIMI, YAHUVEH/
YAHWEH, YAHUSHUA na RUACH ha KODESH wa thamani, kuwa kwanza, na mmezungukwa na wanafiki na watakuwa na hatima ya Yudasi. Ilikuwa tayari imeandikwa.

Yudasi ni mchafuko wa mwisho. Mnaona, huyu Yudasi hakutaka kuweka uchafu huo (wa kuambia huduma hii na nabii huyu kwamba kufanya ushirika ni wa ibilisi, kama
kula nyama ya binadamu (cannibalism) na kunywa damu ya binadamu (vampirism)) kama ukoma kwake. Walijaribu kuwafikia kuwachafua Bibi Arusi Watakatifu, Wakanyaga Mapepo wa YAHUSHUA, hata huyu Mtakatifu anayezungumza haya, ili kuwaongoza kwa yule mpinga kristo. Mayudasi kila mara hufanya vivyo hivyo. Hawataki kuweka uchafu huo kwao wenyewe. Wanataka kuisambaza, kwa hivyo msilie tena kwa ajili ya Mayudasi.

Ujumbe huu ni wa kuhuzunisha mno. Je, mnafikiri YAHUSHUA Alifurahia siku Alipomfichua Yudasi? Lakini tazama Wapendwa, Nitamruhusu Yudasi kujificha kwa muda fulani tu.

Tazameni kote duniani. Wengine wameweka imani yao katika kazi zao. Wengine wanapenda kazi zao zaidi ya MIMI, YAHUVEH/YAHWEH. Wengine wameweka imani yao katika pesa. Wanaona ufalme wao wa pesa ukianguka mbele ya macho yao. Wengine wameweka imani yao kwa wapenzi wao na Ninafunua vitu ambavyo hamngetaka kuona. Ninatenga na Nitaendelea kumtenga yeyote ambaye atamchafua Bibi Arusi WANGU.

Ninawajaribu, je, mnampenda nani zaidi, huyo mke/mume mpagani? Wale wanaodai kuwa wako katika ndoa iliyofungiwa nira na wanaoamini na wakati mke/mume atakaposema, ‘Lazima niwe na wakati wako zaidi,’ je, mtathibitisha kuwa wampenda nani zaidi? Wengi wanao hamu ya kuwa Bibi Arusi wa YAHUSHUA wapo katika jamii hizi? (Mathayo 10:37, Yohana 21:15-17)

Ninawajaribu. Majaribu ya imani yenu ni ya thamani sana kushinda dhahabu. (1 Petro 1:6-7) Hili ndilo jaribio lenu, ni nani mnayependa zaidi?

Kwa wale ambao hawajaolewa, mnalia, mnahuzunika na kusema, ‘Lazima niwe na mchumba.’ Je, mnampenda nani zaidi? Hamjui ni nini mnachoulizia. Hii ndiyo sababu Nilisema kuwa sitaunganisha ndoa zilizofungiwa nira na wasioamini katika hizi Nyakati za Mwisho. Ndoa Nitakazoziunganisha, watanipenda MIMI kwa usawa, watanifanyia kazi MIMI, kutii ROHO WANGU na sio mwili wao. Wale ambao hawajaolewa na hulia na kuhuzunika, hamjui Baraka ambayo Nimewapa. Kinachokuhusu wewe tu ni kunifurahisha MIMI, YAHUVEH/YAHWEH, sio mtu mwingine.Mwishowe, hakuna Bibi Arusi yeyote atakayefungiwa nira na wasioamini. Nitarudia, YAHUSHUA MASIHI Atatumia upanga wa kugawa na kabla Bibi Arusi hajanyakuliwa, kama wapo walipofungiwa nira na wasioamini, YAHUSHUA Atawatenga. Sitawaruhusu Bibi Arusi WANGU kuchafuliwa, ilikuwa tu kwa muda mfupi, kwa kuwa nuru na giza haiwezi kuwa pamoja. Hii ni vita, YAHUSHUA Anapigania Bibi Arusi WAKE, adui hawezi kushinda.Niliweka nuru na nuru na nuru inazidi kung’aa zaidi. Hamna ugumu mnapomweka YAHUVEH/YAHWEH, YAHUSHUA na RUACH ha KODESH kwanza katika maisha yenu na upendo wenu.

