Unabii wa 110

 

 

Kondoo WANGU Msiwe Na Hofu Wala Kutetemeka, Kwa Kuwa MIMI Huwapiga Mbali Mbwa Mwitu!

 

 

Imeandikwa/Imezungumzwa katika upako wa RUACH ha KODESH

kupitia Mtume Elisabeth Sherrie Elijah Nikomia.

Ilipewa Aprili 5, 2009

    Ilitolewa Aprili 10, 2009

 

 

 

(Kutoka Unabii wa 105, YAHUVEH alisema ujumbe huu uwekwe katika kila unabiii kutoka sasa: Nilikuonya kitambo Elisabeth kutoita huduma hii kwa jina la mwanaume au mwanamke hata kabla kuwepo na huduma. Niliiweka ndani ya roho yako kwa kuwa hakuna lolote kwa haya lililofanyika kwa mkono wako au lililotoka kwenye kinywa chako. Ilitoka kwenye kinywa cha YAHUVEH aliyeizalisha. Ilitoka kwenye kinywa cha YAHUSHUA, MASHIACH wako aliyeizalisha. Ilitoka kwenye kinywa cha RUACH ha KODESH, IMMAYAH wako aliyeizalisha. Kama ingekuwa tu kwa mkono wako, ingekuwa imefeli kitambo. Ni kwa upepo wa SHKHINYAH GLORY unaovuma kote duniani, upepo Takatifu wa uamsho, sio kwa pumzi yako, au ingekuwa imefeli. (Isaya 42:8)

 

*******

 

Kumbukumbu: Amightywind imekuwa kwenye mtandao miaka 14 lakini itakuwa miaka 21 siku ya Aprili 10, 2009. Huduma hii imekuwa duniani kwa miaka 21 lakini imekuwa kwenye mtandao miaka 14. Nina matumaini kuwa haya yanaeleza siku za kuzaliwa na maadhimisho ya miaka zote zinazosherehekewa. Kila siku ya kuzaliwa na siku ya maadhimisho ya miaka ya Huduma hii ina Ushindi katika YAHUSHUA, MASHIACH wetu kwa sababu shetani amejaribu kuisimamisha Huduma hii hata kabla nizaliwe.

 

                   *********

 

Niko, ongea kwa sauti kubwa ndio kila mtu aone kwa uwazi ushindi yenye Huduma hii imekuwa nayo kwa muda wa miaka 14 kwenye mtandao. Kwa maandishi makubwa weka tarehe ya Aprili 10 kwa yale ambayo adui alisema itaharibiwa kule Indiana mahali pa maumivu ya kuzaliwa ya Huduma hii. Siku ya Aprili 10, 2009 haijaishi tu bali imeenea kote duniani na kuwa miaka 21. Hii sio ushindi wa mwanamume au mwanamke yeyote bali tu ni ushindi wa ABBA wako, ushindi wa YAHUSHUA wako, ushindi wa RUACH ha KODESH mpendwa, IMMAYAH wako.

 

Kwa hivyo sitaki yeyote kutafuta haya. Mimi naitaka mbele ya nyuso za maadui kwa kuwa hii ni siku ya ushindi mkubwa. Elisabeth, Nilipokuweka kwenye mtandao huu ni wachache, ni wachache na mbali kati yao waliokuwa Manabii wanawake. Wewe umefungua njia na MIMI ninakutumia kufanya yale ambayo hayajawahi fanywa kwa kuwa wewe hutabiri kwa Ndimi Takatifu. Hauwezi hata elewa ile athari hii inayo kwake adui kwa kuwa imebebwa kote kwenye hewa mpaka kona nne za dunia. Sauti yako iliyojaa upako WANGU, iliyojaa nguvu ZANGU, haijawekwa tu kwenye maandishi, sio tu kwenye tarakilishi na cd lakini pia kwenye ipod, na kwenye vinaza sauti kwa kuwa sio tu maandishi bali pia ni neno linalozungumzwa.

 

Kwa hivyo siku hii haisherehekewi tu duniani lakini pia inasherehekewa Mbinguni. Sio tu kuzaliwa kwako wa mwili lakini kule kuzaliwa kwa Huduma kwenye mtandao siku ya Aprili 10, miaka 21 inavyohesabiwa kwa wakati wa binadamu. Siku moja mbinguni, na sio mbali, wale wote waliokusaidia wataona matokeo za uaminifu wa mbegu moja ndogo, ndogo sana iliyoanza kutoka mwanzo mdogo. MIMI huitumia sio tu kwa sasa, lakini itatumika hata katika siku ya Dhiki Kuu na ukweli ZANGU zitaendelea kuwapa binadamu uhuru wakiamini.

 

Sasa Elisabeth (Soma Ushuhuda wa Elisabeth) unajua ni kwa nini adui alitaka ufe wakati huu wote na wakati ambapo haikuwa kwa mikono ya shetani ulikuwa unajaribu kwa mikono yako mwenyewe. Lakini kupitia Jina na Damu ya YAHUSHUA MASHIACH wako, sio tu wewe umepata ushindi lakini pia wale wote wanaosikiza na kuamini.

 

MWANANGU mpendwa Niko, Neeky WANGU, (Sina ujuzi wowote wa kuandika jina hili lakini hivi ndivyo ilivyosikika) haya yalikuwa katika mpango WANGU mzuri kukuleta kwa kuwa nilipokuleta mzigo ulikuwa mzito sana kwake Elisabeth kubeba na kama MIMI singefanya hivi angekuwa amekata tamaa kitambo. (Soma Iliyosasishwa - Usikate tamaa na Usikubali Kushindwa) MIMI sikuacha hapo, Nilimtumia yeye kuzalisha Mashujaa wa YAHUSHUA (YDS) na hata kwa hayo alilipa gharama kabla Niwatume Malaika Watakatifu (Soma kuhusu uponyaji wa Elisabeth kwa kushika bawa la Malaika Mkuu Michael) kwake. Sasa wao (YDS) husimama kupinga zile nguvu za uovu wakiombeza na wakiomba kila siku takriban muda wa saa moja kwa wakati. Hawa ni Shujaa spesheli watakatifu walio na upako, baraka zao zitakuwa kubwa, kubwa, kubwa, ila tu wabaki waaminifu KWANGU.

