UNABII WA 116
Mnapazwa Kutembea Juu Ya Maji Kwa Imani
Imeandikwa/Imezungumzwa katika upako wa RUACH ha KODESH
(ROHO MTAKATIFU) kupitia Mtume Elisabeth Sherrie Elijah Nikomia.
Ilipokelewa Septemba 30, 2009 mwisho wa Yom Kippur
\
Ilitolewa Octoba 14, 2009
(Hii inatoka Unabii wa 105, YAHUVEH alisema iwekwe kwa kila unabiii kutoka sasa na kwenda mbele: Nilikuonya kitambo Elisabeth kutoita hii Huduma jina la mwanaume au mwanamke hata kabla kuweko Huduma. Niliweka kwa roho yako kwa kuwa hii haikutoka kwa mkono wako, hii haikutoka kwa kinywa chako. Ilitoka kwa kinywa cha YAHUVEH aliyeizalisha. Ilitoka kwa kinywa cha RUACH ha KODESH (ROHO MTAKATIFU) aliyeizalisha. Ilitoka kwa kinywa cha YAHUSHUA aliye MASHIACH aliyeizalisha. Kama tu ingekuwa kwa mkono wako, ingekuwa imekosa kuendelea zamani. Ni kwa upepo wa SHKHINYAH GLORY inayopulizia duniani kote, Upepo Takatifu wa Ufufuo. Sio kwa pumzi yako, ama haingefaulu. Isaya 42:8)
*******
Maelezo ya jinzi Unabii huu ulivyopokelewa:
Adam na Elisabeth walikuwa wanazumgumza kwa simu. Walianza kuomba kwa ajili ya kusafiri salama kwa Adam na Kathrnyah kuwatembelea Elisabeth na Niko kwa ajili ya sherehe ya Sukkot.
Hii Unabii wote hauko katika kinaza sauti. Sauti iliyorekodiwa inaanza takriban theluthi moja(1/3) Unabii ukiwa umeendelea.
*******
Neno la Unabii linaanza:
Waambieni waje tarehe tano kwa kuwa hata ingawa sio watano wanaokuzanyika, inasimamia watano werevu (Matayo 25: 1-13). Kwa sababu ya lile neno jipya ambalo limepeanwa, Niko hasikose shabaha kwa ajili ya hii. Kwa kuwa nimeashiria kwamba atakuwa mwenye kuandika kutoka neno lililorekodiwa.
Na hili Neno litakuwa tofauti na mengine kwa kuwa nimeshalithibitisha ninapoitetemesha ulimwengu huu kwa hasira zangu katika siku hii ya hukumu.
Kuweni tayari kuona mamlaka yakianguka. Kumbukeni Saburi 91, hata ingawa unaona 10,000 yakianguka karibu nawe na itaonekana kana kwamba wote waliokuzunguka wanaanguka, kwa kuwa ni mimi YAHUVEH ninayewaangusha kwa hasira zangu!
Lakini wote WALIOWANGU hawapazwi kuniogopa. Kwa kuwa mko katika kiganja cha mkono Wangu na mkono Wangu mwingine unakufunika. Nyinyi ni kama vivaranga na nawaambieni hii sasa ili mapawa yenu yasikwaruzwe kwa kuwa mtayaona yale msiotaka kuyaona na mtasikia yale usiotaka kuyasikia.
Lakini msiruhusu uwoga uwatawale, kumbukeni pahali palipo imani yenu. Msiweke imani yenu katika uchumi, fedha ama katika kazi pahali mmeajriwa ama katika biashara mnazomiliki. Wekeni imani yenu katika MIMI tu, ABBA YAHUVEH na Mwanangu Mzaliwa wa pekee YAHUSHUA ha MASHIACH Masihi wenu na RUACH ha KODESH (ROHO MTAKATIFU) wa dhamana. Wekeni imani yenu na macho yenu kwa ahadi niliowapa. Kuweni wakutembea juu ya maji. Petro hangejua kwamba angeweza kutembea juu ya maji kama hangejitokeza nje ya chombo na kuchukua ile hatua ya kwanza akitembea kuelekea kwa YAHUSHUA. Uwoga ndio uliomfanya kuanza kuzama, lakini macho yake yalipomwona YAHUSHUA tena,
Sauti iliorekodiwa unaanza hapa:
aliweza kutembea juu ya maji tena. Hii ndio natarajia kwenu.