Je, si Niliwaonya ‘Adui wenu hatari watakuwa wale walio katika jamii zenu’? (Micah 7:6, Mathayo 10:36) Ninaonya tena sasa, wale ambao hawataki kutengwa, wale wanaopenda mke/mume wao kushinda MIMI, YAHUVEH/YAHWEH, wale wanaokurushia NENO LANGU usoni mwako na wanakuita wewe Elisabeth [Elisheva] nabii bandia, jua haya, haya si Maneno yako, haya ni Maneno YANGU! Na imeambatanishwa na Maandiko Matakatifu! (Unabii 111 – MIMI, YAHUSHUA MASIHI, Ninawapa Nyinyi Talaka Takatifu, Kwa Wale Wanaoihitaji.)Nilikuwa na Nabii mwingine (Nehemia 13:23-30) aliyewalaani na kuvuta videvu vya wanaume na kuwapiga kofi kwa kufungiwa nira na wasioamini, kwa hivyo wakati mashambulizi yatakapokuja na ndio, yatakuja, kuwa kama Stefano, Bibi Arusi wa YAHUSHUA MASIHI, msitazame tu mawe itakayowagonga lakini mtazame YAHUSHUA. Wanawagonga mawe lakini kwa kweli ni YAHUSHUA/YESU wanaomgonga na ndio, Ninathubutu kuzungumza kwa wale wanaojiita ‘Wakristo’ lakini Ninawaita Wakristo wa Ikabodi.

(Nehemia 13:25 Niliwakemea na kuwalaani. Niliwapiga baadhi ya watu na kung’oa nywele zao. Niliwaapisha kwa jina la Mungu na kusema: “Msiwaoze binti zenu kwa wana wao, wala binti zao wasiolewe na wana wenu wala ninyi wenyewe.Nehemia 13:27 Je, tulazimike sasa kusikia kwamba ninyi pia mmefanya uovu huu mkubwa na kutokuwa waaminifu kwa Mungu wetu kwa kuoa wanawake wa kigeni?)

Kwa hivyo Ninawaacha na Maneno haya. Niliwaambia, ‘Kila kitu kinachoweza kutikisika kitatikiswa’. (Unabii 105, “MIMI, YAHUVEH, Nasema, ‘Katika 2009 Nitatikisa kila kitu kinachoweza kutikiswa!’”) Niliwaonya mbele ya wakati mwaka wa 2010 utakuaje. (Unabii 116, “Lazima Muwe Wanaotembea Juu ya Maji kwa Imani”)Nimezungumza leo hii, BABA YAHUVEH/YAHWEH wenu. Bibi Arusi wa kweli wa YAHUSHUA MASIHI wanaosikia Neno hili watakutafuta na kuthibitisha Neno hili. Wameisikia sauti YANGU. Watasimama nawe, watakuwa waaminifu na kukusaidia. Hawatajali wanachosema wanaume na wanawake. Watasimama na yale wanayojua ni ukweli.

Jua haya pia, Unabii huu unawapa maadui sababu zaidi za kukuchukia, lakini haya si mapya. YAHUSHUA Alichukiwa na Anachukiwa. Je, haya yatakushtua vipi, na nyinyi ndio uso WAKE duniani humu, wale Ninaowaita ‘Bibi Arusi wa YAHUSHUA MASIHI’.

Ilizungumzwa leo hii Februari 19, 2010, Sabato.

Iliisha Saa 6:24 Jioni.Ilizungumzwa katika Upako wa RUACH ha KODESH kwake Mtume Elisabeth Sherrie (Elisheva Eliyahu)

Nikiwakera wengi, na kuwa Baraka kwa wengine. Mtoto, Shujaa, Bibi Arusi wa YAHUSHUA MASIHI/YESU KRISTOWasiliana Nasiwww.amightywind.com

www.almightywind.com* * * * * * *

Hii ni habari iliyotolewa kwenye intaneti inayohusu alichosema Elton John.