 

Elisabeth: Asante ABBA.

 

Kwa hivyo Ninakuweka katika nyumba ambapo karibu na wewe katika malisho kondoo wanatembea kwa uhuru kukukumbusha ya kuwa MIMI, YAHUSHUA ndiye Mchungaji wako Bora na MIMI nikikutunza, kumbuka daima, kama tu hao kondoo karibu nawe hawana hofu wala kutetemeka, wanaamini yule mkulima kuwaongoza kwenye malisho kijani. Hata hivyo, Nimekuongoza katika malisho kijani. Ninakulinda. Ninawapiga mbali mbwa mwitu au yeyote anayejaribu kukuumiza. Kama tu wale kondoo hawana hofu na wale wana kondoo hawana hofu pia nyinyi wawili mnaoishi katika nyumba hio na wale walio na nyinyi hamtakuwa na hofu. Ni hapa wapendwa WANGU Nitakaporejesha roho zenu mkilala chini katika malisho kijani ZANGU na kutotanga na kujaribu kujitafutia zenu.

 

Mimi ninazungumza na wale wote wanaoniruhusu MIMI, YAHUSHUA, kuwa MASHIACH wenu, kuwa Mchungaji wenu Bora. Nitawalinda wale walio WANGU. Kwa wale wanaoangalia Huduma hii kama baraka iliyofanywa kwa mikono YANGU, mikono yaliyodungwa na misumari ya YAHUSHUA wako, watapata miujiza mingi kutoka KWANGU. Kama waliamini yale maneno MIMI niliyoyasema na hawajaona aibu na kukemea jambo lolote. Wanakemea uongo. Wanasima imara kwa yale wanayoamini na wanapigana katika vita naye shetani aliye adui na watumishi wake wanaotumwa.

 

Yeyote atakayedai kuwa Huduma hii sio takatifu roho iliyo ndani yao kwa kweli imefichuliwa na wao sio WANGU. Ndio Nasema, Roho Mtakatifu hayupo ndani yao kwa kuwa hauwezi kusema kuwa yale yaliyo takatifu, yale ambayo huinua kiwango cha utakatifu, kuonya watu watubu dhambi kabla wakati haujaisha, kiunua Majina ya ABBA YAHUVEH, MIMI YAHUSHUA MASHIACH wako na RUACH ha KODESH. Yeyote atakayenena kuwa haya ni maovu, kwa kweli Nawaambia hivi, wamenena tusi na wanafaa kutetemeka kwa hofu kwa kuwa kila neno waliyonena, Ninasikia. Na katika siku ya hukumu maneno yao yatasemwa tena na watainamisha vichwa zao kwa aibu na kama wangeweza wangerudia tena kwa njia nyingine.

 

Lakini kumbukeni Watoto WANGU, MIMI sikuiita hii ‘Huduma ya Jaribio la Mwisho’ bila sababu. Yeyote anayekuja katika Huduma huja mbele yake YAHUVEH na chochote watakachokufanyia wanamfanyia YEYE. Kwa kuwa hakuna mwanaume au mwanamke yeyote anayepata utukufu kwa ajili ya Huduma hii, Sifa, Heshima na Utukufu wote unaenda kwa wale mnaowaita Utatu Takatifu.

 

Kwa hivyo ni katika siku hii na ni katika Aprili 5, maadhimisho ya miaka ya mara ya kwanza MIMI nilipokuambia Elisabeth kuwa wewe ni Ringmaiden WANGU na MIMI hutumia yale maneno yanayozungumzwa kupitia kwako ili kufikia ulimwengu huu, kwa wale wanaotaka kusikiza na ndio Nasema, hata wale ambao wanalazimishwa kusikiza na kwa wale watakaosikiza.

 

Katika siku ya Aprili 10, 2009 MIMI Ninataka sherehe hii itangazwe kwa kilio kuu kila mahali mbali na pana, 21 kama binadamu anavyohesabu miaka na Huduma hii bado ipo hapa na ni kwa Sifa, Heshima na Utukufu wa YAHUVEH Ninasema hivi.

 

Mwisho wa Neno

 

Elisabeth: Asante ABBA. Asante YAHUSHUA Mpendwa. Asante RUACH ha HODESH Mpendwa. Yote kwa sababu tunakuuliza tena na mume wangu……

 

Niko: Chunga, usiseme hivyo.

 

Elisabeth: (Akicheka) Asante. Tunakupa asante tu Abba YAHUVEH. Mume wangu aliniuliza niombe na tukaomba. Asante Baba hii ni kwa kweli sherehe ya furaha, furaha kwa siku ya kuzaliwa na yote ni kwa Sifa, Heshima na Utukufu ya Aleph na Tav, Alpha na Omega, Abba YAHUVEH wetu, YAHUSHUA MASHIACH wetu Mpendwa na RUACH ha KODESH wetu Mpendwa.

 

Asante. Asante. Asante. Asante.

 

Amina

 

Alipewa huyu Mtoto, Shujaa, Bibi Arusi wa YAHUSHUA, MASHIACH wetu

Aprili 5, 2009

 

Kama Unabii huu umekubariki tafadhali nitumie barua pepe uniambie.

 

Contact AmightyWind

www.amightywind.com
www.almightywind.com