Matayo 14:28-31
28 Petro akamwambia, "Bwana, ikiwa ni wewe kweli, amuru nitembee juu ya maji nije kwako."
29 YAHUSHUA akasema, "Haya, njoo." Basi, Petro akashuka kutoka ile mashua, akatembea juu ya maji, akamwendea YAHUSHUA.
30 Lakini alipouona ule upepo, aliogopa, akaanza kuzama; akalia kwa sauti, "Bwana, niokoe!"
31 Hapo, YAHUSHUA akaunyosha mkono wake, akamshika na kumwambia, "Ewe mwenye imani haba! Kwa nini uliona shaka?"
Mnapazwa kutembea juu ya maji kwa imani kwa kuwa yale mtakayoona ulimwenguni, hasa katika mwaka wa 2010, yatafanya mioyo ya wengi kutahayari kwa uwoga. Msiweke imani yenu kwa serikali za ulimwengu huu. Msiweke imani yenu kwa mwanasiasa wowote, kwa kuwa wana matakwa yao wenyewe. Haya ni maneno ninayowaambieni, kwa kuwa nimeanza kutetemesha na haitakoma. Nakataa kuomba mzamaha Sodoma na Komora. Nji yenu yanayoendelea kuhalalisha dhambi, muone nitakayowafanyia. Wale wanaojiita Wakristo na wanaendelea kunyamaza kimya, msininungunikie wakati hamna uhuru tena, kwa kuwa mlinyamaza kimya. Mnawachia wachache walalamike. Mnawachia wengine watete. Hamtambui ya kuwa maadui hawanyamazi? Hamtambui ya kuwa wale wanaotangaza dhambi hawanyamazi? Wanapasa sauti kwa nguvu hata ingawa hawa ni wachache. Watumishi wa shetani hawanyamazi. Kwa nini watumishi wa YAHUSHUA wananyamaza kimya? Na ninapoongea kuhusu watumishi, siwazungumzii kana kwamba ninyi ni watumishi kwa neno mnalolitumia. Nawazungumzia wale wanaotumikia YAHUSHUA. Ni wachache wanaoongea. Niwachache wanaotetea ile iliyotakatifu.
Kumbukeni ya kuwa hukumu uanza katika Nyumba ya Bwana (1 Petro 4:17). Kwa nini makanisa wote hawalalamiki? Ni makanisa mangapi yapo? Katika kila nchi kwa nini makanisa hayalalamiki dhidi ya hizi sheria za machukizo zinazopitishwa. Wanainua na kushusha mabeka yao (kumaanisha hawajali). Wanazingatia tu yale yanayowahuzu. Kwa hivyo mzishangae enyi makanisa mliyo na mapangilio, wakati serikali itakapowakujia na kuchukua uhuru wenu wa kuhubiri na kuweka kiashiria ya kufungwa kwa makanisa yenu. Msishangae wakati ardhi yenu itakapotwaliwa. Msishangae enyi mnaojifuna mkiwa na mamilioni.
Nawazungumzia sasa matajiri – mnaweka imani yenu katika fedha zenu, msishangae wakati itakapokuwa bure ila mchanga tu – majivu mikononi mwenu ( matayo 19:24, Luka 16: 19-31).
Nitawaonyesha.
Nitaionyesha hii dunia.
Wengi wataanza kupata habari kuanzia mwaka wa 2010, lakini nawaonya watoto wangu sasa ili msiseme Baba wenu hakuwaonya. Nawatayarisha sasa ili msishtuke na nawafariji sasa kwa kuwa ABBA wenu hataki mfadhaike mioyoni mwenu, kwa kuwa nawapenda ninyi. Kama vile ilivyokuwa katika siku za hapo awali, nilitenda miujiza na hakuna kitu ambacho kimebadilika. Kwa hivyo mshikilie pindo la vazi la YAHUSHUA.