Elton John adai kuwa Yesu alikuwa shoga19/02/2010Elton John amepata pingamizi kutoka vikundi vya Wakristo baada ya kusema kuwa Yesu alikuwa mwanamume shoga alipohojiwa.Mwanamziki huyu aliye na miaka 62 alisema maneno haya alipohojiwa na gwaride la gazeti la US.Katika hoji, itakayochapishwa kesho Marekani, Elton John alisema: “Ninadhani kuwa Yesu alikuwa mwanamume shoga aliyekua na upendo, ana hekima na anaelewa shida za binadamu.Kwenye msalaba, aliwasamehe wale waliomsulubisha. Yesu alitaka sisi tuwe na upendo na wa kusameheana. Sijui ni nini kinachosababisha watu kuwa wakatili. Jaribu kuwa mwanamke shoga kule Masharaki ya kati – na utauawa.”Stephen Green, mkurugenzi wa Sauti ya Wakristo, alieleza kuwa haya madai ya ushoga ni “upuzi”.Alisema: “Bibilia inasema kuwa Yesu alikuwa bila dhambi na hiyo inamaanisha kuwa ushoga ni dhambi”Hiki ni kilio cha kutaka kuonekana.” Mike Judge, wa Shirikisho la Wakristo, alipinga maneno ya mwanamziki huyu, akisema: “Ingekuwa mwanasiasa maarufu aliyesema maneno haya, ningesema kitu.Lakini huyu ni Elton John na sidhani kuwa kuna yeyote ambaye anamjali.”Vikundi vya Wakristo mashoga walimpongeza Elton, ambaye huonekana mara nyingi na msalaba, walikuwa wamefungua mjadala/mdahalo kuhusu ushoga na kanisa.Jeremy Marks, mwanzishi na mkurugenzi wa “Courage” kikundi cha Wakristo mashoga, alisema: “Hakuna yeyote ajuaye na atawahi kujua kuwa jinsia ya Yesu ilikuwa nini.Kwa kweli, fikra za uhusiano kati ya wanaume, na wanaume na wanawake zilikuwa tofauti wakati huo na haitatambulika leo.Nadhani anaelezea vile anamwona Yesu katika maisha yake na anataka kuwapa moyo kuona hivyo pia.”John Blowers, mshiriki wa Shirika la Uinjilisti wa Wakristo Mashoga, alisema: “Kinachofanyika wakati mwingi kila wakati mjadala huu unatokea ni mjadala huu unagawanyika sana.Jambo la muhimu ni sisi wote ni watoto wa Mungu.”Maneno ya Elton yalisemwa katika hoji iliyopewa mada hii, “Kuna Chuki Nyingi Duniani Humu”.Aliambia gazeti kuwa, kwake, umaarufu haina maana tena.Princess Diana, Gianni Versace, John Lennon, Michael Jackson, wote wamefariki,” alisema.Wawili walipigwa risasi nje ya nyumba zao. Maneno haya hayangefanyika kama hawakuwa maarufu.Umaarufu inawaleta wazimu. Mimi sikuwahi kuwa na mlinzi, kamwe, mpaka Gianni alipokufa. Sipendi kuwa mashuhuri tena.”Mwanamziki huyu pia akafichua vile yeye na mpenzi wake Furnish wanavyoweka upendo wao uendelee kuwa na nguvu.Alisema: “Kila Jumatatu kwa miaka 16, tumetumiana sote kadi, haijalishi tuko wapi duniani humu, kusema vile tunavyopendana.Hatujawahi kuwa na wivu. Tunaongea kuhusu maneno ya ngono, maneno ambayo yangetufanya tuogope hapo awali.”Elton pia alizungumza kuhusu uhusiano wake na dawa za kulevya, akisema: “Kwa watu wengine gramu moja ya cocaine inaweza kukaa mwezi mmoja. Sio mimi. Lazima niimalize, alafu ninataka nyingine.Katika mwisho wa siku, ilisababisha tu moyo wangu kuvunjwa.”


* * * * * * *