Mzidi kuoshwa na damu yake yaliyomwagika.
Simameni katika mavazi yake ya utakatifu na ninawahakikisheni ninyi, maombi yenu yote yanazikika juu Mbinguni.
Tembea katika utakatifu ili shetani asikushtaki. Tembea katika utakatifu ili usililetea aibu jina la YAHUSHUA ha MASHIACH.
Masikio yangu yamefunguliwa kwa hali ya kipekee, tena Elisabeth umelizungumzia hili ulipoomba. Ni kana kwamba ungesikia sindano ikianguka, kwa kuwa siku hii ni la kipekee kwa wale wote wanaozingatia Yom Kippur nilipowaona mkitubu kwa ajili ya yote yasiyonipendeza. Wakati kila hitaji la maombi yenu yalivyoletwa kwangu wakati huo huo hasira zangu zilitetemesha dunia. Kama vile katika hapo awali na Musa, wana wa Israeli walilindwa na wale waliomwabudu mwumbaji mwingine hawakupata ulinzi. Hakuna kilichobadilika. Nitawabariki wale walio wa baraka KWANGU. Nitawalaani wale walio wa laana KWANGU, na kwa hivyo nimezungumza leo, ABBA Wenu YAHUVEH.
[Kama utipitisho hapo awali siku hiyo Kathrynyah alikuwa kwa maombi na katika ulimwengu wa kiroho aliwaona waumini katika YAHUSHUA kama vifaranga vichanga wakihitaji kuongozwa na YAHUSHUA. Alinyoosha mkono wake na alikuwa anatuongoza kama vifaranga vichanga.]
Kwa hivyo imezungumzwa, kwa hivyo imeandikwa Septemba 29, 2009
Mwana, Shujaa, Bibi arusi wa YAHUSHUA ha MASHIACH,
Mtume Elisabeth S. Elijah Nikomia
Barua pepe
revholyfire@yahoo.co.uk
amightywind2k@yahoo.com
Tofuti
www.amightywind.com
www.almightywind.com
Anwani la kutuma Barua:
Amightywind
P.O. Box 40007
Upper Hutt
New Zealand 5018
Saburi 2
1 Mbona mataifa wanafanya ghasia, Na makabila wanatafakari ubatili?
2 Wafalme wa dunia wanajipanga, Na wakuu wanafanya shauri pamoja, Juu ya YAHUVEH, Na juu ya Masihi wake,
3. Na tuvipasue vifungo vyao, Na kuzitupia mbali nasi kamba zao.
4. Yeye aketiye mbinguni anacheka,YAHUVEH anawafanyia dhihaka.
5. Ndipo atakaposema nao kwa hasira yake,na kuwa fadhaisha kwa ghadhabu yake.
6. Nami nimemweka mfalme wangu juu ya Sayuni, mlima wangu mtakatifu.
7 Nitaihubiri amri; YAHUVEH aliniambia, ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa.
8. Uniombe, name nitakupa mataifa kuwa urithi wako, na miisho ya dunia kuwa milki yako.
9. Utawaponda kwa fimbo ya chuma, Na kuwavunja kama chombo cha mfinyanzi.
10. Na sasa, enyi wafalme, fanyeni akili, Enyi waamuzi wa dunia, mwadibiwe.
11. Mtumikieni YAHUVEH kwa kicho, Shangilieni kwa kutetemeka.
12. Mbusuni Mwana, asije akafanya hasira, nanyi mkapotea njiani, Kwa kuwa hasira yake itawaka upesi; heri wote wanaomkimbilia.
Yeremia 26:3
Labda watasikia, na kughairi na kuacha kila mtu nia yake mbaya; ili niyaghairi mabaya niliyokusudia kuwatenda, kwa sababu ya uovu wa matendo yao.
Kumbukumbu la Torati 13:4
Tembeeni kwa kumfuata YAHUVEH, Mungu wenu; mcheni na kushika maagizo yake na kisikia sauti yake, nanyi mtumikieni na kushikamana naye.
Matayo 25: 1-13
1 "Wakati huo, Ufalme wa mbinguni utafanana na wasichana kumi waliochukua taa zao, wakaenda kumlaki bwana arusi.
2 Watano miongoni mwao walikuwa wapumbavu na watano walikuwa wenye busara.
3 Wale wapumbavu walichukua taa zao, lakini hawakuchukua akiba ya mafuta.
4 Lakini wale wenye busara walichukua mafuta katika chupa pamoja na taa zao.
5 Kwa kuwa bwana arusi alikawia kuja, wale wanawali wote wote walisinzia, wakalala.
6 Usiku wa manane kukawa na kelele: `Haya, haya! Bwana arusi anakuja; nendeni kumlaki.`
7 Hapo wale wanawali wote wakaamka, wakazitayarisha taa zao.
8 Wale wapumbavu wakawaambia wale wenye busara: `Tupeni mafuta yenu kidogo maana taa zetu zinazimika.`
9 Lakini wale wenye busara wakawaambia, `Hayatatutosha sisi na ninyi! Afadhali mwende dukani mkajinunulie wenyewe!`
10 Basi, wale wanawali wapumbavu walipokwenda kununua mafuta, bwana arusi akafika, na wale wanawali waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye katika jumba la arusi, kisha mlango ukafungwa.
11 Baadaye wale wanawali wengine wakaja, wakaita: `Bwana, bwana, tufungulie!`
12 Lakini yeye akawajibu, `Nawaambieni kweli, siwajui ninyi."`
13 Kisha YAHUSHUA akasema, "Kesheni basi, kwa maana hamjui siku wala saa.
Luka 16: 19-31
19 "Palikuwa na mtu mmoja tajiri, ambaye alikuwa anavaa mavazi ya bei kubwa sana ya rangi ya zambarau, na ya kitani safi, na kufanya sherehe kila siku.
20 Kulikuwa pia na maskini mmoja jina lake Lazaro, aliyekuwa amejaa vidonda na alikuwa analazwa mlangoni pa nyumba ya huyo tajiri.
21 Lazaro alitamani kula makombo yaliyoanguka kutoka meza ya tajiri; na zaidi ya hayo, mbwa walikuwa wanakuja na kulamba vidonda vyake!
22 "Ikatokea kwamba huyo maskini akafa, malaika wakamchukua, wakamweka karibu na Abrahamu. Na yule tajiri pia akafa, akazikwa.
23 Huyo tajiri, alikuwa na mateso makali huko kuzimu, akainua macho yake, akamwona Abrahamu kwa mbali na Lazaro karibu naye.
24 Basi, akaita kwa sauti: `Baba Abrahamu, nionee huruma; umtume Lazaro angalau achovye ncha ya kidole chake katika maji, auburudishe ulimi wangu, maana ninateseka mno katika moto huu.`
25 Lakini Abrahamu akamjibu: `Kumbuka mwanangu, kwamba ulipokea mema yako katika maisha, naye Lazaro akapokea mabaya. Sasa lakini, yeye anatulizwa, nawe unateswa.
26 Licha ya hayo, kati yetu na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wanaotaka kuja kwenu kutoka huku wasiweze, wala wanaotaka kutoka kwenu kuja kwetu wasiweze.`
27 Huyo aliyekuwa tajiri akasema: `Basi baba, nakuomba umtume aende nyumbani kwa baba yangu,
28 maana ninao ndugu watano, ili awaonye wasije wakaja huku kwenye mateso.`
29 Lakini Abrahamu akamwambia: `Ndugu zako wanao Mose na manabii; waache wawasikilize hao.`
30 Lakini yeye akasema: `Sivyo baba Abrahamu, ila kama mtu atafufuka kutoka wafu na kuwaendea, watatubu.`
31 Naye Abrahamu akasema: `Kama hawawasikilizi Mose na manabii, hawatajali hata kama mtu angefufuka kutoka wafu."`
Matayo 19:24
24 Tena nawaambieni, ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita katika tundu la sindano, kuliko kwa tajiri kuingia katika Ufalme wa mbinguni."